Publicado
Kuondolewa kwa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19
20 de abril de 2023
Maoni haya ya ushauri wa sera hutathmini iwapo Meta inapaswa kuendelea na kuondoa baadhi ya kategoria za taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, au iwapo mbinu isiyo na vizuizi sana inaweza kulingana vyema na maadili na majukumu yake ya haki za binadamu.
I. Muhtasari wa utendaji
Mnamo Julai 2022, Bodi ya Usimamizi ilikubali ombi kutoka Meta la kutathmini iwapo inapaswa kuendelea na kuondoa baadhi ya kategoria za taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, au iwapo mbinu isiyo na vizuizi sana inaweza kulingana vyema na maadili na majukumu yake ya haki za binadamu. Maoni haya ya ushauri wa sera ni jibu la Bodi kwa ombi hilo.
Bodi imefanya uchunguzi wa kina na mashauriano na umma. Kutokana na Meta kushikilia kwamba inataka mbinu moja ya kimataifa ya kushughulikia taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, Bodi ilihitimisha kwamba, maadamu Shirika la Afya Duniani (WHO) linaendelea kutangaza COVID-19 kama dharura la afya ya umma kimataifa, Meta inapaswa kudumisha sera yake ya sasa. Hiyo inamaanisha kwamba inapaswa kuendelea kuondoa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 ambayo ina uwezekano wa kuchangia hatari inayoweza kutokea na madhara mabaya ya kimwili yanayoweza kutokea. Hata hivyo, Bodi imepata kwamba Meta inafaa kuanza mchakato wa kutathmini upya kila mojawapo ya madai 80 ambayo huwa inaondoa kwa sasa, kwa kushirikisha washikadau wengine. Inapaswa pia kuandaa hatua za endapo tangazo la WHO limebatilishwa, ili kulinda uhuru wa kujieleza na haki nyingine za binadamu katika hali hizi mpya. Bodi inapendekeza kwa dhati kwamba Meta ichapishe maelezo kuhusu maombi ya serikali ya kuondoa maudhui kuhusu COVID-19, kuchukua hatua ya kusaidia watafiti huru kwenye majukwaa yake, kutathmini uhusiano uliopo kati ya muundo wa majukwaa yake na taarifa isiyofaa, na kuhimiza ufahamu kuhusu taarifa isiyofaa inayohusu COVID-19 kote duniani.
Usuli
Mapema mnamo 2020, wakati janga kubwa la COVID-19 lilijikita, Meta ilianza kuondoa kutoka kwenye Facebook na Instagram, madai kadhaa ambayo kampuni hiyo ilitambua kama taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19. Orodha ya madai yanayohusiana na COVID-19 ambayo kampuni hiyo huondoa imeundwa wakati janga hilo kubwa lilikuwepo. Leo, Meta huondoa takriban madai 80 tofauti ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 chini ya sera yake ya “Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya umma”, sehemu ndogo ya Viwango vya Jumuiya kuhusu Taarifa isiyofaa iliyoundwa ili kushughulikia mapendekezo ya Bodi katika uamuzi kuhusu “Tiba Inayodaiwa ya COVID”. Maoni haya ya ushauri wa sera yanalenga kipekee hatua ambazo Meta ilichukua wakati wa janga kubwa la COVID-19 chini ya sera yake ya “Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya umma” . Hayashughulikii hatua ambazo Meta imechukua wakati wa janga kubwa la COVID-19 chini ya sera nyingine.
Chini ya sera ya “Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya umma”, Meta huondoa “taarifa isiyofaa wakati wa dharura za afya ya umma wakati mamlaka za afya ya umma zimehitimisha kwamba taarifa ni ya uongo na ina uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea.” Meta ilitegemea mamlaka za afya ya umma kipekee ili kubaini iwapo kanuni hiyo haijatimizwa. Madai 80 ambayo inaondoa kwa sasa ni pamoja na, kwa mfano, kukana kuwepo kwa COVID-19 na kusisitiza kwamba chanjo za COVID-19 zinasababisha hali ya sumaku. Meta iliondoa vipande milioni 27 vya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 kutoka kwenye Facebook na Instagram kati ya Machi 2020 na Julai 2022, milioni 1.3 kati yazo ilirejeshwa kupitia rufaa. Taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 ambayo haitimizi viwango vya kuondolewa vinaweza kukaguliwa ukweli, kuwekewa lebo na au kushushwa. Wakaguzi wa ukweli wanakadiria maudhui (kwa mfano, kama “uongo,” au “yasiyo na muktadha”). Kisha Meta inaiwekea lebo kuwa ni hivyo na kutoa viungo vya makala ya mkaguzi wa ukweli kuhusu mada hiyo. Kampuni hiyo pia inashusha maudhui yaliyo na lebo ya wakaguzi wa ukweli, hii inamaanisha kwamba yanaonekana mara chache zaidi na kwenye milisho ya mtumiaji, kwa kutegemea vigezo kadhaa. Meta pia hutumia “lebo za wastani” kwenye maudhui yanayohusiana na COVID-19. Lebo hizi zina taarifa kama vile, “baadhi ya matibabu ya COVID-19 ambayo hajayaidhinishwa yanaweza kusababisha madhara mabaya,” na kuelekeza watu kwenye kituo cha maelezo kuhusu COVID-19 cha Meta, ambacho kinatoa maelezo kuhusu hatua za kuzuia, chanjo na rasilimali kutoka kwa mamlaka za afya ya umma.
Katika ombi lake kwa Bodi, Meta iliuliza iwapo inafaa kuendelea kuondoa taarifa fulani isiyofaa kuhusu COVID-19. Vinginevyo, kampuni hiyo ilisema kwamba inaweza kuacha kuiondoa na badala yake kushusha maudhui hayo, kuyatuma kwa wahusika wengine wakaguzi wa ukweli, au kuyawekea lebo. Meta ilishikilia kutumia mbinu moja ya kimataifa kushughulikia taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, badala ya kutumia mbinu mbalimbali kulingana na nchi au eneo. Kulingana na kampuni hiyo, kutumia mbinu ya ujanibishaji wa sera katika kiwango kunaweza kusababisha ukosefu wa uwazi kwa watumiaji na utekelezwaji mbovu, na haina uwezo wa kutumia mbinu kama hiyo. Katika kuzingatia ombi hilo, Bodi ilifanya mashauriano ya kina na umma. Hizi zilijumuisha misururu ya mikutano ya mtandaoni na washiriki kutoka duniani kote, uliofanywa kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii, ambapo Bodi ilisikia kutoka kwa wataalamu na washikadau mbalimbali.
Matokeo muhimu na mapendekezo
Bodi imepata kwamba kuendelea kuondoa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 ambayo “ina uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili” wakati wa dharura la afya ya umma kote duniani kunaambatana na maadili na majukumu ya Meta ya kulinda haki za binadamu. Awali Bodi ilichunguza iwapo ingefaa zaidi kwa Meta kuchukua mbinu iliyojanibishwa zaidi kushughulikia taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 katika kiwango. Hata hivyo, Meta ilisisitiza kwamba hii haiwezekani bila kuhujumu pakubwa uwazi na usawa kwa watumiaji na kuongeza makosa kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza sera yake. Wasiwasi wa Meta unaweza kuwa na msingi. Hata hivyo, kwa kufungia nje chaguo hili, Meta imekandamiza juhudi za Bodi za kuoanisha maoni yanayoshindana kutoka kwa washikadau na Wanachama wa Bodi kuhusu jinsi ya kushughulikia vyema zaidi taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 na vilevile kuheshimu haki za binadamu, hususan haki ya kuwa na uhuru wa kujieleza. Mapendekezo 18 yaliyo kwenye maoni haya ya ushauri wa sera, ambayo nyingi yao yametolewa muhtasari hapo chini, yanatumika chini ya kizuizi hiki.
Bodi inapendekeza kwamba Meta:
Iendelee kuondoa maudhui ya uongo kuhusu COVID-19 yaliyo na “uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara yanayoweza kutokea ya kimwili wakati wa dharura linaloendelea la afya ya umma kote duniani,” huku ikianzisha ukaguzi wa wazi na jumlishi na tathmini upya wa madai 80 ambayo imeondoa kwa sasa. Dharura la afya ya umma linafanya kuwepo kwa hatari mbaya na ya moja kwa moja kwa afya. Kutokana na Meta kushikilia matumizi ya mbinu moja ya kimataifa kushughulikia taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, Bodi imepata kwamba Meta ni sahihi katika kushughulikia hatua zake za kipekee za sasa za kuondoa taarifa isiyofaa iliyo na uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili, kama iliyobainishwa na mamlaka za afya ya umma. Meta, miongoni mwa mambo mengine, haijarudi kwa mamlaka zinazofaa za afya ili kuziuliza kutathmini upya madai ambayo huwa inaondoa. Wala kuendesha mashauriano mapana na washikadau na wataalamu ili kutathmini upya madai binafsi au sera kwa jumla. Kwa kuwa Meta bado haijashiriki katika mchakato wa ukaguzi wa ukweli ili kubadilisha sera yake (ambalo ni jukumu la Meta), Bodi haiwezi kutoa pendekezo la kubadilishwa kwa sera ambayo inaweza kuathiri kwa njia isiyo na uwiano, wale walio hatarini.
Hata hivyo, kwa kuwa hatupo tena katika hatua za awali za janga, ili kutimiza majukumu yake ya kulinda haki za binadamu, Meta inapaswa kutathmini kila mara iwapo masharti ya kuondoa maudhui yaliyobainishwa kwenye sera zake, yanaendelea kutimizwa. Kwa hivyo inafaa kuanzisha mchakato wa wazi wa kukagua kila mara madai 80 ambayo yanafaa kuondolewa, kwa kushauriana na washikadau mbalimbali. Washikadau wanapotoa ushahidi wazi wa hatari ya kusababisha madhara ya kimwili ndipo ni vyema kulijumuisha kwenye orodha ya madai yanayofaa kuondolewa. Meta inapaswa kushriki na umma matokeo ya ukaguzi huu wa mara kwa mara.
Kuchunguza ujanibishaji wa mbinu yake. Meta inahitaji kupanga cha kufanya wakati WHO imeacha kuainisha COVID-19 kama dharura la afya duniani, lakini mamlaka za afya ya umma za nchi husika zinaendelea kuibainisha kama dharura la afya ya umma. Bodi inapendekeza kuanzishwa kwa mchakato wa utathmini wa kutambua hatua itakazochukua katika hali kama hii. Hatua hizi zinapaswa kushughulikia taarifa isiyofaa yenye uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari kubwa inayoweza kutokea, bila kuingia uhuru wa kujieleza kote duniani. Tathmini ya hatari inapaswa kujumuisha kutathmini iwapo inawezekana kujanibisha utekelezaji wa sera zake.
Kutathmini athari ya muundo wa jukwaa lake. Wataalamu waliibua wasiwasi kwamba muundo wa majukwaa ya Meta unachangia pakubwa taarifa isiyofaa yenye madhara inayohusu afya. Kwa sababu ya madai haya, Bodi inapendekeza kwamba Meta itathmini athari ambayo chaguo zake za muundo zinaletwa kwa haki za binadamu. Kampuni hiyo inapaswa kuzindua tathmini ya athari kwa haki za binadamu kuhusu jinsi mlisho wake, algorithi za mapendekezo na vipengele vingine vinavyochangia pakubwa taarifa isiyofaa yenye madhara inayohusu afya na athari zake.
Iongeze uwazi kuhusu maombi ya serikali. Wakati wa janga kubwa, kuliibuliwa wasiwasi kuhusu jinsi Meta inavyokagua maudhui yanayohusiana na COVID-19 kwa maagizo ya serikali. Hii ina tatizo hususan pale ambapo serikali zilikuwa zinatuma maombi ili kukamata waandamanaji wa amani au watetezi wa haki za binadamu, kudhibiti mazungumzo kuhusu vyanzo vya janga hilo kubwa, na kunyamazisha wale waliosuta au kuhoji mwitikio wa serikali kwa janga la afya ya umma. Umoja wa Mataifa umeibua wasiwasi kwamba baadhi ya serikali zimetumia janga hili kubwa kama kisingizio cha kuvuruga misingi ya demokrasia. Meta inapaswa kuwa na uwazi na kuripoti mara kwa mara kuhusu maombi ya washikadau wa serikali ya kukagua maudhui chini ya sera ya "Taarifa isiyofaa kuhusu afya ya umma wakati wa dharura za afya ya umma”.
Kufadhili utafiti huru na kuhimiza uelewa wa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19. Bodi ilisikia kutoka kwa wataalamu kwamba juhudi pana zaidi za kuelewa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, na ufaafu wa mwitikio wa Meta kwa jambo hilo, zinahujumiwa na ukosefu wa uwezo wa kufikia data na utafiti wa kampuni hiyo. Ukosefu wa data pia umeweka changamoto kwa Bodi inapotathmini ufaafu wa ombi hili la maoni ya ushauri wa sera. Bodi inatambua kwamba kwa kulinganishwa na kampuni nyingine za mitandao ya kijamii, Meta imechukua hatua kubwa kushiriki data na watafiti wa nje, ambao wengi wao waliiambia Bodi kuhusu umuhimu wa zana za Meta kama vile CrowdTangle, na Facebook Open Research na Transparency (FORT). Wakati huohuo, watafiti pia wamelalamikia ugumu wa kufikia zana kama vile FORT. Meta inapaswa kuendelea kufanya zana hizi ziweze kupatikana, huku pia ikiboresha ufikiaji wao na kuruhusu watafiti wa nje kufikia data ambayo haipo hadharani. Bodi pia inapendekeza kwamba kampuni hiyo ifanye utafiti na kuchapisha data kuhusu juhudi zake za kutekeleza sera zake za COVID-19, na kwamba ichapishe matokeo ya utafiti wake kuhusu “lebo za wastani” ambayo ilishiriki na Bodi. Hatimaye, inapendekeza kwamba Meta ichukue hatua za kupanua ufikiaji wa data ya kampuni hadi kwa Global Majority, almaarufu Global South, watafiti na vyuo vikuu, na kwamba iwezeshe mipango ya masomo ya kidijitali kote ulimwenguni.
Iongeze usawa, uwazi na uthabiti katika kuondolewa kwa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19. Ili kutimiza majukumu yake ya kulinda haki za binadamu, ni sharti Meta pia ihakikishe kwamba kanuni zake ni wazi kwa watumiaji. Ili kufikia hili, kampuni hiyo inapaswa kueleza jinsi kila kategoria kuhusu madai ya COVID-19 ambayo huwa inaondoa huchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea. Inapaswa pia kueleza msingi wa tathmini yake kwamba dai fulani ni uongo na kuunda rekodi ya mabadiliko yoyote kwenye orodha ya madai ambayo huwa inaondoa. Ili kuwezesha matumizi sawa ya kanuni zake kwenye lugha na maeneo yote, kampuni hii inapaswa kutafsiri mwongozo wake wa kindani kwa wakaguzi wa maudhui kwa lugha inazotumia. Meta pia inapaswa kulinda haki ya watumiaji ya kupata suluhu kwa kupanua uwezo wa watumiaji wa kukata rufaa dhidi ya lebo za ukaguzi wa ukweli, na kwa kuhakikisha kwamba rufaa kama hizo hazikaguliwi na wakaguzi wa ukweli waliofanya uamuzi wa kwanza.
II. Ombi kutoka Meta
1. Ombi hili la maoni ya ushauri wa sera linahusu sera ya Meta ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, kama ilivyoainishwa katika sera ya kampuni ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura ya afya ya umma.. Sera hii ni sehemu ya Kiwango cha Jumuiya kuhusu Taarifa isiyofaa. Meta ilitumia Bodi ombi la maoni haya ya ushauri wa sera mnamo Julai 2022, ikiuliza Bodi ikiwa inapaswa kuendelea kuondoa maudhui fulani kuhusu COVID-19 chini ya sera hii au kama mbinu isiyo na vikwazo vingi sana italingana vyema na maadili ya kampuni na wajibu wa haki za binadamu.
2. Meta ilieleza katika ombi lake kwamba chini ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa sera ya dharura ya afya ya umma, inaondoa taarifa isiyofaa ambapo “ina uwezekano wa kuchangia moja kwa moja hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea” wakati wa dharura ya afya ya umma. Sera hii imefafanuliwa kwa kina zaidi katika Sehemu ya III, hapa chini. Katika kubainisha iwapo taarifa isiyofaa inakidhi kiwango hiki, kampuni hushirikiana na mamlaka ya afya ya umma kwa ujuzi na utaalam ili kutathmini uongo wa madai mahususi na iwapo yana uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea. Tathmini hii hufanywa katika kiwango cha kimataifa. Meta ilieleza Bodi kwa uwazi kwamba mbinu iliyopimwa na iliyojanibishwa ya kutekeleza sera haiwezekani bila kuhujumu pakubwa uwazi na usawa kwa watumiaji na kuongeza makosa kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza sera. Kwa taarifa isiyofaa ambayo haifikii kigezo hiki cha juu, Meta hutumia hatua zingine kama vile kushusha, kuweka lebo au kufanya ukaguzi wa ukweli.
3. Katika kuendeleza mbinu yake ya kukabiliana na taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 kuanzia Januari 2020 hadi Februari 2021 (tazama Sehemu ya III, hapa chini), Meta ilishauriana na wataalam zaidi ya 180 kutoka fani mbalimbali, wakiwemo wataalam wa afya ya umma na magonjwa ya kuambukiza, wataalam wa usalama wa taifa na usalama wa umma, - na watafiti wa taarifa isiyofaa, wakaguzi wa ukweli, na wataalam wa uhuru wa kujieleza na haki za kidijitali. Meta pia ilishauriana na washikadau wa kikanda. Meta ilibainisha kuwa kuna mapendekezo na mitazamo tofauti na wakati mwingine inayokinzana kutoka kwa wataalam kutoka fani mbalimbali na washikadau kutoka kanda mbalimbali za dunia, kama ilivyoelezwa zaidi hapa chini. Meta ilisema kuwa katika kupitisha sera ya sasa, iliamua kwamba hatari zinazohusiana na taarifa fulani isiyofaa ni muhimu vya kutosha kufanya uondoaji kuwa muhimu kutokana na dharura ya afya ya umma ya kimataifa iliyoundwa na janga la COVID-19. Katika ombi lake kwa Bodi, Meta ilieleza kuwa muktadha unaohusu COVID-19 umebadilika tangu Meta ilipoamua kuondoa baadhi ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 zaidi ya miaka miwili iliyopita. Mabadiliko hayo yameifanya kampuni kuzingatia ikiwa kuondoa taarifa hizo zisizofaa bado ni muhimu. Meta ilibaini mabadiliko matatu ili yaweze kuzingatiwa na bodi.
4. Kwanza, kulingana na Meta, kuna mabadiliko katika mfumo wa ikolojia wa maelezo kuhusu COVID-19. Mwanzoni mwa janga hili, ukosefu wa mwongozo wenye mamlaka ulisababisha kuwa ukosefu wa taarifa ambao ulihimiza kuenea kwa taarifa isiyofaa. Leo, kampuni hiyo ilibainisha, mengi yamebadilika. Watu wanaweza kupata taarifa za kuaminika kuhusu virusi na mamlaka za afya ya umma ambazo zinaweza kuwafahamisha na kuathiri tabia za wale walio katika hatari.
5. Pili, Meta ilibaini kuwa kwa sababu ya chanjo na mabadiliko ya aina tofauti za magonjwa, COVID-19 haina hatari sana kuliko ilivyokuwa mapema 2020. Kwa maendeleo na usambazaji wa chanjo zinazofaa, sasa kuna njia ya kuzuia na kupunguza ukali wa dalili za COVID-19. Zaidi ya hayo, kulingana na wataalam wa afya ya umma, aina za sasa husababisha ugonjwa mbaya zaidi kuliko aina za awali, na matibabu yanaendelea kubadilika haraka.
6. Tatu, Meta ilisema kuwa mamlaka ya afya ya umma yanatathmini kikamilfu ikiwa COVID-19 imebadilika na kuwa hali isiyo kali sana na “mamlaka zingine za afya ya umma zinabaini kuwa baadhi ya maeneo duniani yameanza kubadilika hadi hali isiyo kali ya janga hilo.” (Ombi la maoni ya ushauri wa sera ya Meta, ukurasa wa 14) Meta ilitaja taarifa zilizotolewa na Dk. Anthony Fauci nchini Marekani, Tume ya Ulaya, na Waziri wa Afya ya Umma wa Thailand, za kuunga mkono uchunguzi huu.
7. Hata hivyo, Meta alikiri kwamba mwendo wa janga hilo umekuwa tofauti ulimwenguni kote. Katika ombi lake kwa Bodi, kampuni iliandika:
Ingawa chanjo, matibabu, na mwongozo wa kimamlaka unazidi kupatikana katika nchi zenye mapato ya juu, wataalam wanatabiri kwamba ufikiaji utachelewa kwa watu katika nchi zenye mapato ya chini zilizo na mifumo duni ya huduma za afya. Tofauti kubwa zaidi hivi sasa ni kati ya mataifa yaliyoendelea, (…) na mataifa yenye maendeleo duni. (…) Asilimia themanini ya watu katika nchi zenye mapato ya juu wamepokea angalau dozi moja ya chanjo hiyo, kinyume na asilimia 13 tu ya watu katika nchi zenye mapato ya chini. Nchi zenye mapato ya chini pia zina uwezekano mkubwa wa kuwa na mifumo ya huduma za afya yenye uwezo mdogo, uchumi duni, na imani ndogo katika mwongozo wa serikali, yote mambo haya yataongeza changamoto katika kutoa chanjo kwa watu na kuwatibu wale walioambukizwa COVID-19.
(Ombi la maoni ya ushauri wa sera ya Meta, ukurasa wa 3)
Maswali ya Meta kwa Bodi
8. Kwa kuzingatia yaliyo hapa juu, Meta iliwasilisha chaguo zifuatazo za sera kwa Bodi ili kuzingatiwa: Sehemu ya III, hapa chini, inatoa maelezo zaidi kuhusu hatua hizi:
- Kuendelea kuondoa taarifa fulani isiyofaa kuhusu COVID-19: Chaguo hili linamaanisha kuendelea na mbinu ya sasa ya Meta ya kuondoa maudhui ya uongo ambayo ‘yanaweza kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea katika dharura ya afya ya umma. Meta inasema kuwa chini ya chaguo hili, kampuni hiyo hatimaye itaacha kuondoa taarifa isiyofaa ikiwa haileti hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea na inaomba mwongozo wa Bodi kuhusu jinsi kampuni inapaswa kubaini hili.
- Hatua za upunguzaji wa dharura kwa muda: Chini ya chaguo hili, Meta inaweza kuacha kuondoa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 na badala yake kupunguza usambazaji wake. Hii inaweza kuwa hatua ya muda, na kampuni hiyo inaomba mwongozo wa Bodi kuhusiana na ni wakati gani inafaa kuacha kuitumia iwapo itatekelezwa.
- Ukaguzi wa ukweli na wahusika wengine: Chini ya chaguo hili, maudhui ambayo kwa sasa yanafaa kuondolewa yangetumwa kwa wahusika wengine wakaguzi huru wa ukweli kwa ajili ya kufanyiwa tathmini. Katika ombi lake kwa Bodi, Meta inasema kwamba “idadi ya wakaguzi wa ukweli wanaopatikana kukadiria maudhui itakuwa na kipimo kila wakati. Ikiwa Meta ingetekeleza chaguo hili, wakaguzi wa ukweli hawangeweza kuangalia maudhui yote ya COVID-19 kwenye majukwaa yetu, na baadhi ya maudhui hayo hayangekaguliwa kwa usahihi, kushushwa na kualamisha.” (Ombi la maoni ya ushauri wa sera ya Meta, ukurasa wa 16)
- Lebo: Chini ya chaguo hili, Meta ingeweka lebo kwenye maudhui ambazo zingezuia watumiaji kuona maudhui lakini yangetoa viungo vya moja kwa moja vya kufikia taarifa halali. Meta inazingatia hii kama hatua ya muda na inataka kupata mwongozo wa Bodi kuhusu vigezo ambavyo kampuni hiyo inafaa kuzingatia katika kuamua kuacha kutumia lebo hizi.
9. Meta ilisema kwamba kila mojawapo ya chaguo hizi ina manufaa na mapungufu yake, hususan kuhusiana na uwezo wa kufanywa kwa kiwango, usahihi na kuhusiana na idadi ya maudhui yanayoathirika. Kampuni hiyo ilisisitiza sana kwamba sera hiyo inapaswa kuwa mwafaka kwa eneo zote, huku ikiwa thabiti na inayoweza kutekelezeka kimataifa. Kuhusiana na sera mahususi za nchi, Meta ilisema kwamba: “Kwa sababu za kiufundi, tunapendekeza kwa dhati kudumisha sera za kimataifa kuhusu COVID-19, tofauti na sera za nchi au eneo mahususi. Katika ombi lake kwa Bodi, Meta ilisema: “Utekelezaji wa sera katika kiwango cha nchi unaweza kusababisha utekelezwaji kupita kiasi wakati kundi moja la wakaguzi wa soko linashughulikia nchi nyingi, na utekelezwaji kwa kiwango cha chini kwa sababu maudhui yanaweza kuenea katika nchi na maeneo.” (Ombi la maoni ya ushauri wa sera ya Meta, ukurasa wa 17, kijachini 37.) (Kwa maelezo zaidi kuhusu utekelezwaji uliopimwa na uliojanibishwa, tazama aya ya 61 hapa chini.)
III. Sera ya Meta inayohusu Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya umma
10. Kwa kuchochewa na janga la COVID-19 na kuongezeka kwa taarifa isiyofaa iliyoonekana kwenye majukwaa yake, Meta ilianza kuondoa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 mnamo Januari 2020. Sera yake, na aina ya madai ambayo yanaweza kuondolewa, yalibadilika katika muda wa miaka miwili iliyofuata na kufikia katika sehemu ya sasa ya Taarifa Isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya katika Kiwango cha Jumuiya kuhusu Taarifa Isiyofaa na ukurasa ulioambatishwa wa Kituo cha Msaada.
11. Kiwango cha Jumuiya kuhusu Taarifa Isiyofaa kinaanza na mantiki ya sera inayofafanua mbinu ya Meta ya taarifa isiyofaa, ikiwemo uondoaji, ukaguzi wa ukweli, ushushaji na lebo kama hatua za utekelezaji. Kulingana na kampuni, huondoa tu taarifa isiyofaa pale ambapo “ina uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea. Kisha sera inabainisha aina nne za taarifa isiyofaa inayoweza kuondolewa: (1) madhara ya kimwili au vurugu (2) Taarifa isiyofaa yenye Madhara Inayohusu Afya; (3) kuingiliwa kwa wapiga kura au sensa; na (4) midia iliyobadilishwa (msisitizo umeongezwa).
12. Sehemu ya Taarifa isiyofaa yenye Madhara Inayohusu Afya katika Kiwango cha Jumuiya kuhusu Taarifa Isiyofaa ina kategoria ndogo tatu: (i) taarifa isiyofaa kuhusu chanjo; (ii) taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya umma; na (iii) kutangaza au kutetea dawa za miujiza zenye madhara kwa maswala ya kiafya (msisitizo umeongezwa). Ingawa viwango vingine vya jumuiya vinaweza kutumika kwa madai ya COVID-19, maoni haya ya ushauri wa sera yanalenga kikamilifu sehemu ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura ya afya ya umma katika sera ya Taarifa isiyofaa, kwa kuwa yanatumika kwa janga la COVID-19. Haipaswi kusomwa kuzungumzia sera zingine.
Kuondolewa kwa madai ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19
13. Sera inayohusu Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya ummainasema:
Tunaondoa taarifa isiyofaa nyakati za dharura za afya ya umma wakati mamlaka za afya ya umma zimehitimisha kwamba taarifa hiyo ni ya uongo na ina uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea, ikijumuisha kwa kuchangia kwa hatari ya watu binafsi kupata au kueneza ugonjwa hatari au kukataa chanjo husiani. Tunatambua dharura za afya ya umma kwa ushirikiano na mamlaka za kimataifa na ndani za afya. Hii kwa sasa inajumuisha madai ya uongo inayohusiana na COVID-19 ambayo yamethibitishwa na mamlaka za wataalamu wa afya, kuhusu kuwepo au kina cha virusi, jinsi ya kutibu au kuvizuia, jinsi virusi hivyo husambazwa au ni nani aliye na kingamwili, na madai ya uongo yasiyohimiza mazoea mema ya afya yanayohusiana na COVID-19 (kama vile kupimwa, kukaa mbali na wengine, kuvaa barakoa ya uso na kupata chanjo ya COVID-19). Bofya hapa kwa seti kamili ya kanuni kuhusiana na taarifa isiyofaa ambayo haturuhusu kuhusiana na COVID-19 na chanjo.
14. Chini ya sera hii, Meta huondoa taarifa isiyofaa wakati vipengele vitatu vinaporidhika: 1) kuna dharura la afya ya umma; 2) dai hilo ni la uongo; na 3) dai hilo lina uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea. Ikitumia kiwango hiki kwa janga la COVID-19, Meta ilitegemea hitimisho la mamlaka ya afya ya umma kubaini madai 80 ambayo yanaweza kuondolewa. Madai haya, ambayo husasishwa mara kwa mara, na maswali ya kawaida kuhusu jinsi sera inatekelezwa, yanapatikana kupitia ukurasa huu wa Kituo cha Msaada.
15. Kama ilivyoelezwa katika sera, madai haya 80 yamewekwa katika kategoria tano zifuatazo: (1) madai kuhusu kuwepo au ukali wa COVID-19, hii inajumuisha madai ambayo yanakana kuwepo kwa COVID-19 au kudhoofisha ukali wake, kwa mfano madai kwamba hakuna mtu ambaye alifariki kutokana na COVID-19; (2) maambukizi na kinga ya COVID-19, ambayo inajumuisha madai kwamba COVID-19 inaambukizwa na teknolojia za 5G; (3) matibabu ya uhakika au mbinu za kuzuia COVID-19, kama vile zile zinazothibitisha kwamba krimu za kupaka zinaweza kuponya au kuzuia maambukizi ya virusi vya korona; (4) kukatisha mazoea bora ya afya, kwa mfano madai kwamba barakoa za uso zina minyoo hatari ya nano au kwamba chanjo za COVID-19 hubadilisha DNA ya watu au kusababisha usumaku; (5) upatikanaji wa huduma muhimu za afya, ambazo zinajumuisha madai kwamba hospitali zinaua wagonjwa ili kupata pesa nyingi, au ili kuuza viungo vya watu.
16. Meta ilieleza katika ombi lake kwamba inategemea yafuatayo kutathmini ikiwa kuna dharura ya afya ya umma: (1) ikiwa Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza dharura ya afya ya umma; (2) iwapo WHO iliteua ugonjwa kuwa wa kuambukiza, unaweza kuuwa au hatari kubwa; au (3) katika tukio ambalo tathmini ya hatari ya WHO haipatikani, Meta hukubali uteuzi wa mamlaka ya afya kuhusu dharura ya afya ya umma kwa nchi fulani Kama Meta ilivyoeleza, WHO iliishauri kampuni hiyo kwamba, wakati wa dharura iliyotangazwa, “kuna hatari kubwa ya madhara ya kimwili yasiyoweza kurekebishwa kwa watu binafsi wakati hatari ya kuambukizwa kiwango cha maambukizi, uhusiano kati ya kuambukizwa na hatari, na viwango vya maradhi na vifo vinapokuwa juu isivyo kawaida.” (Ombi la Meta la maoni ya ushauri wa sera, ukurasa wa 6) WHOilitangaza mlipuko wa COVID-19 kuwa “Hoja ya Kimataifa kuhusu Dharura ya Afya ya Umma” mnamo Januari 30, 2020.
17. Kulingana na sera yake, katika muktadha wa dharura za afya ya umma, Meta hutegemea wataalam wa mamlaka ya afya ya umma kubainisha uongo, na kama dai la uongo “lina uwezekano wa kuchangia moja kwa moja hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea”. Meta ilifahamisha Bodi kwamba inategemea wataalam wa afya ya umma, kama vile WHO na Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), katika kutathmini madai ambayo kwa sasa yanaweza kuondolewa. Hapo awali, Meta pia imeshauriana na, kwa mfano, wakuu wa nchi wa UNICEF na Wizara ya Afya ya Kitaifa ya Pakistani (ombi la Meta la maoni ya ushauri wa sera, ukurasa wa 6). Kulingana na sampuli za mawasiliano kati ya Meta na mamlaka ya afya ya umma ambayo Bodi imekagua, Meta inabainisha madai, kwa sehemu, kupitia ufuatiliaji wa majukwaa yake na kuyawasilisha kwa mashirika ya afya ya umma ili yatathminiwe, badala ya mamlaka ya afya ya umma kutambua au kufafanua madai yanayopaswa kuondolewa. Katika mfano wa mawasiliano na mamlaka moja ya afya ya umma inayotoa tathmini hii, Meta ilibainisha dai (kwamba chanjo za COVID-19 husababisha mshtuko wa moyo) na ikauliza mamlaka ya afya ya umma ikiwa ni ya uongo na kama inaweza kusababisha chanjo kukataliwa. Mamlaka ya afya ya umma ilijibu ikitumia vyanzo na uchambuzi ili kuunga mkono hitimisho kwamba “hakuna ushahidi kwamba chanjo za COVID-19 husababisha mshtuko wa moyo.” Ilibainisha visa vilivyoripotiwa vya myocarditis (kuvimba kwa misuli ya moyo) baada ya chanjo, haswa kwa vijana wazima na vijana wadogo. Mamlaka ya afya ya umma pia ilihitimisha kwamba “hofu isiyo na msingi kuhusu chanjo zinazosababisha mshtuko wa moyo (myocardial infarction) au hali zingine za moyo zinaweza kusababisha chanjo kukataliwa.”
18. Sera ya taarifa isiyofaa ya Meta inajumuisha vighairi, ambapo kampuni huruhusu aina fulani za matamshi kuondolewa. Kwa mfano, taarifa zinazoangazia siasa au maamuzi ya kisiasa, kama vile “Mamlaka ya COVID hayafanyi kazi” au “kampuni za chanjo zinataka tu kupata pesa,” zinaruhusiwa. Maudhui yanayoshirikiwa yenye ucheshi na kejeli wazi kwa mfano “Damu ya Brad Pitt pekee ndiyo inayoweza kuponya COVID [emoji mbili za kucheka],” hayakiuki sera. Madai ambayo yanaeleza tajriba ya kibinafsi au uzoefu yanaruhusiwa ambapo: maudhui hayo yanashiriki uzoefu wa kibinafsi wa mtu fulani; utambulisho wa mtu unatajwa waziwazi katika chapisho; na maudhui hayatoi madai ya dhahiri au kujumuisha mwito wa kuchukua hatua. Maudhui ambayo yanakisia, yanahoji au yanayoonyesha kutokuwa na uhakika, kwa mfano, “Je, chanjo husababisha ugonjwa wa tawahudi?” pia yanaruhusiwa.
19. Meta hutegemea mfumo wake wa kawaida wa utekelezaji wa kiwango wa zana za kiotomatiki (au viainishaji), wasimamizi wa maudhui na timu za ndani za kutatua maudhui ili kuondoa madai yaliyoorodheshwa chini ya sera ya taarifa isiyofaa. Kampuni ilifahamisha Bodi kuwa imewafunza waainishaji katika lugha 19 ili kubaini uwezekano wa ukiukaji wa sera hii. Wasimamizi wa maudhui wanaotekeleza sera ya taarifa isiyofaa hupewa miongozo ya ndani, ikijumuisha mwongozo wa jinsi ya kutambua maudhui ambayo yanafaa kusalia kwenye jukwaa kama ya ucheshi, kejeli au hadithi ya kibinafsi, kama ilivyoelezwa kwenye ukurasa wa Kituo cha Msaada. Kipande cha maudhui kinapoondolewa, mtumiaji ana chaguo la “kutokubaliana na uamuzi huo.” Ukaguzi haujahakikishiwa lakini baadhi ya maamuzi hukaguliwa wakati wa kukata rufaa wakati kuna uwezo wa kufanya hivyo. Meta ilifahamisha Bodi kwamba kati ya Machi 2020 na Julai 2022, kampuni hiyo iliondoa vipande milioni 27 vya maudhui kwa ajili ya kuwa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 kwenye Facebook na Instagram. Kati ya milioni 27 zilizoondolewa, milioni 1.3 zilirejeshwa kupitia rufaa ambayo iliweza kutathminiwa.
Ukaguzi wa ukweli wa mhusika mwingine na ushushaji wa taarifa isiyofaa
20. Maudhui ambayo hayamo chini ya orodha ya madai ambayo yanaweza kuondolewa lakini yanaweza kujumuisha taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 yanaweza kufanyiwa ukaguzi wa ukweli na wahusika wengine. Teknolojia ya mafunzo ya mashine hutambua machapisho ambayo huenda yakawa na taarifa isiyofaa na kuyatuma kwa wakaguzi wengine wa ukweli. Washirika wa Meta walio na mashirika huru ya ukaguzi wa ukweli ya kukagua na kuweka lebo maudhui. Kampuni haitathmini utendaji wa mkaguzi wa ukweli. Inategemea Shirika la Kimataifa la Ukaguzi wa Ukweli (IFCN) kutathmini mashirika na kuhakikisha ubora. Mashirika ya ukaguzi wa ukweli hutathminiwa na IFCN kwa kufuata Kanuni ambazo zinajumuisha sharti la kutopendelea upande wowote na haki, uwazi wa vyanzo, uwazi kuhusu ufadhili na sera wazi na kweli ya marekebisho.
21. Maudhui yanayotumwa kwenye foleni ya ukaguzi wa ukweli yanaweza kuonekana chini ya mlisho wa watumiaji kwa muda, hasa ikiwa yanasambaa, kabla ya kukaguliwa. Meta hutumia kanuni ya uorodheshaji ili kutanguliza maudhui kwa wakaguzi wa ukweli, na maudhui yanayosambaa yanapewa kipaumbele katika foleni ya wakaguzi wa ukweli. Kujibu swali la Bodi, Meta ilifahamisha Bodi kuwa maudhui mengi katika foleni ya ukaguzi wa ukweli hayakaguliwi kamwe na wakaguzi wa ukweli. Kulingana na Meta, maudhui mengi kwenye foleni sio ya uongo, madai ambayo Meta haikutoa ushahidi wake. Kulingana na Meta, washirika wa ukaguzi wa ukweli hutanguliza madai ya uongo au uhadaaji ulio wazi ambayo hayana msingi wowote na ambayo yanafaa kwa wakati, yanaovuma na maalum. Wakaguzi wa ukweli pia wanaweza kupata maudhui ya kukagua kwa hiari yao wenyewe, nje ya foleni iliyotolewa na Meta.
22. Machapisho na matangazo kutoka kwa wanasiasa hayastahiki kufanyiwa ukaguzi wa ukweli. Meta inafafanua “wanasiasa” kama “wagombea wanaogombea nafasi ya ofisi, wasimamizi wa sasa wa ofisi—na, kwa kuongeza, wengi wa wateule wao wa baraza la mawaziri—pamoja na vyama vya kisiasa na viongozi wao.” Kulingana na Meta, sera hii ipo kwa sababu “matamshi ya kisiasa [katika demokrasia iliyokomaa yenye vyombo huria vya habari] ndiyo hotuba iliyochunguzwa zaidi [na] matamshi ya kisiasa yenye vizuizi [...] ingewaacha watu wakiwa na ufahamu mdogo kuhusu yale ambayo viongozi wao waliochaguliwa wanasema na kuwaacha wanasiasa kutowajibika kwa maneno yao.”
23. Wakaguzi wa ukweli wanaweza kukadiria maudhui kuwa ya “uongo,” “yaliyobadilishwa,” “ya uongo kiasi” au “muktadha unaokosekana.” Meta itaweka maudhui lebo ipasavyo na kutoa kiungo cha makala ya mkaguzi wa ukweli kuhusu mada hiyo. Ili kusoma makala hayo, lazima mtumiaji aondoke kwenye Facebook na aende kwenye ukurasa mwingine, matumizi ya data ya ziada inahitajika. Hii inamaanisha kutoza gharama za ziada kwa baadhi ya watumiaji, katika nchi ambako majukwaa ya Meta haijakadiriwa (kumaanisha kuwa watumiaji hawalipi data au ada nyinginezo za ufikiaji wa programu za Meta kwenye simu ya mkononi). Maudhui yaliyo na lebo ya “uongo” na “yaliyobadilishwa” hufunikwa na skrini ya onyo ambayo huficha maudhui, na kuhitaji mtumiaji kubofya ili kuyaona. Maudhui yaliyo na lebo ya “uongo kiasi” na “muktadha unaokosekana” hayafichwi. Meta aliiambia Bodi kuwa katika kipindi cha siku 90 hadi Desemba 9, 2022, kwa machapisho ambayo yaliyowekwa lebo ya “uongo” au “yaliyobadilishwa,” na yaliyofunikwa na skrini iliyoficha maudhui, asilimia 10 ya watumiaji wa Facebook na asilimia 43 ya watumiaji wa Instagram walifungua chapisho hilo ili kuona maudhui hayo. Katika kipindi hicho, Meta iliripoti machapisho ambayo yalipata lebo ya “uongo,” “yaliyobadilishwa,” “uongo kiasi” au “muktadha uliokosekana”, kwa wastani, na asilimia 3 ya watumiaji wa Facebook na asilimia 19 ya watumiaji wa Instagram walibofya kwenye “Angalia. Kwanini.” Hii humpeleka mtumiaji kwenye skrini tofauti ambayo hutoa maelezo kuhusu kwa nini maudhui yalikadiriwa na viungo vya makala ya mkaguzi wa ukweli.
24. Kipande cha maudhui kinapowekwa lebo na wakaguzi wa ukweli, Meta itakiweka chini katika milisho ya watumiaji. Nguvu ya kushushwa inayotumika kwa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 iliyo na lebo za “uongo,” “iliyobadilishwa” na “uongo kiasi” ni ya juu zaidi kuliko ile inayotumika kwa maudhui yenye lebo ya “muktadha unaokosekana.” Kulingana na Meta, athari za ushushaji ambapo kipande cha maudhui kitaonekana kwenye mlisho wa mtumiaji binafsi zitatofautiana. Maudhui ambayo mtumiaji huona yamebinafsishwa kwao kwa lengo fulani, kulingana na Meta, la kuonyesha mtumiaji maudhui ambayo kuna uwezekano mkubwa wa kuwavutia. Kushushwa kwa kipande cha maudhui kunaweza kusababisha alama zake za uorodheshaji kupunguzwa. Haimaanishi kuwa maudhui yatakuwa na idadi au asilimia maalum ya mara ambazo zimetazamwa. Uwezekano wa mtumiaji mahususi kuona kipande cha maudhui ambacho kimeshushwa itategemea jinsi alama ya uorodheshaji ilivyo kwa kipande hicho cha maudhui ikilinganishwa na vipande vingine vya maudhui kwenye mlisho wa mtumiaji. Kwa hivyo, ushushaji huathiri kipande cha maudhui kwa njia tofauti kulingana na mtumiaji na orodha ya maudhui yake. Maudhui yanaposhirikiwa katika kikundi au na mtumiaji aliye na idadi kubwa ya wafuasi, alama zake za uorodheshaji kwa wale wanaofuata na wanaojihusisha mara kwa mara na kikundi au ukurasa huo huenda zikawa za juu kuliko, au sawa na, alama za uorodheshaji wa maudhui mengine katika mlisho. Hii ina maana kuwa huenda ushashaji usiwe na athari inayokusudiwa.
25. Ambapo mkaguzi wa ukweli ataamua kuwa maudhui yaliyoundwa na ukurasa au kikundi yanakiuka sera ya kampuni ya taarifa isiyofaa, wadhibiti wa ukurasa au wasimamizi wa kikundi wanaweza kukata rufaa. Wasifu kwenye Facebook hauna chaguo la kukata rufaa kwa lebo ya ukaguzi wa ukweli. Ukiukaji wa vikundi unaweza kukatiwa rufaa kupitia programu ya Facebook kwenye IOS na Android au kwenye kivinjari cha wavuti. Ukiukaji wa ukurasa hauwezi kukatiwa rufaa kupitia kivinjari cha wavuti. Kulingana na Kituo cha Msaada cha Facebook, “kipengele hiki cha kukata rufaa ndani ya bidhaa kinapatikana tu kwa wasimamizi wa vikundi na wadhibiti wa kurasa katika baadhi ya nchi kwa sasa. Mtu mwingine yeyote bado anaweza kutuma rufaa kwa wakaguzi wa ukweli kupitia barua pepe.”
26. Katika ombi lake kwa Bodi, Meta ilieleza kwamba “idadi ya wakaguzi wa ukweli wanaopatikana kukadiria maudhui itakuwa na kipimo kila wakati. Katika kuitaka Bodi kutathmini mbinu tofauti zinazopatikana kushughulikia taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, Meta ilieleza kuwa ikiwa kampuni ingetegemea ukaguzi wa ukweli pekee, wakaguzi wa ukweli hawataweza kuangalia maudhui yote kuhusu COVID-19 kwenye majukwaa. Kwa hivyo, baadhi ya taarifa isiyofaa haitakaguliwa kwa usahihi, kushushwa na kuwekewa lebo.
Kutumia lebo
27. Meta pia inatumia aina mbili za kile inachokiita, “matibabu yaliyofahamishwa yasiyokuwa na upendeleo” (NITs): lebo za matibabu yasiyokuwa na upendeleo; na Ukweli kuhusu matibabu ya X yaliyofahamishwa, au FAXIT. Hutumika moja kwa moja na Meta na hazihusishi wakaguzi wa ukweli. FAXIT hutoa taarifa iliyobinafsishwa kuhusu maudhui yaliyoshirikiwa katika chapisho kabla ya kumwelekeza mtumiaji kwenye kituo cha taarifa. Meta ina lebo mbili za FAXIT: (1) “Chanjo za COVID-19 hupitia vipimo vingi vya usalama na ufanisi na kisha kufuatiliwa kwa karibu”; na (2) “Baadhi ya matibabu ambayo hayajaidhinishwa kuhusu COVID-19 yanaweza kusababisha madhara makubwa.” Lebo huwekwa kwenye maudhui yoyote ambayo kiainishaji hubainisha kuwa yanajadili COVID-19. Maudhui yanaweza kuwa ya kweli au ya uongo na lebo haitoi tamko lolote kuhusu maudhui haswa. NIT zote zinaelekeza watumiaji kwenye kituo cha Meta cha taarifa kuhusu COVID-19.
28. Wakati wa majadiliano kuhusu ombi hili la maoni ya ushauri wa sera, Meta ilifahamisha Bodi kwamba itapunguza NIT zake kuanzia tarehe 19 Desemba 2022. Uamuzi huo ulitokana na jaribio la kimataifa ambalo timu za Meta za Bidhaa na Uadilifu zilifanya kuhusu ufanisi wa NITs ili kudhibiti makadirio ya kipimo ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 kwenye jukwaa. Jaribio hilo lilihusisha kikundi cha udhibiti kilichoendelea kuona NIT za COVID-19 bila vizuizi vyovyote. Vikundi vitatu vya ziada vya majaribio pia vilianzishwa: kwanza, kikundi ambacho kingeweza kuona mojawapo ya kila moja ya NIT za COVID-19 baada ya kila siku tatu; pili, kikundi ambacho kingeweza kuona mojawapo ya kila moja ya NIT za COVID-19 baada ya kila siku 30; na tatu, kundi ambalo halikuona lebo hata kidogo. Kulingana na kampuni, kikundi cha pili (kikundi ambacho kingeweza kuona kila moja ya NIT kila baada ya siku 30) kilikuwa na kiwango cha juu zaidi cha wastani cha kubofya kwa taarifa zilizoidhinishwa kati ya vikundi vyote, ikiwemo kikundi cha udhibiti. Muda wa wastani uliotumika kutazama NIT pia ulikuwa wa juu zaidi kwa kikundi hiki. Zaidi ya hayo, “hakukuwa na urejeshaji muhimu wa kitakwimu” katika makadirio ya kipimo ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 kati ya kikundi cha udhibiti na vikundi vya majaribio. Kulingana na matokeo ya jaribio, Meta ilifahamisha Bodi kwamba ilikuwa imefikisha idadi ya NIT za COVID-19 ambazo watumiaji wangeweza kuona kwenye majukwaa yao kwa mojawapo ya kila aina ya lebo ya COVID-19 kila baada ya siku 30, kuanzia Desemba 19, 2022. Baada ya hapo, Meta iliarifu Bodi kwamba kampuni hiyo imeacha kutumia NIT zote za COVID-19, ili watumiaji waweze kuonyeshwa idadi iliyopunguzwa ya lebo. Hii ni kuhakikisha kwamba NIT pia zinafaa katika majanga mengine ya afya ya umma.
Adhabu
29. Meta hutumia adhabu za kiwango cha akaunti na za kikundi ambazo huathiri uenezaji wa taarifa isiyofaa. Wasifu, ukurasa au kikundi kinachochapisha maudhui ambayo yameondolewa au yenye lebo ya ‘uongo” au “yamebadilishwa” chini ya sera hii, itapata onyo na kuondolewa kwenye mapendekezo, haitaweza kuchuma fedha, na madirisha ibukizi yataanza kuonekana kwa wanaotembelea ukurasa au kikundi ili kuwafahamisha kwamba ukurasa huu umeshiriki taarifa isiyofaa, mara tu kiwango cha juu cha onyo kitakapofikiwa. Kulingana na ukurasa wa Kituo cha Msaada, kurasa, vikundi na akaunti za Instagram zinaweza pia kuondolewa “ikiwa zimeshiriki maudhui ambayo yanakiuka sera za COVID-19 na chanjo na pia zimejitolea kushiriki maelezo mengine ya kukatisha tamaa kwenye jukwaa.”
IV. Uhusiano wa nje
30. Wakati wa kuandaa maoni haya ya ushauri wa sera, Bodi ya Usimamizi ilishirikiana na washikadau na Meta kwa njia kadhaa.
Maoni ya umma
31. Bodi ya Usimamizi ilipokea maoni 181 ya umma mnamo Agosti 2022 kuhusiana na maoni haya ya ushauri wa sera. Maoni manne kati ya hayo yalitoka Marekani ya Latini na Visiwa vya Karibea, matano kutoka Asia ya Kati na Kusini, nane kutoka Pasifiki ya Asia na Oceania, 81 kutoka Ulaya na 83 kutoka Marekani na Kanada. Bodi haikupokea maoni yoyote ya umma kutoka Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini au kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
32. Masuala yaliyoangaziwa na mawasilisho yanajumuisha:
- Wasilisho kutoka Taasisi ya Utafiti ya Khazanah (PC-10703), taasisi ya utafiti wa sera nchini Malaysia, ilionyesha viwango tofauti vya upatikanaji wa taarifa za afya zinazoaminika katika nchi mbalimbali na viwango mbalimbali vya hatari kutokana na kuacha taarifa isiyofaa bila kukagua. Iwapo lazima kuwe na mbinu ya kimataifa, wasilisho linapendekeza kwamba Meta isikose kwa tahadhari na iendelee kuondoa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19. Wasilisho hilo pia lilitoa maoni kuhusu ukosefu wa ufafanuzi wazi wa “madhara ya kimwili yanayoweza kutokea” na umuhimu wa kuelewa muktadha, ufuatiliaji unaoendelea, na uwazi kuhusu utekelezaji ili kuhakikisha kuwa matumizi ya kiwango hiki yanaweza kutathminiwa ipasavyo.
- Mawasilisho ya Muungano wa Uhuru wa Raia wa Marekani (PC-10759) yaliibua wasiwasi kwamba ugumu wa kutofautisha, kwa kiwango, kati ya ukweli na uongo, na kati ya maoni, uzoefu na uthibitisho wa ukweli, inamaanisha kuwa Meta itazuia matamshi ambayo yanapaswa kuruhusiwa.
- Wasilisho kutoka kwa shirika lisilo la faida la Marekani la Asian Americans Advancing Justice (PC-10751) lilibainisha “ushutumu” wa Wamerikani wa Asia kama kuwajibika kuleta virusi Marekani.
- Wasilisho kutoka kwa Profesa Simon Wood wa Chuo Kikuu cha Edinburgh (PC-10713) lilionyesha wasiwasi kwamba wakaguzi wa ukweli hawana maarifa ya kutosha ya kiufundi ili kukagua ukweli wa karatasi na ushahidi changamano wa kisayansi.
- Mawasilisho kutoka kwa Media Matters for America (PC-10758) yaliangazia athari za mfumo wa ukaguzi wa Meta katika kudhoofisha juhudi za kushughulikia taarifa isiyofaa. Kwa sababu watu maarufu, wanasiasa, waandishi wa habari na watumiaji wengine mashuhuri walipewa “utekelezaji ulio polepole” kwa ukiukaji wa maudhui, taarifa isiyofaa iliruhusiwa kusalia kwenye jukwaa.
- Mawasilisho kadhaa yalibainisha wajibu wa Meta wa kushughulikia hatari kwa usalama wa umma kutokana na ufikiaji wake na jukumu la mifumo yake katika kusambaza taarifa isiyofaa. Hoja ziliibuliwa kuhusu utoshelevu wa lebo na ushushaji katika kushughulikia hatari ya madhara. Kwa mfano, wasilisho kutoka kwa makamu mkuu wa rais wa Center of Internet and International Studies (PC-10673) yalionyesha wasiwasi kwamba lebo hazitoshi kushughulikia taarifa isiyofaa inayosambazwa na wanasiasa na washawishi maarufu. Hii ni kwa sababu, “kuweka lebo kwenye chapisho haitoshi kwa hatari inayoweza kutokea. Kuruhusu uchapishaji wa maelezo ya uongo ambayo yanaongeza uwezekano wa kifo au ugonjwa mbaya ni kukwepa uwajibikaji.”
- Mawasilisho kadhaa yalipendekeza kutegemea lebo na ushushaji badala ya kuondoa maelezo ya taarifa isiyofaa. Wasilisho moja kutoka kwa Msaidizi wa Profesa Saiph Savage wa Northeastern University na Universidad Nacional Autónoma de México (UNAM) (PC-10519) liliangazia athari za sera ya uondoaji na adhabu husika kwa jumuiya na sauti asili, ikibainisha kuwa jumuiya asili “zimejieleza kwa njia tofauti kuhusu mazoea bora ya kutibu COVID-19 kutokana na imani zao za kidini.”
33. Ili kusoma maoni ya umma yaliyowasilishwa kuhusu maoni haya ya ushauri wa umma, tafadhali bofya hapa.
Vikao vya washikadau wa kikanda
34. Bodi ilishiriki katika mashauriano zaidi ya washikadau kupitia msururu wa vikao vya washikadau wa kikanda. Bodi, kwa ushirikiano na mashirika ya kiraia, ilifanya vikao sita na washikadau kutoka Amerika Kaskazini, Amerika ya Kusini, Afrika, Asia na Ulaya. Kupitia vikao hivi, Bodi ilizungumza na takriban watu 100 wanaowakilisha mashirika ya ukaguzi wa ukweli, mashirika na wataalam wa afya ya umma, watafiti wa taarifa isiyofaa, wataalam wa kusoma, kuandika na kuwasiliana kidijitali na watetezi wa haki za binadamu. Mazungumzo haya yalifanyika chini ya Kanuni ya Chatham House ili kuhakikisha majadiliano wazi na kulinda washiriki.
35. Mada na matatizo yafuatayo yalijitokeza kupitia mashauriano haya:
- Masuala ya kawaida katika kanda yanajumuisha: ukosefu wa data na changamoto ya kupima ukubwa wa taarifa isiyofaa katika nchi, na athari za sera zilizopo za Meta, kwa kuzingatia ukosefu wa ufikiaji wa data ya Meta na utafiti wa ndani; kiasi kikubwa cha taarifa isiyofaa kuhusu ukali wa virusi, matibabu ya nyumbani au matibabu mbadala (ikiwemo utangazaji wa dawa ya klorini), uhusiano wa hatua za janga kwa teknolojia ya 5G na taarifa isiyofaa ya kupinga chanjo; wasiwasi kwamba sera ya uondoaji inaweza kusababisha utekelezaji kupita kiasi ambao unaweza kukandamiza matamshi; hitaji la kushughulikia usanifu msingi wa Facebook unaotangaza taarifa isiyofaa; wasambazaji wakuu wa taarifa isiyofaa kuwa na nia ya kifedha na/au ya kisiasa ya kutangaza maudhui haya; Taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 sio tu kwamba inazidisha mzozo wa afya ya umma, lakini inadhoofisha imani ya watu katika taasisi, mawasiliano ya kisayansi na matibabu ya kisayansi na matibabu kama vile chanjo.
- Masuala yaliyotambuliwa na washikadau katika Marekani ya Latini yanajumuisha; ukaguzi wa ukweli unaweza kuwa na ufanisi lakini taarifa isiyofaa mara nyingi huwekwa lebo baada ya maudhui kufikia hadhira inayolengwa; hoja zilizoibuliwa kwamba ukaguzi wa ukweli hauwezi kuongezwa na kwamba kuna ufikiaji mdogo sana katika lugha zingine isipokuwa Kiingereza; unyanyasaji uliopangwa dhidi ya wanasayansi ambao wanakashifu taarifa isiyofaa; wakaguzi binafsi wa ukweli wametishwa na kunyanyaswa, wengine wamekimbia nchi au maeneo kwa kuhofia usalama wao wa kimwili; mashirika ya ukaguzi wa ukweli yameshtakiwa kwa ajili ya kukagua ukweli na yamelazimika kutetea mashitaka hayo, kwa kutumia rasilimali zao ambazo tayari zilikuwa chache; wanasiasa na watu maarufu hawako chini ya ukaguzi wa ukweli; wataalam wa afya ya umma na wahudumu wa afya hawana ujuzi au uwezo wa kukabiliana kikamilifu na kampeni za taarifa isiyofaa, hasa zile zinazoendelezwa na washawishi wenye sifa mbaya au watendaji wenye mapendeleo ya kisiasa au kiuchumi, kama vile utangazaji wa dawa mbadala zisizofaa za COVID-19.
- Masuala yaliyotambuliwa na washikadau katika Amerika Kaskazini yanajumuisha: wataalamu wa matibabu waliripoti mkazo mkubwa uliowekwa kwa watoa huduma za afya ili kushughulikia taarifa isiyofaa, inayohitaji wakati na rasilimali nyingi na hivyo kusababisha uchovu; hitaji la mbinu bora zaidi za kukata rufaa kwa watumiaji ambao wameondoa maudhui; hoja kwamba utafiti mwingi unaochunguza makadirio ya kipimo ya taarifa isiyofaa na ufanisi wa hatua mbalimbali unazingatia Marekani na Ulaya Magharibi; hoja zilizoibuliwa kuwa ukaguzi wa ukweli hauwezi kuongezwa na una ufikiaji mdogo katika lugha zisizo za Kiingereza; hitaji la adhabu ya akaunti yenye ufanisi zaidi; hoja kwamba kutofautiana katika uondoaji wa taarifa isiyofaa kunaweza kuthibitisha nadharia zilizopo za njama; matatizo ya udhibiti wa maudhui kwa umbizo la video.
- Masuala yaliyotambuliwa na washikadau katika bara la Asia yanajumuisha: taarifa isiyofaa ilienea mwanzoni mwa janga hili na imesambazwa kupitia mitandao ya kijamii na midia ya zamani; simulizi za taarifa isiyofaa katika nchi nyingi zinazolenga watu wachache au watu walio katika mazingira hatarishi, kama vile wafanyakazi wahamiaji au watu wachache wa dini, kama wasambazaji wa virusi; ukaguzi wa ukweli hauwezi kusonga kwa kasi sawa na taarifa isiyofaa na mara nyingi huja kwa kuchelewa; serikali zimetumia vitisho kutoka kwa taarifa isiyofaa kulenga mashirika ya vyombo vya habari na kuzuia sauti pinzani; makala yaliyokaguliwa ukweli hayawezi kufikiwa au ya kuvutia kama vile maudhui ambayo yana taarifa isiyofaa; uratibu mkubwa kati ya mashirika ya ukaguzu wa ukweli katika eneo hilo ungefaa kwani masimulizi sawa yanaenea kutoka nchi moja hadi nyingine; mashirika ya ukaguzi wa ukweli hayana nyenzo za kutoa nakala za ukaguzi wa ukweli katika lugha anuwai zinazozungumzwa katika nchi nyingi.
- Masuala yaliyobainishwa na washikadau barani Afrika yanajumuisha: viongozi wa kidini barani Afrika walikuwa wasambazaji mashuhuri wa taarifa isiyofaa; serikali na vyama vya upinzani vimekuwa wasambazaji mashuhuri wa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19; kutokuwa na imani na serikali na taasisi za umma kumeunda mazingira mazuri ya taarifa isiyofaa kuenea; mamlaka za afya ya umma zimekabiliwa na changamoto kubwa katika mawasiliano yao ya umma na kuna tofauti kubwa kati ya nchi kuhusu ufanisi wa mamlaka za afya ya umma na upatikanaji wa rasilimali; ukaguzi wa ukweli haupatikani katika lugha zote na hii inapunguza ufanisi wake.
- Masuala yaliyobainiswa na washikadau huko Uropa yanajumuisha: athari za taarifa isiyofaa zitatofautiana baina ya nchi na nchi, kulingana na viwango vya ujuzi wa kusoma na kuandika kidijitali, imani kwa serikali na taasisi za afya ya umma, na mazingira ya midia wazi; wengine waliibua hoja kwamba kuondolewa kwa taarifa isiyofaa kutazuia mjadala wa wazi kuhusu masuala yanayowahusu wananchi; wengine wanasema kuwa watu walio katika mazingira magumu zaidi ndio walioathiriwa zaidi na taarifa isiyofaa, kama vile watu wasio na kinga, watoto, wale walio na uwezo mdogo wa kusoma na kuandika wa kidijitali, ufikiaji mdogo wa midia mbalimbali, na watu ambao wanakosa ufikiaji wa mfumo wa afya wa kutosha; athari za kuzuia taarifa isiyofaa kwenye mchakato wa kufanya maamuzi ya watu; wengine walitaja hitaji la kuchukua hatua zinazoruhusu watu kujadili kwa uwazi hatua za afya ya umma kama vile matumizi ya barakoa za uso au kujitenga na watu; wengine walisema kwamba taarifa isiyofaa iliyoondolewa kutoka kwa jukwaa moja huhamia kwa urahisi hadi nyingine, kunahitajika kuwa na mbinu iliyoratibiwa; hitaji la kuunda njia ya kuzuia, badala ya kujibu, kwa taarifa ya uongo; haja ya kutangaza taarifa nzuri na sahihi kwenye majukwaa ya Meta.
Uhusiano wa Meta
36. Baada ya Meta kuwasilisha ombi lake la maoni haya ya ushauri wa sera, kati ya Julai na Desemba 2022, Bodi iliwasilisha maswali 50 kwa kampuni. Yalishughulikiwa na Meta ama kwa njia ya maandishi au mazungumzo katika vipindi vitatu vya maswali na majibu. Maswali arobaini yalijibiwa kikamilifu na 10 yalijibiwa kwa sehemu. Majibu hayo ya sehemu yalihusiana na maombi ya kuchanganua data kulingana na eneo na lugha, utafiti wa ndani kuhusu ufanisi wa hatua mbalimbali za utekelezaji, na jinsi kampuni ilivyopima mazingatio ya ushindani na ushauri wa kitaalamu katika kubuni sera yake. Bodi iliwasilisha maswali kuhusu: Data ya ndani au utafiti wa Meta wa makadirio ya kipimo ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 kwenye majukwaa ya Meta ulimwenguni kote na kugawanywa kulingana na nchi na lugha; mchakato na hatua zinazotumika kutekeleza sera ya uondoaji na data kuhusu idadi ya uondoaji; ripoti ya umma kuhusu data ya utekelezaji kwa kiwango cha jamii kuhusu taarifa isiyofaa; jukumu la mamlaka za afya ya umma na wataalam katika kuandaa na kutekeleza sera ya uondoaji; utafiti wowote kuhusu ufanisi na athari za uondoaji wa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19; utafiti wowote kuhusu ufanisi na athari za hatua nyingine, ikiwemo ukaguzi wa ukweli, lebo wastani na ushushaji; jukumu la mashirika ya wahusika wengine ya ukaguzi wa ukweli; adhabu zilitumika kwa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19; miongozo ya ndani inayotekeleza sera ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19; kama kampuni ilikuwa imetathmini athari za mpango wa kukagua ufanisi wa sera ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19; mchakato wa ushirikishwaji wa washikadau na wataalam walioshauriwa wakati wa uundaji wa sera hii na jinsi Meta ilivyotathmini mchango uliopokelewa; uwezekano wa kupitisha utekelezwaji wa sera kwa sehemu mbili ambapo uondoaji utatekelezwa katika baadhi ya nchi lakini sio nyingine; na hatua mbadala za ziada, ikiwemo uwekezaji katika ujuzi wa kusoma na kuandika kidijitali.
V. Mfumo wa uchanganuzi wa Bodi na tathmini ya sera Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya jamii
37. Katika ombi lake, Meta kuuliza Bodi ikiwa inapaswa kuendelea kuondoa maudhui fulani kuhusu COVID-19 chini ya sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya jamii au kama mbinu isiyo na vikwazo vingi sana italingana vyema na maadili ya kampuni na wajibu wa haki za binadamu. Ili kujibu swali hili, Bodi inachanganua ikiwa sera hiyo inalingana na maadili na ahadi za haki za binadamu za Meta, ikijumuisha ikiwa ni muhimu na sawia kwa wakati huu, au ikiwa kampuni inapaswa kutumia mbinu isiyo na vizuizi zaidi kushughulikia taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19. Mapendekezo yatokanayo na uchanganuzi huu yamebainishwa katika sehemu ya mwisho ya maoni haya ya ushauri wa sera.
38. Katika kuelezea mkakati ambao Meta ilitumia katika kuunda sera yake ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, Meta iliangazia tofauti kubwa katika tathmini ya hatari na hatua za kupunguza kati ya wataalam katika taaluma mbalimbali na washikadau katika mikoa tofauti. Bodi, katika utafiti wake na ushirikishwaji wa washikadau, pia ilisikia misimamo pinzani na inayokinzana kuhusu hatari zinazohusika katika kuacha taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 kwenye majukwaa na ufanisi wa hatua mbalimbali katika kushughulikia hatari hizo.
39. Hakuna suluhu moja iliyokubaliwa kwa tatizo la taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 na hatari inayoleta kwa haki za binadamu, maisha na afya, hasa wale wanaoweza kudhuriwa. Mtazamo wenye msingi zaidi wa kikanda unaweza kuanzisha kiungo muhimu kati ya taarifa isiyofaa na madhara ya kimwili yanayoweza kutokea. Hata hivyo, Bodi ililazimika izingatie uwakilishi wa Meta kuhusu vikwazo vya sasa vya mifumo yake iliyopo na jinsi masimulizi ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 yanavyoenea duniani kote. Wanachama wa Bodi walijibu masuala haya kwa njia tofauti na maoni haya ya ushauri wa sera yanapatanisha, kwa kadiri inavyowezekana, mitazamo mbalimbali kuhusu Bodi. Ni matokeo ya maelewano makini kuhusu hitaji ngumu la kuwajibikia mbinu tofauti za taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 kote ulimwenguni huku kukiwa na dharura ya afya ya umma, kwa kuzingatia vizuizi vya kiufundi vinavyodaiwa na Meta. Kwa hivyo, haiwezi kuwakilisha maoni ya kibinafsi ya kila Mwanachama wa Bodi.
Maadili ya Meta
40. Maadili ya Meta yameorodheshwa katika utangulizi wa Viwango vya Jumuiya ya Facebook, ambapo thamani ya “Sauti” inaelezewa kama “kubwa,” Meta imeweka kikomo cha “Sauti” katika kuhudumia maadili mengine manne, mawili kati ya hayo manne, ni muhimu hapa: “Usalama” na “Heshima” Kulinda thamani ya “Usalama,” Meta “huondoa maudhui yanayoweza kuchangia hatari ya madhara kwa usalama wa kimwili wa watu.” Thamani ya “Heshima” inasema kwamba “watu wote ni sawa kwa heshima na haki” na watumiaji wanatarajiwa “heshimu wengine na sio kuwanyanyasa au kuwadhalilisha wengine.”
41. Bodi imeona kuwa sera ya Meta ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya umma inatii maadili ya Meta ya “Sauti,” “Usalama,” na “Heshima.” Wakati wa dharura ya afya ya umma, hatari ya madhara ni kubwa, na thamani ya “Sauti” inaweza kuwa na kizuizi ili kuhudumia thamani ya “Usalama” kwa taarifa isiyofaa ya kiafya “huenda ikachangia moja kwa moja hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea.” Madhara yanayoweza kutokea kutokana na taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 yatawafikia watu walio hatarini zaidi, ikiwemo watu walio na kinga dhaifu na watu walio na hali zingine, watu wenye ulemavu, jamii masikini na wazee na wafanyakazi wa afya.
Wajibu wa Meta wa Haki za Binadamu
42. Mnamo tarehe 16, Machi 2021, Meta ilitangaza Sera yake ya Haki za Binadamu za Shirika, ambapo inaangazia kujitolea kwake kwa kuheshimu haki kulingana na Kanuni za Uongozi za UN kuhusu Biashara na Haki za Binadamu (UNGPs). UNGP, zilizoidhinishwa na Baraza la Haki za Binadamu la UN mnamo 2011, zina mfumo wa hiari wa majukumu ya haki za binadamu ya biashara za kibinafsi.
43. Kwa mujibu wa Kanuni ya 12 ya UNGPs, wajibu wa makampuni ya biashara kuheshimu haki za binadamu unarejelea haki za binadamu zinazotambulika kimataifa, zinazoeleweka, kwa kiwango cha chini, kama zile zilizorejelewa katika Mswada wa Kimataifa wa Haki za Binadamu. Hili ni pamoja na Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR) na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (ICESCR). Wajibu huu unamaanisha kwamba makampuni “yanapaswa kuepuka kukiuka haki za binadamu za wengine na yanapaswa kushughulikia athari mbaya za haki za binadamu ambazo yanahusika nayo” (Kanuni ya 11). Makampuni yanatarajiwa: “(a) Kuepuka kusababisha au kuchangia athari mbaya za haki za binadamu kupitia shughuli zao, na kushughulikia athari hizo zinapotokea; (b) Kutaka kuzuia au kupunguza athari mbaya za haki za binadamu ambazo zinahusishwa moja kwa moja na utendakazi, bidhaa au huduma zao na uhusiano wao wa kibiashara, hata kama hazijachangia athari hizo” (Kanuni ya 13).
44. Kanuni ya 17 inaeleza zaidi kwamba ili “kutambua, kuzuia, kupunguza, na kuwajibika kwa jinsi wanavyoshughulikia athari zao mbaya za haki za binadamu,” makampuni yanapaswa “kutekeleza haki za binadamu kwa uangalifu.” Utaratibu huu unapaswa kujumuisha kutathmini athari halisi na zinazoweza kutokea za haki za binadamu, kuunganisha na kuchukua hatua kulingana na matokeo, na kufuatilia majibu, na kuwasiliana jinsi athari zinavyoshughulikiwa. Jukumu la kufanya uangalizi wa haki za binadamu linaendelea, kwa kutambua kwamba hatari za haki za binadamu zinaweza kubadilika kadiri shughuli za biashara na muktadha wa uendeshaji unavyoendelea. Hatimaye, Kanuni ya 20 inabainisha kuwa makampuni ya biashara yanapaswa kufuatilia ufanisi wa majibu yao, kulingana na viashiria vya ubora na kiasi vinavyofaa, na kuzingatia maoni kutoka kwa vyanzo vya ndani na nje, ikiwemo washikadau walioathirika.
45. Uchambuzi wa Bodi katika maoni haya ya ushauri wa sera ulitokana na viwango vifuatavyo vya haki za binadamu:
- Haki ya uhuru wa kujieleza, kama ilivyolindwa chini ya Kifungu cha 19, aya ya 2 ya ICCPR. Kifungu hiki kinatoa ulinzi zaidi kwa uhuru wa kujieleza kupitia midia yoyote, na bila kujali mipaka. Haki ya uhuru wa kujieleza inahusu pia haki ya kutafuta, kupokea, na kutoa maelezo ya kila aina.
- Haki ya kuishi (Kifungu cha 6, ICCPR): kila mwanadamu ana haki ya asili ya kuishi.
- Haki ya afya (Kifungu cha 2 na 12, ICESCR): haki ya kila mtu kufurahia kiwango cha juu kinachoweza kufikiwa cha afya ya kimwili na kiakili. Kifungu cha 12(2) kinasema kwamba utambuzi wa haki hiyo unajumuisha “uundaji wa hali ambazo zingehakikisha huduma zote za matibabu na uangalizi wa matibabu wakati wa ugonjwa.” Inajumuisha “vigezo msingi vya afya,” kama vile ufikiaji wa elimu na maelezo yanayohusiana na afya na pia “ushiriki wa idadi ya watu katika kufanya maamuzi yote yanayohusiana na afya katika viwango vya jamii na kitaifa.” ( Maoni ya Jumla Nambari 14, ICESCR, aya ya 11.) Ufikivu wa maelezo unajumuisha haki ya kutafuta, kupokea na kutoa maelezo na mawazo kuhusu masuala ya afya. Kuheshimu haki ya afya inamaanisha kulinda majadiliano halali ya masuala ya afya ya umma.
- Haki ya kufurahia manufaa ya maendeleo ya kisayansi na matumizi yake (Kifungu cha 15(1)(b), ICESCR).
- Haki ya kutobaguliwa: (Kifungu cha 26, ICCPR): Kifungu cha 26 kinakataza ubaguzi na kinawahakikishia watu wote ulinzi sawa na madhubuti dhidi ya ubaguzi kwa misingi ya sifa yoyote iliyolindwa.
- Haki ya kupata suluhu mwafaka (Kifungu cha 2, ICCPR):
46. Mwandishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya uhuru wa kujieleza amesisitiza umuhimu wa haki ya uhuru wa kujieleza katika muktadha wa janga la COVID-19, akibainisha kwamba “kutangaza upatikanaji wa maelezo huimarisha uendelezaji wa afya, maisha, uhuru na utawala bora" na “kuonya dhidi ya ubaguzi wa maoni.” ( A/HRC/44/49, para. 2, 52.) Taarifa isiyofaa wakati wa dharura ya afya ya umma inaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa haki za watu kupata taarifa za kuaminika, mwongozo na rasilimali za afya, ambazo ni muhimu kwa ajili ya ulinzi wa haki ya afya na haki ya kuishi. Kama vile Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa ilivyobainisha, “uongo na propaganda huwanyima watu uhuru wa kujitegemea, uwezo wa kufikiri kwa makini, au kujiamini wenyewe na vyanzo vya habari, na haki ya kushiriki katika aina ya mjadala unaoboresha hali ya kijamii.” ( A/HRC/44/49, aya ya 60.) Mwandishi Maalum pia alibainisha jinsi “maelezo ya uongo yanavyozidishwa na algorithi na miundo ya biashara ambayo imeundwa ili kutangaza maudhui ya kuvutia ambayo huwafanya watumiaji washiriki kwenye majukwaa” na alitoa wito kwa makampuni “kujibu hoja hizi, kwenda zaidi ya kuboresha udhibiti wa maudhui hadi kukagua miundo yao ya biashara.” ( A/HRC/47/25, aya ya 16, 95.)
47. Kifungu cha 19 huruhusu haki ya uhuru wa kujieleza kuwekewa vikwazo chini ya masharti fulani na yenye vizuizi, yanayojulikana kama majaribio ya sehemu tatu wa uwazi, uhalali, na hitaji, ambayo pia inajumuisha tathmini ya uwiano. Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa maoni na kujieleza amependekeza kuwa Kifungu cha 19, aya ya 3 ya ICCPR inatoa mfumo muhimu wa kuongoza mazoea ya udhibiti wa maudhui ya majukwaa na kwamba makampuni yanapaswa kuhusisha sera zao za maudhui na kanuni za haki za binadamu ( A/HRC/38/35, aya ya 10-11, A/74/486, aya ya 58). Bodi imekiri hilo ingawa ICCPR haileti wajibu kwa Meta kama inavyofanya kwa majimbo, Meta imejitolea kuheshimu haki za binadamu kama ilivyobainishwa katika UNGP. ( A/74/486, aya ya 47- 48). Kwa hivyo, sera za kampuni zinapotofautiana na viwango vya hali ya juu, lazima Majimbo yakutane ili kuhalalisha vizuizi vya matamshi, Meta lazima itoe maelezo ya busara ya tofauti ya sera, kulingana na viwango vya haki za binadamu ambavyo wamejitolea kuheshimu (aya ya 47-48).
Uhalali (uwazi na upatikanaji wa sheria)
48. Kizuizi chochote cha uhuru wa kujieleza kinapaswa kupatikana na kwa njia wazi kabisa, katika upeo, maana, na athari, ili kutoa mwongozo kwa watumiaji na wakaguzi wa maudhui kuhusu maudhui ambayo yanaruhusiwa na yasiyoruhusiwa kwenye jukwaa. Ukosefu wa uwazi au usahihi unaweza kusababisha kutofuatana na sheria kutekelezwa kiholela. ( A/HRC/47/25, aya ya 40).
49. Katika uamuzi wake wa “ Tiba ya COVID inayodaiwa” [2020-006-FB-FBR], Bodi ilipendekeza kwamba Meta iweke Viwango wazi na vinavyoweza kufikiwa vya Jumuiya kuhusu taarifa isiyofaa kuhusu afya, kwa kuleta pamoja na kufafanua kanuni zilizopo katika mahali pamoja (ikiwemo kufafanua maneno muhimu kama vile taarifa isiyofaa). Uundaji wa kanuni hii unapaswa kuhusisha “nadharia ambazo zinaonyesha maana ya tafsiri na matumizi ya kanuni [hizi]” ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa watumiaji.” Kujibu pendekezo la Bodi, Meta iliunda Kiwango cha Jumuiya kuhusu Taarifa Isiyofaa. Pia ilichapisha makala katika Kituo chake cha Msaada ambayo hutoa orodha ya madai ambayo yanaweza kuondolewa na pia maswali ya kawaida kuhusu jinsi sera hiyo inavyotekelezwa, ikiwemo jinsi kampuni inavyoshughulikia ucheshi, kejeli na hadithi za kibinafsi chini ya sera hiyo. Bodi inaipongeza kampuni hiyo kwa kuchukua hatua hizi.
50. Madai yaliyoondolewa chini ya sera hii na mapangilio kulingana na jinsi yalivyo mapana au mahususi. Kwa mfano, madai kadhaa ambayo kwa sasa yanaweza kuondolewa yamefafanuliwa kwa ufupi na Meta (k.m. “madai kwamba maagizo kuhusu COVID-19 ya kujitenga na watu ni njia tu ya kusakinisha miundombinu ya teknolojia ya mawasiliano isiyotumia waya ya 5G”), huku mengine yameelezwa zaidi (k.m. “madai kwamba kujitenga na watu/kimwili hakusaidii kuzuia kusambaa kwa COVID-19”). Bodi haijachanganua kama kizuizi katika kila moja ya madai haya kiko wazi vya kutosha, kwa kuwa jukumu la kuhakikisha usahihi na uwazi ni la Meta kwanza. Bodi inabainisha kuwa Meta inapaswa kuwa na taarifa kuhusu madai ambayo yamesababisha matatizo ya utekelezaji wa juu au chini, ambayo inaweza kuashiria maswala muhimu yasiyo dhahiri. Zaidi ya hayo, Bodi inabainisha kuwa madai mahususi yanayoweza kuondolewa chini ya sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 yametolewa katika ukurasa wa Kituo cha Msaada. Ukurasa hauna kumbukumbu ya mabadiliko, ambayo inaweza kuruhusu watumiaji kuona wakati dai limeongezwa, kuondolewa au kuhaririwa.
51. Ili kulinganisha vyema sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura ya afya ya umma na viwango vya uhalali, Bodi hutoa mapendekezo ya 1, 2, 3, 4, na 11 yaliyofafanuliwa kwa kina katika sehemu ya VI, hapa chini.
Lengo halali
52. Vizuizi vya uhuru wa kujieleza lazima vifuate lengo halali, linalojumuisha ulinzi wa haki za wengine na afya ya umma, miongoni mwa malengo ya ziada. Kamati ya Haki za Kibinadamu imetafsiri neno “haki” kujumuisha haki za binadamu kama inavyotambuliwa katika ICCPR na kwa ujumla zaidi katika sheria za kimataifa za haki za binadamu.( Maoni ya Jumla 34 aya ya 28).
53. Sera ya Meta ya Taarifa Isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya umma inaelekezwa kwenye malengo halali ya kulinda afya ya umma wakati wa hali hatari ya kiafya, na pia kulinda haki ya watu kufikia maelezo, haki ya kuishi, haki ya afya, haki ya kufurahia manufaa ya maendeleo ya sayansi na matumizi yake, na haki ya kutobaguliwa.
Umuhimu na uwiano
Muhtasari
54. Vizuizi vyovyote vya uhuru wa kujieleza “lazima viwe muhimu ili kufikia utendakazi wao wa ulinzi; lazima viwe chombo cha ukali wa chini zaidi miongoni mwa vile vyote vinavyoweza kufikia utendakazi wao wa ulinzi; lazima vilingane na masilahi yanayopaswa kulindwa” (Maoni ya Jumla Nambari 34, aya ya 34).
55. Kwa sababu zilizofafanuliwa hapa chini, Bodi imeona kwamba sera inayoidhinisha Meta kuondoa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 “huenda ikachangia moja kwa moja hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea” wakati wa dharura ya afya ya umma ni muhimu na ina uwiano. Kwa hivyo, kimsingi, inalingana na maadili ya kampuni na majukumu yake ya haki za binadamu. Kwa kutangaza dharura ya afya ya umma, mamlaka ya afya ya umma ya Umoja wa Mataifa inathibitisha kwamba kuna tukio la ajabu, ambalo ni hatari kwa afya ya umma au maisha ya watu, kupitia ugonjwa kuenea kimataifa unaosababisha “hatari kubwa na ya moja kwa moja” (WHO Kanuni ya Kimataifa ya Afya ya 2005). Kwa kuzingatia tangazo la WHO la dharura ya afya ya umma duniani kuhusiana na COVID-19, ugonjwa ambao matokeo yake hayakuwa na uhakika, yangeweza kubadilika na yangeweza kuua, Bodi inagundua kuwa majibu ya Meta yalikuwa sawia. Bodi ya Uangalizi inaelewa kuwa chini ya hali kama hizo za dharura, taarifa fulani isiyofaa yenye madhara inayohusu afya, haswa inaposambazwa kwa kiwango kikubwa au na washawishi maarufu, inaweza kusababisha madhara makubwa ya afya ya umma na kuathiri vibaya haki za watu binafsi ndani na nje ya majukwaa ya Meta. Bodi inatambua kwamba katika kipindi muhimu cha dharura ya afya ya umma, huenda isiwezekane kufanya mashauriano madhubuti ya hapo awali na wataalam wengi kuhusu madai ya mtu binafsi ya taarifa isiyofaa. Katika kutathmini uwiano wa mbinu ya Meta, Bodi pia ilizingatia msimamo wa kampuni kwamba mbinu ya ujanibishaji ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 haikuwezekana.
56. Hata hivyo, hali ya COVID-19 inapobadilika, umuhimu na uwiano lazima ubadilike pia. Bodi inatambua kuwa athari za COVID-19 hutofautiana duniani kote. Hii inategemea uenezi wa virusi, mifumo ya afya ya nchi, na ubora wa nafasi ya kiraia ambayo inaruhusu watu kupokea na kushiriki maelezo kuhusu COVID-19, kati ya mambo mengine. Ingawa tangazo la dharura la WHO kuhusu COVID-19 bado linaendelea kutumika (na lilirejelewa mnamo Januari 2023), katika sehemu nyingi za ulimwengu, visa vya COVID-19 vimepungua na hatua za dharura zimepunguzwa kwa kiasi kikubwa. Hii inachangia ugumu wa kutekeleza mbinu ya kimataifa ambayo inakidhi jaribio la uwiano. Kama ilivyoainishwa katika pendekezo la 1 hapa chini, Meta inapaswa kuanza mchakato ulio uwazi na jumuishi ili kubaini iwapo madai yoyote kati ya 80 yanayoweza kuondolewa sio ya uongo au “yanaweza kuchangia moja kwa moja hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea.” Mchakato huo unapaswa kujumuisha utaratibu wa maoni yanayopingwa kusikilizwa na kuzingatiwa. Haya yanafaa kujumuisha maoni yanayotofautiana ndani ya jumuiya ya wanasayansi, wataalamu wa uhuru wa kujieleza, na ya wale walio na utaalamu kuhusu jinsi taarifa isiyofaa inavyosambazwa mtandaoni pamoja na athari zake. Bodi pia inatoa wito kwa Meta katika pendekezo la 4 hapa chini, kwamba ianze mchakato wa kutambua hatari za haki za binadamu ambazo zinaweza kuendelea katika baadhi ya nchi, na kujiandaa kwa mbinu iliyojanibishwa zaidi ili kupunguza hatari hizo pindi hali ya dharura ya afya ya kimataifa itakapomalizika.
Mchango wa Mshikadau
57. Washikadau katika maeneo mengi duniani kote walizungumza na Bodi kuhusu wanasiasa, viongozi wa kidini, washawishi na mamlaka za matibabu ambao waliendeleza taarifa isiyofaa, ambao wakaguzi wa ukweli, wataalam wa kisayansi, na mamlaka ya afya ya umma hawakuweza kuwafuatilia. Washikadau katika kila mkoa pia walizungumzia athari za taarifa isiyofaa za watu kugeukia matibabu mbadala au kuhusu utayari wao wa kupata chanjo. Walibainisha kuwa taarifa isiyofaa iliathiri utayari wa watu kufuata mwongozo wa afya ya umma au kuchukua hatua za kuzuia. Aina hii ya taarifa isiyofaa ilisisitizwa na washikadau kama hatua za kuzuia na kudhibiti hatari zinazokatisha tamaa, ambazo zinaathiri idadi ya watu kwa ujumla, na kuathiri vibaya vikundi vilivyo hatarini kama vile watu wasio na kinga, watu wenye ulemavu, watu walio na hali ya awali ya kiafya, wazee, maskini na jumuiya zilizotengwa. (Kwa maelezo zaidi kuhusu data ya COVID-19, angalia dashibodi ya WHO.) Tafiti madhubuti kuhusu athari za taarifa isiyofaa mtandaoni zinaonyesha ongezeko la kutozingatia mwongozo wa afya ya umma na punguzo linalowezekana ;a kukubali vipimo vya kiafya au chanjo ya siku zijazo. Bodi inazingatia madhara mengine yaliyoripotiwa ambayo yametokana na taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, ikiwemo kudhoofisha imani kwa mamlaka ya kisayansi na afya ya umma. Hili linatatiza utekelezwaji mzuri wa hatua za afya ya umma zinazohusiana na COVID-19 na kwa majanga mengine ya afya ya umma. Madhara mengine yaliyoripotiwa ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 yanajumuisha mashambulizi ya moja kwa moja, unyanyasaji na kesi za kimkakati dhidi ya mashirika ya ukaguzi wa ukweli na wakaguzi binafsi wa ukweli.
58. Wataalam pia walibaini kuwa baada ya Meta kuanza kuondoa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, idadi ya jumla ya taarifa isiyofaa kwenye jukwaa ilipunguzwa sana na wakabishana kuwa bila hatua hizo kuwepo, taarifa isiyofaa itasambaa tena na maudhui ya kupinga chanjo kwenye majukwaa ya kijamii kama Facebook yatatawala mazungumzo. Wataalamu hao walibainisha kuwa ukosefu wa uwazi na ufikiaji wa data ya Meta au utafiti wa ndani hukatisha juhudi za kupata ushahidi wazi wa ufanisi wa hatua za kushughulikia taarifa isiyofaa, ikiwemo uondoaji. Hata hivyo, washikadau kote ulimwenguni, walitoa hoja kwa Bodi hiyo kwamba maadamu kuna upotezaji mkubwa wa maisha ya binadamu na hatari ya afya ya watu wengi, lazima kampuni iendelee kuchukua hatua za haraka na kukubali kwamba lazima makosa yoyote yawe upande wa kuokoa maisha yaliyo hatarini, haswa watu wanaoweza kudhuriwa zaidi. Ingawa upatikanaji wa taarifa za kisayansi za kuaminika kuhusu COVID-19 umeboreka kwa kiasi kikubwa tangu janga hili kuanza, ufikiaji wa taarifa hizo unatofautiana kati ya nchi na jumuiya, na ukubwa wa taarifa za uongo na za kupotosha umesababisha kupata na kutathmini taarifa zilizopo za kisayansi kuwa vigumu kwa watu ulimwenguni kote na kudhoofisha manufaa ya ufikiaji. Kuhusu suala hili, kwa mfano, wasilisho kutoka Taasisi ya Utafiti ya Khazanah (PC-10703), taasisi ya utafiti wa sera nchini Malaysia, ilionyesha viwango tofauti vya upatikanaji wa taarifa za afya zinazoaminika katika nchi mbalimbali na viwango mbalimbali vya hatari kutokana na kuacha taarifa isiyofaa bila kukagua. Msimamo huo uliungwa mkono na wataalam na washikadau wengine kutoka sehemu mbalimbali za dunia, hasa kutoka nchi zenye viwango vya chini vya mapato. Iwapo lazima kuwe na mbinu ya kimataifa, uwasilishaji wa Taasisi ya Utafiti ya Khazanah inapendekeza, Meta isikose kuwa na tahadhari na kuendelea kuondoa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19.
59. Kama Meta ilivyotambulika katika ombi lake kwa Bodi, uelekeo wa janga hili utaendelea kutofautiana kote ulimwenguni. Kuna tofauti muhimu katika viwango vya chanjo, uwezo wa mfumo wa huduma za afya na rasilimali, na uaminifu katika mwongozo wenye mamlaka. Haya huchangia athari zisizo sawa za virusi kwa watu walio katika mazingira magumu zaidi katika nchi tofauti. Ingawa chanjo zimetengenezwa na zinapatikana kwa urahisi nchini Marekani na nchi nyingine duniani kote, hii haionyeshi mwelekeo wa kimataifa. Kwa maneno ya Meta: Asilimia themanini ya watu katika nchi zenye mapato ya juu wamepokea angalau dozi moja ya chanjo hiyo, kinyume na asilimia 13 tu ya watu katika nchi zenye mapato ya chini. Nchi zenye mapato ya chini pia zina uwezekano mkubwa wa kuwa na mifumo ya huduma za afya yenye uwezo mdogo, uchumi duni, na imani ndogo katika mwongozo wa serikali, yote mambo haya yataongeza changamoto katika kutoa chanjo kwa watu na kuwatibu wale walioambukizwa COVID-19.” (Ombi la maoni ya ushauri wa sera ya Meta, ukurasa wa 15, Julai 2022) Kwa kutaja kesi chache tu zinazoonyesha tofauti kubwa katika viwango vya chanjo, kufikia Februari 2023, chini ya asilimia 20 ya idadi ya watu nchini Iraki wamekamilisha mfululizo msingi, na chini ya asilimia 1 wamepata dozi ya nyongeza. Nchini Bulgaria, karibu asilimia 30 ya idadi ya watu wamekamilisha mfululizo msingi. Idadi hiyo ni asilimia 13 nchini Syria na chini ya asilimia 5 huko Papua New Guinea na Haiti. Wataalamu kadhaa walioshauriwa na Bodi walionya kuhusu hatari ya kutegemea taarifa na data ambayo inazingatia sana nchi za Magharibi kwa sera na mbinu ya kimataifa. Wataalamu hawa pia walibaini mtazamo finyu wa kijiografia wa tafiti nyingi zinazohusu taarifa isiyofaa na taarifa ya uongo.
60. Mnamo Januari 2023, WHO ilibainisha kuwa ingawa “dunia iko katika nafasi nzuri zaidi kuliko ilivyokuwa wakati wa kilele cha maambukizi ya Omicron mwaka mmoja uliopita, zaidi ya vifo 170,000 vinavyohusiana na COVID-19 vimeripotiwa ulimwenguni kote ndani ya wiki nane zilizopita” na mifumo ya afya “kwa sasa inatatizika na COVID-19 na kutunza wagonjwa walio na mafua na virusi katika mfumo wa upumuaji (RSV), uhaba wa wafanyakazi wa afya, na wafanyikazi wa afya waliochoka.” WHO pia iliangazia kwamba “COVID-19 unaendelea kusambaa sana katika nchi nyingi ambazo haziwezi kutoa [chanjo, matibabu, na uchunguzi] kwa watu wanaohitaji sana, wazee na wafanyakazi wa afya.” Kamati ya WHO ilibainisha kuwa “ chanjo kukataliwa na taarifa isiyofaa kuendelea kuenea kunaendelea kusababisha vikwazo zaidi kwa utekelezaji wa hatua muhimu za afya ya umma.”
Msisitizo wa Meta kuhusu mbinu ya kimataifa
61. Meta inakubali kwamba uelekeo wa janga hili umekuwa tofauti kote ulimwenguni, na tofauti kubwa zaidi ikiwa kati ya mataifa “zilizoendelea” na “zisizoendelea”. Katika kutafuta mwongozo wa Bodi, kampuni yote iliondoa mbinu iliyojanibishwa, ikisema kwamba kutumia hatua kama hizo za utekelezaji “zitaleta hoja kubwa za uwazi na usawa, kusababisha hali mbaya ya matumizi ya mtumiaji, na kutoweza kutekelezeka.” Kulingana na Meta, kupitisha hatua mahususi za utekelezwaji za kikanda au nchi, kwa kiwango kikubwa kungesababisha ukosefu wa uwazi kwa watumiaji kuhusu sera na adhabu zitakazotumika kwa kipande cha maudhui, ikizingatiwa jinsi watumiaji na maelezo yanavyoenea mipakani. Mbinu hii inaweza kuhitaji sera ngumu zaidi na ndefu “inayoonyesha ni wapi na chini ya hali gani madai tofauti yanaondolewa , kushushwa, au kuwa chini ya utekelezaji mwingine.” Kulingana na kampuni hiyo, kwa sasa haina uwezo wa kutumia mbinu iliyojanibishwa na kuitengeneza itahitaji rasilimali na wakati mwingi, na hivyo kufanya mbinu hii kutowezekana katika siku zijazo. Ilisema kuwa “utekelezaji wa sera katika kiwango cha nchi unaweza kusababisha utekelezwaji kupita kiasi wakati kundi moja la wakaguzi wa soko linashughulikia nchi nyingi, na utekelezwaji kwa kiwango cha chini kwa sababu maudhui yanaweza kuenea katika nchi na maeneo.” Kwa kuzingatia hili, Meta ilisema kuwa sera iliyopendekezwa inapaswa kuwa sahihi kwa mikoa yote, “huku ikiwa ni thabiti na inayoweza kutekelezeka kimataifa.”
Uchambuzi
62. Katika kufikia uamuzi wake kuhusu suala la uwiano, Bodi ilizingatia mambo mbalimbali yakiwemo: (i) madhara yanayoweza kutokea kwa haki za binadamu katika dharura inayoendelea ya afya ya umma; (ii) wjaibu wa uhuru wa kujieleza; (iii) Masharti husika ya Viwango vya Jumuiya kwamba maudhui ambayo yanaweza kuondolewa ni lazima yachukuliwe kuwa si ya kweli na ambayo yana uwezekano wa kuchangia moja kwa moja madhara ya kimwili na yanayoweza kutokea; iv) usanifu wa jukwaa ambao, kulingana na baadhi ya wataalam, unaweza kuchangia katika utangazaji wa maudhui hatari (tazama pendekezo la 10 kuhusu hitaji la kufanya Tathmini ya Athari za Haki za Kibinadamu kwenye chaguo za muundo wa jukwaa); (v) hoja kuu zilizoibuliwa kuhusu uwezo wa kufanywa kwa kiwango na ufanisi wa hatua za kudhibiti maudhui baada ya kuondolewa (kama ilivyoelezwa katika aya zifuatazo kuhusu ukaguzi wa ukweli, ushushaji na kuweka lebo); na (vi) uwakilishi wa Meta kwamba mbinu iliyopimwa na iliyojanibishwa haikuwezekana katika kutekeleza sera yake.
63. Kwa kuzingatia msisitizo wa Meta kuhusu mbinu ya kimataifa, na ingawa COVID-19 inaendelea kuteuliwa na WHO kuwa “Dharura ya Afya ya Umma ya Hoja ya Kimataifa”, Bodi haiwezi kupendekeza mabadiliko ya jinsi Meta inavyotekeleza sera yake ya kimataifa bila ukaguzi wa ziada unaofaa, na tathmini na kampuni ya athari za sera zake pamoja na zana anuwai za utekelezaji. Kupendekeza mabadiliko katika hali hizi kunaweza kuathiri kwa njia isiyo sawa wanaoweza kudhuriwa zaidi kote ulimwenguni Hii inajumuisha watu wazee, wasio na kinga, na walio na hali zilizopo za kiafya, pamoja na jamii maskini na zilizotengwa zilizo na rasilimali chache, maeneo ya kiraia dhaifu zaidi, hakuna vyanzo vingine vya taarifa zinazoaminika, na mifumo duni ya afya au ukosefu wa ufikiaji wa huduma za afya. Kama ilivyobainishwa hapa juu, Bodi inatambua kwamba wakati wa kipindi kigumu zaidi cha mgogoro wa afya ya umma, Meta ilitumia hatua za kipekee. Bodi inaelewa kuwa kampuni ilihitaji kuchukua hatua za kipekee wakati wa dharura ya afya ya umma iliyotangazwa, kama vile katika kesi hii, kwa kuondoa kategoria zote za taarifa isiyofaa kulingana na tathmini iliyotolewa na mamlaka ya afya ya umma kwa madhumuni ya kuzuia madhara yanayoweza kutokea. Bodi imegundua kuwa hatua hizo zilikuwa sawia kutokana na hali ya kipekee ya janga hili.
64. Hata hivyo, lazima hatua hizo za kipekee ziwe za muda, ziundwe madhubuti kulingana na mahitaji ya mazingira na kutambuliwa hadharani. Kadiri mazingira yanavyobadilika ndivyo uchanganuzi wa umuhimu na ulinganifu unavyobadilika. Kwa kuzingatia hali inayobadilika ya janga, lazima Meta sasa ifanye mchakato wa mashauriano madhubuti kwa haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha kuwa uondoaji wa kiotomatiki wa madai mahususi hauzuii mjadala unaohusu maswala ya mapendeleo ya umma au kusababisha ushawishi usiofaa wa kiserikali kwa usimamizi wa maudhui kwenye Meta. Mchakato wa mashauriano unapaswa kutegemea utaalamu wa kundi tofauti la washikadau, ikiwemo sauti pinzani, (kama ilivyoonyeshwa katika pendekezo la 1, hapa chini). Bodi inabainisha kuwa Kanuni ya 17 ya UNGP inasema kwamba “kutambua, kuzuia, kupunguza na kuwajibika kwa jinsi wanavyoshughulikia athari zao mbaya za haki za binadamu,” lazima makampuni ya biashara lazima yatekeleze uchunguzi unaoendelea wa haki za binadamu, ambao unajumuisha, “kutathmini athari halisi na zinazoweza kutokea za haki za binadamu, kuunganisha na kuchukua hatua kulingana na matokeo, kufuatilia majibu, na kuwasiliana jinsi athari zinashughulikiwa.” Kwa kuongezea, kama ilivyoelezwa na Kanuni ya 20 ya UNGP, kampuni inapaswa kufuatilia ufanisi wa majibu yao, “kulingana na viashiria vya ubora na kiasi vinavyofaa, na kuzingatia maoni kutoka kwa vyanzo vya ndani na nje, ikiwemo washikadau walioathirika.”
65. Kama ilivyobainishwa hapa juu, katika kufikia hitimisho lake, Bodi ilizingatia kama hatua zisizo kali za uondoaji wa maudhui zinaweza kushughulikia ukubwa wa taarifa isiyofaa na kulinda afya ya umma wakati wa dharura ya afya ya umma, na pia haki za watu ndani na nje ya jukwaa. Kwanza, ingawa kuongeza lebo za ukaguzi wa ukweli kwenye maudhui hutoa njia ya kusahihisha taarifa bila kuiondoa, washikadau kadhaa, pamoja na taarifa zilizotolewa na Meta, zinaonyesha uwezo mdogo wa zana hii kushughulikia kasi na ukubwa wa taarifa isiyofaa yenye madhara inayohusu afya inayoweza kuwa na madhara wakati wa dharura ya afya ya umma. Meta ilifahamisha Bodi kuwa wakaguzi wa ukweli hawawezi kukagua idadi kubwa ya maudhui kwenye foleni yao. Meta pia ilisema kuwa haitaweza kuongeza mpango wa ukaguzi wa ukweli, kwa kuwa mashirika haya ni ya wahusika wengine ambayo hayadhibitiwi au kumilikiwa na Meta. Zaidi ya hayo, kizuizi kilichojumuishwa katika mpango hufanya hatua hii kutokuwa na ufanisi. Meta hairuhusu wakaguzi wake wa ukweli kukagua maudhui yanayoshirikiwa na wanasiasa, ambayo yanajumuisha wagombea wanaowania nyadhifa hizo, walio na nyadhifa zao kwa sasa na waliowateua, na vyama vya siasa na viongozi wao. Kama ilivyoripotiwa na kuthibitishwa na washikadau kutoka kila eneo, watumiaji wa aina hii wamekuwa waenezaji maarufu wa taarifa isiyofaa. Uthibitishaji na wakaguzi wa ukweli huchukua muda mrefu zaidi kuliko uondoaji wa kiotomatiki kwa kiwango, ambao unaweza kuwa sababu ya kuamua wakati wa kushughulika na taarifa mbaya isiyofaa katika muktadha wa mgogoro wa afya ya umma. Hatua hii pia hurejelea mtumiaji kwa makala ambayo kwa kawaida huwa nje ya jukwaa (na kwa hivyo haiwezi kufikiwa na watu ambao hawana rasilimali za kutumia data ya ziada). Mara nyingi makala haya huwa ya kiufundi na wakati mwingine changamano, kinyume na ujumbe mfupi na wa kusisimua ambao taarifa isiyofaa huenezwa. Wasilisho kutoka kwa Profesa Simon Wood wa Chuo Kikuu cha Edinburgh (PC-10713) liliangazia wasiwasi kwamba wakaguzi wa ukweli hawana maarifa ya kutosha ya kiufundi ili kukagua ukweli wa karatasi na ushahidi changamano wa kisayansi.
66. Pili, ingawa ushushaji huathiri pale ambapo maudhui yataonekana katika mlisho wa mtumiaji, hali iliyobinafsishwa ya mlisho wa kila mtumiaji inamaanisha kuwa ni vigumu kubaini athari ya kipimo hiki kwa urijali au ufikiaji wa kipande cha maudhui. Alama ya kiwango cha kipande cha maudhui inalenga kuwaonyesha watumiaji maudhui ambayo “yanaweza kuwavutia zaidi,” na maudhui yaliyoshirikiwa katika kikundi au na ukurasa ambao mtumiaji anafuata huenda yakaorodheshwa kwa kiwango cha juu Kwa hivyo, haijulikani ikiwa ushushaji unaweza kushughulikia ipasavyo ufikiaji wa maudhui yanayoshirikiwa na watumiaji walio na wafuasi wengi au maudhui yaliyoshirikiwa katika kikundi. Ushushaji unaweza kuwa na athari ndogo zaidi kwa watumiaji wanaofuata akaunti, kurasa au vikundi vingi ambavyo hushiriki mara kwa mara taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, kutokana na orodha ya jumla ya maudhui kwenye milisho yao. Inaonekana pia kuwa kampuni haina data kuhusu watumiaji ambao wana uwezekano mdogo wa kufikia maudhui yaliyoshushwa, hata kama maudhui hayo yalishushwa kwa kiasi kikubwa. Ushushaji pekee hauambatani na onyo au adhabu Hatimaye, kwa vile watumiaji hawawezi kukata rufaa dhidi ya ushushaji wa maudhui yao, chaguo hili litaibua hoja muhimu kuhusu kuwatendea watumiaji kwa haki.
67. Tatu, kulingana na utafiti wa ndani wa kampuni, hakuna ushahidi kwamba lebo wastani zinafaa katika kuwafikia watumiaji kwa kiwango kikubwana kujulisha ujuzi au mitazamo yao. Meta hutumika NIT (au lebo wastani) kupitia mfumo wa kiotomatiki unaotambua mada ya COVID-19 kwenye chapisho. Lebo hizi hutoa kiungo cha Kituo cha Maelezo ya COVID-19, ambacho hutoa maelezo halali kuhusu COVID-19. Kulingana na Meta, utafiti wa awali wa kampuni kwenye lebo hizi ulionyesha kuwa “kadirio la mibofyo” (kiwango ambacho watumiaji wanabofya lebo ili kuona maelezo halali) hupungua kadri mtumiaji anavyoona NIT. Meta iliarifu Bodi zaidi kuwa kampuni hiyo imeacha kutumia NIT za COVID-19. Kulingana na Meta, lebo hizi hazina athari inayoweza kugunduliwa kwa uwezekano wa watumiaji kusoma, kuunda au kushiriki tena taarifa isiyofaa iliyokaguliwa ukweli au kuzuia maudhui ya chanjo. Hatimaye, kampuni iliripoti kwamba utafiti wa awali ulionyesha kuwa huenda lebo hizi zisiwe na athari kwa maarifa ya watumiaji na mitazamo ya chanjo.
68. Kwa jumla, Bodi inahitimisha kwamba, kwa kuzingatia msisitizo wa Meta kuhusu mbinu ya kimataifa ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 na tangazo linaloendelea la dharura la WHO, Meta inapaswa kuendelea kutumia sera yake ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 ambayo inaweza kuchangia moja kwa moja katika hatari ya kimwili inayoweza kutokea. Wakati huo pia, inapaswa kuanza kufanya mchakato thabiti na jumuishi wa uchunguzi wa madai yanayoondolewa sasa. Ili kulinganisha vyema sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura ya afya ya umma na viwango vya umuhimu na uwiano, Bodi hutoa mapendekezo ya 1, 4, 5, 9, 10, 12, 13, 14, 15, na 18 yaliyofafanuliwa kwa kina katika sehemu ya VI, hapa chini.
VI. Mapendekezo
Mapendekezo ya sera ya maudhui
69. Pendekezo la 1: Kwa kuzingatia tangazo la Shirika la Afya Ulimwenguni kwamba COVID-19 ni dharura ya afya ya kimataifa na msisitizo wa Meta kuhusu mbinu ya kimataifa, Meta inapaswa kuendelea na mbinu yake iliyopo ya kuondoa maudhui ya uongo kuhusu COVID-19 ambayo “yana uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea.” Wakati huohuo, inapaswa kuanza mchakato wazi na jumuishi wa tathmini thabiti na ya mara kwa mara ya kila moja ya madai 80 ambayo yanaweza kuondolewa ili kuhakikisha kuwa: (1) kila moja ya madai mahususi kuhusu COVID-19 ambayo yanaweza kuondolewa ni ya uongo na “yana uwezekano wa kuchangia moja kwa moja hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea”; na (2) Ahadi za haki za binadamu za Meta zinatekelezwa ipasavyo (k.m., kanuni za uhalali na umuhimu). Kulingana na mchakato huu wa kutathmini upya, Meta inapaswa kubainisha kama madai yoyote sio ya uongo tena au “yana uwezekano wa kuchangia moja kwa moja katika hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea.” Iwapo Meta itagundua kuwa madai yoyote si ya uongo tena au “hayana uwezekano tena wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea,” madai kama hayo hayapaswi kuondolewa tena chini ya sera hii. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta inapotangaza mchakato wa kutathmini upya na inapotangaza mabadiliko yoyote kwa madai 80 kwenye ukurasa wa Kituo cha Msaada.
70. Sehemu ndogo zilizo hapa chini zinaangazia mapendekezo ya Bodi kuhusu mbinu bora za kufanya tathmini upya ya madai ambayo yanaweza kuondolewa chini ya sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura ya afya ya umma. Kila moja ya mapendekezo madogo yatazingatiwa kama mapendekezo tofauti kutoka kwa pendekezo la 1, kumaanisha kuwa Bodi itakagua hatua za Meta ili kutekeleza mapendekezo hayo kando.
Pendekezo la 1A: Ushauri mpana wa mtaalam na washikadau
71. Lazima kampuni iweke mchakato, kwa haraka iwezekanavyo, ili kuzingatia seti pana ya mitazamo katika kutathmini ikiwa uondoaji wa kila dai kunahitajika kulingana na hali ya dharura. Wataalamu na mashirika yanayoshauriwa yanafaa kujumuisha wataalam wa afya ya umma, wataalam wa kinga, wataalam wa virusi, watafiti wa magonjwa ya kuambukiza, watafiti wa taarifa isiyofaa na taarifa ya uongo, wataalam wa sera za teknolojia, mashirika ya haki za binadamu, wakaguzi wa ukweli na wataalam wa uhuru wa kujieleza. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta inapochapisha maelezo kuhusu michakato yake ya kushauriana na kundi tofauti la wataalamu kuhusu sera yake ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya umma, pamoja na taarifa kuhusu athari za mazungumzo hayo kwenye sera yake.
72. Kama ilivyoelezwa hapa juu, Bodi inakubali kuwa kampuni ilihitaji kuchukua hatua za kipekee wakati wa dharura ya afya ya umma iliyotangazwa, katika kesi hii, kwa kuondoa kategoria zote za taarifa isiyofaa kwa msingi wa tathmini iliyotolewa na mamlaka moja ya afya ya umma. Bodi inatambua kwamba wakati wa dharura ya afya ya umma, haiwezekani kufanya mashauriano madhubuti ya hapo awali na wataalamu tofauti kuhusu madai ya mtu binafsi. Walakini, kwa haraka iwezekanavyo, lazima kundi pana la wataalam na washikadau lishauriwe kutokana na taarifa zinazoendelea kubadilika kuhusu janga na maoni mbalimbali yanayohusu mbinu bora ya kushughulikia taarifa isiyofaa inayohusiana na janga hili. Kama vile kampuni hiyo ilivyosema, ililazimika ibadilishe msimamo wake kuhusu angalau madai mawili ambayo yaliondolewa hapo awali, moja kuhusu asili ya virusi na lingine kuhusu kiwango cha vifo vya COVID-19. Ushauri mpana na uwazi zaidi kuhusu mchango huo ni muhimu kwa ajili ya kufanya maamuzi bora na kujilinda dhidi ya udhibiti usio na msingi.
73. Bodi iliuliza Meta ikiwa madai ambayo yamejumuishwa katika orodha yake ya “usichapishe” (kwa sababu yanachukuliwa kuwa ya uongo na “huenda yanachangia moja kwa moja hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea”) yametathminiwa upya ili kuzingatia athari za mabadiliko matatu yaliyoainishwa kwenye ombi la kampuni. Meta iliarifu Bodi kuwa haina taarifa za kuunga mkono hitimisho kwamba madai ya sasa yanayoondolewa sio ya uongo tena au hayana uwezekano tena wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara yanayoweza kutokea. Hata hivyo, kampuni hiyo haijarejea kwa mamlaka husika za afya ya umma ili kuziomba kutathmini upya madai hayo. Kampuni haijafanya mashauriano na washikadau au wataalam ili kutathmini upya madai ya mtu binafsi au sera ya jumla. Kulingana na Meta, kampuni ilichagua kugeukia Bodi na ombi la maoni ya ushauri wa sera, badala ya kufanya ushiriki wa washikadau wa nje katika kubadilisha sera yake, ili isicheleweshe ombi hilo. Bodi inaipongeza Meta kwa kutafuta maoni kutoka nje kuhusu sera iliyoundwa wakati wa dharura ya kimataifa, na kwa kutambua hitaji la kutathminiwa upya. Walakini, jukumu la kampuni la kuheshimu haki za binadamu halikomei hapo. Kuweka mchakato wa kutathmini kama uondoaji unaoendelea kwa kila dai ni muhimu kungehakikisha kwamba kampuni inatekeleza ukaguzi unaofaa, kama ilivyo kwa UNGP.
Pendekezo la 1B: Muda wa ukaguzi
74. Meta inapaswa kubainisha muda wa ukaguzi huu (k.m., kila baada ya miezi mitatu au sita) na ifanye hili hadharani ili kuhakikisha ilani na mchango unatolewa. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta inapochapisha kumbukumbu za mkutano wake wa ukaguzi hadharani, kwa mtindo sawa na uchapishaji wake wa kumbukumbu za mijadala yake ya sera za umma katika Kituo chake cha Uwazi.
Pendekezo la 1C: Taratibu za kukusanya maoni ya umma
75. Meta inapaswa kueleza mchakato wazi wa ukaguzi wa mara kwa mara, ikijumuisha njia za watu binafsi na mashirika yanayovutiwa kupinga tathmini ya dai mahususi (k.m., kwa kutoa kiungo kwenye ukurasa wa Kituo cha Msaada kwa maoni ya umma, na mashauriano ya mtandaoni). Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta inapounda utaratibu wa maoni ya umma na kushiriki maelezo kuhusu athari ya maoni hayo kwenye michakato yake ya ndani na Bodi.
Pendekezo la 1D: Mwongozo kuhusu aina ya taarifai inayopaswa kuzingatiwa na kutathminiwa
76. Ukaguzi wa Meta kuhusu madai unapaswa kujumuisha utafiti wa hivi punde zaidi kuhusu uenezi na athari za taarifa hiyo isiyofaa ya afya mtandaoni. Hii inapaswa kujumuisha utafiti wa ndani kuhusu ufanisi wa kiasi wa hatua mbalimbali zinazopatikana kwa Meta, ikiwa ni pamoja na uondoaji, ukaguzi wa ukweli, ushushaji na lebo wastani. Kampuni inapaswa kuzingatia hali ya janga hili katika mikoa yote ambayo inafanya kazi, haswa zile ambazo majukwaa yake yana chanzo kikuu cha taarifa na ambapo kuna jumuiya ndogo za watu wanaojua kusoma na kuandika kidijitali, nafasi duni za kiraia, ukosefu wa vyanzo vya taarifa za kuaminika, na mifumo dhaifu afya. Meta pia inapaswa kutathmini ufanisi wa utekelezaji wake wa madai haya. Meta inapaswa kukusanya, ikiwa tayari haina, taarifa kuhusu madai ambayo yamesababisha matatizo ya utekelezaji wa juu au chini. Taarifa hii inapaswa kujulisha ikiwa dai linapaswa kuendelea kuondolewa au linapaswa kushughulikiwa kupitia hatua zingine. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limekelezwa Meta inaposhiriki data kuhusu ukaguzi wake wa utekelezaji wa sera na kuchapisha maelezo haya hadharani.
Pendekezo la 1E: Mwongozo wa kutoa uwazi kuhusu kufanya maamuzi
77. Ili kutoa uwazi kuhusu aina za wataalamu walioshauriwa, mchango wao, utafiti wa ndani na nje unaozingatiwa na jinsi taarifa hizo zilivyoathiri matokeo ya uchanganuzi, Meta inapaswa kuipa Bodi muhtasari wa msingi wa uamuzi wake kwa kila dai. Muhtasari huo unapaswa kujumuisha hasa msingi wa uamuzi wa kampuni wa kuendelea kuondoa dai. Meta inapaswa pia kufichua jukumu ambalo, ikiwa lipo, wafanyikazi wa serikali au taasisi walikuwa nalo katika kufanya maamuzi yake. Iwapo kampuni itaamua kuacha kuondoa dai fulani, kampuni inapaswa kueleza msingi wa uamuzi huo (ikiwemo: (a) mchango ambao ulisababisha kampuni kubaini kwamba dai hilo sio la uongo tena; (b) mchango ambao, ikiwemo chanzo chake, uliosababisha kampuni kubaini dai hilo halichangii tena moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea, na kama tathmini hiyo inatumika katika nchi zilizo na viwango vya chini zaidi vya chanjo na miundombinu duni ya afya ya umma; (c) ikiwa kampuni iliamua kwamba mfumo wake wa utekelezaji ulisababisha utekelezwaji wa madai mahususi kupita kiasi; (d) ikiwa kampuni ilibaini kwamba dai halienei tena kwenye jukwaa.) Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta inaposhiriki tathmini ya mchakato wake wa tathmini ya sera. Taarifa hii inafaa kulingana na sababu zilizoorodheshwa hadharani katika chapisho la Kituo cha Msaada kwa ajili ya mabadiliko yoyote yaliyofanywa kwa sera, kama ilivyobainishwa katika aya ya kwanza ya pendekezo hili.
78. Pendekezo la 2:Meta inapaswa kutoa ufafanuzi wazi wa sababu kila aina ya madai yanayoweza kuondolewa “huenda yakachangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea.” Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa wakati Meta itarekebisha ukurasa wa Kituo cha Msaada ili kutoa ufafanuzi huu.
79. Kwa sasa, ukurasa wa Kituo cha Msaada unatoa mfano wa kiungo kati ya dai mahususi na kwa nini na jinsi linachangia kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea kwa “kuongeza uwezekano wa kuambukizwa au kueneza virusi, au kuwa na athari mbaya kwenye uwezo wa mfumo wa afya ya umma kukabiliana na janga hilo.” Ukurasa huo kisha unabainisha aina tano za taarifa za uongo ambazo, kulingana na Meta, zinakidhi kiwango cha “uwezekano wa kuchangia kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea.” Ukurasa wa Kituo cha Msaada, hata hivyo, hauelezi kwa utaratibu jinsi kila kategoria ya madai yanayoweza kuondolewa inakidhi kiwango kilichowekwa. Meta inapaswa kueleza kwa uwazi jinsi kila aina ya madai inavyoweza kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanyoweza kutokea na vyanzo vya taarifa ambayo kampuni ilitegemea kufikia hitimisho hilo.
80. Pendekezo la 3: Meta inapaswa kufafanua sera yake ya Taarifa kuhusu afya wakati wa dharura ya afya ya umma kwa kueleza kwamba hitaji la taarifa kuwa za “uongo” inarejelea taarifa za uongo kulingana na ushahidi bora uliopo wakati sera hiyo ilipotathminiwa upya hivi majuzi zaidi. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta inapofafanua sera katika ukurasa husika wa Kituo cha Usaidizi.
81. Angalau mara mbili, Meta imelazimika kurekebisha madai yanayoweza kuondolewa wakati maelezo yanayojulikana yanabadilika, au mabadiliko ya ugonjwa yalifanya dai kuwa sio sahihi au halijakamilika. Makosa yanaweza kufanywa, data au utafiti mpya unaweza kupinga makubaliano yaliyopo, au ufafanuzi wa dai unaweza kuhitaji kurekebishwa. Kwa kuzingatia ukweli huu, na ili kuweka wazi kuwa Meta inaelewa kuwa ina wajibu wa kuendelea kutathmini upya kwamba madai mahususi yanakidhi kiwango kikubwa katika sera yake, Meta inapaswa kufafanua sera ili kuweka wazi kuwa tathmini inategemea ushahidi bora unaopatikana kwa wakati huo na inaweza kubadilika.
Mapendekezo ya utekelezwaji
82. Pendekezo la 4: Meta inapaswa kuanzisha mara moja mchakato wa tathmini ya hatari ili kutambua hatua zinazofaa na sawia ambazo inapaswa kuchukua, kulingana na uamuzi huu wa sera na mapendekezo mengine yaliyotolewa katika maoni haya ya ushauri wa sera, WHO inapoondoa dharura ya afya ya kimataifa ya COVID-19, lakini mamlaka nyingine za afya ya umma nchini zinaendelea kutaja COVID-19 kama dharura ya afya ya umma. Mchakato huu unapaswa kulenga kutumia hatua za kushughulikia taarifa isiyofaa yenye madhara yanayoweza kuchangia kwa hatari kubwa na inayoweza kutokea ya maisha halisi, bila kuathiri haki ya jumla ya uhuru wa kujieleza kote duniani. Tathmini ya hatari inapaswa kujumuisha: (1) tathmini madhubuti ya maamuzi ya muundo na njia mbadala mbalimbali za sera na utekelezaji; (2) athari zao kwa uhuru wa kujieleza, haki ya afya na maisha na haki zingine za binadamu; na (3) tathmini ya uwezekano wa mbinu ya utekelezaji iliyojanibishwa. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta itakapowasilisha hadharani mipango yake ya jinsi itakavyofanya tathmini ya hatari na kufafanua mchakato wa tathmini ya kugundua na kupunguza hatari na kusasisha ukurasa wa Kituo cha Msaada na maelezo haya.
83. Pendekezo la 5: Meta inapaswa kutafsiri miongozo ya utekelezaji wa ndani katika lugha zinazotumika kwenye majukwaa ya kampuni. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limekelezwa Meta itakapotafsiri miongozo yake ya utekelezaji wa ndani na kusasisha Bodi kuhusiana na hili.
84. Wasimamizi wa maudhui wanaweza kufikia miongozo ya kina ya utekelezaji wa ndani ambayo hutoa maelezo ya ziada kuhusu jinsi ya kutambua maudhui yanayokiuka na maudhui ambayo yanapaswa kusalia kwenye jukwaa chini ya mojawapo ya vizuizi vilivyobainishwa (k.m. ucheshi, kejeli, hadithi za kibinafsi, maoni). Ili kuhakikisha kuna utekelezaji thabiti katika sehemu mahususi za dunia, Meta inahitaji kuhakikisha kuwa miongozo hii imetolewa na inafikiwa na wasimamizi katika lugha ambayo wanatumia.
85. Hapo awali Bodi ilipendekeza kuwa Meta itafsiri mwongozo wake wa utekelezaji wa ndani unaotolewa kwa wasimamizi katika lugha ambayo wanatumia kukagua maudhui (tazama, maamuzi ya kesi ya “Kurejesha maneno ya Kiarabu,” [ 2022-003-IG-UA]; na “Boti ya Myanmar,” [ 2021-007-FB-UA]). Katika jibu lake kwa bodi, Meta ilisema kwamba [kuwa] na seti moja ya miongozo ya sera ya ndani katika lugha ambayo wakaguzi wetu wote wa maudhui wanazungumza kwa ufasaha... ndiyo njia bora ya kuhakikisha utekelezwaji sanifu wa kimataifa wa sera zetu zinazoendelea kubadilika haraka... Kwa sababu mwongozo huu unabadilika haraka (unasasishwa kila mara kwa ufafanuzi na lugha mpya ikijumuisha maneno mahususi ya kudhalilisha ya soko), kutegemea tafsiri kunaweza kusababisha ucheleweshaji usio wa kawaida na tafsiri zisizoaminika.”
86. Kwa kuwa Meta ilitoa maelezo yaliyo hapa juu, tathmini huru ya utekelezaji wa Meta wa sera zake nchini Israeli na Palestina ilibainisha ukosefu wa uwezo wa lugha ya wasimamizi wa maudhui kama mojawapo ya sababu za utekelezaji wa kupita kiasi wa sera za Meta katika Kiarabu (tazama, Biashara kwa Wajibu wa Kijamii wa “ Ukaguzi wa Haki za Binadamu Kutokana na Athari za Meta nchini Israel na Palestina mnamo Mei 2021”). Kwa kuzingatia matokeo haya, na kwa kuzingatia utata wa miongozo ya ndani na tafsiri tofauti wanayotoa kwa wasimamizi wa maudhui, Bodi inaamini kwamba hatari ya utekelezwaji wa juu au chini wa sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura ya afya ya umma ni wa kweli. Meta inapaswa kupunguza hatari hizi ili kuhakikisha kuwa matumizi ya sera yake yanalingana katika lugha na maeneo.
87. Pendekezo la 6: Rufaa za mtumiaji za lebo ya ukaguzi wa ukweli zinapaswa kukaguliwa na mkaguzi tofauti wa ukweli na yule aliyefanya tathmini ya kwanza. Ili kuhakikisha kuna haki na kukuza ufikiaji wa suluhu kwa watumiaji ambao maudhui yao yamekaguliwa ukweli, Meta inapaswa kurekebisha mchakato wake ili kuhakikisha mkaguzi tofauti wa ukweli ambaye tayari hajafanya tathmini ya dai lililotolewa, anaweza kutathmini uamuzi wa kulazimisha lebo.Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta itakapotoa utaratibu kwa watumiaji kukata rufaa kwa mkaguzi tofauti wa ukweli, na inaposasisha sera zake za ukaguzi wa ukweli kwa utaratibu huu mpya wa kukata rufaa.
88. Pendekezo la 7: Meta inapaswa kuruhusu wasifu (sio kurasa na vikundi pekee) ambao una maudhui yaliyowekwa lebo na wakaguzi wa ukweli wanaotekeleza sera ya taarifa isiyofaa ya Meta, kukata rufaa dhidi ya lebo hiyo kwa mkaguzi mwingine wa ukweli kupitia kipengele cha rufaa ya ndani ya bidhaa. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta itakapotoa kipengele cha kukata rufaa kwa wasifu katika masoko yote na kuonyesha kuwa watumiaji wanaweza kukata rufaa dhidi ya lebo za ukaguzi wa ukweli kupitia data ya utekelezaji.
89. Rufaa za watumiaji ni kipengele muhimu cha kusahihisha hitilafu na kuhakikisha haki ya mtumiaji ya kupata suluhu. Wakaguzi wa ukweli hukagua maudhui ambayo hutofautiana kwa kiasi kikubwa katika utata, maudhui ya kiufundi na muktadha. Baadhi ya hitilafu haziwezi kuepukika. Maoni moja ya umma yaliibua hoja kwamba wakaguzi wa ukweli hawana ujuzi wa kisayansi na kiufundi wa kukagua ukweli wa makala changamano za kisayansi zinazoshirikiwa kwenye jukwaa. Lebo za ukaguzi wa ukweli husababisha matokeo kwa watumiaji. Mkaguzi wa ukweli anapotumia lebo kwenye maudhui, lebo hiyo inaweza kusababisha onyo ikiwa maudhui yana lebo ya “uongo” au “yamebadilishwa.” Mkusanyiko wa maonyo utasababisha vizuizi vya vipengele na ushushaji wa maudhui yaliyoshirikiwa na wasifu huo. Utekelezaji wa pendekezo hili utawaruhusu watumiaji kuwaarifu wakaguzi wa ukweli wakati wanaamini kwamba kosa limefanywa na kushiriki maelezo ya ziada ili kuwezesha ukaguzi.
90. Pendekezo la 8: Meta inapaswa kuongeza uwekezaji wake katika mipango ya kusoma na kuandika kidijitali kote ulimwenguni, ikizipa kipaumbele nchi zilizo na viashirio vya chini vya uhuru wa midia (k.m. alama ya Freedom House ya Uhuru wa Vyombo vya Habari) na matumizi ya juu ya mitandao ya kijamii. Uwekezaji huu unapaswa kujumuisha mafunzo ya maalum ya kujua kusoma na kuandika. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta itakapochapisha makala kuhusu ongezeko la uwekezaji wake, ikibainisha kiasi kilichowekezwa, asili ya mipango na nchi zilizoathiriwa, na taarifa iliyo nayo kuhusu athari za mipango hiyo.
91. Meta ilijulisha Bodi, kwa kujibu swali, kwamba katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kampuni imewekeza zaidi ya dola milioni saba za Marekani za “kusaidia watu kuboresha ujuzi wao wa midia na kupunguza kikamilifu kiasi cha taarifa isiyofaa ambayo hushirikiwa.” Kulingana na vyanzovilivyotolewa na Meta, uwekezaji huu ulilenga zaidi Marekani. Meta imeshirikiana na mashirika katika nchi zingine ili kutoa kampeni za mitandao ya kijamii au matangazo yanayolenga ujuzi wa midia.
92. Uchunguziwa kutathminiathari za uwekezaji wa Meta katika mipango ya ujuzi wa midia nchini Marekani (mpango mmoja katika ushirikiano na PEN America na nyingine na Taasisi ya Poynter) ilipata maboresho makubwa katika uwezo wa washiriki kutathmini taarifa za mtandaoni. Kwa mfano, uwezo wa washiriki wa kugundua taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 uliboreshwa kutoka wastani wa asilimia 53 hadi 82 baada ya hatua kuchukuliwa. Mpango wa ujuzi wa kidijitali wa wazee ulisababisha maboresho ya asilimia 22 katika uwezo wa washiriki kuhukumu kwa usahihi vichwa vya habari kuwa vya kweli au sio kweli baada ya kuchukua kozi.
93. Pendekezo la 9: Kwa akaunti na mitandao moja ya mashirika ya Meta ambayo yanakiuka sera ya taarifa isiyofaa mara kwa mara, Meta inapaswa kufanya au kushiriki utafiti uliopo kuhusu madhara ya mfumo wake wa adhabu uliotangazwa hivi karibuni, ikiwemo data yoyote kuhusu jinsi mfumo huu umeundwa ili kuzuia ukiukaji huu. Utafiti huu unapaswa kujumuisha uchanganuzi wa akaunti zinazotangaza au kuratibu kampeni za taarifa isiyofaa ya afya. Tathmini inapaswa kutathmini ufanisi wa adhabu za kuacha kuchuma mapato ambazo Meta hutumia kwa sasa, katika kushughulikia motisha/manufaa ya kifedha ya kushiriki taarifa hatari na za uongo au za kupotosha. Bodi itazingatia kwamba pendekezo hili limetekelezwa Meta itakaposhiriki matokeo ya uchunguzi huu na Bodi na kuripoti muhtasari wa matokeo katika Kituo cha Uwazi.
Mapendekezo ya uwazi
94. Pendekezo la 10: Meta inapaswakuzindua tathmini ya athari kwa haki za binadamu kuhusu jinsi mlisho wa Meta, algorithi za mapendekezo na vipengele vingine vya muundo vinavyochangia pakubwa taarifa isiyofaa yenye madhara inayohusu afya na athari zake. Tathmini hii inapaswa kutoa maelezo kuhusu vipengele muhimu katika algorithi ya viwango vya mlisho ambayo huchangia katika utangazaji wa taarifa isiyofaa yenye madhara inayohusu afya, aina ya taarifa isiyofaa inayoweza kutangazwa kupitia algorithi za Meta, na vikundi ambavyo vinavyoathiriwa zaidi na aina hii ya taarifa isiyofaa (na kama vinalengwa haswa na chaguo za muundo wa Meta). Tathmini inapaswa pia kuweka hadharani utafiti wowote wa awali ambao Meta imefanya ambao unatathmini athari za algorithi zake na chaguo za muundo wa kutangaza taarifa isiyofaa kuhusu afya. Bodi itazingatia kuwa pendekezo limetekelezwa Meta inapochapisha tathmini ya athari za haki za binadamu, ambayo ina uchanganuzi kama huo.
95. Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza alielezea majibu ya majukwaa ya mitandao ya kijamii kwa taarifa isiyofaa inayohusiana na COVID-19, ikiwemo uondoaji wa Meta wa taarifa isiyofaa na mpango wa wahusika wengine kufanya ukaguzi wa ukweli kama “chanya kwa ujumla” lakini “haitoshi” kushughulikia changamoto zinazosababishwa na taarifa ya uongo. Mwandishi Maalum aliangazia hitaji la kufanya “ukaguzi wa kina wa mtindo wa biashara ambao unategemea sana vichochezi vya taarifa ya uongo na isiyofaa.” ( A/HRC/47/25, aya ya 65-67.)
96. Bodi ina wasiwasi kuwa Meta haijafanya tathmini ya athari za haki za binadamu kuhusu jinsi vipengele vya muundo wa majukwaa yake na hatua za sasa zinavyoathiri afya ya umma na haki za binadamu, kama vile haki za maisha, afya, ufikiaji wa taarifana usemi wa mawazo na maoni kuhusu janga hili na hatua zinazohusiana na afya ya umma. Meta inapaswa kuhakikisha kuwa ina ufikiaji wa taarifa zote zinazohitajika ili kutathmini ipasavyo athari zinazoweza kujitokeza katika haki za binadamu. Kwa kuzingatia tofauti katika upatikanaji wa taarifa za kutosha na zinazoweza kufikiwa, chanjo muhimu, dawa na matibabu, na ugawaji wa rasilimali za udhibiti wa maudhui duniani kote, tathmini ya athari za haki za binadamu ni muhimu ili kutathmini hatari zinazotokana na uenezi wa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 ambayo inaweza kusababisha madhara ya kimwili inayoweza kutokea katika bidhaa za Meta ulimwenguni kote.
97. Pendekezo la 11: Meta inapaswa kuongeza kumbukumbu ya mabadiliko kwenye ukurasa wa Kituo cha Msaada inayotoa orodha kamili ya madai yanayoweza kuondolewa chini ya sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati dharura ya afya ya umma.Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limekelezwa wakati kumbukumbu ya mabadiliko inapoongezwa kwenye ukurasa wa Kituo cha Msaada.
98. Viwango vya Jumuiya hutoa kumbukumbu ya mabadiliko ili kuwaonya watumiaji kuhusu mabadiliko katika sera zinazotekelezwa. Hata hivyo, ukurasa wa Kituo cha Usaidizi ambao una madai mahususi yanayoweza kuondolewa chini ya sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura ya afya ya ummahaitoi kumbukumbu ya mabadiliko au njia zozote kwa watumiaji kubaini wakati orodha ya madai imesasishwa au kurekebishwa. Kwa hivyo nyongeza ni vigumu kufuatilia nyongeza au mabadiliko yoyote kwa madai ambayo yanaweza kuondolewa.
99. Meta iliieleza Bodi kuwa kati ya Machi 2020 na Oktoba 2022, madai mbalimbali yameongezwa kwenye orodha ya madai yaliyoondolewa chini ya sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura ya afya ya jamiina madai mengine yameondolewa au kufanyiwa marekebisho.
100. Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza amesema kwamba watu wote wanapaswa kuwa na “ufikiaji halisi wa zana za mawasiliano zinazohitajika ili kujifunza kuhusu mgogoro wa afya ya umma.” ( A/HRC/44/49, aya ya 63(b)). Kuongeza kumbukumbu ya mabadiliko kwenye Kituo cha Msaada kunaweza kulingana na kanuni ya uhalali, kuwajulisha watumiaji kwa uwazi wakati madai mahususi yanaondolewa. Uwazi zaidi kuhusu jinsi orodha ya madai inavyobadilika ingefaidi watumiaji huku makubaliano ya kisayansi na ufahamu wa athari za afya ya umma kutokana na janga la COVID-19 ukiendelea.
101. Ongezeko la kumbukumbu ya mabadiliko katika Kituo cha Msaada pia kunaweza kuwasaidia watumiaji walio na maoni tofauti kupinga tathmini iliyofanywa na mamlaka ya afya ya umma kuhusu uongo au uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea, kuhusiana na pendekezo la kwanza na pili. Mbinu hii itashughulikia wajibu wa Meta wa haki za binadamu unaohusiana na afya ya umma, huku ikiwezesha sauti pinzani ili kupinga madai ambayo hawakubaliani nayo.
102. Pendekezo la 12: Meta inapaswa kutoa data ya kila robo mwaka ya utekelezaji kuhusu Taarifa isiyofaa katika Ripoti ya Utekelezaji ya Kila Robo, iliyogawanywa kulingana na aina ya taarifa isiyofaa (yaani, madhara ya kimwili au vurugu, taarifa isiyofaa yenye madhara inayohusu afya, uingiliaji wa wapiga kura au sensa, au midia iliyodanganywa) pamoja na nchi na lugha. Data hii inapaswa kujumuisha taarifa kuhusu idadi ya rufaa na idadi ya vipande vya maudhui yaliyorejeshwa Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta itakapoanza kujumuisha data ya utekelezaji kwenye sera ya Taarifa isiyofaa katika ripoti za utekelezaji za kampuni.
103. Ripoti ya Utekelezaji wa Viwango vya Jumuiya (CSER) ambayo Meta hutoa kila robo mwaka inaonyesha vipande vya maudhui ambavyo vilichukuliwa hatua chini ya Viwango mbalimbali vya Jumuiya. Hata hivyo, ripoti hii haina data yoyote ya utekelezaji kwenye sera ya kampuni ya Taarifa isiyofaa. Bodi inaelewa kuwa hii ni kwa sababu Kiwango cha Jumuiya kuhusu Taarifa isiyofaa kilianzishwa rasmi mnamo Machi 2022. Meta ilifahamisha Bodi kwamba kampuni hiyo haina data yamakadirio ya kipimo ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 kwenye majukwaa yake. Kulingana na Meta, hivyo ndivyo ilivyo kwa sababu ya ufafanuzi unaobadilika wa kile kinachojumuisha taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 na ugumu wa kupata ulinganifu wenye maana kati ya makadirio ya kipimo ya kabla na baada ya sera.
104. Meta, hata hivyo, imeweza kupima makadirio ya kipimo kwa muda wa kipindi kifupi Kulingana na kampuni hiyo, kati ya Machi 1, 2022, na Machi 21, 2022, maudhui yanayohusiana na COVID-19 yalijumuisha asilimia 1-2 ya mwonekano wa machapisho ya Facebook nchini Marekani. Miongoni mwa maoni haya, Meta inakadiria kuwa takriban asilimia 0.1 inahusika na maudhui ambayo yanakiuka sera za Taarifa isiyofaa na Madhara.
105. Bodi ilipokea maoni mengi kutoka kwa washikadau duniani kote yakiangazia kwamba ukosefu wa taarifa zinazopatikana hadharani kuhusu idadi ya vipande vya maudhui yanayochukuliwa hatua chini ya sera ya Taarifa isiyofaa, miongoni mwa pointi nyingine muhimu za data, hudhoofisha uwezo wa watafiti na washikadau kutathmini ufanisi wa majibu yaliyopo ya Meta kwa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19. Lazima Meta itoe data ili kutathmini iwapo utekelezwaji wa sera unaleta matokeo chanya mengi ya uongo na unahitaji kurekebishwa ili kupunguza hatari ya utekelezaji kupita kiasi. Kuhusiana na hili, Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza, ameangazia “ukosefu wa uwazi na ufikiaji wa data ambao unatatiza tathmini yenye lengo la ufanisi wa hatua” zilizotumika ili kukabiliana na taarifa isiyofaa mtandaoni. Hili pia huzuia washikadau kujua iwapo sera zimetumika mara kwa mara kote ulimwenguni. ( A/HRC/47/25, aya ya 65).
106. Hapo awali Bodi ilipendekeza kuwa Meta igawanye Data yake ya Ripoti ya Utekelezaji wa Kiwango cha Jumuiya kulingana na nchi na lugha (“Wasiwasi wa Kipunjab kuhusu RSS nchini India,” [ 2021-003-FB-UA] uamuzi wa kesi, pendekezo la kwanza). Ili kujibu, Meta imejitolea kubadilisha metriki zake na imeweka lengo la kuzizindua mwishoni mwa 2023. Kugawanya data ya utekelezaji kulingana na nchi au lugha ni muhimu kwa kuelewa upeo wa tatizo katika sehemu mbalimbali duniani na ufanisi wa kiasi wa hatua za utekelezaji za kampuni. Bodi na, muhimu zaidi, washikadau wa Meta wanazuiwa kuelewa kikamilifu na ipasavyo kuhusu ufanisi wa sera ya sasa ya kampuni ya kimataifa na mbinu ya utekelezaji wa kushughulikia taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 bila data yoyote muhimu ambayo inaweza kuruhusu watafiti na mashirika ya kiraia kutathmini juhudi za kampuni.
107. Pendekezo la 13:Meta inapaswa kuunda sehemu katika “Ripoti yake ya Utekelezaji wa Viwango vya Jumuiya” ili kuripoti kuhusu maombi ya watendaji wa serikali kukagua maudhui yasera yaTaarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa ukiukaji wa dharura za afya ya umma . Ripoti hiyo inafaa kujumuisha maelezo kuhusu idadi ya maombi ya ukaguzi na uondoaji kulingana na nchi na shirika la serikali, na idadi ya maombi yanayokataliwa na kukubaliwa na Meta. Bodi itazingatia kuwa hii imetekelezwa wakati Meta itachapisha sehemu tofauti kwenye maelezo yake “Ripoti ya Utekelezwaji wa Viwango vya Jumuiya” kuhusu maombi kutoka kwa watendaji wa serikali ambayo yanasababisha uondoaji wa aina hii kiukaji wa sera.
108. Katika kesi ya “Muziki wa Uingereza” [ 2022-007-IG-MR], Bodi ilipendekeza kwamba Meta “ichapishe data kuhusu ukaguzi wa maudhui ya watendaji wa serikali na maombi ya uondoaji kwa ajili ya ukiukaji wa Viwango vya Jumuiya.” Katika kilele cha janga la COVID-19, kuliibuliwa wasiwasi kuhusu jinsi Meta inavyokagua maudhui yanayohusiana na COVID-19 kwa maagizo ya serikali. Mtindo huu unaweza kuwa mbaya zaidi katika nchi ambapo serikali hutoa maombi kama hayo ili kuwakandamiza waandamanaji wenye amani au watetezi wa haki za binadamu wanaokosoa sera za serikali au kunyamazisha mijadala ya umma. Wakati wa janga hilo, Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za uhuru wa kukusanyika na kujumuika kwa amani, ameibua wasiwasi kuhusu serikali duniani kote kutumia janga hili kama kisingizio cha kuweka hali ya hatari au vinginevyo kukwepa mahitaji ya mchakato na ukaguzi wa kitaasisi na mizani iliyopo katika jamii ya kidemokrasia. Hili liliathiri haki msingi za binadamu, kama vile haki ya kuandamana kwa amani ( A/HRC/50/42, aya ya 18; A/77/171, aya ya 40, 67). Ripoti ya kina kuhusu maombi ya watendaji wa serikali kukagua maudhui chini ya sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya ummaitatoa utaratibu unaofaa kwa watumiaji, kulingana na kanuni ya uhalali, hasa wale walio katika nchi hatari zilizo na maeneo dhaifu ya kiraia.
109. Mwandishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za uhuru wa kukusanyika na kujumuika kwa amani alipendekeza kwamba lazima makampuni ya teknolojia yahakikishe kwamba bidhaa zao hazitumiwi na serikali kufuatilia au kudhibiti “wanaharakati wanaounga mkono haki za kijamii.” (A/77/171, aya ya 71). Bodi inapongeza dhamira ya Meta ya kuwawezesha watetezi wa haki za binadamu dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni, ufuatiliaji, na madai ya udhibiti kutoka kwa serikali kama ilivyoainishwa katika Sera ya Kampuni ya Haki za Binadamu za Shirika.. Uwazi kuhusu maombi ya serikali ya kukagua na/au kuondoa maudhui chini ya Kiwango cha Jumuiya cha Meta kuhusu Taarifa Isiyofaa kutaonyesha dhamira hii.
110. Pendekezo la 14:Meta inapaswa kuhakikisha zana zilizopo za utafiti, kama vile CrowdTangle na Facebook Open Research and Transparency (FORT) zinaendelea kufanywa zipatikane na watafiti. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta itakapoeleza hadharani wajibu wake wa kushiriki data kupitia zana hizi kwa watafiti.
111. Pendekezo la 15: Meta inapaswa kuanzisha njia kwa watafiti kutoka nje kupata ufikiaji wa data isiyo ya umma ili kusoma kwa uhuru athari za hatua za sera zinazohusiana na uondoaji na usambazaji mdogo wa taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19, huku ikihakikisha kuwa njia hizi zinalinda haki ya faragha ya watumiaji wa Meta na haki za binadamu ndani na nje ya jukwaa. Data hii inapaswa kujumuisha metriki ambazo hazikutolewa hapo awali, ikiwemo kiwango cha kurudia uhalifu unaohusiana na hatua za taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta itakapofanya hifadhidata hizi zipatikane kwa watafiti wa nje na kuthibitisha hili na Bodi.
112. Mwandishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza alibainisha ugumu wa kushughulikia taarifa ya uongo, kwa kiasi fulani kutokana na ukosefu wa taarifa za kutosha zinazopatikana hadharani ambazo zingewawezesha watumiaji, watafiti na wanaharakati kuelewa na kueleza asili ya tatizo. ( A/HRC/47/25, aya ya 3, 67, 81). Kufikia sasa, Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza anapendekeza kutoa data kwa ajili ya “utafiti, utungaji sera, ufuatiliaji na tathmini” (A/HRC/47/25, aya ya 104).
113. CrowdTangle ni zana ambayo watafiti wa nje wanaweza kutumia kufuatilia “akaunti na vikundi vya umma vyenye ushawishi kwenye Facebook na Instagram” na kuchanganua mienendo inayofaa, ikijumuisha taarifa isiyofaa. Hifadhidata ya zana inajumuisha watumiaji wote walioidhinishwa/wa umma, wasifu na akaunti, kama za wanasiasa, wanahabari, midia na wachapishaji, watu maarufu, timu za michezo na watu wengine maarufu. Inajumuisha pia vikundi na kurasa za umma zilizo juu ya kizingiti cha ukubwa fulani kulingana na nchi. Inashiriki data kuhusu tarehe na aina ya maudhui yaliyochapishwa, ukurasa, akaunti au kikundi ambacho kilishiriki maudhui, idadi na aina ya mwingiliano na maudhui, na kurasa au akaunti nyingine za umma ambazo zilishiriki. Haifuatilii ufikiaji wa maudhui, data au maudhui yoyote yaliyotumwa na akaunti za kibinafsi, maudhui ya kulipia au yaliyohamasishwa, au maelezo ya idadi ya watu wanaotumia maudhui. CrowdTangle ina data kwenye kurasa vikundi na wasifu ulioidhinishwa zaidi ya milioni saba za Facebook, na zaidi ya akaunti milioni mbili za umma za Instagram.
114. Mnamo 2022, ripoti za habari zilidai kwamba Meta inapanga kufunga CrowdTangle. Ingawa Meta haijathibitisha hadharani, Bodi inasisitiza kuwa zana za utafiti zinafaa kuimarishwa badala ya kusitishwa na kampuni. Hii itawawezesha watafiti wa nje kuelewa athari za bidhaa za Meta, ikiwemo kuhusu taarifa isiyofaa ya COVID-19.
115. Bodi inabainisha juhudi za Meta katika kusanidi zana ya Facebook Open Research and Transparency (FORT) ya Facebook, ambayo hutoa seti mbalimbali za data zinazolindwa na faragha kwa wasomi na watafiti. Kulingana na kampuni hiyo, Jukwaa la Mtafiti la FORT linawapa wanasayansi wa kijamii kupata taarifa nyeti katika mazingira yanayodhibitiwa kuhusu “data ya tabia ya watu wengi ili kuchunguza na kuelezea hali ya kijamii.” Hata hivyo, ripoti zimejitokeza kuhusu upungufu wa zana kwa ajili ya utafiti wa kitaaluma, kama vile “masharti ya matumizi ya vizuizi” ya Meta au watafiti kupewa taarifa zisizotosha kufanya uchambuzi busara. Licha ya hayo, Bodi inatambua kuwa katika muktadha wa kampuni zingine za mitandao ya kijamii, Meta imechukua hatua kubwa kushiriki data na watafiti wa nje na Bodi inahimiza Meta kufanya zaidi.
116. Katika shughuli zote za ushirikishaji wa washikadau zilizofanywa kwa maoni haya ya ushauri wa sera, watafiti wamesisitiza mara kwa mara hitaji la zana hizi kufuatilia mienendo inayohusiana na taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19. Ukosefu wa ufikiaji wa data muhimu pia umeweka changamoto kwa Bodi inapotathmini ufaafu wa ombi la maoni ya ushauri wa sera. Kwa ufahamu wa Bodi, baadhi ya data hizi hazipatikani kwa kampuni yenyewe, ilhali baadhi zinapatikana lakini haziwezi kushirikiwa na washikadau kutoka nje, pamoja na Bodi. Meta inapaswa kuwapa watafiti uwezo wa kufikia data husika ili kufuatilia makadirio ya kipimo ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 kwenye jukwaa na ufanisi wa hatua mahususi za kuishughulikia. Taarifa kama hizo pia ni muhimu katika kufanya tathmini ya athari za haki za binadamu iliyojadiliwa hapa juu.
117. Pendekezo la 16: Meta inapaswa kuchapisha matokeo ya utafiti wake kuhusu lebo wastani na za ukaguzi wa ukweli ambazo ilishiriki na Bodi wakati wa mchakato wa kutoa maoni ya ushauri wa sera ya COVID-19. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa wakati Meta itachapisha utafiti huu hadharani katika Kituo hake ccha Uwazi.
118. Bodi inathamini maelezo ambayo Meta ilishiriki na Bodi kuhusu ufanisi wa NIT na ushushaji wa maudhui, kama vile matokeo ya majaribio ambayo kampuni iliendesha ili kutathmini ufanisi unaoendelea wa NIT. Bodi ina maoni kwamba matokeo ya majaribio haya yanapaswa kushirikiwa zaidi na watafiti kutoka nje wanaotaka kuelewa athari za majibu ya kampuni ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19.
119. Pendekezo la 17: Meta inapaswa kuhakikisha kuna upatikanaji sawa wa data kwa watafiti duniani kote. Ingawa watafiti barani Ulaya watakuwa na njia ya kutuma maombi ya ufikiaji wa data kupitia Sheria ya Huduma za Kidijitali (DSA), Meta inapaswa kuhakikisha haitoi faharasa zaidi ya watafiti kutoka vyuo vikuu vya utafiti vya Global North. Utafiti wa makadirio ya kipimo ya taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 na athari za sera za Meta utaunda ufahamu wa jumla na majibu ya baadaye ya taarifa isiyofaa yenye madhara inayohusu afya katika hali hii ya dharura na ya baadaye. Iwapo utafiti huo inaangazia isivyo sawa katika Global North, majibu yatakuwa pia. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta inaposhiriki hadharani mpango wake wa kuwapa watafiti duniani kote ufikiaji wa data sawa na unaotolewa kwa nchi za Umoja wa Ulaya chini ya DSA.
120. Utafiti mwingi kuhusu mtiririko wa taarifa ya uongo unaonyesha kwa njia isiyo sawia mienendo na mifumo inayotokea nchini Marekani na Ulaya Magharibi. Hili linaweza kusababisha hatua za sera za maudhui kuandaliwa kulingana na matatizo mahususi ya maeneo haya. Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza alibainisha wito kutoka kwa mashirika ya raia kwa ajili ya utafiti zaidi kuhusu athari za taarifa ya uongo kwa “jamii zinazoweza kudhuriwa na zenye watu wachache,” akitoa mfano wa kampeni za taarifa ya uongo zilizotegemea utambulisho ambazo zilichochea vita vya kikabila nchini Ethiopia na Myanmar. ( A/HRC/47/25, aya ya 26). Meta inapoongeza ufikiaji wa watafiti wa nje kwa kufuata Sheria ya Huduma za Kidijitali na pia kudumisha FORT yake yenyewe, kampuni inapaswa kuhakikisha uwakilishi wa wasomi na watafiti kutoka duniani kote.
121. Pendekezo la 18: Meta inapaswa kutathmini athari za mfumo wa Ukaguzi wa Pili wa Majibu ya Mapema (ERSR) kuhusu ufanisi wa utekelezaji wake wa sera ya Taarifa isiyofaa, na kuhakikisha kuwa Mapendekezo ya 16 na 17 katika maoni ya ushauri wa sera ya Bodi kuhusu mpango wa ukaguzi wa Meta yanatumika na mashirika yanayochapisha maudhui yanayokiuka sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura ya afya ya umma. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa Meta itakaposhiriki matokeo yake na Bodi na kuyatangaza hadharani.
122. Kulingana na Meta, mpango wa ukaguzi uliwekwa ili kupunguza makosa ya usimamizi chanya wa uwongo wenye hatari zaidi. Sehemu ya kwanza ya mpango wa ukaguzi ni mfumo wa Ukaguzi wa Pili wa Majibu ya Mapema (ERSR) ambao huhakikisha ukaguzi wa ziada wa binadamu, kuhusu maudhui yanayoweza kukiuka ambayo yamechapishwa na watu mahususi wanaotambulika. Meta huhifadhi orodha za watu wanaotambulika kulingana na mtu ambaye kampuni imeamua kuwa ana haki ya kupokea manufaa ambayo ESR hutoa. Mashirika yanaweza kuchukua muundo wa kurasa za Facebook, wasifu wa Facebook, na akaunti za Instagram na yanaweza kuwakilisha watu binafsi na vikundi au mashirika. Watumiaji wengi waliojumuishwa katika orodha hizi ni watu maarufu, makampuni makubwa, viongozi wa serikali na wanasiasa.
123. Katika maoni yake ya ushauri wa sera kuhusu mpango wa ukaguzi wa Meta, Bodi ilipendekeza kwamba Meta ianzishe “vigezo wazi na vya umma vya ustahiki wa kuzuia makosa kulingana na shirika” ambavyo vitatofautisha kati ya “watumiaji ambao usemi wao unastahili ulinzi wa ziada kutoka kwa mtazamo wa haki za binadamu” na “vinavyojumuishwa kwa sababu za biashara.”
124. Wanasiasa wameruhusiwa kutokuwa sehemu ya mpango wa mhusika mwingine wa ukaguzi wa ukweli. Hii ina maana kwamba taarifa za uongo zinazoshirikiwa na wanasiasa, ambazo hazijaondolewa vinginevyo chini ya sera ya Taarifa Isiyofaa Yenye Madhara Inayohusu Afya, haziwezi kukaguliwa na kuwekewa lebo na wakaguzi wengine wa ukweli. Meta pia ilieleza kuwa haijatathmini athari za mfumo wa ESR kwenye ufanisi wa sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 kwani ESR iliundwa kuzuia makosa katika utekelezaji badala ya kutathmini ufanisi wa Kiwango mahususi cha Jumuiya. Kwa hivyo, timu za ndani za kampuni hazifuatilii au kuchanganua data kuhusu athari zake kwenye sera ya Taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19.
125. Kulingana na utafiti wa ndani na pia ushirikishwaji wa washikadau kwa maoni haya ya ushauri wa sera kuhusu COVID-19, Bodi iligundua kuwa wasambazaji wengi wa taarifa isiyofaa ni wasemaji maarufu kama vile watu mashuhuri, wanasiasa, watendaji wa serikali na watu wa kidini ambao wanaweza kuwa mashirika yanayostahiki manufaa ya mpango wa ESR. Kwa mfano, mawasilisho kutoka kwa Media Matters for America (PC-10758) yaliangazia athari za mfumo wa ukaguzi wa Meta katika kudhoofisha juhudi za kushughulikia taarifa isiyofaa. Kwa vile watu maarufu, wanasiasa, waandishi wa habari na watumiaji wengine mashuhuri walipewa “utekelezaji ulio polepole” kwa ukiukaji wa maudhui, taarifa isiyofaa iliruhusiwa kusalia kwenye jukwaa. Mwandishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza pia aliibua wasiwasi kuhusu “taarifa zisizo za kuaminiwa” zinazosambazwa na “watu maarufu kwenye jukwaa,” akibainisha kwamba “inaweza kusababisha madhara makubwa, yawe yamekusudiwa kwa nia mbaya au la.” Watendaji wa serikali pia wamesambaza “madai ya kutojali mara nyingi” kuhusu asili ya virusi, upatikanaji wa dawa za kukabiliana na dalili, na hali ya COVID-19 nchini mwao, miongoni mwa madai mengine. Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa alipendekeza kuwawajibisha maafisa wa umma kwa kauli na matendo yao. ( A/HRC/44/49, aya ya 41, 45, 63(c); tazama pia A/HRC/47/25, aya ya 18 kuwatambua watu maarufu kama wasambazaji wa taarifa isiyofaa kwa ujumla zaidi.)
126. Taarifa isiyofaa iliyochapishwa na watu wanaotambulika chini ya mpango wa ESR ambayo yanaweza kuchangia moja kwa moja katika hatari ya madhara ya kimwili yanayoweza kutokea kwa afya na usalama wa umma, itaondolewa kwa kuzingatia sera ya Taarifa Isiyofaa Yenye Madhara Inayohusu Afya. Hata hivyo, taarifa isiyofaa ambayo kwa kawaida ingestahili kukaguliwa ukweli au kuwekewa lebo, lakini kwa sababu inachapishwa na watu wanaotabulika kama vile wanasiasa, sio tu kwamba hayafai kufanyiwa ukaguzi wa ukweli na wahusika wengine bali pia yananufaika kutokana na ucheleweshaji wa utekelezaji kwa sababu ya ukaguzi wa ziada wa binadamu unaotolewa na mfumo wa ERSR. Hii ina maana kwamba taarifa isiyofaa kuhusu COVID-19 ambayo sio mojawapo ya madai 80 yaliyobainishwa, ambayo yamechapishwa na watu wanaotambulika, yanaweza kusalia kwenye jukwaa bila lebo ya ukaguzi wa ukweli na huenda yasikaguliwe kabisa.
*Dokezo la kiutaratibu:
Maoni ya Bodi ya ushauri wa sera yanatayarishwa na majopo ya Wanachama watano na kuidhinishwa na wengi wa wanachama wa Bodi. Maamuzi ya Bodi hayawakilishi maoni ya kibinafsi ya Wanachama wote.
Kwa maoni haya ya ushauri wa sera, utafiti huru ulipangwa kwa niaba ya Bodi. Bodi ilisaidiwa na taasisi huru ya utafiti yenye makao yake makuu katika Chuo Kikuu cha Gothenburg, ambayo inashirikisha timu ya zaidi ya wanasayansi hamsini wa kijamii kutoka mabara sita, pamoja na zaidi ya wataalamu 3,200 wa kila nchi kutoka kote ulimwenguni. Bodi pia ilisaidiwa na Duco Advisors, shirika la ushauri linalolenga miingiliano ya siasa za ulimwengu, uaminifu na usalama na teknolojia. Bodi pia ilisaidiwa na Memetica, shirika ambalo linajihusisha na utafiti wa chanzo huria kuhusu mienendo ya mitandao ya kijamii, ambalo pia lilitoa uchanganuzi.
Volver a Decisiones de casos y opiniones consultivas sobre políticas