Anulado

Boti ya Myanma

Bodi ya Usimamizi imebadilisha uamuzi wa Facebook wa kuondoa chapisho katika Kiburma chini ya Kiwango chake cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki.

Tipo de decisión

Estándar:

Políticas y temas

Tema
Libertad de expresión, Política
Estándar comunitario
Lenguaje que incita al odio

Regiones/Países

Ubicación
Myanmar

Plataforma

Plataforma
Facebook

Muhtasari wa kesi

Bodi ya Usimamizi imebadilisha uamuzi wa Facebook wa kuondoa chapisho katika Kiburma chini ya Kiwango chake cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki. Bodi ilipata kuwa chapisho hilo halikulenga watu wa China, lakini jimbo la China. Hasa, ilitumia matamshi yenye matusi kurejelea sera la serikali ya China katika Hong Kong kama sehemu ya majadiliano ya kisiasa kwenye jukumu la serikali ya China katika Myanmar.

Kuhusu kesi hii

Mnamo Aprili 2021, mtumiaji wa Facebook aliyeonekana kuwa katika Myanmar alichapisha katika Kiburma kwenye kalenda yao ya matukio. Chapisho hilo lilijadili njia za kubana ufadhili katika Myanmar kufuatia upinduzi wa serikali katika Myanmar mnamo Februari tarehe 1, 2021. Lilipendekeza kuwa mapato ya ushuru upewe Kamati Inayowakilisha Pyidaungsu Hlutaw (CRPH), kikundi cha wabunge waliopinga upinduzi wa serikali. Chapisho hilo lilipokea karibu mitazamo nusu milioni na hakuna watumiaji wa Facebook ambao waliliripoti.

Facebook ilitafsiri kuwa huenda sehemu inayokiuka ya chapisho la mtumiaji “watu wa Hong Kong, kwa sababu Wachina waliwanyanyasa, walibadilisha benki zao kwenda Uingereza, na sasa (Wachina) hawawezi kuwagusa (Hong Kong people, because the fucking Chinese tortured them, changed their banking to UK, and now (the Chinese) they cannot touch them).” Facebook iliondoa chapisho hilo chini ya Kiwango chake cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki. Hii inapiga marufuku maudhui yanayolenga mtu au kikundi cha watu kutegemea rangi, kabila au taifa lao la uasili kwa “istilahi au maneno machafu kwa lengo la kutusi.”

Wakaguzi wanne wa maudhui waliochunguza chapisho hilo wote walikubaliana kuwa lilikiuka kanuni za Facebook. Katika rufaa yao kwa Bodi, mtumiaji alitaka kuwa walichapisha maudhui hayo ili “kukomesha utawala wa kikatili wa jeshi.”

Matokeo muhimu

Kesi hii inaangazia umuhimu wa kuzingatia maudhui wakati wa kutekeleza sera za matamshi ya chuki, sawa na umuhimu wa kulinda matamshi ya kisiasa. Hii ni muhimu hasa katika Myanmar kwa kuwa upinduzi wa serikali wa Februari 2021 na majukumu muhimu ya Facebook kama njia ya mawasiliano katika nchi hiyo.

Chapisho hilo lilitumia maneno ya Kiburma ya “$တရုတ်,” ambayo Facebook ilitafsiri kama “Wachina wapumbavu” (au “sout ta-yote”). Kulingana na Facebook, neno “ta-yote” “linachukuliwa kitamaduni na kiisimu kama kupitana kwa utambulisho/maana kati ya nchi ya China na watu wa China.” Facebook ilitaja kuwa kwa sababu ya hali ya neno hili na ukweli kuwa mtumiaji “hakuonyesha wazi kuwa istilahi hiyo inarejelea nchi/serikali ya China,” iligundua kuwa “mtumiaji, kwa chini kabis, anarejelea watu wa China.” Kwa hivyo, Facebook iliondoa chapisho hilo chini ya Kiwango chake cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki.

Kwa kuwa neno hilo linatumika katika Kiburma kurejelea jimbo na watu kutoka kwenye jimbo hilo, muktadha ni muhimu katika kufahamu maana lengwa. Vipengele kadhaa vilishawishi Bodi kuwa mtumiaji hakuwa anawalenga watu wa China, lakini alilenga jimbo la China.

Sehemu ya chapisho hilo ambayo huenda ilikiuka kanuni za Facebook inarejelea sera za kifedha za China katika Hong Kong kama “ukatili” au “unyanyasaji,” na si vitendo vya watu binafsi au watu wa China katika Myanmar. Watafsiri wa Bodi walitaja kuwa, katika hali hii, neno “ta-yote” lilirejelea jimbo. Wakiulizwa kama kunaweza kuwa na utata wowote katika rejeleo hili, watafsiri hawakuonyesha shaka yoyote. Watafsiri wa Bodi pia walitaja kuwa chapisho hilo lilikuwa na istilahi ambazo zinatumika kwa kawaida na serikali ya Myanmar na ubalozi wa China ili kuwasiliana na kila mmoja. Kuongezea, huku watu nusu milioni walitazama chapisho hilo na zaidi ya watu 6,000 walilishiriki, hakuna watumiaji ambao waliliripoti. Maoni ya umma pia yalifafanua toni ya jumla ya chapisho hilo kama majadiliano ya kisiasa.

Kwa kuwa chapisho hilo halikuwalenga watu kutegemea uasili, kabila, au nchi ya uasili, lakini lililenga jimbo, Bodi iligundua kuwa halikukiuka Kiwango cha Jumuiya ya Facebook ya Matamshi ya Chuki.

Uamuzi wa Bodi ya Usimamizi

Bodi ya Usimamizi inabatilisha uamuzi wa Facebook wa kuondoa maudhui hayo, na kuhitaji chapisho hilo kurejeshwa.

Katika taarifa ya ushauri wa sera, Bodi inapendekeza kwamba Facebook:

  • Hakikisha kuwa Viwango vyake vya Utekelezaji wa Ndani vinapatikana katika lugha ambayo wapatanishi wa maudhui hukagua maudhui. Ikiwa ni muhimu kupatia kipaumbele, Facebook inafaa kulenga kwanza muktadha ambapo hatari za haki za binadamu ni hatari zaidi.

*Mihtasari ya kesi hutoa maelezo mafupi ya kesi na haina thamani ya kurejelewa.

Uamuzi kamili wa kesi

1. Muhtasari wa uamuzi

Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa Facebook wa kuondoa maudhui chini ya Viwango vyake vya Jumuiya kuhusu Semi za Chuki. Bodi ilipata kuwa chapisho hilo halikuwa matamshi ya chuki.

2. Maelezo ya kesi

Mnamo Aprili 2021, mtumiaji wa Facebook aliyeonekana kuwa katika Myanmar alichapisha katika Kiburma kwenye kalenda yao ya matukio. Chapisho hilo lilijadili njia za kubana ufadhili katika Myanmar kufuatia upinduzi wa serikali katika Myanmar mnamo Februari tarehe 1, 2021. Lilipendekeza kuwa mapato ya ushuru upewe Kamati Inayowakilisha Pyidaungsu Hlutaw (CRPH), kikundi cha wabunge waliopinga upinduzi wa serikali. Chapisho hilo lilitazamwa karibu mara 500,000, karibu hisia 6,000 na lilishirikiwa karibu mara 6,000. Hakuna watumiaji wa Facebook ambao waliripoti chapisho hilo.

Facebook ilitafsiri kuwa huenda sehemu inayokiuka ya chapisho la mtumiaji “watu wa Hong Kong, kwa sababu Wachina waliwanyanyasa, walibadilisha benki zao kwenda Uingereza, na sasa (Wachina) hawawezi kuwagusa (Hong Kong people, because the fucking Chinese tortured them, changed their banking to UK, and now (the Chinese) they cannot touch them).” Facebook iliondoa chapisho hilo kama “Daraja la 2” la Matamshi ya Chuki chini ya Kiwango chake cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki siku baada ya kuchapishwa. Hii inapiga marufuku maudhui yanayolenga mtu au kikundi cha watu kutegemea rangi, kabila au taifa lao la uasili kwa “istilahi au maneno machafu kwa lengo la kutusi.”

Kushirikiwa tena kwa chapisho, kulingana na Facebook, “iliteuliwa otomatiki kama sehemu ya sampuli na kutumwa kwa mhakiki binadamu ili itumiwe katika mafunzo ya uwekaji kwenye kikundi.” Hii inajumuisha Facebook kuunda vikundi vya data vya mifano ya maudhui yanayokiuka na yasiyokiuka ili kufunza michakato yake ya otomatiki ya kugundua na kutekeleza ili kutabiri kama maudhui yanakiuka kanuni za Facebook. Mkaguzi aliamua kuwa chapisho lililoshirikiwa lilikiuka Kiwango cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki. Huku madhumuni ya mchakato yalikuwa kuunda vikundi vya maudhui ili kufunza kiainishaji, mara tu chapisho lililoshirikiwa lilipatikana kuwa linakiuka, lilifutwa.

Kwa sababu chapisho lililoshirikiwa lilipatikana kuwa limekiuka kanuni za Facebook, “Boti ya Kitengo cha Usimamizi” ilitambua otomatiki chapisho asili kwa ajili ya ukaguzi. Facebook ilifafanua kuwa Boti ya Kitendo cha Usimamizi ni akaunti ya ndani ya Facebook ambayo haifanyi uitathmini wowote wa maudhui lakini inafanya “vitendo anuwai katika mfumo mzima wa utekelezwaji kutegemea maamuzi yaliyofanywa na binadamu au otomatiki.” Wakaguzi wawili binadamu kisha walichanganua chapisho asili, na wote waliamua kuwa lilikuwa Matamshi ya Chuki ya “Daraja la 2”. Maudhui yaliyondolewa. Mtumiaji alikata rufaa ya uondoleaji kwa Facebook, ambapo mkaguzi wa nne binadamu aliunga mkono uondoleaji huo. Kwa mujibu wa Facebook, “wakaguzi wa maudhui katika kesi hii wote walikuwa wanachama wa timu ya ukaguzi wa maudhui ya Kiburma katika Facebook.” Mtumiaji kisha aliwasilisha rufaa yao kwa Bodi ya Uangalizi.

3. Mamlaka na upeo

Bodi ina mamlaka ya kukagua uamuzi wa Facebook kufuatia rufaa kutoka kwa mtumiaji ambaye chapisho lake liliondolewa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria Ndogo Kifungu cha 2, Sehemu ya 2.1). Bodi inaweza kudumisha au kutengua uamuzi huo (Kifungu cha 3 cha Mkataba, Sehemu ya 5). Maamuzi ya Bodi ni ya lazima na yanaweza kujumuisha taarifa za ushauri wa sera na mapendekezo. Mapendekezo haya hayana masharti lakini lazima Facebook iyatolee maoni (Kifungu cha 3 cha Mkataba, Sehemu ya 4). Bodi ni utaratibu huru wa malalamiko ya kushughulikia migogoro kwa njia ya uwazi na inayofuata kanuni.

4. Viwango muhimu

Bodi ya Usimamizi ilizingatia viwango vifuatavyo katika uamuzi wake:

I. Viwango vya Jumuiya ya Facebook

Viwango vya Jumuiya ya Facebook vinafafanua semi za chuki kama “mashumbulio ya moja kwa moja kwa watu kulingana na kile tunachokiita sifa zilizolindwa — asili ya rangi, kabila, asili ya kitaifa, dini, mwelekeo wa kijinsia, utambulisho wa kijinsia, na ulemavu au ugonjwa hatari.” Chini ya “Daraja la 2”, maudhui yaliyopigwa marufuku yanajumuisha kulaani, inayofafanuliwa kama “maneno au istilahi chafu kwa lengo la matusi, ikijumuisha, japo haina kikomo kwa: fuck, bitch, motherfucker.”

II. Maadili ya Facebook

Maadili ya Facebook yameorodheshwa katika utangulizi wa Viwango vya Jumuiya. Maadili ya “Sauti” yametajwa kuwa “muhimu”:

Kila mara, lengo la Viwango vyetu vya Jumuiya limekuwa ni kutengeneza mahali pa kujieleza na kuwapa watu sauti. […] Tunataka watu waweze kuzungumza kwa uwazi kuhusu masuala yaliyo muhimu zaidi kwao, hata kama baadhi ya watu wanaweza kutokubaliana nayo au kuona kuwa ni ya kupingwa.

Facebook imeweka kikomo cha “Sauti” katika kuhudumia maadili manne na mawili kati ya hayo manne, ni muhimu hapa:

“Usalama”. Tumejitolea kufanya Facebook kuwa mahali salama. Kujieleza kwa kutishia watu kuna uwezo wa kuhofisha, kutenga au kunyamazisha wengine na hakukubaliki kwenye Facebook.

“Hadhi” : Tunaamini kwamba watu wote wako sawa kihadhi na kihaki. Tunatarajia kwamba watu wataheshimu hadhi ya wenzao na hawatadhulumu au kuwashusha wenzao hadhi.

III. Viwango vya haki za binadamu

Kanuni za Mwongozo wa Umoja wa Mataifa juu ya Biashara na Haki za Binadamu (UNGP), zilizoidhinishwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mnamo 2011, zina mfumo wa hiari wa majukumu ya haki za binadamu ya biashara za kibinafsi. Mnamo 2021, Facebook ilitangazaSera yake ya Haki za Binadamu za Shirika, ambapo ilianzisha kujitolea kwake katika kuwakilisha haki za kibinadamu kwa mujibu wa UNGP. Kigezo ambacho Bodi ilitumia katika kuchambua kesi hii kilitoka katika viwango vifuatavyo vya haki za binadamu:

  1. Uhuru wa kujieleza: Kifungu cha 19, Agano la Kimataifa kuhusu Haki za Raia na Kisiasa ( ICCPR), Maoni ya Jumla Nambari 34, Kamati ya Haki za Kibinadamu, 2011
  2. Majukumu ya biashara: Biashara, haki za kibinadamu na maeneo yaliyoathiriwa na vurugu: dhidi ya ripoti kitendo zaidi ( A/75/212), Kikundi cha Umoja wa Mataifa cha Kazi kuhusu suala la haki za kibinadamu na mashirika ya miamala na biashara nyingine

5. Taarifa ya mtumiaji

Mtumiaji alitaja kuwa rufaa yao kwa Bodi kwamba walichapisha maudhui haya ili “kukomesha mamlaka ya jeshi ya kikatili” na kutoa ushauri kwa viongozi wa kidemokrasia katika Myanmar. Mtumiaji pia alisisitiza haja ya kubanwa kwa ufadhili wa mamlaka ya jeshi ya Myanmar. Mtumiaji alijitambua kama “mwanaharakati” na kushuku kuwa watoa habari wa mamlaka ya jeshi ya Myanmar waliripoti chapisho lao. Mtumiaji pia alitaja kuwa “mtu anayefahamu Lugha ya Myanmar” anafaa kukagua chapisho lao.

6. Ufafanuzi wa maamuzi wa Facebook

Facebook iliondoa maudhui kama shambulio la “Darala ja 2” chini ya Kiwango cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki, hasa kwa kukiuka sera yake inayopiga marufuku maneno ya matusi ya kulaani yanayolenga watu kutegemea rangi, kabila na/au taifa lao la asili. Kwa mujibu wa Facebook, maudhui yanayodaiwa kukiuka yalizingatiwa kuwa shambulio la watu wa China.

Maudhui hayo yalijumuisha kirai katika Kiburma “$တရုတ်,” ambacho timu ya kikanda ya Facebook ilitafsiri kama “fucking Chinese” (au “sout ta-yote"). Timu ya kikanda ya Facebook ilitaja kuwa “$” inaweza kutumika kama ufupi wa “စောက်” au “sout,” inayoweza kufasiriwa kama “fucking.” Kwa mujibu wa timu ya Facebook, neno “ta-yote” “linachukuliwa kitamaduni na kiisimu kama kupitana kwa utambulisho/maana kati ya nchi ya China na watu wa China.” Facebook ilipatia Bodi mwongozo muhimu wa siri ya ndani ambao huwa inapatia wapatanishi wake, au Viwango vya Utekelezwaji wa Ndani, kuhusu lugha bainishi inayowalenga watu kutegemea sifa zilizolindwa na dhana zinazohusiana na sifa zilizolindwa.

Facebook pia ilitaja katika uamuzi wake kanuni kuwa kufuatia upinduzi wa serikali wa Februari 2021 “kulikuwa na ripoti za kuongezeka kwa kauli zinazopinga China” katika Myanmar na kuwa “watu kadhaa wa China waliumia, kufungwa au kuuawa katika shambulizi la moto linalodaiwa kuhusu kiwanda cha nguo kinachofadhiliwa na China katika Yangon,Myanmar.” Katika kujibu swali kutoka kwa Bodi, Facebook ilitaja kuwa haikuwa na mawasiliano yoyote na mamlaka ya jeshi la Myanmar kuhusu chapisho hili.

Facebook ilitaja kuwa kwa sababu ya hali ya neno “ta-yote” na ukweli kwamba mtumiaji huyo “hakuonyesha kwa uwazi kuwa istilahi hiyo inarejelea nchi/serikali ya China,” Facebook ilibainisha kuwa “mtumiaji, kwa kiasi sana, anawarejelea watu wa China.” Hivyo, Facebook ilitaja kuwa kuondolewa kwa chapisho hilo lilipatana na Kiwango chake cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki.

Facebook pia ilitaja kuwa uondolewaji wake ulifuatana na thamani zake za “Heshima” na “Usalama”, zikisawazishwa dhidi ya thamani ya “Sauti.” Kwa mujibu wa Facebook, laana yenye matusi yanayolenga watu wa China “inaweza kusababisha hatari kwa watu hao” na “inadunisha, kuondoa ubinadamu, na kufanya heshima ya kibinafsi kuwa ndogo.”

Facebook ilihoji kwamba uamuzi wake ulilingana na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu. Facebook iliandika kuwa uamuzi wake ulifuata mahitaji ya sheria ya haki za kibinadamu kimataifaya sheria, dai halali, umuhimu na sehemu sawa. Kwa mujibu wa Facebook, sera yake ilikuwa “kufikiwa kwa urahisi” katika Viwango vya Jumuiya na “chaguo la maneno ya mtumiaji ulipatikana hasa ndani ya marufuku kuhusu istilahi za matusi.” Isitoshe, uamuzi wa kuondoa maudhui hayo ulikuwa halali ili kulinda “haki za wengine dhidi ya maumivu na ubaguzi.” Hatimaye, uamuzi wake wa kuondoa maudhui hayo ulikuwa “muhimu na sawasawa” kwani “uwekaji pamoja wa maudhui yaliyo na uchafu yaliyoelekezwa kwa watu wa China ‘huunda mazingira ambapo matendo ya vurugu huenda yakavumiliwa kwa kiasi kikubwa na kuzalishwa upya katika jamii,’” kwa kutaja umamuzi wa Bodi 2021-002-FB-UA unaohusiana na Zwarte Piet. Facebook ilitaja kuwa ilikuwa inafanana kwa sababu “kesi zote mbili zilihusisha matamshi ya chuki yaliyolenga watu kwa msingi wa uasili au kabila lao.”

7. Mawasilisho ya wahusika wengine

Bodi ya Usimamizi ilipokea maoni 10 ya umma yanayohusiana na kesi hii. Maoni matano kati ya maoni hayo yalitoka Pasifiki Asia na Australia na Pasifiki, hasa Myanmar, na tano yalitoka Marekani na Kanada. Bodi ilipokea maoni kutoka kwa washikadau ikijumuisha watetezi wa haki za kibinadamu na mashirika ya jamii ya kiraia yanayolenga uhuru wa kujieleza na matamshi ya chuki katika Myanmar.

Mawasilisho yalisimamia mada ikiwa ni pamoja na tafsiri na uchanganuzi wa neno “sout ta-yote,” ama maudhui hayo yalikuwa shambulio la China au watu wa China; ama chapisho hilo lilikuwa la hotuba ya kisiasa ambayo inafaa kulindwa kwa muktadha wa mgogoro katika Myanmwar; ama kulikuwa na ongezeko la matamshi ya kupinga China katika Myanmar kufuatia ugeuzi wa serikali Februari 2021; uhusiano kati ya China na utawala wa jeshi la Myanma; na matendo ya usawazishaji wa maudhui ya Facebook, hasa matumizi, mafunzo na ukaguzi wa zana za otomatiki za Facebook kwa ajili ya maudhui ya lugha ya Kiburma.

Ili kusoma maoni ya umma yaliyowasilishwa kuhusu kesi hii, tafadhali bofya hapa.

8. Uchambuzi wa Bodi ya Usimamizi

Kesi hii inaangazia umuhimu wa maudhui wakati wa kutekeleza sera za maudhui zilizoundwa ili kuwalinda watumiaji dhidi ya matamshi ya chuki, huku pia wakiheshimu hotuba ya kisiasa. Hii hasa ni muhimu katika Myanmar kwa sababu ya mapinduzi ya serikali ya Fabruari 2021 na umuhimu wa Facebook kama njia ya mawasiliano. Bodi iliangalia swali la iwapo maudhui haya yanapaswa kurejeshwa kwa Facebook kupitia lenzi tatu: Viwango vya Jumuiya ya Facebook; maadili ya kampuni na wajibu wake wa haki za binadamu.

8.1 Utiifu wa Viwango vya Kijamii

Bodi iligundua kuwa kurejesha maudhui haya kunafuatana na Kiwango cha Jumuiya ya Facebook kuhusu Matamshi ya Chuki. Sera ya Facebook inapiga marufuku “istilahi chafu zilizo na lengo la matusi” zinazolenga mtu au watu kutegemea uasili, kabila, au taifa la asili. Bodi inahitimisha kuwa chapisho hilo halikulenga watu, lakini badala yake lililenga sera ya kiserikali ya China katika Hong Kong, lililotolewa kwa muktadha wa kujadili jukumu la serikali ya China katika Myanmar.

Zaidi ya maoni ya umma, Bodi pia ilitafuta tasfiri mbili za matini hayo. Hii ilijumuisha tafsiri kutoka kwa mzungumzaji wa Kiburma anayepatikana ndani ya Myanmar na mzungumzaji mwingine wa Kiburma anayepatikana nje ya Myanmar. Maoni ya umma na watafsiri wa Bodi waligundua kuwa katika Kiburma, neno sawa linatumika kurejelea majimbo na watu kutoka kwa jimbo hilo. Kwa hivyo, muktadha ni muhimu katika kufahamu maana lengwa. Hii ni muhimu hasa kwa kutumia sera ya Facebook ya Matamshi ya Chuki. Wakati ambao maudhui hayo yaliondolewa, Kiwango cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki kilitaja kuwa kinapiga marufuku uvamizi dhidi ya watu kutegemea taifa la asili lakini hakipigi marufuku mashambulizi dhidi ya nchi.

Bodi ilizingatia vipengele kadhaa katika kuamua kuwa chapisho hili halikuwalenga watu wa China kutegemea kabila, uasili, au taifa la asili. Kwanza, chapisho pana linapendekeza njia za kubana uhusiano wa kifedha na mamlaka ya kijeshi na kutoa msaada wa kifedha wa kusaidia CRPH. Pili, sehemu ya chapisho inayodaiwa kukiuka inarejelea sera za kifedha za China katika Hong Kong kama “ukatili” au “hukumu”, na wala si vitendo vya watu binafsi au watu wa China katika Myanmar. Tatu, huku ukosefu wa kuripoti chapisho lililoshirikiwa sana kila mara huwa haimaanishi kuwa linakiuka, zaidi ya watu 500,000 walitazama, zaidi ya watu 6,000 walishiriki chapisho hilo na hakuna watumiaji waliloliripoti. Nne, watafsiri wote wawili waliosaidia Bodi walionyesha kuwa, huku istilahi hiyo sawa inatumika kurejelea jimbo na watu wake, hapa ilirejelea jimbo. Walipoulizwa kuhusu utata wowote unaoweza kutokea katika marejeleo haya, watafsiri hawakuonyesha shaka yoyote. Tano, watafsiri wote wawili walitaja kuwa chapisho hilo lina istilahi ambazo huwa zinatumika kawaida na serikali ya Myanmar na balozi la China ili kuwasiliana na kila moja. Mwisho, maoni ya umma kimsingi yalidokeza kipindi cha jumla cha chapisho kama la majadiliano ya kisiasa.

Kwa hivyo, kwa kuwa uchafu huo haukulenga watu kutegemea uasili, ukabila, au taifa la asili, lakini ulilenga jimbo, Bodi inahitimisha kuwa haukiuki Kiwango cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki cha Facebook. Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa marufuku kuhusu kuwalenga watu kutegemea sifa zilizolindwa yasiwekwe kwa njia ambayo inakinga serikali au taasisi dhidi ya ukosoaji. Bodi inatambua kuwa matamshi ya chuki ya kupinga China ni jambo la kushughulikiwa, lakini chapisho hili linarejelea jimbo la China.

Bodi haikubaliani na hoja ya Facebook kuwa uamuzi wake wa kuondoa maudhui haya yalifuata vigezo vya Bodi katika uamuzi wa kesi 2021-002-FB-UA (ambapo Bodi ilishikilia uondoaji wa picha za watu katika sura nyeusi). Katika kesi hiyo, Facebook ilikuwa na kanuni dhidi ya picha za watu katika sura nyeusi, na Bodi iliruhusu Facebook kutumia kanuni hiyo kwa maudhui yaliyojumuisha picha za sura nyeusi za Zwarte Piet. Hapa, kwa kulinganisha, muktadha wa chapisho hilo linaonyesha kuwa lugha iliyotumika haikukiuka kanuni za Facebook hata kidogo.

Wakati wa uamuzi wa Bodi kuhusiana na kesi hii, Facebook ilisasisha Kanuni yake ya Jumuiya ya Matamshi ya Chuki ili kutoa taarifa zaidi kuhusu inavyopiga marufuku “dhana” zinazohusiana na sifa zilizolindwa katika hali fulani. Kanuni hii mpya inasema kuwa Facebook “inahitaji taarifa ya ziada na/au muktadha” kwa ajili ya utekelezaji na kuwa watumiaji hawafai kuchapisha “Maudhui yanayovamia dhana, taasisi, mawazo, matendo, au imani zinazohusika na sifa zilizolindwa, ambazo zina uwezekano mkubwa wa kuchangia athari mbaya ya kimwili, unyanyasaji au ubaguzi dhidi ya watu wanaohusika na sifa iliyolindwa.”

Kwa kuwa haikuwa sehemu ya Kiwango cha Jumuiya wakati ambapo Facebook iliondoa maudhui haya, na Facebook haikupingana kuwa iliondoa maudhui hayo chini ya Kiwango hiki kilichosasishwa kwa Bodi, Bodi haikuchanganua matumizi ya sera hii kwa kesi hii. Hata hivyo, Bodi inadokeza kuwa “dhana, taasisi, mawazo, matendo, au imani” zinaweza kusimamia masafa mapana ya kujieleza, ikijumuisha hotuba ya kisiasa.

8.2 Utiifu wa maadili ya Facebook

Bodi inahitimisha kuwa kurejesha maudhui haya kunapatana na imani za Facebook. Ijapokuwa kanuni za Facebook za “Heshima” na “Usalama” ni muhimu, hasa katika muktadha wa mapinduzi ya Februari 2021 katika Myanmar, maudhui haya hayakuweka hatari kwa kanuni hizi kuwa ingeweza kuonyesha kuondoa “Sauti”. Bodi pia iligundua kuwa chapisho hilo lina usemi wa kisiasa ambao ni wa kati kwa thamani ya “Sauti”.

8.3 Utiifu wa wajibu wa haki za binadamu wa Facebook

Bodi inahitimisha kuwa kurejesha maudhui kunaendana na majukumu ya haki za kibinadamu za Facebook kama biashara. Facebook imejitolea kuheshimu haki za kibinadamu chini ya Kanuni Zinazoongoza Kanuni za Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na Haki za Kibinadamu. (UNGP). Sera yake ya Haki za Kibinadamu za Shirika inasema kuwa hii inajumuisha Agano la Kimataifa kuhusu Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR).

Kifungu cha 19 cha ICCPR kinatoa nafasi ya ulinzi pana wa kujieleza. Ulinzi huu “hasa uko juu” kwa usemi na mjadala wa kisiasa, ikijumuisha kuhusu taasisi za umma (Maoni ya Jumla ya 34, aya ya 38). Kifungu cha 19 kinahitaji vizuizi vya taifa kuhusu usemi ili kuridhisha kipimo cha sehemu tatu cha uhalali, ustahiki, na umuhimu na usawa. Bodi inahitimisha kuwa hatua za Facebook hazikuridhisha majukumu yake kama biashara chini ya kipimo hiki.

I. Kutii sheria (uwazi na upatikanaji wa sheria)

Kanuni ya kutii sheria chini ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu inahitaji kanuni zinazotumika na majimbo kubana usemi ili uwe unaoeleweka na unaoweza kufikiwa ( Maoni ya Jumla ya 34,, aya ya 25). Kanuni zinazobana kujieleza lazima pia “zitoe mwongozo wa kutosha kwa waliohukumiwa na utekelezaji wao ili kuwawezesha kuwa na uhakika kuhusu aina za usemi zimewekewa kikomo vizuri na aina zisizo na kikomo” ( Maoni ya Jumla ya 34, aya ya 25).

Kiwango cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki kimepiga marufuku maneno machafu yanayolenga watu kutegemea uasili, kabila, au taifa la asili. Facebook iliambia Bodi hiyo kwa sababu ya ugumu katika “kugundua lengo kwa kipimo, Facebook inazingatia kirai cha ‘fucking Chinese’ kama inayorejelea watu wa China na nchi au serikali ya China, isipokuwa mtumiaji akitoa muktadha zaidi kwamba inarejelea nchi au serikali pekee.” Kanuni ya kukosa dhidi ya kuondolewa haijatajwa katika Kiwango cha Jumuiya.

Bodi inahitimisha kuwa mtumiaji alitoa muktadha zaidi kwamba chapisho hilo lilirejelea jimbo au nchi, ilivyodokezwa katika uchanganuzi wa Bodi wa Viwango vya Jumuiya vya Matamshi ya Chuki (Kitengo cha 8.1 hapo juu). Wakaguzi anuwai wa Facebook walifikia hitimisho tofauti kando na watafsiri wa Bodi, watu waliowasilisha maoni ya umma, na huenda wengi kati ya watumiaji hao zaidi ya 500,000 waliotazama chapisho hilo na hawakuliripoti. Kwa sababu ya utofauti huu, Bodi inauliza maswali kuhusu utoshelevu wa mwongozo wa ndani wa Facebook, rasilimali na mafunzo yanayotolewa kwa wapatanishi wa maudhui.

Kwa sababu ya Bodi kupata kuwa mtumiaji hakukiuka sera ya Facebook ya Matamshi ya chuki, Bodi haiamui kama sera isiyo ya umma ya kukataa kuondolewa kunakiuka kanuni ya uhalali. Hata hivyo, Bodi ina wasiwasi kuwa sera ya kukataa kuondolewa wakati maneno machafu yanaweza kufasiriwa ilivyoelekezwa ama kwa watu au kwa jimbo haiko wazi kutoka kwa Viwango vya Jumuiya. Kwa jumla, Facebook inafaa kufanya mwongozo wa ndani wa umma ambao hubadilisha ufasiri wa Viwango vyake vya Jumuiya vinavyoegemea umma.

II. Lengo halali

Uzuiaji wowote wa jimbo kuhusu usemi unafaa kufuatilia mojawapo ya malengo halali yaliyoorodheshwa katika ICCPR. Hii inajumuisha “haki za wengine.” Kwa mujibu wa Facebook, sera yake ya Matamshi ya Chuki inalenga kuwalinda watumiaji dhidi ya ubaguzi. Bodi inakubali kuwa hii ni lengo halali.

III. Umuhimu na uwiano

Kanuni ya umuhimu na uwiano chini ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu inahitaji kuwa vizuizi vya usemi “lazima viwe vinafaa ili kufanikisha kazi yao ya ulinzi; lazima viwe ni vyombo vya ukali wa chini zaidi kati ya vile vinavyoweza kufikia lengo lao la ulinzi; lazima viwe na uwiano na mapendeleo ya kulindwa" ( Maoni ya Jumla ya 34, aya ya 34). Katika kesi hii, kutegemea ufasiri wake wa maudhui, Bodi iliamua kuwa kuweka vikwazo kwenye chapisho hili kunaweza kufanikisha jukumu la ulinzi.

UNGP inasema kuwa biashara zinafaa kutenda ujanja unaofaa wa haki za kibinadamu unaoendelea ili kufikia athari za shughuli zao (UNGP 17) na kukiri kuwa hatari ya majeraha ya haki za kibinadamu yameimarishwa katika miktadha iliyoathiriwa na migogoro (UNGP 7). Kikundi cha Umoja wa Mataifa Kinachofanya Kazi kuhusu suala la haki za kibinadamu na mashirika ya miamala anuwai na biashara nyingine iligundua kuwa majukumu ya biashara yanafaa kuakisi uchangamano mkubwa na hatari ya madhara katika visa fulani ( A/75/212, aya za 41-49). Vile vile, ikiwa uamuzi 2021-001-FB-FBR Bodi ilipendekeza kuwa Facebook “ihakikishe utoshelevu wa rasilimali na tajiriba ya kutathmini hatari za maumivu kutoka kwa akaunti zenye ushawishi kote ulimwenguni,” kutambua kuwa Facebook inafaa kutenga umakinifu kwa maeneo yaliyo na hatari za juu.

Katika kesi hii, Bodi ilipata kuwa majukumu haya yaliyoimarishwa hayafai kusababisha uondoleaji wa chaguo-msingi, huku uwezekano uko juu katika kuacha maudhui hatari na kuondoa maudhui yanayoleta hatari kidogo au isiyokuwepo. Huku wasiwasi wa Facebook kuhusu matamshi ya chuki katika Myanmar una msingi mzuri, pia lazima ichukue utunzaji maalum wa kutotoa uhakiki na usemi wa kisiasa, katika hali hii kuunga mkono uongozi wa kidemokrasia.

Bodi ilitaja kuwa sera ya Facebook ya kudhania mapema kuhusu matamshi machafu yanayotaja taifa la asili (katika kesi hii “$တရုတ်”) inarejelea majimbo nawatu kunaweza kusababisha utekelezaji usio na usawa katika baadhi ya miktadha ya kiisimu, kama huu, ambapo neno moja linatumika kwa dhana zote mbili. Bodi ilidokeza kuwa athari ya uondoleaji huu ilienda zaidi ya kesi hiyo, huku Facebook ikionyesha kuwa ilitumika katika mafunzo ya kibainishi kama mfano wa maudhui yaliyokiuka Kiwango cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki.

Kwa sababu ya yaliyo hapo juu, viwango vya haki za kibinadamu kimataifa vinaunga mkono urejeshaji wa maudhui hayo kwenye Facebook.

9. Uamuzi wa Bodi ya usimamizi

Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa Facebook wa kuondoa maudhui na inataka kwamba maudhui hayo yarejeshwe. Facebook ina wajibu chini ya Mkataba wa Bodi wa kutumia uamuzi huu kwa maudhui sambamba, na inafaa kualamisha maudhui haya kama yasiyokiuka ikiwa yatatumika kwenye mafunzo ya kibainishi.

10. Pendekezo la sera

Facebook inafaa kuhakikisha kuwa Viwango vyake vya Ndani vya Utekelezwaji vinapatikana katika lugha ambapo wapatanishi wa maudhui wanakagulia maudhui hayo. Ikiwa ni muhimu kupatia kipaumbele, Facebook inafaa kulenga kwanza muktadha ambapo hatari za haki za binadamu ni hatari zaidi.

*Dokezo la kiutaratibu:

Maamuzi ya Bodi ya Usimamizi hutayarishwa na majopo ya Wanachama watano na kuidhinishwa na wengi wa wanachama wa Bodi. Maamuzi ya Bodi hayawakilishi maoni ya kibinafsi ya Wanachama wote.

Kwa uamuzi wa kesi hii, utafiti huru ulipangwa kwa niaba ya Bodi. Taasisi huru ya utafiti yenye makao yake makuu katika Chuo Kikuu cha Gothenburg na iliyotoa timu ya zaidi ya wanasayansi wa kijamii 50 kutoka mabara sita, pamoja na zaidi ya wataalamu 3,200 wa kila nchi kutoka kote ulimwenguni, walitoa ushauri wa kitaalamu kuhusu muktadha wa jamii na kisiasa na utamaduni. Kampuni ya Lionbridge Technologies, LLC, ambayo wataalamu wake wanajua lugha zaidi ya 350 na hufanya kazi kutoka miji 5,000 ulimwenguni kote, ilitoa utaalamu wa kiisimu.

Volver a Decisiones de casos y opiniones consultivas sobre políticas