Decisão de múltiplos casos

Mahojiano ya Mpatanishi wa Mateka wa Thai

Bodi ilikagua machapisho mawili ya Facebook yaliyo na sehemu mbili zinazokaribia kufanana za mahojiano ya video ya shirika la habari la Sky News na mpatanishi wa mateka wa Thai anayeeleza juhudi zake za kuachilia huru mateka waliozuiliwa na Hamas. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hizo, kampuni ilibatilisha maamuzi yake kwanza na ikarejesha kila moja ya machapisho hayo.

2 casos incluídos neste pacote

Anulado

FB-XO941WWQ

Kesi kuhuhu watu na mashirika hatari kwenye Facebook

Plataforma
Facebook
विषय
Matukio ya Habari,Vurugu,Vita & Mgogoro
Padrão
Watu na mashirika hatari
Localização
Israeli,Maeneo ya Palestina,Thailandi
Date
Publicado em 18 de Abril de 2024
Anulado

FB-U3Y5VV2E

Kesi kuhuhu watu na mashirika hatari kwenye Facebook

Plataforma
Facebook
विषय
Matukio ya Habari,Vurugu,Vita & Mgogoro
Padrão
Watu na mashirika hatari
Localização
Israeli,Maeneo ya Palestina,Thailandi
Date
Publicado em 18 de Abril de 2024

Huu ni uamuzi kwa ufupi.Uamuzi wa ufupi huchunguza kesi ambapo Meta imebatilisha uamuzi wake wa kwanza kuhusu kipande cha maudhui baada ya Bodi kupeleka kesi hiyo kwa kampuni na kujumuisha taarifa kuhusu makosa ambayo Meta imekiri. Huwa unaidhinisha na jopo la Wanachama wa Bodi, badala ya Bodi kamili, hauhusishi maoni ya umma na hayana thamani ya kutumika katika marejeleo ya Bodi. Maamuzi kwa ufupi huleta mabadiliko moja kwa moja kwenye maamuzi ya Meta, yakitoa uwazi kuhusu masahihisho haya, huku pia yakitambua maeneo ambayo Meta inaweza kuboresha utekelezaji wake.

Muhtasari

Bodi ilikagua machapisho mawili ya Facebook yaliyo na sehemu mbili zinazokaribia kufanana za mahojiano ya video ya shirika la habari la Sky News na mpatanishi wa mateka wa Thai anayeeleza juhudi zake za kuachilia huru mateka waliozuiliwa na Hamas. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hizo, kampuni ilibatilisha maamuzi yake kwanza na ikarejesha kila moja ya machapisho hayo.

Kuhusu Kesi hizi

Mnamo Desemba 2023, watumiaji wawili walikata rufaa dhidi ya maamuzi ya Meta ya kuondoa machapisho yako, kila mojawapo likiwa na klipu zinazokaribia kufanana za mahojiano yaliyopeperushwa na Sky News mnamo Novemba 2023. Video hii inaangazia mpatanishi kutoka Thailandi ambaye aliongoza timu isiyo rasmi ya wapatanishi na kusaidia katika kuachiliwa huru kwa raia ya Thai ambao walishikwa mateka na Hamas mnamo tarehe 7 Oktoba nchini Israeli.

Kwenye klipu hiyo, anayehojiwa anaeleza sehemu yake katika upatanisho. Anasema kuwa anaamini mateka hao wa Thailandi na mateka wote “walikuwa wanalindwa vyema” na Hamas kwa sababu wanafuata sheria ya Kiislamu na kwamba Hamas hawakuwa wameweka masharti yoyote ya kuachiliwa huru kwa mateka wa Thailandi.

Mpatanishi huyo, ambaye anahurumia hali ya Wapalestina, anataja miongo ya kile anachoeleza kuwa kukandamizwa kwa Wapalestina na Israeli katika Maeneo Wanapokaa. Anasisitiza kuwa Hamas ilikuwa “inalenga wanajeshi” na kusema kwamba Hamas ilikuwa na haki ya kushika watu mateka “ili kuwasaidia Wapalestina” na “kufanya ulimwengu kuangazia jinsi Israeli inavyoshughulikia Wapalestina.”

Kwenye rufaa yake kwa Bodi, watumiaji wote walisema kwamba walichapisha video hiyo ili kuangazia taarifa za mpatanishi wa Thailandi, lakini kwa sababu tofauti. Mtumiaji mmoja alisema kwamba nia yake ilikuwa ni kuangazia mahojiano ambayo “yanaonyesha Hamas kwa mtazamo wa usawa zaidi” hali inayokinzana na mitazamo ya kawaida ya “Mashine ya propaganda ya Magharibi.” Mtumiaji aliashiria kwenye makunuu kuwa mpatanishi anakataa kuendelea dhana hiyo na kuendelea kueleza kuwa chapisho lake lilikuwa limedhibitiwa awali kwa sababu maudhui yalitaja shirika mahususi la kisiasa. Kwenye chapisho la pili, mtumiaji, aliyechapisha video bila manukuu au maoni zaidi, alisema kwamba “alikuwa akisuta watu wanaoshiriki ambao wanadanganya na kufanya hila” katika kuunga mkono Hamas.

Meta awali iliondoa chapisho hilo kwenye Facebook, ikitaja sera yake dhidi ya Watu na Mashirika Hatari, ambayo chini yake, kampuni imekataza maudhui “yanayosifu,” “kuunga mkono pakubwa” au “kuwakilisha” watu na mashirika ambayo imebainisha kuwa ni hatari. Hata hivyo, sera hiyo inatambua kuwa “watumiaji wanaweza kushiriki maudhui yanayojumuisha marejeleo kwa mashirika na watu binafsi hatari katika muktadha wa mijadala ya kijamii na kisiasa. Hii inajumuisha kuripoti maudhui, kujadili bila upendeleo wowote au kushutumu mashirika na watu binafsi hatari au shughuli zao.

Baada ya Bodi kufahamisha Meta kuhusu kesi hii, kampuni hiyo ilibaini kuwa machapisho hayo “hayajumuishi manukuu yoyote yanayokukuza, kuunga mkono au kuwakilisha mtu au shirika hatari.” Isitoshe, video hiyo “awali ilishirikiwa na shirika la Sky News, na vituo vingine vya habari, kwenye Facebook… na [kwa hivyo] inapatikana chini ya upeo wake wa kuripoti habari.” Meta ilirejesha machapisho yote mawili.

Mamlaka na Upeo wa Bodi

Bodi ina mamlaka ya kukagua uamuzi wa Meta kufuatia rufaa kutoka kwa mtumiaji ambaye maudhui yake yaliondolewa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria ndogo za Kifungu cha 3, Sehemu ya 1).

Pale ambapo Meta inakiri kuwa ilikosea na ibatilishe uamuzi wake katika kesi inayoratibiwa kukaguliwa na Bodi, Bodi inaweza kuchagua kesi hiyo ili kuifanyia uamuzi kwa ufupi (Sheria ndogo Kifungu cha 2, Sehemu ya 2.1.3). Bodi hupitia uamuzi wa kwanza ili kuongeza uelewa wa mchakato wa uratibu wa maudhui, ili kupunguza makosa na kuongeza haki kwa watu wanaotumia Facebook na Instagram.

Umuhimu wa Kesi

Kesi hizi zinasisitiza hali ambayo imedumu ya utekelezaji kupita kiasi wa Viwango vya Jumiya kuhusu Watu na Mashirika Hatari vya kampuni hiyo, kama ilivyoangaziwa kwenye maamuzi ya awali na Bodi. Kuendelea kuwepo kwa makosa katika utekelezaji wa sera hii kunapungua ufikiaji wa mtumiaji wa uwezo wa kutoa maoni yasiyoegemea upande wowote, kuripoti habari na machapisho ya kulaani, hali inayohujumu uhuru wa kujieleza.

Katika uamuzi wa awali, Bodi ilihimiza Meta “ijumuishe data tondoti zaidi kuhusu viwango vya makosa kwenye Viwango vya Jumuiya kuhusu Watu na Mashirika Hatarikatika ripoti yake ya uwazi,” ( Kutengwa kwa Öcalan, pendekezo nambari 12), ambalo kampuni hiyo ilikataa kutekeleza baada ya tathmini ya uwezekano.

Zaidi ya hayo, Bodi imependekeza kujumuishwa kwa “vigezo na mifano ya kuonyesha kwenye sera ya Meta dhidi ya Viwango vya Jumuiya kuhusu Watu na Mashirika Hatari ili kuongeza uelewa wa vighairi, hususan kuhusu majadiliano yasiyoegemea upande wowote na kuripoti habari,” ili kutoa mwongozo mkubwa kwa wakaguzi binadamu ( Chapisho lililoshirikiwa la Al Jazeera, pendekezo nambari. 1). Pendekezo hili hususan ni muhimu kwa kuwa linahusiana na kuondolewa kwa chapisho la habari kuhusu tishio la vurugu kutoka Izz al-Din al Qassam, kitengo cha kijeshi cha kikundi cha Hamas cha Upalestina. Bodi pia imeshauri Meta “itathmini usahihi wa wakaguzi wanaotekeleza kighairi cha kuripoti habari ili kutambua matatizo ya kimfumo yanayosababisha makosa ya utekelezaji,” ( Kutajwa kwa neno Taliban katika Kuripoti Habari, pendekezo nambari 5). Ingawa Meta imeripoti utekelezaji kwenye mapendekezo yote mawili, katika Kutajwa kwa Taliban katika Kuripoti Habari, pendekezo nambari 5, hawajachapisha taarifa ya kuonyesha haya.

Bodi imependekezwa maboresho kwenye uratibu wa machapisho yaliyo na video, kwa kutoa mwito kwa kampuni kupitisha “mabadiliko ya mwongozo wa bidhaa na/au utendakazi yanayoruhusu ukaguzi wa usahihi zaidi wa video ndefu ,” ( Waziri Mkuu wa Kambodia, pendekezo nambari 5). Katika kujibu, Meta ilisema kwamba “ingeendelea kusisiitizia maboresho mpya kwa michakato ya ukaguzi wa video ndefu na metriki ya uundaji na tathmini” katika Sasisho la kila Robo la Robo ya 3 ya 2023 kwenye Bodi ya Usimamizi.

Bodi inaamini kwamba utekelezaji kamili wa mapendekezo haya unaweza kupunguza idadi ya makosa ya utekelezaji wa sera ya Meta dhidi ya Watu na Mashirika Hatari.

Uamuzi

Bodi imebatilisha maamuzi ya awali ya Meta wa kuondoa maudhui hayo. Bodi inatambua masahihisho ambayo Meta ilifanya kwenye kosa lake la kwanza baada ya Bodi kujulisha Meta kuhusu kesi hizo.

Voltar para Decisões de Casos e Pareceres Consultivos sobre Políticas