Anulado
Hotuba ya jenerali wa Brazil
22 de Junho de 2023
Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa kwanza wa Meta wa kuruhusu video ya Facebook inayoonyesha jenerali wa Brazil akiwaambia watu “kwenda kwenye Bunge la Kitaifa na Mahakama ya Juu.”
Muhtasari wa Kesi
Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa kwanza wa Meta wa kuruhusu video ya Facebook ambayo inaonyesha jenerali wa Brazili akiwaambia watu “waingie barabarani,” na “kwenda kwenye Bunge la Kitaifa na Mahakama ya Upeo.” Ingawa Bodi inakubali kwamba Meta ilianzisha tathmini na hatua kadhaa za kupunguza hatari wakati na baada ya uchaguzi, kwa kuzingatia hatari inayoweza kutokea kutokana na majukwaa yake kutumiwa kuchochea vurugu katika muktadha wa uchaguzi, Meta inapaswa kuendelea kuongeza juhudi zake za kuzuia, kupunguza na kushughulikia matokeo mabaya. Bodi inapendekeza kwamba Meta iunde mfumo wa kutathmini juhudi zake za uadilifu wa uchaguzi ili kuzuia majukwaa yake kutumika kuendeleza vurugu za kisiasa.
Kuhusu kesi hii
Uchaguzi wa urais wa Brazili mnamo Oktoba 2022 ulikuwa na mgawanyiko mkubwa, na madai yaliyoenea na kuratibiwa mtandaoni na nje ya mtandao yaliyotilia shaka uhalali wa uchaguzi. Yalijumuisha wito wa kuingilia jeshi kati, na kuvamia majengo ya serikali ili kusitisha mpito wa serikali mpya. Hatari iliyoongezeka ya vurugu za kisiasa haikupungua baada ya Rais mteule Luiz Inacio Lula da Silva kutwaa madaraka mnamo Januari 1, 2023, huku machafuko ya kiraia, maandamano na kupiga kambi mbele ya kambi za kijeshi zikiendelea.
Siku mbili baadaye, mnamo Januari 3, 2023, mtumiaji wa Facebook alichapisha video inayohusiana na uchaguzi wa 2022 wa Brazil. Manukuu yaliyoandikwa kwa Kireno yalijumuisha mwito wa “kuteka” Bunge la Brazili kama "njia mbadala ya mwisho.” Video hiyo pia inaonyesha sehemu ya hotuba iliyotolewa na jenerali maarufu wa Brazili anayeunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais wa zamani Jair Bolsonaro. Katika video hiyo, jenerali aliyevaa sare anatoa wito kwa watu “waingie barabarani” na “kwenda kwenye Bunge la Kitaifa ... [na] Mahakama ya Upeo.” Msururu wa picha zinafuata, ikijumuisha moja ya moto unaochoma jumba la The Three Powers Plaza jijini Brasília, linalositiri ofisi za rais, Bunge na Mahakama ya Upeo ya Brazil. Matini yanayolandana na picha hiyo yanasema, katika Kireno, “Come to Brasília! (Njoo Brasilia!) Lets Storm it! (Acha tuivamie) Let’s besiege the three powers.” (Hebu tuliteke nyara the three powers) Matini yaliyolandanishwa kwenye picha nyingine yanasema “we demand the source code,” (tunataka tupewe msimbo chanzi), kauli mbiu ambayo waandamanaji wametumia kukosoa mashine za upigaji kura kwa njia ya kielektroniki nchini Brazil.
Siku ambayo maudhui yalichapishwa, mtumiaji aliyaripoti kwa kukiuka Kiwango cha Jumuiya kuhusu Vurugu na Uchochezi cha Meta, ambacho kinakataza wito wa kuingia kwa nguvu katika maeneo yenye hatari kubwa. Kwa jumla, watumiaji wanne waliripoti maudhui hayo mara saba kati ya Januari 3 na 4. Kufuatia ripoti ya kwanza, maudhui hayo yalikaguliwa na wakaguzi wa maudhui na kupata kwamba hayakiuki sera za Meta. Mtumiaji huyo alikata rufaa dhidi ya uamuzi huo, lakini uamuzi huo ukaungwa mkono na mkaguzi wa pili wa maudhui. Siku iliyofuata, ripoti zingine sita zilikaguliwa na wakaguzi watano tofauti, wote walipata kwamba maudhui hayo hayakukiuka sera za Meta.
Mnamo Januari 8, wafuasi wa rais wa zamani Bolsonaro walivamia Bunge la Kitaifa, Mahakama ya Upeo na ofisi za rais ziliopo katika “Three Powers Plaza” huko Brasilia, wakiwatishia polisi na kuharibu mali. Mnamo Januari 9, Meta ilitangaza ghasia za Januari 8 kuwa “tukio la ukiukaji” chini ya sera yake ya Watu Mashirika Hatari na ikasema itaondoa “maudhui ambayo yanaunga mkono au kusifu vitendo hivi.” Kampuni hiyo pia ilitangaza kuwa “imebainisha Brazil kama Eneo Lenye Hatari Kubwa kwa Muda” na “imekuwa ikiondoa maudhui yanayowataka watu kuchukua silaha au kuvamia kwa nguvu Bunge, Ikulu ya Rais na majengo mengine ya serikali.”
Kutokana na hatua ya Bodi kuchagua kesi hii, Meta ilibaini kwamba uamuzi wake wa kujirudia wa kuacha maudhui hayo kwenye Facebook ulifanywa kimakosa. Mnamo Januari 20, 2023, baada ya Bodi kuorodhesha kesi hii, Meta iliondoa maudhui.
Matokeo muhimu
Kesi hii inazua hoja kuhusu ufanisi wa juhudi za uadilifu wa uchaguzi wa Meta katika muktadha wa Uchaguzi Mkuu wa Brazil wa 2022, na kwingineko. Ingawa kupinga uadilifu wa uchaguzi kwa ujumla huchukuliwa kuwa ni hotuba iliyolindwa, katika hali fulani, madai yaliyoenea ambayo yanajaribu kuhujumu uchaguzi yanaweza kusababisha vurugu. Katika kesi hii, dhamira ya mzungumzaji, maudhui ya hotuba na ufikiaji wake, na pia uwezekano wa madhara yanayoweza kutokea kutokana na muktadha wa kisiasa wa Brazili wakati huo, yote yalitoa sababu ya kuondolewa kwa chapisho hilo.
Ili chapisho likiuke sheria za Meta za kuwataka watu waingie kwa nguvu katika maeneo yenye hatari kubwa, ni lazima eneo hilo lichukuliwe kuwa lenye “hatari kubwa,” na ni lazima liwe katika eneo ambalo limebainishwa kivyake kama “eneo lenye hatari kubwa kwa muda.” Kwa vile chapisho hilo lilikuwa wito usio na utata wa kuingia kwa nguvu katika majengo ya serikali yaliyo katika Three Powers Plaza huko Brasília (“maeneo yenye hatari kubwa” yaliyo katika “eneo lenye hatari kubwa kwa muda,” huko Brazil), maamuzi ya kwanza ya Meta ya kuruhusu maudhui haya wakati wa ghasia za kisiasa zilizokithiri yalionyesha ukiukaji wazi wa sheria zake.
Bodi ina wasiwasi mkubwa kwamba licha ya machafuko ya kiraia nchini Brazili wakati maudhui hayo yalichapishwa, na kuenea kwa maudhui sawa na hayo katika wiki na miezi kabla ya ghasia za Januari 8, wasimamizi wa maudhui wa Meta walikagua mara kwa mara maudhui haya na wakabaini kuwa hayakiuki na wakashindwa kuyatuma ili kufanyiwa ukaguzi zaidi. Zaidi ya hayo, Bodi ilipouliza Meta taarifa kuhusu madai mahususi yanayohusiana na uchaguzi kwenye majukwaa yake kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa Brazil, kampuni hiyo ilisema kuwa haina data kuhusu kuenea kwa madai hayo. Maudhui katika kesi hii hatimaye yaliondolewa zaidi ya wiki mbili baadaye, ambapo tukio la ukiukaji lilikuwa tayari limetokea, na baada tu ya Bodi kuleta kesi hiyo kwa Meta.
Katika kujibu swali kutoka kwa Bodi, Meta ilisema kuwa haitumii metriki maalum kupima ufanisi wa juhudi zake za uadilifu wa uchaguzi kwa ujumla. Kwa hivyo, Bodi inaona kwamba Meta inapaswa kuunda mfumo wa kutathmini juhudi za kampuni za uadilifu wa uchaguzi, na kwa ajili ya kuripoti kwa umma kuhusu mada hiyo. Hili linalenga kuipa kampuni data inayofaa ili kuboresha mfumo wake wa udhibiti wa maudhui kwa ujumla na kuamua jinsi ya kutumia rasilimali zake katika miktadha ya uchaguzi. Bila taarifa za aina hii, Bodi na umma haiwezi kutathmini ufanisi wa juhudi za Meta za uadilifu wa uchaguzi kwa upana zaidi.
Uamuzi wa Bodi ya Usimamizi
Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa awali wa Meta wa kuacha chapisho hilo.
Bodi pia inapendekeza kwamba Meta:
- Iunde mfumo wa kutathmini juhudi zake za uadilifu wa uchaguzi. Hii inajumuisha kuunda na kushiriki metriki kwa ajili ya ufanisi wa juhudi za uadilifu wa uchaguzi, pamoja na zinazohusiana na utekelezaji wa Meta wa sera zake za maudhui na mbinu yake ya kushughulikia matangazo.
- Ibainishe katika Kituo chake cha Uwazi kwamba, pamoja na Itifaki ya Sera ya Mgogoro, kampuni huendesha itifaki zingine katika jaribio lake la kuzuia na kushughulikia hatari inayoweza kutokana na madhara yanayotokea katika miktadha ya uchaguzi au matukio mengine yenye hatari ya juu.
* Mihtasari ya kesi hutoa maelezo mafupi ya kesi na haina thamani ya kurejelewa katika kesi za baadaye.
Uamuzi kamili wa kesi
1. Muhtasari wa uamuzi
Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa kwanza wa Meta wa kuruhusu video ya Facebook inayoonyesha jenerali wa Brazil akiwaambia watu “waingie barabarani,” na “kwenda kwenye Bunge la Kitaifa na Mahakama ya Upeo.” Wito huo ulifuatwa na picha ya Three Powers Plaza huko Brasília, ambako majengo hayo ya serikali yapo, yakiwa yamewaka moto, yenye maandishi ya juu yanayosema “Come to Brasília! (“Njoo Brasília!) Lets storm it! (Acha tuivamie) Let’s besiege the three powers.” (Hebu tuliteke nyara the three powers) Bodi inaona taarifa hizi kuwa wito wazi na usio na utata wa kuvamia na kuchukua udhibiti wa majengo haya katika muktadha wa wafuasi wa Bolsonaro wanaopinga matokeo ya uchaguzi na kutaka kuingilia jeshi kati ili kukomesha kipindi cha mpito cha serikali. Baada ya Bodi kuorodhesha chapisho hili ili likaguliwe, Meta ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na kuliondoa kwenye Facebook.
Kesi hii inazua hoja zaidi kuhusu ufanisi wa juhudi za uadilifu wa uchaguzi wa Meta katika muktadha wa Uchaguzi Mkuu wa Brazil wa 2022, na kwingineko. Kupinga uadilifu wa uchaguzi kwa ujumla huchukuliwa kuwa kama matamshi yaliyolindwa, lakini katika hali fulani, madai yaliyoenea mtandaoni na nje ya mtandao ya kujaribu kuhujumu uchaguzi, kama vile katika kesi hii, yanaweza kusababisha vurugu vya nje ya mtandao. Huko Brazil, kila ishara ya onyo ilikuwepo kwamba vurugu kama hiyo ingeweza kutokea. Ingawa Bodi inakubali kwamba Meta ilianzisha tathmini na hatua kadhaa za kupunguza hatari wakati na baada ya uchaguzi, kwa kuzingatia hatari inayoweza kutokea kutokana na majukwaa yake kutumiwa kuchochea vurugu katika muktadha wa uchaguzi, Meta inapaswa kuendelea kuongeza juhudi zake za kuzuia, kupunguza na kushughulikia matokeo mabaya. Awamu ya baada ya uchaguzi inapaswa kuangaziwa katika juhudi za Meta za uadilifu wa uchaguzi ili kushughulikia hatari ya vurugu katika muktadha wa mpito wa mamlaka.
Kwa hivyo Bodi inapendekeza kwamba Meta iunde mfumo wa kutathmini juhudi za kampuni za uadilifu wa uchaguzi, na kwa ajili ya kuripoti kwa umma kuhusu mada hiyo. Mfumo kama huo unapaswa kujumuisha metriki za ufanisi wa vipengele muhimu vya juhudi za Meta za uadilifu wa uchaguzi, kuruhusu kampuni sio tu kutambua na kurekebisha makosa, lakini pia kufuatilia jinsi hatua zake zinavyofaa katika hali mbaya. Bodi pia inapendekeza kwamba Meta itoe ufafanuzi kuhusu itifaki na hatua mbalimbali ilizo nazo za kuzuia na kushughulikia hatari inayoweza kutokea ya madhara katika miktadha ya uchaguzi na matukio mengine yenye hatari ya juu. Hii inajumuisha kutaja na kuelezea itifaki hizo, lengo lao, hatua za mawasiliano kati yao na jinsi zinavyotofautiana. Itifaki kama hizo zinahitaji kuwa na ufanisi zaidi, kuwa na mfuatilio wazi wa amri, na kuwa na wafanyikazi wa kutosha, haswa wakati wa kufanya kazi katika muktadha wa uchaguzi na hatari kubwa ya ghasia za kisiasa. Mapendekezo haya yanaweza kusaidia kuboresha mfumo wa kampuni wa udhibiti wa maudhui kwa ujumla kwa kuweka Meta katika nafasi nzuri ya kuzuia majukwaa yake yasitumike kuendeleza vurugu za kisiasa na kuboresha majibu yake kwa vurugu zinazohusiana na uchaguzi kwa ujumla zaidi.
2. Maelezo ya kesi na historia
Mnamo Januari 3, 2023, mtumiaji wa Facebook alichapisha video inayohusiana na uchaguzi wa 2022 wa Brazil. Manukuu yaliyoandikwa kwa Kireno yalijumuisha mwito wa “kuteka” Bunge la Brazili kama "njia mbadala ya mwisho.” Video hiyo ya dakika moja na sekunde 32 inaonyesha sehemu ya hotuba iliyotolewa na jenerali maarufu wa Brazil anayeunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais wa zamani Jair Bolsonaro. Katika video hiyo, jenerali aliyevaa sare anatoa wito kwa watu “waingie barabarani” na “kwenda kwenye Bunge la Kitaifa ... [na] Mahakama ya Upeo.” Msururu wa picha zinafuata, ikijumuisha moja ya moto unaochoma jumba la The Three Powers Plaza jijini Brasília, linalositiri ofisi za rais, Bunge na Mahakama ya Upeo ya Brazil. Matini yanayolandana na picha hiyo yanasema, katika Kireno, “Come to Brasília! (Njoo Brasilia!) Lets Storm it! (Acha tuivamie) Let’s besiege the three powers.” (Hebu tuliteke nyara the three powers) Matini yaliyolandanishwa kwenye picha nyingine yanasema “we demand the source code,” (tunataka tupewe msimbo chanzi), kauli mbiu ambayo waandamanaji wametumia kukosoa mashine za upigaji kura kwa njia ya kielektroniki nchini Brazil. Video hiyo ilichezwa zaidi ya mara 18,000 na haikushirikiwa.
Siku mbili kabla ya maudhui hayo kuchapishwa, mpinzani wa Bolsonaro katika uchaguzi Luiz Inácio Lula da Silva alikuwa ameapishwa kama rais wa Brazil baada ya kushinda uchaguzi uliorudiwa wa urais mnamo Oktoba 30, 2022 kwa asilimia 50.9 ya kura. Vipindi vya kabla, kati, na baada ya duru mbili za upigaji kura viliwekwa alama ya hatari kubwa ya vurugu za kisiasa, zilizochochewa na madai kuhusu udanganyifu wa uchaguzi unaokuja. Zilitokana na uwezekano wa mashine za kielektroniki za kupigia kura za Brazil kudukuliwa. Kabla ya uchaguzi huo, Rais wa wakati huo Bolsonaro alichochea ukosefu wa imani katika mfumo wa uchaguzi, akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu bila ushahidi wa kuunga mkono na kudai kwamba mashine za kielektroniki za kupigia kura sio za kutegemewa. Baadhi ya maafisa wa kijeshi waliunga mkono madai kama hayo ya udanganyifu katika uchaguzi na walizungumza wakisema wanapendelea kutumia jeshi kama mpatanishi katika mizozo ya uchaguzi. Matukio kadhaa ya matangazo ya kisiasa kushambulia uhalali wa uchaguzi kwenye majukwaa ya Meta yaliripotiwa. Yalijumuisha machapisho na video zinazoshambulia mamlaka ya mahakama na kuhamasisha mapinduzi ya kijeshi. Zaidi ya hayo, Global Witness ilichapisha ripoti kuhusu Brazil ikielezea jinsi matangazo ya kisiasa ambayo yalikiuka Viwango vya Jumuiya yalivyoidhinishwa na kampuni na kusambazwa kwenye majukwaa ya Meta. Matokeo hayo yalifuatilia ripoti kama hizo kutoka kwa shirika kuhusu nchi zingine kama vile Myanmar na Kenya.
Kipindi cha baada ya uchaguzi kiliambatana na machafuko ya kiraia, yakiwemo maandamano, vizuizi barabarani, na kupiga kambi mbele ya kambi za kijeshi ili kutoa wito kwa vikosi vya jeshi kutengua matokeo ya uchaguzi. Kulingana na wataalamu walioshauriwa na Bodi, video katika kesi hii ilionekana mtandaoni kwa mara ya kwanza mnamo Oktoba 2022, mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi kujulikana; maudhui kama hayo yalisalia kwenye majukwaa tofauti ya mitandao ya kijamii hadi kufikia ghasia za Januari 8. Mnamo Desemba 12, 2022, siku hiyohiyo ushindi wa Lula ulithibitishwa na Mahakama ya Juu ya Uchaguzi, kundi la waandamanaji wanaounga mkono Bolsonaro lilijaribu kuingia katika makao makuu ya Polisi ya Shirikisho huko Brasília. Matendo kadhaa ya uharibifu yalifanyika. Mnamo Desemba 24, 2022, kulikuwa na jaribio la kulipua bomu karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa nchi hiyo huko Brasília. Mtu aliyehusika na shambulio hilo alikamatwa na kukiri kwamba lengo lake lilikuwa kuvutia dhamira yao ya kupinga mapinduzi.
Hatari iliyoongezeka ya vurugu za kisiasa nchini Brazil haikupungua wakati rais mpya aliyechaguliwa alipoapishwa mnamo Januari 1, 2023. Kulingana na utafiti ulioidhinishwa na Bodi, madai ya uwongo kuhusu mashine za kupigia kura yalifikia kilele kwenye majukwaa ya Meta baada ya duru ya kwanza na ya pili ya upigaji kura, na tena katika wiki zilizofuata baada ya ushindi wa Lula. Zaidi ya hayo, katika siku zilizotangulia Januari 8, wafuasi wa Bolsonaro walitumia kauli mbiu kadhaa fiche kutangaza maandamano huko Brasília ambayo yalilenga sana majengo ya serikali. Mashirika mengi ya ugavi yalionekana kuwa yamefanikiwa kupitia vituo vya mawasiliano isipokuwa Facebook.
Mashirika ya kimataifa ya uchunguzi wa uchaguzi kama vile Organization of American States na Carter Center yaliripoti kwamba hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa udanganyifu na kwamba uchaguzi ulifanyika kwa njia huru na ya haki licha ya shinikizo za wapiga kura walio na msimamo mkali. Wizara ya Ulinzi ya Brazil pia ilichunguza rasmi uchaguzi na ikaripoti kwamba hakuna ushahidi wowote wa hitilafu au udanganyifu, ingawa baadaye ilitoa taarifa inayokinzana kwamba vikosi vya kijeshi “haviondoi uwezekano wa udanganyifu.” Huko Brazil, Wizara ya Ulinzi inasimamia kazi ya vikosi vya jeshi.
Mvutano ulifikia kilele mnamo Januari 8, wakati wafuasi wa Rais wa zamani Bolsonaro walivamia Bunge la Kitaifa, Mahakama ya Juu na ofisi za rais ziliopo katika “Three Powers Plaza” huko Brasilia zilizorejelewa katika maudhui ya kesi hiyo, wakiwatishia polisi na kuharibu mali. Takriban watu 1,400 walikamatwa kwa kushiriki katika ghasia hizo za Januari 8, huku takriban 600 wakiwa bado rumande.
Kufuatia matukio ya Januari 8, Umoja wa Mataifa ulilaani matumizi ya vurugu, ukisema kuwa huo ulikuwa ni “kilele cha upotoshaji unaoendelea wa ukweli na uchochezi wa vurugu na chuki kutoka kwa watendaji wa kisiasa, kijamii na kiuchumi ambao wamekuwa wakichochea hali ya kutoaminiana, migawanyiko, na uharibifu kwa kukataa matokeo ya uchaguzi wa kidemokrasia.” Ilirudia kusema imejitolea na ina imani katika taasisi za kidemokrasia za Brazil. Maoni ya umma na wataalamu walioshauriwa na Bodi walionyesha athari mbaya ambayo madai yaliyotilia shaka uadilifu wa mfumo wa uchaguzi wa Brazil yalikuwa nayo katika kuchochea mgawanyiko wa kisiasa na kuwezesha vurugu za kisiasa nje ya mtandao (Angalia maoni ya umma kutoka kwa Dangerous Speech Project [PC-11010], LARDEM - Clínica de Direitos Humanos da Pontifícia Universidade Católica do Paraná [PC-11011], Instituto Vero [PC-11015], ModeraLab [PC-11016], Campaign Legal Center [PC-11017], Center for Democracy & Technology [PC-11018], InternetLab [PC-11019], na Coalizão Direitos na Rede [PC-11020]).
Mnamo Januari 9, 2023, Meta ilitangaza ghasia za Januari 8 kuwa “tukio linalokiuka” chini ya sera ya Watu Mashirika Hatari na ikasema itaondoa “maudhui ambayo yanaunga mkono au kusifu vitendo hivi.” Kampuni hiyo pia ilitangaza kuwa “kabla ya uchunguzi” ilikuwa “imeteua Brazil kama Eneo Lenye Hatari Kubwa kwa Muda” na “imekuwa ikiondoa maudhui yanayowataka watu kuchukua silaha au kuvamia kwa nguvu Bunge, Ikulu ya Rais na majengo mengine ya serikali.”
Mnamo Januari 3, siku hiyohiyo ambayo maudhui hayo yalichapishwa, mtumiaji fulani aliyaripoti kwa kukiuka Viwango vya Jumuiya ya Meta kuhusu Vurugu na Uchochezi, ambavyo vimeharamisha miito ya “kuingia katika maeneo kwa nguvu . . .endapo kuna ishara za muda za ongezeko la hatari ya vurugu au madhara ya nje ya mtandao.” Kwa jumla, watumiaji wanne waliripoti maudhui hayo mara saba kati ya Januari 3 na 4. Kufuatia ripoti ya kwanza, maudhui hayo yalikaguliwa na mkaguzi binadamu na kupata kwamba hayakiuki sera za Meta. Mtumiaji huyo alikata rufaa dhidi ya uamuzi huo, lakini uamuzi huo ukaungwa mkono na mkaguzi wa pili binadamu. Siku iliyofuata, ripoti zingine sita zilikaguliwa na wakaguzi watano tofauti, wote walipata kwamba maudhui hayo hayakukiuka sera za Meta. Maudhui hayo hayakupendekezwa kwa wataalam wa maswala ya sera au mada kwa ukaguzi wa ziada. Katika kujibu swali la Bodi, Meta ilifafanua kuwa watu saba waliokagua maudhui hayo walikuwa wanaishi Ulaya. Kulingana na Meta, wote walikuwa wakizungumza Kireno kwa ufasaha na walikuwa na utaalam wa lugha na tamaduni wa kukagua maudhui ya Brazil.
Kutokana na hatua ya Bodi kuchagua kesi hii, Meta ilibaini kwamba uamuzi wake wa kujirudia wa kuacha maudhui hayo kwenye Facebook ulifanywa kimakosa. Mnamo Januari 20, 2023, baada ya Bodi kuorodhesha kesi, Meta iliondoa maudhui hayo, ikaweka onyo dhidi ya akaunti ya muundaji wa maudhui hayo na kuweka kikomo cha vipengele vya saa 24, hatua iliyomzuia kuunda maudhui mapya ndani ya kipindi hicho. Licha ya hatua ya Meta, uwasilishaji wa maoni ya umma wa kikundi cha kiraia cha Ekō kwa Bodi na ripoti zingine zilisisitiza kuwa maudhui sawa yalisalia kwenye Facebook hata baada ya kesi hii kuletwa kwa Meta na Bodi (PC-11000).
3. Mamlaka na upeo wa Bodi ya Usimamizi
Bodi ina mamlaka ya kukagua uamuzi wa Meta kufuatia rufaa kutoka kwa mtu ambaye aliripoti hapo awali maudhui ambayo yaliruhusiwa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria ndogo za Kifungu cha 3, Sehemu ya 1). Bodi inaweza kudumisha au kubatilisha uamuzi wa Meta (Kifungu cha 3, Sehemu ya 5 ya Mkataba), na kampuni itafuata uamuzi huu (Kifungu cha 4 cha Mkataba). Meta pia lazima itathmini uwezekano wa kutekeleza uamuzi wake kuhusiana na maudhui yanayofanana yaliyo katika muktadha tofauti (Kifungu cha 4 cha Mkataba). Uamuzi wa Facebook unaweza kujumuisha mapendekezo yasiyo ya kufunga ambayo Meta lazima iyajibu (Kifungu cha 3 cha Mkataba, Sehemu ya 4); Kifungu cha 4). Pale ambapo Meta inajitolea kushughulikia mapendekezo, Bodi hufuatilia utekelezaji wake.
Bodi inapochagua kesi kama hii, ambapo Meta inakubali baadaye kwamba ilifanya makosa, Bodi hukagua uamuzi wa kwanza, ili kusaidia kuongeza ufahamu wa vigezo vya sera na michakato ya udhibiti wa maudhui ambayo ilichangia hitilafu. Kisha Bodi hutaka kushughulikia masuala ambayo inabainisha na sera au michakato msingi ya Meta. Bodi pia inalenga kutoa mapendekezo kwa Meta ili kuboresha usahihi wa utekelezaji na kuwatendea watumiaji ipasavyo kutoka sasa.
4. Vyanzo vya mamlaka na mwongozo
Viwango vifuatavyo na kesi za awali zilikuwa msingi wa uchanganuzi wa Bodi katika kesi hii:
I. Maamuzi ya Bodi ya Usimamizi:
Maamuzi muhimu zaidi ya awali ya Bodi ya Usimamizi yanajumuisha:
- “ Kusimamishwa kwa Rais wa Zamani Trump” (uamuzi wa kesi 2021-001-FB-FBR): Bodi ilibainisha kuwa, katika miktadha ya uchaguzi, majukumu ya haki za binadamu ya Meta yanahitaji kuruhusu kujieleza kisiasa huku ikiepuka hatari kubwa kwa haki nyingine za binadamu.
- “Boti ya Myanmar” (uamuzi wa kesi 2021-007-FB-UA): Bodi ilionyesha umuhimu wa kulinda hotuba za kisiasa wakati wa migogoro ya kisiasa.
- “Shirika la Masuala ya Mawasiliano ya Tigray” (uamuzi wa kesi 2022-006-FB-MR): Bodi iliangazia wajibu wa Meta wa kuanzisha mfumo ulio na kanuni na uwazi wa kudhibiti maudhui katika maeneo yenye migogoro ili kupunguza hatari za majukwaa yake kutumiwa kuchochea vurugu.
- “Katuni ya Knin” (uamuzi wa kesi 2022-001-FB-UA): Bodi iliitaka Meta kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu jinsi maudhui yanavyokaguliwa na wataalam wa masuala.
II.Sera za maudhui za Meta:
Kiwango cha Jumuiya kuhusu Vurugu na Uchochezi
Chini ya Kiwango cha Jumuiya kuhusu Vurugu na Uchochezi, Meta haikubali “kauli ya lengo au utetezi, mwito wa kitendo, au kauli za kutamani makuu au za masharti za kuingia kwa nguvu kwenye maeneo (ikijumuisha lakini hakuna kikomo kwa maeneo ya kuabudu, vituo vya elimu, maeneo ya kura, au maeneo yanayotumika kuhesabu kura) ambapo kuna ishara za muda za hatari kubwa ya vurugu au madhara nje ya mtandao.” Mtazamo wa sera wa Kiwango hiki cha Jumuiya ni “kuzuia madhara yanayoweza kutokea nje ya mtandao ambayo yanaweza kuhusiana na maudhui” yanayoonekana kwenye mifumo ya Meta. Wakati huohuo, Meta inatambua kwamba “watu kwa kawaida wanaonyesha madharau au kutokubaliana kwa kutoa vitisho au kuita vurugu katika njia za kimzaha.” Kwa hivyo Meta huondoa maudhui wakati kampuni inaamini “kuna hatari halisi ya madhara ya kimwili au vitisho vya moja kwa moja kwa usalama wa umma.” Katika kubaini kama tishio ni la kuaminika, Meta pia huzingatia “lugha na muktadha.”
Uchanganuzi wa Bodi pia ulitokana na kujitolea kwa Meta kwa “Sauti,” ambayo kampuni inaeleza kuwa “muhimu,” na thamani yake ya “Usalama.”
III. Wajibu wa Meta wa Haki za Binadamu
Kanuni za Mwongozo wa Umoja wa Mataifa juu ya Biashara na Haki za Binadamu (UNGP), zilizoidhinishwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mnamo 2011, zina mfumo wa hiari wa majukumu ya haki za binadamu ya makampuni. Mnamo 2021, Meta ilitangazaSera yake ya Haki za Binadamu za Shirika, ambapo ilisisitiza tena kujitolea kwake katika kuwakilisha haki za kibinadamu kwa mujibu wa UNGP.
Kigezo ambacho Bodi ilitumia katika kuchambua wajibu wa Meta kwa haki za binadamu katika kesi hii kilitokana na viwango vifuatavyo vya kimataifa:
- Haki ya uhuru wa kuwa na maoni na kujieleza: Kifungu cha 19 na 20, Agano la Kimataifa kuhusu Haki za Raia na Kisiasa ( ICCPR), Maoni ya Jumla Nambari 34, Kamati ya Haki za Kibinadamu, 2011; Karatasi ya Utafiti 1/2019 kuhusu Uchaguzi katika Enzi ya Kidijitali (2019): Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa maoni na kujieleza, anaripoti: A/HRC/38/35 (2018) na A/74/486 (2019); Mpango wa Utekelezaji wa Rabat, ripoti ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu: A/HRC/22/17/Add.4 (2013).
- Haki ya kufanya mkutano kwa amani: Kifungu cha 21, ICCPR: Maoni ya Jumla Nambari 37, Kamati ya Haki za Binadamu, 2020.
- Haki ya kuishi: Kifungu cha 6, ICCPR.
- Haki ya kushiriki katika maswala ya umma na haki ya kupiga kura: Kifungu cha 25, ICCPR.
5. Mawasilisho ya mtumiaji
Katika rufaa yao kwa Bodi, mtumiaji aliyeripoti maudhui alisema kwamba “tayari wameripoti video hii na video zingine nyingi kwa Facebook na jibu huwa ni moja kila wakati, kwamba haikiuki Viwango vya Jumuiya.” Mtumiaji huyo alihusisha zaidi uwezekano wa maudhui hayo kuchochea vurugu na hatua zinazochukuliwa na watu nchini Brazil “ambao hawakubali matokeo ya uchaguzi.”
6. Mawasilisho ya Meta
Bodi ilipowasilisha kesi hii kwa Meta, kampuni ilibaini kuwa uamuzi wake wa kwanza wa kuruhusu maudhui haukuwa sahihi. Meta iliipa Bodi uchambuzi mpana wa muktadha wa kijamii na kisiasa wa Brazil kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa urais ili kuhalalisha - ingawa ilicheleweshwa – uondoaji wa maudhui katika kesi hii. Baadaye iliipatia Bodi sababu zinazowezekana ambazo “huenda zimechangia” kwa hitilafu inayoendelea ya utekelezaji.
Meta ilieleza mtazamo wake kwamba “marejeleo mengi ya 'kuzingira' maeneo yenye hatari kubwa katika manukuu na video hayaongezi moja kwa moja hadi kiwango cha 'kulazimisha kuingia' chini ya sera ya [Vurugu na Uchochezi].” Hata hivyo, “mseto wa kuwaita watu ‘Wakuje Brasília! Lets storm it! (Acha tuivamie) Let’s besiege the three powers (Acha tudhibiti mamlaka hizi tatu)’ pamoja na picha ya mandharinyuma ya Three Powers Plaza ikiwaka moto hufanya dhamira ya kuingia kwa nguvu katika maeneo haya maarufu kuwa wazi.”
Kulingana na Meta, maudhui hayo hayakufaulu kupata posho ya kustahiki kuwa ya habari ingawa ilikubali kuwa majukwaa yake ni “maeneo muhimu kwa mijadala ya kisiasa, haswa kuhusu uchaguzi.” Katika hali hii, thamani ya mapendeleo ya umma ya maudhui haikuzidi hatari ya madhara kutokana na “wito wake wazi wa vurugu” na “hatari iliyoongezeka ya madhara ya nje ya mtandao baada ya uchaguzi wa Rais wa Brazil na kuapishwa kwa Lula.” Meta haikupata dalili kwamba maudhui yalishirikiwa ili kushutumu au kuhamasisha kuhusu wito wa vurugu. Kampuni inashikilia kuwa uamuzi wake wa mwisho wa kuondoa maudhui unalingana na maadili yake na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.
Ili kushughulikia uchaguzi na hali zingine za mgogoro, Meta imeweka tathmini kadhaa za hatari na hatua za kupunguza ambazo zinaendeshwa na timu tofauti na zinaweza kutumika kwa wakati mmoja au kwa kujitegemea. Kila moja ina "safu" au "viwango" tofauti kulingana na tathmini husika ya hatari:
- Sera ya Uwekaji Kipaumbele Uadilifu wa Nchi (yaani, mfumo wa kuweka viwango hatari), unaoendeshwa na timu ya bidhaa ndani ya Meta, hutoa mfumo wa kuweka kipaumbele uwekezaji wa rasilimali za bidhaa kwa muda mrefu. Ingawa Meta inaelezea mchakato huu kama usioshughulikia majanga ya muda mfupi, hutathmini nchi zote mara mbili kwa mwaka kwa hatari/tishio zinazojitokeza.
- Kituo cha Uendeshaji wa Bidhaa za Uadilifu (IPOCs), huleta pamoja timu shirikishi ya wataalamu wa masuala kutoka kwa kampuni ili “kujibu kwa wakati halisi matatizo na mienendo inayoweza kutokea.” IPOCs zimeundwa ili kutathmini kwa haraka seti kubwa ya masuala, kutambua hatari, na kuamua jinsi ya kukabiliana nayo katika muktadha wa mgogoro au hali ya hatari kubwa. IPOCs huitwa Vituo vya Uendeshaji Uchaguzi wakati zinalenga uchaguzi haswa.
- Vituo vya Uendeshaji wa Uchaguzi hutoa “ufuatiliaji kwa wakati halisi kuhusu masuala muhimu ya uchaguzi, kama vile jitihada za kuzuia watu kupiga kura, ongezeko la barua taka, uwezekano wa kuingiliwa na mataifa ya kigeni, au ripoti za maudhui ambayo yanakiuka sera za [Meta]”, na “kufuatilia utangazaji wa habari na shughuli zinazohusiana na uchaguzi katika mitandao mingine ya kijamii na vyombo vya habari vya zamani.” Vituo hivyo huipa Meta “mtazamo wa pamoja na husaidia kufuatilia maudhui ambayo yanaweza kuvuma” ili “kuharakisha” muda wa kampuni kukabiliana na vitisho hivi. Sehemu ya maandalizi ya Kituo cha Uendeshaji wa Uchaguzi inahusisha “mpango wa kina wa kuondoa vitisho vinavyoweza kutokea – kutoka kwa unyanyasaji hadi ugandamizaji wa mpiga kura – na kuunda mifumo na taratibu mapema ili kujibu kwa ufanisi.”
- Hatimaye, Itifaki ya Sera ya Mgogoro ni mfumo wa Meta uliotumiwa kutengeneza majibu mahususi ya sera kwa muda maalum kuhusu mgogoro unaojitokeza. Meta iliunda itifaki hii ili kushughulikia pendekezo la Bodi ya Usimamizi katika kesi ya kusimamishwa kwa akaunti ya Rais wa Zamani Trump. Chini ya itifaki hii, Meta huanzisha kategoria tatu za mgogoro, kulingana na ambayo kampuni inachukua seti fulani ya hatua ili kupunguza hatari. Mgogoro wa Kategoria ya 1, kwa mfano, huchochewa na “ongezeko la utekelezaji wa sheria au shughuli za kijeshi” au “uchaguzi uliopangwa wa hatari kubwa au tukio la ghafla.”
Kituo cha Uendeshaji wa Uchaguzi kilichoshughulikia uchaguzi mkuu wa 2022 wa Brazil ambacho kiliendeshwa katika vituo tofauti kuanzia Septemba hadi Novemba 2022, pamoja na wakati wa duru ya kwanza na ya pili ya uchaguzi. Hata hivyo, hakukuwa na Kituo cha Uendeshaji Uchaguzi (au IPOC) wakati maudhui yalipochapishwa tarehe 3 Januari 2023. Meta iliteua “machafuko ya baada ya uchaguzi” kuwa mgogoro chini ya Itifaki ya Sera ya Mgogoro ili kusaidia kampuni kutathmini njia bora ya kupunguza hatari za maudhui.
Katika kujibu swali kutoka kwa Bodi kuhusu mienendo ya kidijitali kwenye majukwaa ya Meta kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa Brazil, kampuni hiyo ilisema kuwa kama sehemu ya “kazi yake ya maandalizi na majibu ya uchaguzi, timu kadhaa zilitambua mienendo ya maudhui yanayohusiana na uchaguzi na ikajumuisha katika mkakati [wao] wa kupunguza hatari.” Yalijumuisha: “(i) hatari zinazohusiana na uchochezi au uenezi wa vitisho vya vurugu; (ii) taarifa isiyofaa; na (iii) uadilifu wa biashara, unaojumuisha hatari zinazohusiana na matumizi mabaya ya tangazo yenye maudhui hatari... au majaribio ya kufanya kampeni kwa njia zinazoongoza au kupotosha mijadala ya umma.” Meta ilisema kuwa “matokeo, miongoni mwa mambo mengine, yalisaidia kufahamisha idadi kadhaa ya kupunguza bidhaa na sera.” Hata hivyo, Meta haina “data ya makadirio ya kipimo” kuhusu madai mahususi (k.m. ya ulaghai katika uchaguzi, wito wa kwenda Brasília au kuvamia majengo ya serikali ya shirikisho kwa lazima, wito wa kuingilia jeshi kati), kwa sababu kwa ujumla, mifumo ya utekelezaji ya kampuni “umeanzishwa kufuatilia kwa kuzingatia sera wanazokiuka.”
Bodi iliuliza Meta maswali 15 kwa maandishi, yakiwemo 5 ya kufuatilia jinsi Vituo vya Uendeshaji wa Uchaguzi hufanya kazi. Maswali yanayohusiana na: viwango vya sera vinavyopatikana vya kushughulikia tabia iliyoratibiwa kwenye mifumo ya Meta; hatari zilizotambuliwa kabla ya uchaguzi wa 2022 wa Brazil; uhusiano kati ya Kituo cha Uendeshaji wa Uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa Brazil na Itifaki ya Sera ya Mgogoro; jinsi Meta huweka vizuizi wakati inatofautisha kati ya upangaji halali wa kisiasa na hatua hatari zilizoratibiwa; mitindo ya kidijitali kwenye mifumo ya Meta nchini Brazil kabla, wakati na baada ya uchaguzi; na uwezo wa lugha wa wasimamizi wa maudhui ambao walikagua maudhui ya kesi.
Meta ilijibu maswali 13. Meta haikujibu maswali mawili, moja lililohusu uhusiano kati ya matangazo ya kisiasa na taarifa isiyofaa, na lingine lililohusu idadi ya uondoaji wa kurasa na akaunti wakati Kituo cha Uendeshaji wa Uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa 2022 Brazil kilikuwa kimefunguliwa. Meta pia ilifahamisha Bodi kuwa kampuni haikuwa na data zaidi ya jumla kuhusu udhibiti wa maudhui katika muktadha wa uchaguzi wa Brazil wa 2022 inayoweza kushirikiwa na Bodi, pamoja na idadi ya uondoaji wa maudhui ambayo tayari yalishirikiwa hadharani. Meta ilieleza zaidi kuwa kampuni hiyo haitathmini utendakazi wake katika muktadha wa uchaguzi dhidi ya seti fulani ya vipimo vya mafanikio na vigezo. Meta iliibua hitaji la kuweka kutanguliza rasilimali wakati wa kujibu maswali ya Bodi, na kusema kuwa itakuwa vigumu kutoa data iliyoombwa ndani ya muda wa kufanya maamuzi ya kesi.
7. Maoni ya umma
Bodi ya Usimamizi ilipokea maoni 18 ya umma yanayohusiana na kesi hii. Maoni kumi na moja kati ya hayo yalitoka Amerika ya Kusini na Karibea, matatu kutoka Marekani na Kanada, mawili kutoka Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, moja kutoka Asia Pacific na Oceania, na moja kutoka Asia ya Kati na Kusini. Zaidi ya hayo, mnamo Februari 2023, Bodi ilipanga mkutano na washikadau kutoka Brazil na Amerika ya Kusini kuhusu mada ya “Udhibiti wa Maudhui na Mipito ya Kisiasa.”
Mawasilisho hayo yalihusu mada zifuatazo: mkusanyiko wa madai yenye madhara kuhusu ulaghai wa uchaguzi na wito wa mapinduzi ya kijeshi kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa Brazil wa 2022; taarifa zisizofaa kuhusu uchaguzi; Juhudi za uadilifu wa uchaguzi wa Meta; Wajibu wa Meta wa kulinda haki za watumiaji katika muktadha wa mpito wa madaraka kidemokrasia; uhusiano kati ya kukataa uchaguzi na vurugu za kisiasa; na umuhimu wa wakaguzi wa maudhui kufahamu muktadha wa kisiasa wa eneo husika.
Ili kusoma maoni ya umma yaliyowasilishwa kuhusu kesi hii, tafadhali bofya hapa.
8. Uchambuzi wa Bodi ya Usimamizi
Bodi ilichunguza ikiwa maudhui haya yanafaa kuondolewa kwa kuchanganua sera za maudhui ya Meta, wajibu, na maadili ya haki za binadamu. Kesi hii ilichaguliwa kwa sababu inaruhusu Bodi kutathmini jinsi Meta inavyotofautisha mpangilio wa amani kwenye majukwaa yake na uchochezi au upangaji wa vitendo vya vurugu, hasa katika muktadha wa mpito wa mamlaka. Zaidi ya hayo, kesi hiyo inaruhusu Bodi kuchunguza juhudi za Meta za uadilifu wa uchaguzi kwa ujumla zaidi, na hasa nchini Brazil, ikizingatiwa kuwa muda wa baada ya uchaguzi ni wakati muhimu sana wa kupinga uadilifu wa uchaguzi na kuhakikisha kwamba matokeo halali ya uchaguzi yanaheshimiwa. Kwa hivyo, Bodi inaona kwamba juhudi za uadilifu za uchaguzi za Meta zinapaswa kuhusisha mchakato wenyewe wa uchaguzi na kipindi cha baada ya uchaguzi, kwa kuwa kipindi hicho cha baadaye pia kinaweza kuathiriwa na udanganyifu, taarifa zisizofaa zinazohusiana na uchaguzi na vitisho vya vurugu. Kesi hii ni miongoni mwa kesi ambazo Bodi imezipa kipaumbele cha kimkakati chini ya “nafasi ya Uchaguzi na urais”.
8.1 Utiifu wa sera za maudhui za Meta
I. Kanuni za maudhui
Vurugu na Uchochezi
Bodi imegundua kuwa maudhui katika kesi hii yanakiuka uzuizi wa Kiwango cha Jumuiya kuhusu Vurugu na Uchochezi kwa maudhui yanayoitaka watu kuingia kwa lazima katika maeneo fulani yenye hatari ya juu. Bodi imegundua kwamba ingawa thamani ya Meta ya “Sauti” inafaa hasa katika michakato ya uchaguzi, ikiwemo kipindi cha baada ya uchaguzi, kuondoa maudhui hayo ni muhimu katika kesi hii ili kuendeleza thamani ya Meta ya “Usalama.’
Ili kukiuka sera isiyokubali wito wa kuingia kwa nguvu katika maeneo yenye hatari kubwa, maeneo mawili yenye “hatari kubwa” yanahitajika. Kwanza, ni lazima eneo hilo lichukuliwe kuwa lenye “hatari kubwa,” na pili, lazima liwe katika eneo ambalo limeteuliwa kando kama “eneo lenye hatari kubwa kwa muda.” Maagizo mahususi ya Meta kwa wakaguzi wa maudhui ni “kutoa wito wa hatua, kauli za dhamira, kauli za utetezi, na kauli za matamanio ya kuingia kwa nguvu maeneo yenye hatari kubwa ndani ya Eneo Lenye Hatari Kubwa kwa Muda.”
Meta inafafanua "eneo lenye hatari kubwa" kama "eneo, la kudumu au la muda, ambalo linachukuliwa kuwa na hatari kubwa kwa sababu ya uwezekano wa kulengwa kufanya vurugu.” Maeneo ya kudumu yenye hatari kubwa yanajumuisha “maeneo ya kazi au makazi ya watu walio katika hatari kubwa au familia zao (kwa mfano, makao makuu ya shirika la habari, vituo vya matibabu, maabara, vituo vya polisi, ofisi za serikali, nk.); vituo vinavyotumika wakati wa uchaguzi wa ndani, kikanda, na kitaifa kama kituo cha kuandikisha wapiga kura, eneo la kupigia kura, kituo cha kuhesabia kura (kwa mfano maktaba ya eneo, jengo la serikali, kituo cha jamii au cha kiraia, n.k.) au kituo kinachotumika kusimamia uchaguzi. ” Kulingana na Meta, Bunge la Brazil, Mahakama Kuu na afisi za Rais zote ni “maeneo yenye hatari kubwa” ya kudumu kwa sababu ya kuwa sehemu za kazi au makazi ya watu walio katika hatari kubwa au familia zao.
Uteuzi wa ziada wa “Eneo Lenye Hatari Kubwa kwa Muda" wa eneo pana au eneo la karibu unajumuisha “eneo lolote ambalo limeteuliwa kwa muda na [Meta] kwa muda uliowekwa.” Eneo lililoteuliwa kuwa Eneo Lenye Hatari Kubwa kwa Muda kulingana na vipengele vingi, ikiwemo “ikiwa vurugu ya ubaya wa juu ilitokea wakati wa maandamano kwenye eneo hilo katika muda wa siku 7 zilizopita;” “ushahidi wa ongezeko la hatari ya unyanyasaji unaohusishwa na machafuko ya kiraia au uamuzi wa mahakama wenye utata katika eneo hilo;” “tathmini kutoka kwa watekelezaji wa sheria, ripoti za usalama wa ndani, au mshirika anayeaminika kwamba kuna uwezekano wa vurugu kutokea katika eneo hilo;” “ushahidi wa maandamano yaliyopangwa au yanayoendelea kwenye eneo hilo au maandamano yaliyopangwa au yanayoendelea kwenye eneo ambapo mratibu ametaka silaha zitumike au kuletwa katika eneo la maandamano;” na “tathmini iliyofanywa na timu za ndani kwamba masuala ya usalama yanazidi athari inayoweza kutokea kwenye usemi wa kujilinda na kujiamulia.” Baada ya Eneo Lenye Hatari Kubwa kubainishwa, jina uteuzi huo hushirikiwa na timu za ndani za Meta. Ingawa uteuzi kama huo una kikomo cha muda, kampuni hutoa viendelezi mara kwa mara. Kulingana na Meta, uteuzi wa Eneo Lenye Hatari Kubwa kwa Muda hufanya maudhui yakaguliwe kwa haraka “kabla ya watumiaji kuyaripoti.”
Kwa uchaguzi wa 2022, Meta iliteua nchi nzima ya Brazil kama Eneo Lenye Hatari Kubwa kwa Muda. Uteuzi huo ulianzishwa mnamo Septemba 1, 2022 kulingana na tathmini ya Meta ya ongezeko la hatari ya vurugu inayohusiana na machafuko yanayoendelea ya kiraia na yanayohusiana na uchaguzi. Uteuzi huo uliongezwa ili kujumuisha uchaguzi wa Oktoba 2022 na matokeo yake, hadi Februari 22, 2023. Uteuzi huo ulikuwepo wakati maudhui ya kesi yalipochapishwa.
Kulingana na Meta, lazima uteuzi wote ukuwepo ili kipande cha maudhui kukiuka sera, ambayo ndivyo ilivyokuwa kwa chapisho lililokuwa likichambuliwa. Kulingana na Meta, hitaji la vipengele viwili husaidia kuhakikisha kuwa wito wa maandamano haukandamizwi kwa upana na kwamba ni maudhui tu ambayo yanaweza kusababisha vurugu ndio yataondolewa.
Kwa kuzingatia yaliyo hapa juu, Bodi inachukulia maamuzi ya kwanza ya Meta kwamba maudhui yanapaswa kusalia kwenye jukwaa wakati wa hatari kubwa ya vurugu za kisiasa kama ukiukaji wazi wa kiwango chake, kwa sababu yalijumuisha wito usio na utata wa kuingia kwa nguvu katika majengo ya serikali yaliyo katika Three Powers Plaza huko Brasília, ambayo ni “maeneo yenye hatari kubwa” yaliyo katika “eneo lenye hatari kubwa kwa muda,” huko Brazil.
II. Hatua ya Utekelezaji
Kulingana na Meta, wasimamizi saba binadamu waliokuwa na utaalamu unaohitajika wa lugha na tamaduni walikagua maudhui. Meta haiwaelekezi wakaguzi wa kiwango kurekodi sababu zao za kufanya maamuzi. Bodi ilipochagua kesi hii, timu za ndani za Meta zilifanya uchanganuzi ambao ulihitimisha kuwa vipengele tatu vinavyowezekana “huenda vilichangia” kwa hitilafu inayoendelea ya utekelezaji: (1) huenda wakaguzi hawakuelewa dhamira ya mtumiaji (wito wa kuchukua hatua) labda kwa sababu ya ukosefu wa alama za uakifishaji uliosababisha maudhui kufasiriwa vibaya kama maoni yasiyokuwa na upendeleo kuhusu tukio; au (2) wakaguzi walifanya uamuzi usio sahihi licha ya kuwepo kwa miongozo sahihi kutokana na sasisho mengi kuhusu jinsi ya kushughulikia maudhui yanayohusiana na matukio yenye hatari kubwa kutoka vyanzo mbalimbali; au (3) huenda wakaguzi hawajaona ukiukaji katika video.
Vipengele vya 1 na 3 vipendekeza kuwa wasimamizi hawakukagua maudhui haya kwa makini wala kuitazama video kikamilifu, kwani uwezekano wa ukiukaji wa sera za Meta ulionekana wazi. Hata hivyo, Meta haitoi maelezo yoyote kuhusu kwa nini maudhui hayakutumwa kwa wataalamu wa sera kwa ajili ya uchanganuzi zaidi. Maudhui hayakukaguliwa licha ya ukweli kwamba yalitoka katika nchi ambayo, wakati maudhui yalipochapishwa na kuripotiwa, iliteuliwa kuwa “Eneo Lenye Hatari Kubwa kwa Muda” kutokana na sera ambayo hutumika tu wakati uteuzi huu umewekwa. Maudhui pia hayakukaguliwa licha ya muktadha wa jumla wa mtandaoni na nje ya mtandao nchini Brazil (Tazama Sehemu ya 2).
Tayari Meta iliiarifu Bodi kwamba kwa kawaida wakaguzi wa maudhui huwa hawawezi kutazama kikamilifu video. Hata hivyo, katika hali yenye hatari kubwa ya vurugu, ambapo vigezo mahususi vya sera vimewekwa, Bodi ingetarajia wakaguzi wa maudhui watazame video kikamilifu, pamoja na kukagua maudhui ambayo yanaweza kukiuka.
Kuhusiana na kipengele cha 2, ingawa Meta ilisema hufahamisha wakaguzi wa kiwango kuhusu uteuzi wa Eneo Lenye Hatari Kubwa kwa Muda, kampuni inakubali mapungufu yanayoweza kutokea katika ujumuishaji wake na hatua nyingine mahususi za kupunguza hatari za uchaguzi. Ujumuishaji wa taarifa za aina hii huwezesha wakaguzi wa maudhui kugundua, kuondoa au kukagua maudhui yenye matatizo kama vile video katika kesi hii. Ukweli kwamba hatua tofauti za tathmini na kupunguza zilikuwa zimewekwa nchini Brazili wakati huo unaonyesha kwamba zina uwezekano wa kuhitaji kuelezwa vyema na kuwa na mfuatilio wazi zaidi ili kufanya juhudi za kampuni hiyo za uadilifu wa uchaguzi kuwa na matokeo zaidi.
Licha ya uamuzi wa mwisho wa Meta kuondoa maudhui, bodi ina wasiwasi mkubwa kwamba hata kwa machafuko ya kiraia nchini Brazil wakati maudhui hayo yalichapishwa, na kuenea kwa maudhui sawa ya mtandaoni miezi na wiki kadhaa kabla ya ghasia za Januari 8, wasimamizi wa maudhui wa Meta walikagua mara kwa mara maudhui haya na wakabaini kuwa hayakiuki na wakashindwa kuyatuma ili kufanyiwa ukaguzi zaidi licha ya viashiria vya muktadha vilivyomo. Wasiwasi huu unachangiwa na ukweli kwamba Bodi ilipouliza Meta taarifa kuhusu madai mahususi yanayohusiana na uchaguzi kwenye majukwaa yake kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa Brazil, kampuni hiyo ilisema kuwa haina data kama hiyo ya makadirio ya kipimo (tazama Sehemu ya 6). Maudhui katika kesi hii hatimaye yaliondolewa zaidi ya wiki mbili baadaye, baada ya tukio la ukiukaji ambalo lilikuwa tayari limetokea, na baada tu ya Bodi kuleta kesi hiyo kwa Meta.
Meta ilikubali kuongezeka kwa hatari ya vurugu nchini Brazili, kwanza kwa kupitisha hatua mbalimbali za kutathmini hatari kabla, wakati na baada ya maudhui kuchapishwa, na pia moja kwa moja kwa Bodi wakati kampuni iliamua kuondoa maudhui hayo hatimaye. Hata hivyo, wakaguzi wa kampuni hiyo waliendelea kushindwa kutekeleza ipasavyo Viwango vyake vya Jumuiya, hasa sera yenyewe ya Kiwango cha Jumuiya kuhusu Vurugu na Uchochezi inayochochewa na uteuzi wa Eneo Lenye Hatari Kubwa kwa Muda. Ukweli kwamba maudhui hayakukaguliwa kabla ya uteuzi wa Bodi, licha ya uwazi wa ukiukaji unaoweza kutokea, na kwamba kulikuwa na maudhui sawa yaliyosambazwa kwenye Facebook wakati huo (Tazama Sehemu ya 2 na 8.2), inaonyesha huenda vituo vya ukaguzi visiwe wazi na vyenye ufanisi wa kutosha (Tazama kesi ya katuni ya Knin). Inaonyesha pia hitaji la Meta kuboresha ulinzi wake unaohusisha uchaguzi. Kama vile Bodi ilivyobaini katika maamuzi ya awali, ni muhimu kwa wakaguzi wa viwango kuwa na ujuzi wa kutosha wa lugha na muktadha na kupewa zana na vituo vinavyohitajika ili kukagua maudhui ambayo yanaweza kukiuka.
III. Uwazi
Bodi inatambua kuwa Meta ilifanya juhudi muhimu ili kulinda uadilifu wa uchaguzi wa 2022 nchini Brazil. Mnamo Agosti 2022, kipindi cha kampeni kilipoanza rasmi, Meta ilitangaza hadharani mipango yake inayohusiana na uchaguzi nchini. Kampuni hiyo ilishirikiana Mahakama ya Juu ya Uchaguzi ya Brazil kuongeza lebo kwenye machapisho yanayohusu uchaguzi kwenye Facebook na Instagram, “ikiwaelekeza watu kwenye taarifa za kuaminika kwenye tovuti ya Haki ya Uchaguzi.” Kulingana na Meta, hii ilisababisha “ongezeko la mara 10” katika ziara za tovuti. Ushirikiano pia uliruhusu Mahakama ya Juu ya Uchaguzi kuripoti maudhui yanayoweza kukiuka moja kwa moja kwenye Meta. Meta ilipanga vipindi vya mafunzo kwa maafisa wa uchaguzi kote nchini Brazili ili kueleza Viwango vya Jumuiya vya kampuni na jinsi taarifa isiyofaa kwenye Facebook na Instagram inavyoshughulikiwa. Meta pia ilipiga marufuku utangazaji unaolipishwa “unaotilia shaka uhalali wa uchaguzi ujao.” Zaidi ya hayo, kampuni iliweka kikomo kiwango cha usambazaji kwenye WhatsApp ili ujumbe usambazwe kwa kikundi kimoja cha WhatsApp kwa wakati mmoja. Hatimaye, Meta iliripoti idadi kadhaa ya vipande vya maudhui vilivyoondolewa chini ya Viwango mbalimbali vya Jumuiya, kama vile sera za Vurugu na Uchochezi, Matamshi ya Chuki, Dhuluma na Unyanyasaji, na jumla ya idadi ya mibofyo kwenye lebo za uchaguzi ambayo iliwaelekeza watumiaji kwenye taarifa halali kuhusu uchaguzi wa Brazil.
Hata hivyo, ilipoulizwa na Bodi kuhusu juhudi zake za uadilifu wa uchaguzi katika muktadha wa uchaguzi wa Brazil wa 2022, Meta ilisema kuwa kampuni haitumii metriki mahususi za kupima mafanikio ya juhudi zake za uadilifu wa uchaguzi kwa ujumla, zaidi ya kuripoti data kuhusu uondoaji wa maudhui, mionekano, na mibofyo kwa lebo za uchaguzi. Bodi pia inabainisha kuwa, kutokana na ufichuzi wa Meta katika Kituo chake cha Uwazi na mabadilishano na Bodi, haiko wazi kabisa jinsi hatua na itifaki tofauti za tathmini ya hatari huendeshwa (Tazama Sehemu ya 6 hapa juu), kwa kujitegemea au kwa usawa. Meta inapaswa kufafanua hatua za mawasiliano kati ya itifaki hizi tofauti, ieleze zaidi jinsi zinavyotofautiana na jinsi utekelezaji wa sera za maudhui unavyoathiriwa nazo.
Maoni kadhaa ya umma (Ekō [PC-11000], Dangerous Speech Project [PC-11010], ModeraLab [PC-11016], Campaign Legal Center [PC-11017], InternetLab [PC-11019], na Coalizão Direitos na Rede [PC-11020]) yaliyopokelewa na Bodi ilisema kuwa juhudi za kampuni hiyo kulinda uchaguzi nchini Brazil hazikutosha. Ingawa Bodi inakubali changamoto zinazojitokeza katika kudhibiti maudhui kwa kiwango, jukumu la Meta la kuzuia, kupunguza na kushughulikia athari mbaya za haki za binadamu linaongezeka katika miktadha ya uchaguzi na miktadha mingine yenye hatari kubwa, na inahitaji kampuni kuweka ulinzi bora dhidi yao. Hitilafu ya utekelezaji katika kesi hii haionekani kuwa tukio la pekee. Kulingana na Ekō (PC-11000), maudhui sawa yalisalia kwenye Facebook hata baada ya ghasia za Januari 8.
Uwazi zaidi unahitajika ili kutathmini ikiwa hatua za Meta zinatosha katika miktadha yote ya uchaguzi. Ukosefu wa data unaopatikana kwa Bodi kukagua ulidhoofisha uwezo wa Bodi wa kutathmini ipasavyo kama makosa ya utekelezaji katika kesi hii, na hoja zilizoibuliwa na washikadau tofauti, ni dalili ya suala la kimfumo katika sera na mazoea ya utekelezaji ya kampuni. Pia iliathiri uwezo wa Bodi wa kutoa mapendekezo mahususi zaidi kwa Meta kuhusu jinsi ya kuboresha zaidi juhudi zake za uadilifu wa uchaguzi duniani kote.
Ufichuzi wa data wa sasa wa Meta, hasa uondoaji wa maudhui, hautoi picha kamili ya matokeo ya hatua za uadilifu wa uchaguzi ambazo inaweka katika soko fulani. Kwa mfano, hazijumuishi usahihi wa utekelezaji unaohusiana na sera muhimu katika miktadha ya uchaguzi, kama vile Viwango vya Jumuiya kuhusu Vurugu na Uchochezi, wala asilimia ya matangazo ya kisiasa yaliyoidhinishwa awali na Meta lakini ikapatikana kuwa inakiuka sera zake. Kufanya ukaguzi wa takwimu kwa kutumia vipimo kama hivi kungeruhusu Meta sio tu kurekebisha makosa, lakini pia kufuatilia jinsi hatua zake vina ufanisi wakati kuipata kwa usahihi ni jambo la muhimu sana.
Bila taarifa za aina hii, Bodi na umma haiwezi kutathmini ufanisi wa juhudi za Meta za uadilifu wa uchaguzi kwa upana zaidi. Hili ni muhimu kwa kuzingatia kwamba matukio mengi ya vurugu za kisiasa mara nyingi hutokana na au kuchochewa na mizozo inayohusiana na uchaguzi, ambapo maudhui hatari yalisalia mtandaoni ili kutangulia au kuandamana na vurugu za nje ya mtandao (Tazama “Boti ya Myanmar” (2021-007-FB-UA), “ Shirika la Masuala ya Mawasiliano ya Tigray” (2022-006-FB-MR), na “ Kusimamishwa kwa Rais wa zamani Trump” (2021-001-FB-FBR)).
Kwa hivyo, Bodi inaona kwamba Meta inapaswa kuunda mfumo wa kutathmini juhudi za kampuni za uadilifu wa uchaguzi, na kwa ajili ya kuripoti kwa umma kuhusu mada hiyo. Hili linalenga kuipa kampuni data inayofaa ili kuboresha mfumo wake wa udhibiti wa maudhui kwa ujumla na kuamua jinsi ya kutumia vyema rasilimali zake katika miktadha ya uchaguzi. Inapaswa pia kusaidia Meta kutumia maarifa ya ndani kwa njia ifaayo na kutambua na kutathmini kampeni zilizoratibiwa za mtandaoni na nje ya mtandao zinazolenga kutatiza michakato ya kidemokrasia. Zaidi ya hayo, mfumo huu unapaswa kuwa wa manufaa kwa Meta kuanzisha vituo vya kudumu vya kutoa mlisho, na kuamua hatua za kuchukuliwa wakati vurugu za kisiasa zinaendelea baada ya michakato ya uchaguzi kukamilika rasmi. Hatimaye, Bodi inabainisha kuwa, kama ilivyoelezwa hapa juu, maelezo kati ya hatua na itifaki tofauti za tathmini ya hatari za Meta, kama vile IPOCs, sera ya Uwekaji Kipaumbele Uadilifu wa Nchi, na Itifaki ya Sera ya Mgogoro (Tazama Sehemu ya 6 hapa juu) katika muktadha unaohusiana na uchaguzi yanahitajika kukaguliwa na kufafanuliwa vyema kwa umma.
8.2 Utiifu wa wajibu wa haki za binadamu wa Meta
Uhuru wa kujieleza (Kifungu cha 19 ICCPR)
Haki ya uhuru wa kutoa maoni na kujieleza ni “nguzo kuu ya jamii za kidemokrasia, na mdhamini wa michakato ya uchaguzi yenye huru na ya haki, na mazungumzo ya umma na ya kisiasa yenye maana na uwakilishi” (Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza, Karatasi ya Utafiti 1/2019, uk. wa 2). Kifungu cha 19 cha ICCPR kinatoa nafasi ya ulinzi pana wa kujieleza, hasa kwa usemi wa kisiasa. Pale ambapo serikali imeweka vikwazo dhidi ya usemi, vikwazo hivyo lazima vitimize masharti ya kutii sheria, uhalali, umuhimu na ulinganifu (Kifungu cha 19, aya ya 3 ya ICCPR). Masharti haya mara nyingi huitwa “jaribio la sehemu tatu.” Halmashauri hutumia mfumo huu kutafsiri ahadi za hiari za haki za binadamu za Meta.
I. Kutii sheria (uwazi na upatikanaji wa sheria)
Kanuni ya kutii sheria chini ya sheria ya kimataifa kuhusu haki za kibinadamu inahitaji sheria zinazodhibiti kujieleza kuwa wazi na zinazoweza kufikiwa (Maoni ya Jumla Nambari 34, katika aya ya 25). Ilitumika kwa sheria za makampuni ya mitandao ya kijamii, Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza amesema zinapaswa kuwa wazi na mahususi ( A/HRC/38/35, aya ya 46). Watu wanaotumia majukwaa ya Meta wanapaswa kufikia na kuelewa sheria, na wakaguzi wa maudhui wanapaswa kuwa na mwongozo wazi kuhusu utekelezaji wao.
Bodi imeona kwamba, kama inavyotumika kwa ukweli wa kesi hii, katazo la Meta la maudhui inayotaka watu kuingia kwa nguvu katika maeneo fulani yenye hatari kubwa limebainishwa waziwazi, na hali halisi ambazo katazo hilo linatumika ziko wazi pia. Maudhui ya kesi yanaweza kueleweka kwa urahisi na mtumiaji na wakaguzi wa maudhui kuwa yanakiuka, hasa katika muktadha wa Brazil wa machafuko ya kiraia. Kwa hivyo, Bodi inazingatia matakwa ya kutii sheria kutimizwa.
II. Lengo halali
Vikwazo dhidi ya uhuru wa kujieleza (Kifungu cha 19, ICCPR) lazima vifuate lengo halali. Sera ya Vurugu na Uchochezi inalenga “kuzuia madhara yanayoweza kutokea nje ya mtandao” kwa kuondoa maudhui ambayo yanaleta “hatari halisi ya madhara ya kimwili au vitisho vya moja kwa moja kwa usalama wa umma.” Sera hii inatekeleza lengo halali la kulinda haki za wengine, kama vile haki ya maisha (Kifungu cha 6, ICCPR), pamoja na utulivu wa umma na usalama wa taifa (Kifungu cha 19, aya ya 3, ICCPR). Katika miktadha ya uchaguzi, sera hii pia inaweza kufuata lengo halali la kulinda haki ya wengine ya kupiga kura na kushiriki katika masuala ya umma (Kifungu cha 25, ICCPR).
III. Umuhimu na uwiano
Kanuni ya umuhimu na usawa inatoa vizuizi vyovyote vya uhuru wa kujieleza “lazima viwe vinafaa ili kufanikisha kazi yao ya ulinzi; lazima viwe ni vyombo vya ukali wa chini zaidi kati ya vile vinavyoweza kufikia lengo lao la ulinzi; [na] lazima viwe na usawa na mapendeleo ya kulindwa" ( Maoni ya Jumla Nambari 34, aya ya 33 na 34). Kama ilivyokuwa katika kesi za awali zinazohusisha uchochezi wa vurugu, Bodi hupata vipengele sita vya Mpango wa Utekelezaji wa Rabat wa Umoja wa Mataifa kuwa muhimu kubaini umuhimu na uwiano wa kizuizi (tazama, kwa mfano: Kesi ya kusimamishwa kwa Rais wa zamani Trump).
Bodi inatambua kwamba katika mazingira mengi ya kisiasa, kupinga uadilifu wa uchaguzi au mfumo wa uchaguzi ni utekelezaji halali wa haki za watu za uhuru wa kujieleza na kuandamana, hata kama kuna matukio ya vurugu pekee. Kwa sababu ya ujumbe wao wa kisiasa, wanafurahia kiwango cha juu cha ulinzi (Maoni ya Jumla Na. 37, aya ya 19 na 32). Bodi inabainisha, hata hivyo, kwamba sivyo ilivyo hapa. Kuna mstari muhimu unaotofautisha kati ya usemi wa kisiasa uliolindwa na uchochezi wa vurugu ili kubatilisha matokeo ya uchaguzi halali wa wananchi. Kulingana na vipengele vilivyoainishwa katika Mpango wa Utekelezaji wa Rabat, kigezo cha kizuizi cha usemi kilifikiwa wazi katika kesi hii. Bodi imegundua kuwa vipengele kadhaa katika maudhui ya kesi ni muhimu kwa uchanganuzi wake: wito wa “kuzingira” Bunge la Brazil kama “njia mbadala wa mwisho” na “kuvuruga” “three powers”; video iliyo na wito kutoka kwa jenerali maarufu wa Brazil “kuingia mtaani” na “kwenda kwa Bunge la Kitaifa … [na] Mahakama ya Juu; picha ya majengo ya serikali ya shirikisho yanayowaka moto katika mandharinyuma; na hitaji la “msimbo chanzo.” Vyote viko chini ya muktadha mpana wa Brazil wa wafuasi wa Bolsonaro wanaopinga matokeo ya uchaguzi na kuomba mapinduzi ya kijeshi, wito usio na utata wa kuvamia na kudhibiti majengo ya serikali. Dhamira ya mzungumzaji, maudhui ya usemi na ufikiaji wake, na pia uwezekano wa madhara yanayoweza kutokea kutokana na muktadha wa kisiasa wa Brazil wakati huo, yote yalihalalisha uondoaji wa chapisho hilo.
Maudhui hayo yalichapishwa katika muktadha wa hatari iliyoongezeka ya vurugu za kisiasa, huku wito ukienea kwa vikosi vya jeshi kutengua matokeo ya uchaguzi. Wakati huohuo, kauli mbiu fiche zilikuwa zikitumiwa kuendeleza maandamano yaliyolenga majengo ya serikali huko Brasília (Tazama Sehemu ya 2). Katika suala hili, taarifa ambazo Bodi ilipokea kupitia maoni kadhaa ya umma, ikijumuisha kutoka ITS Rio – Modera Lab (PC-11016), Coalizão Direitos na Rede (PC-11020), InternetLab (PC-11019), na Ekō (PC-11000), ambayo yaliunga mkono utafiti ulioidhinishwa na Bodi, yote yanaonyesha kuwa maudhui sawia yalikuwa yakisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii kabla ya matukio ya Januari 8. Pia yanasisitiza ukaribu wa wafuasi wa Bolsonaro kuvamia majengo katika Three Powers Plaza, na kuhamamisha jeshi kuingilia kati, ikiwemo kupitia mapinduzi ya kijeshi.
Kwa kuzingatia yaliyo hapa juu, Bodi inaona kwamba uondoaji wa maudhui unalingana na wajibu wake wa haki za binadamu. Kuondoa maudhui ni jibu la lazima na lenye uwiano ili kulinda haki ya maisha ya watu, wakiwemo maafisa wa umma, na utulivu wa umma nchini Brazil. Uondoaji wa sehemu hii ya maudhui na sawia pia ni muhimu na wenye uwiano ili kulinda haki ya wakaazi wa Brazil ya kupiga kura na kushiriki katika masuala ya umma, katika muktadha ambapo majaribio ya kuhujumu mabadiliko ya kidemokrasia ya mamlaka yalikuwa yakiendelea.
Mifumo ya ukaguzi ya Meta kuendelea kushindwa kubainisha ipasavyo ukiukaji katika video au kufanya ukaguzi zaidi na kuondoa maudhui ya kesi ni jambo la kutatanisha, ambalo Bodi inaamini kuwa Meta itakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kushughulikia iwapo kampuni itatekeleza mapendekezo yaliyo hapa chini. Ingawa Meta ilichukua hatua chanya ili kuboresha juhudi zake za uadilifu wa uchaguzi nchini Brazil, haijafanya vya kutosha kushughulikia matumizi mabaya yanayoweza kutokea ya majukwaa yake kupitia kampeni zilizoratibiwa za aina hiyo ambazo zimeonekana nchini Brazil. Katika kesi hii, maudhui ambayo yaliruhusiwa na kusambazwa sana yalionekana kuwa ya aina ya kawaida ya taarifa isiyofaa na ya uchochezi iliyoripotiwa kusambazwa kwenye majukwaa ya Meta nchini Brazil wakati huo. Inathibitisha zaidi madai kwamba akaunti zenye ushawishi zilizo na mamlaka makubwa ya uhamasishaji kwenye majukwaa ya Meta zilikuwa na jukumu la kukuza vurugu. Kama ilivyoonyeshwa kwenye maoni ya umma, Bodi ilipokea (Tazama, Instituto Vero [PC-11015], ModeraLab [PC-11016], InternetLab [PC-11019], Instituto de Referência em Internet e Sociedade [PC-11021]), ukaguzi huo na uwezekano wa uondoaji wa sehemu mahususi za maudhui kutoka kwa mifumo ya Meta haitoshi na haifai wakati maudhui kama hayo ni sehemu ya hatua iliyopangwa na iliyoratibiwa ambayo inalenga kutatiza michakato ya kidemokrasia. Juhudi za uadilifu wa uchaguzi na itifaki za mgogoro zinahitaji kushughulikia mienendo hii mipana ya kidijitali.
8.3 Maudhui yanayofanana yenye muktadha usiolingana
Bodi inaelezea wasiwasi wake kuhusu usambazaji wa maudhui sawa na yale yanayochanganuliwa katika miezi iliyotangulia ya ghasia za Januari 8 nchini Brazil. Kwa kuzingatia kuwa Meta imeshindwa mara kwa mara kubaini maudhui haya kuwa yanakiuka, Bodi itatilia maanani matumizi ya Meta ya uamuzi wake kwa maudhui yanayofanana na muktadha sawia ambao umebaki kwenye majukwaa ya kampuni, isipokuwa yanaposhirikiwa ili kulaani au kuongeza ufahamu kuhusu hotuba ya jenerali na wito wa kuvamia majengo ya Three Powers Plaza huko Brasília.
9. Uamuzi wa Bodi ya usimamizi
Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa awali wa Meta wa kuruhusu maudhui hayo.
10. Mapendekezo
A. Utekelezaji
- Meta inapaswa kuunda mfumo wa kutathmini juhudi za kampuni za uadilifu wa uchaguzi. Inajumuisha kuunda na kushiriki metriki kwa ajili ya ufanisi wa juhudi za uadilifu wa uchaguzi, pamoja na zinazohusiana na utekelezaji wa Meta wa sera zake za maudhui na mbinu ya kampuni ya kushughulikia matangazo. Bodi itazingatia kuwa pendekezo hili limetekelezwa wakati Meta itaunda mfumo huu (pamoja na maelezo ya vipimo na malengo ya vipimo hivyo), kulifichua katika Kituo cha Uwazi cha kampuni, ikianza kuchapisha ripoti mahususi za nchi, na kufichua hadharani mabadiliko yoyote ya juhudi zake za uadilifu wa uchaguzi mkuu kutokana na tathmini hii.
B. Uwazi
- Meta inapaswa kufafanua katika Kituo chake cha Uwazi kwamba, pamoja na Itifaki ya Sera ya Mgogoro, kampuni huendesha itifaki zingine katika jaribio lake la kuzuia na kushughulikia hatari inayoweza kutokana na madhara yanayotokea katika miktadha ya uchaguzi au matukio mengine yenye hatari ya juu. Pamoja na kutaja na kuelezea itifaki hizo, kampuni inapaswa pia kuelezea lengo lao, hatua za mawasiliano kati ya itifaki hizi tofauti, na jinsi zinavyotofautiana. Bodi itazingatia pendekezo hili limetekelezwa wakati Meta itachapisha taarifa hizi katika Kituo chake cha Uwazi.
* Dokezo la kiutaratibu:
Maamuzi ya Bodi ya Usimamizi yanatayarishwa na majopo ya Wanachama watano na kuidhinishwa na wengi wa wanachama wa Bodi. Maamuzi ya Bodi hayawakilishi maoni ya kibinafsi ya Wanachama wote.
Kwa uamuzi wa kesi hii, utafiti huru ulipangwa kwa niaba ya Bodi. Bodi ilisaidiwa na taasisi huru ya utafiti yenye makao yake makuu katika Chuo Kikuu cha Gothenburg ambayo inashirikisha timu ya zaidi ya wanasayansi wa kijamii 50 kutoka mabara sita, pamoja na zaidi ya wataalamu 3,200 wa kila nchi kutoka kote ulimwenguni. Bodi pia ilisaidiwa na Duco Advisors, shirika la ushauri linalolenga miingiliano ya siasa za ulimwengu, uaminifu na usalama na teknolojia. Memetica, shirika ambalo linajihusisha na utafiti wa chanzo huria kuhusu mienendo ya mitandao ya kijamii, pia ilitoa uchanganuzi. Utaalam wa lugha ulitolewa na Lionbridge Technologies, LLC, ambayo wataalamu wake wanajua lugha zaidi ya 350 na hufanya kazi kutoka miji 5,000 ulimwenguni kote.
Voltar para Decisões de Casos e Pareceres Consultivos sobre Políticas