Overturned

Hoteli nchini Ethiopia

Mtumiaji alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuruhusu chapisho la Facebook lililotaka hoteli moja katika eneo la Amhara nchini Ethiopia kuchomwa moto. Kesi hii inaangazia makosa ya Meta katika kutekeleza sera yake dhidi ya mwito wa ghasia katika nchi inayokumbwa na vita vya silaha na machafuko ya kiraia. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hiyo, kampuni hiyo ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na ikaondoa chapisho hilo.

Type of Decision

Summary

Policies and Topics

Topic
Violence, War and conflict
Community Standard
Violence and incitement

Region/Countries

Location
Ethiopia

Platform

Platform
Facebook

Huu ni uamuzi kwa ufupi.Uamuzi wa ufupi huchunguza kesi ambapo Meta ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza kuhusu kipande cha maudhui baada ya Bodi kupeleka kesi hiyo kwa kampuni. Uamuzi huu unajumuisha maelezo kuhusu makosa ambayo Meta ilikiri. Huidhinishwa na jopo la Wanachama wa Bodi, si Bodi kamili. Huwa hauzingatii maoni ya umma wala hauna thamani ya kutumiwa kama marejeleo kwa Bodi. Uamuzi kwa ufupi hutoa uwazi kuhusu masahihisho ya Meta na kuangazia maeneo ambayo kampuni inaweza kuboresha utekelezaji wa sera zake..

Muhtasari wa kesi

Mtumiaji alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuruhusu chapisho la Facebook lililotaka hoteli moja katika eneo la Amhara nchini Ethiopia kuchomwa moto. Kesi hii inaangazia makosa ya Meta katika kutekeleza sera yake dhidi ya mwito wa ghasia katika nchi inayokumbwa na vita vya silaha na machafuko ya kiraia. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hiyo, kampuni hiyo ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na ikaondoa chapisho hilo.

Maelezo na historia ya kesi

Mnamo Aprili 6, 2023, mtumiaji wa Facebook alichapisha picha na nuku lililotaka hoteli moja katika eneo la Amhara nchini Ethiopia kuchomwa moto. Mtumiaji huyo alidai kuwa hoteli hiyo inamilikiwa na jenerali wa Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Ethiopia. Chapisho hilo pia lilijumuisha picha ya hoteli hiyo, anwani yake na jina la jenerali.

Mtumiaji alichapisha maudhui haya wakati wa mvutano mkubwa wa kisiasa katika eneo la Amhara wakati maandamano yalikuwa yakifanyika kwa siku kadhaa ya kupinga mpango wa serikali wa kuondia kikosi cha kijeshi cha eneo hilo.

Chini ya sera ya Meta ya Vurugu na Uchochezi, kampuni hiyo huondoa maudhui ambayo yanatoa wito wa vurugu kali. Katika rufaa yao kwa Bodi, mtumiaji ambaye aliripoti maudhui alisema kuwa chapisho hilo linataka vurugu na linakiuka Viwango vya Jumuiya ya Meta.

Awali Meta iliacha maudhui hayo kwenye Facebook. Bodi ilipowasilisha kesi hii kwa Meta, iliamua kwamba chapisho hilo lilikiuka sera yake ya Vurugu na Uchochezi, na kwamba uamuzi wake wa awali wa kuruhusu maudhui haukuwa sahihi. Kampuni hiyo kisha iliondoa maudhui hayo kwenye Facebook.

Mamlaka na upeo wa Bodi

Bodi ina mamlaka ya kukagua uamuzi wa Meta kufuatia rufaa kutoka kwa mtumiaji ambaye maudhui yake yaliondolewa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria ndogo za Kifungu cha 3, Sehemu ya 1).

Pale ambapo Meta inakiri kwamba ilikosea na ibatilishe uamuzi wake katika kesi inayoshughulikiwa ili ikaguliwe na Bodi, Bodi inaweza kuchagua kesi hiyo ili kuifanyia uamuzi kwa ufupi (Sheria ndogo Kifungu cha 2, Sehemu ya 2.1.3). Bodi hupitia uamuzi wa kwanza ili kuongeza uelewa wa mchakato wa uratibu wa maudhui, ili kupunguza makosa na kuongeza haki kwa watu wanaotumia Facebook na Instagram.

Umuhimu wa kesi

Kesi hii inaangazia makosa ya Meta katika kutekeleza sera yake dhidi ya mwito wa ghasia katika nchi inayokumbwa na vita vya silaha na machafuko ya kiraia. Miito kama hiyo yai vurugu husababisha hatari kubwa ya vurugu za karibu na inaweza kuzidisha hali hiyo chinichini.inaweza kuzidisha hali hiyo kwenye ardhi. Ndio maana Bodi ilipendekeza Meta “itathmini uwezekano wa kuanzisha utaratibu endelevu wa ndani unaoipatia utaalamu, uwezo na uratibu unaohitajika ili kukagua na kujibu maudhui kwa ufanisi kwa muda wote wa mgogoro,” ( Shirika la Masuala ya Mawasiliano ya Tigray,pendekezo la nambari 2). Meta iko katika mchakato wa kuzindua timu ya uratibu wa janga ili kutoa uangalizi maalum wa shughuli katika mizozo inayokaribia na inayojitokeza. Bodi itaendelea kufuatilia utekelezaji wa utaratibu mpya pamoja na sera zilizopo, ili kuhakikisha Meta inawatendea watumiaji kwa haki zaidi katika maeneo yaliyoathirika.

Bodi pia ilipendekeza kwa ma Meta iidhinishe tathmini huru ya uchunguzi wa haki za binadamu kuhusu jinsi Facebook na Instagram zimetumiwa kueneza matamshi ya chuki na uvumi ambao haujathibitishwa unaoongeza hatari ya vurugu nchini Ethiopia na kuchapisha ripoti kikamiliful ( Watuhumiwa wa uhalifu huko Raya Kobo, pendekezo la nambari 3). Meta ilielezea pendekezo hili kama kazi ambayo tayari inafanya lakini haikuchapisha maelezo ili kuonyesha utekelezaji.

Uamuzi
Bodi imebatilisha uamuzi wa kwanza wa Meta wa kuruhusu maudhui hayo. Bodi inatambua masahihisho ambayo Meta ilifanya kwenye kosa la kwanza baada ya Bodi kujulisha Kampuni kuhusu kesi hiyo.

Return to Case Decisions and Policy Advisory Opinions