أسقط
Maoni ya Kudhalilisha Kuhusu Watu walioko Gaza
تم النشر بتاريخ 18 نَيْسان 2024
Mtumiaji alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuacha chapisho la Facebook lililodai kuwa Hamas ilitokana na watu wa Gaza na kuwalinganisha na “kundi la washenzi.” Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hiyo, kampuni hiyo ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na ikaondoa chapisho hilo.
Huu ni uamuzi kwa ufupi.Uamuzi wa ufupi huchunguza kesi ambapo Meta imebatilisha uamuzi wake wa kwanza kuhusu kipande cha maudhui baada ya Bodi kupeleka kesi hiyo kwa kampuni na kujumuisha taarifa kuhusu makosa ambayo Meta imekiri. Huwa unaidhinisha na jopo la Wanachama wa Bodi, badala ya Bodi kamili, hauhusishi maoni ya umma na hayana thamani ya kutumika katika marejeleo ya Bodi. Maamuzi kwa ufupi huleta mabadiliko moja kwa moja kwenye maamuzi ya Meta, yakitoa uwazi kuhusu masahihisho haya, huku pia yakitambua maeneo ambayo Meta inaweza kuboresha utekelezaji wake.
Muhtasari
Mtumiaji alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuacha chapisho la Facebook lililodai kuwa Hamas ilitokana na watu wa Gaza na inaonyesha “matamanio yao ya dhati zaidi,” kwa kuwalinganisha na “kundi la washenzi.” Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hiyo, kampuni hiyo ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na ikaondoa chapisho hilo.
Kuhusu Kesi
Mnamo Desemba 2023, mtumiaji alichapisha picha kwenye Facebook iliyo na maandishi, pamoja na picha ya mwanaume ambaye jina lake halijatajwa, linaloonyesha mtazamo kuwa “umma kwa jumla” katika ukanda wa Gaza si “waathiriwa” wa Hamas badala yake, kwamba kundi hilo la wanamgambo liliibuka kama “uakisi wa kweli” wa “matamanio ya dhati zaidi ya kundi la washenzi.” Picha hiyo iliyochapishwa upya ilikuwa na manukuu ya uidhinishaji yaliyojumuisha maneno, “ukweli.” Chapisho hilo lilitazamwa mara isiozidi 500.
Chini ya sera ya Meta dhidi ya Matamshi ya Chuki, Meta imepiga marufuku maudhui yanayolenga mtu au kikundi cha watu kwa msingi wa sifa zao zinazolindwa, hasa kutaja ulinganisho kwa “ubinadamu duni” na kujumuisha “ushenzi” kama mfano. Katika maudhui haya, kurejelea “umma ya jumla ya Gaza” ni rejeleo lisilo la moja kwa moja la Wapalestina walioko Gaza, hivyo kulenga sifa zinazolindwa za ukabila na uraia.
Katika taarifa ya kukata rufaa ya kesi hii kwa Bodi, mtumiaji alibainisha kuwa chapisho hilo “lilijumuisha kauli ya kudhalilisha,” kwa kutoa taarifa ya jumla kuhusu watu wa Gaza.
Baada ya Bodi kuwasilisha kesi hii kwa Meta, kampuni ilibaini kuwa maudhui hayo yalikiuka sera ya Meta dhidi ya Matamshi ya Chuki, na uamuzi wake wa awali wa kuruhusu maudhui haukuwa sahihi. Kampuni hiyo kisha iliondoa maudhui hayo kwenye Facebook.
Mamlaka na Upeo wa Bodi
Bodi ina mamlaka ya kukagua uamuzi wa Meta kufuatia rufaa kutoka kwa mtumiaji ambaye aliripoti maudhui ambayo yaliachwa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria ndogo za Kifungu cha 3, Sehemu ya 1).
Meta inapokiri kwamba ilikosea na ibatilishe uamuzi wake katika kesi inayoshughulikiwa ili ikaguliwe na Bodi, Bodi inaweza kuchagua kesi hiyo ili kuifanyia uamuzi kwa ufupi (Sheria ndogo Kifungu cha 2, Sehemu ya 2.1.3). Bodi hukagua uamuzi wa kwanza ili kuongeza ufahamu wa mchakato wa uratibu wa maudhui unaohusika, kupunguza makosa na kuongeza haki kwa watumiaji wa Facebook na Instagram.
Umuhimu wa Kesi
Kesi hii inaangazia makosa katika utekelezaji wa Meta wa sera yake dhidi ya Matamshi ya Chuki, hususan kuhusiana na maudhui yanayoshambulia watu kulingana na sifa zao zinazolindwa. Makosa ya uratibu huwa na madhara hasa katika nyakati ambapo mgogoro wa kivita unaendelea. Kwa hivyo, kunapaswa kuwekwa desturi pana za uratibu wa maudhui.
Kesi ya Katuni ya Knin pia ina matamshi ya chuki yanayolenga sifa iliyolindwa – kabila – kurejelea kundi moja la kikabila kama panya bila kuwataja moja kwa moja. Hata hivyo, kesi ya Katuni ya Knin ilihitaji muktadha wa kihistoria na kitamaduni ili kufasiri usawiri wa kundi la kikabila kwa njia ya ishara, ilhali maudhui katika kesi hii yanahusisha moja kwa moja maoni ya kudhalilisha zaidi kwa jamii nzima, jambo ambalo linapaswa kueleweka kama kurejelea watu kwa sifa iliyolindwa.
Katika uamuzi wa Katuni ya Knin, Bodi ilipendekeza kwamba, Meta inapaswa “kufafanua Kiwango cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki na mwongozo unaotolewa kwa wakaguzi, ikieleza kuwa hata marejeleo yasiyo wazi kwa vikundi vinavyolindwa hayaruhusiwi na sera wakati marejeleo yangeeleweka vizuri,” (uamuzi wa Katuni ya Knin, pendekezo nambari 1) ambao Meta imeripoti kutekeleza sehemu yake. Katika Robo ya 4 ya 2022, Meta iliripoti kwamba “waliongeza lugha kwenye Viwango vya Jumuiya na mwongozo wa sera ya wakaguzi na kueleza kwamba matamshi ya chuki yasiyo ya moja kwa moja yataondolewa ikiwa yatapendekezwa na wakaguzi wa maudhui mengine kwa wataalamu wa ukaguzi ambapo Meta inaweza kuelewa nia ya mtumiaji.” Bodi inazingatia kuwa pendekezo hilo limetekelezwa kiasi kwa kuwa masasisho hayakufanywa kwenye Viwango vya Jumuiya bali tu kwenye utangulizi wa jumla wa Viwango vya Jumuiya.
Bodi inaamini kuwa utekelezaji kamili wa pendekezo hili unaweza kupunguza idadi ya makosa ya utekelezaji chini ya sera ya Meta dhidi ya Matamshi ya Chuki.
Uamuzi
Bodi imebatilisha uamuzi wa kwanza wa Meta wa kuruhusu maudhui hayo. Bodi inatambua masahihisho ambayo Meta ilifanya kwenye kosa la kwanza baada ya Bodi kujulisha Meta kuhusu kesi hiyo.
العودة إلى قرارات الحالة والآراء الاستشارية المتعلقة بالسياسة