Overturned
Mwahabari Anayekumbuka Mkutano wa Gaza
April 4, 2024
Mwanahabari alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuondoa chapisho la Facebook lililokuwa likitoa kumbukumbu za hali alizopitia binafsi akihoji Abdel Aziz Al-Rantisi, mwasisi mwenza wa Hamas. Kesi hii inaangazia tatizo linalojirudia katika utekelezaji kupita kiasi wa sera ya kampuni hiyo dhidi ya Watu na Mashirika Hatari, hususan kuhusiana na machapisho yasiyoegemea upande wowote. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hiyo, kampuni hiyo ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na ikarejesha chapisho hilo.
Huu ni uamuzi kwa ufupi.Uamuzi wa ufupi huchunguza kesi ambapo Meta imebatilisha uamuzi wake wa kwanza kuhusu kipande cha maudhui baada ya Bodi kupeleka kesi hiyo kwa kampuni na kujumuisha taarifa kuhusu makosa ambayo Meta imekiri. Huwa unaidhinisha na jopo la Wanachama wa Bodi, badala ya Bodi kamili, hauhusishi maoni ya umma na hayana thamani ya kutumika katika marejeleo ya Bodi. Maamuzi kwa ufupi huleta mabadiliko moja kwa moja kwenye maamuzi ya Meta, yakitoa uwazi kuhusu masahihisho haya, huku pia yakitambua maeneo ambayo Meta inaweza kuboresha utekelezaji wake.
Muhtasari wa Kesi
Mwanahabari alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuondoa chapisho la Facebook lililokuwa likitoa kumbukumbu za hali alizopitia binafsi akihoji Abdel Aziz Al-Rantisi, mwasisi mwenza wa Hamas. Kesi hii inaangazia tatizo linalojirudia katika utekelezaji kupita kiasi wa sera ya kampuni hiyo dhidi ya Watu na Mashirika Hatari, hususan kuhusiana na machapisho yasiyoegemea upande wowote. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hiyo, kampuni hiyo ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na ikarejesha chapisho hilo.
Maelezo na Historia ya Kesi
Punde baada ya tukio la shambulizi la tarehe 7 Oktoba 2023, mwanahabari alichapisha kwenye Facebook kumbukumbu zake zilizoandikwa za mahojiano aliyofanya na Abdel Aziz Al-Rantisi, mwanzilishi mwenza wa Hamas, ambalo ni shirika lililobainishwa katika Ngazi ya 1 ya sera za Meta dhidi ya Watu na Mashirika Hatari. Chapisho hilo lilieleza ziara ya mwanachama huyo kwenye Gaza, mambo aliyokumbana nayo na wanachama wa Hamas na wenyeji, na vilevile hali ya kutafuta na kumhoji al-Rantisi. Chapisho hilo lina picha, ikiwa ni pamoja na za Al-Rantisi, anayehoji na wanamgambo wa Hamas wenye barakoa.
Katika rufaa yake kwa Bodi, mtumiaji alieleza kwamba nia ya chapisho lilikuwa ni kufahamisha umma kuhusu hali aliyopitia katika ukanda wa Gaza na mahojiano yake na mmoja wa waasisi halisi wa Hamas.
Meta iliondoa chapisho hilo kwenye Facebook, ikitaja sera yake ya Watu na Mashirika Hatari, ambayo chini yake, kampuni hiyo huondoa maudhui fulani kuhusu watu na mashirika ambayo imebainisha kuwa hatari. Hata hivyo, sera hiyo inatambua kuwa “watumiaji wanaweza kushiriki maudhui yanayojumuisha marejeleo kwa mashirika na watu binafsi hatari katika muktadha wa mijadala ya kijamii na kisiasa. Hii inajumuisha kuripoti maudhui, kujadili bila upendeleo wowote au kushutumu mashirika na watu binafsi hatari au shughuli zao.
Baada ya Bodi kujulisha Meta kuhusu kesi hii, kampuni hiyo ilibaini kuwa “maudhui hayo yalilenga kuongeza ufahamu kuhusu hali iliyopo” na kwa hivyo halikukiuka Viwango vya Jumuiya kuhusu Watu na Mashirika Hatari. Meta ilitaja posho ya majadiliano ya kijamii na kisiasa katika muktadha wa “maelezo yasiyoegemea upande wowote na ya kufahamisha kuhusu shughuli au tabia za Watu na Mashirika Hatari.” Zaidi ya hayo, Meta ilisema kwamba “muktadha wa majadiliano ya kijamii na kisiasa imetajwa moja kwa moja katika maudhui hayo kwa hivyo hakuna utata kuhusu nia ya mtumiaji” katika kesi hii.
Mamlaka na Upeo wa Bodi
Bodi ina mamlaka ya kukagua uamuzi wa Meta kufuatia rufaa kutoka kwa mtumiaji ambaye maudhui yake yaliondolewa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria ndogo za Kifungu cha 3, Sehemu ya 1).
Pale ambapo Meta inakiri kuwa ilikosea na ibatilishe uamuzi wake katika kesi inayoratibiwa kukaguliwa na Bodi, Bodi inaweza kuchagua kesi hiyo ili kuifanyia uamuzi kwa ufupi (Sheria ndogo Kifungu cha 2, Sehemu ya 2.1.3). Bodi hupitia uamuzi wa kwanza ili kuongeza uelewa wa mchakato wa uratibu wa maudhui, ili kupunguza makosa na kuongeza haki kwa watu wanaotumia Facebook na Instagram.
Umuhimu wa Kesi
Kesi hii inaangazia utekelezaji kupita kiasi wa sera ya Meta dhidi ya Watu na Mashirika Hatari, hususan kuripoti habari kuhusu mashirika ambayo kampuni hiyo imebainisha kuwa hatari. Hili ni tatizo linalojirudia, ambalo limekuwa likitokea mara kwa mara wakati wa mgogoro kati ya Israel-Hamas, ambapo mojawapo ya mashirika limebainishwa kuwa hatari. Bodi imetoa mapendekezo kadhaa yanayohusiana na posho la kuripoti habari chini ya sera yake dhidi ya Watu na Mashirika Hatari. Makosa yanayoendelea katika utekelezaji wa posho hii muhimu inaweza kuzuia pakubwa uhuru wa kujieleza, uwezo wa umma kufikia taarifa na kuhujumu majadiliano ya umma.
Katika uamuzi wa awali, Bodi ilipendekeza kwamba Meta “iweke vigezo na mifano ya kuonyesha kwenye sera ya Meta dhidi ya Watu na Mashirika Hatari ili kuongeza uelewa wa vighairi, hususan kuhusu majadiliano yasiyoegemea upande wowote, kulaani na kuripoti habari,” (Chapisho la Al Jazeera Lililoshirikiwa, pendekezo nambari 1). Ripoti ya Meta kuhusu kutekeleza kwake pendekezo hili ilionyeshwa kupitia taarifa zilizochapishwa. Katika sasisho la sera dhidi ya Watu na Mashirika Hatari la tarehe 29 Desemba 2023, Meta imerekebisha maelezo yake na sasa inatumia neno “utukuzaji” badala ya “sifa” katika Viwango vyake vya Jumuiya.
Zaidi ya hayo, Bodi pia ilipendekeza kwamba Meta “inapaswa kutathmini usahihi wa wakaguzi kutekeleza posho ya kuripoti chini ya sera ya Mashirika na Watu Binafsi Hatari ili kubaini masuala ya kimfumo yanayosababisha makosa ya utekelezaji ( Kutajwa kwa Taliban katika Kuripoti Habari, pendekezo la nambari 5); Meta imeripoti kutekeleza pendekezo hili lakini haijachapisha maelezo yoyote ili kuonyesha utekelezaji huu.
Katika hali za uratibu otomatiki, Bodi imeitaka Meta itekeleze utaratibu wa ukaguzi wa ndani ili kuendelea kuchanganua sampuli za uwakilishi wa takwimu za maamuzi ya uondoaji otomatiki ili kubatilisha na kujifunza kutoka kwa makosa hayo ya utekelezaji (Dalili za Saratani ya Matiti na Picha ya Uchi, pendekezo nambari 5), ambalo Meta imeripoti kuwa imetekeleza.
Bodi inaamini kwamba utekelezaji kamili wa mapendekezo haya unaweza kupunguza idadi ya makosa ya utekelezaji wa sera ya Meta dhidi ya Watu na Mashirika Hatari.
Uamuzi
Bodi imebatilisha uamuzi wa awali wa Meta wa kuondoa maudhui hayo. Bodi inatambua masahihisho ambayo Meta ilifanya kwenye kosa la kwanza baada ya Bodi kujulisha Meta kuhusu kesi hiyo.