एकाधिक मामले का निर्णय
Ripoti kuhusu Waathiriwa wa Ubakaji wa Israeli
4 अप्रैल 2024
Mtumiaji alichapisha maamuzi ya Meta ya kuondoa machapisho mawili ya Facebook yanayoeleza vurugu za ngono zilizofanywa na wanamgambo wa Hamas wakati wa mashambulizi ya kigaidi ya tarehe 7 Oktoba 2023 dhidi ya Israeli. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hizo, kampuni ilibatilisha maamuzi yake kwanza na ikarejesha machapisho hayo.
2 इस बंडल में केस शामिल हैं
FB-YCJP0Q9D
Kesi kuhuhu watu na mashirika hatari kwenye Facebook
FB-JCO2RJI1
Kesi kuhuhu watu na mashirika hatari kwenye Facebook
Huu ni uamuzi kwa ufupi.Uamuzi wa ufupi huchunguza kesi ambapo Meta imebatilisha uamuzi wake wa kwanza kuhusu kipande cha maudhui baada ya Bodi kupeleka kesi hiyo kwa kampuni na kujumuisha taarifa kuhusu makosa ambayo Meta imekiri. Huwa unaidhinisha na jopo la Wanachama wa Bodi, badala ya Bodi kamili, hauhusishi maoni ya umma na hayana thamani ya kutumika katika marejeleo ya Bodi. Maamuzi kwa ufupi huleta mabadiliko moja kwa moja kwenye maamuzi ya Meta, yakitoa uwazi kuhusu masahihisho haya, huku pia yakitambua maeneo ambayo Meta inaweza kuboresha utekelezaji wake.
Muhtasari wa Kesi
Mtumiaji alichapisha maamuzi ya Meta ya kuondoa machapisho mawili ya Facebook yanayoeleza vurugu za ngono zilizofanywa na wanamgambo wa Hamas wakati wa mashambulizi ya kigaidi ya tarehe 7 Oktoba 2023 dhidi ya Israeli. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hizo, kampuni ilibatilisha maamuzi yake kwanza na ikarejesha machapisho hayo.
Maelezo na Historia ya Kesi
Mnamo Oktoba 2023, mtumiaji wa Facebook alipakia machapisho mawili tofauti, moja baada na jingine, yaliyokuwa na maudhui yanayoangazia video ya mwanamke anayeeleza kuhusu kubakwa vya wanawake wa Israeli na Hamas wakati wa mashambulizi ya kigaidi ya tarehe 7 Oktoba. Manukuu hayo yana “tahadhari ya uchochezi” na anayezungumza kwenye video anawatahadharisha watumiaji kuhusu maudhui ya kuogofya. Video hiyo inaendelea kuonyesha picha ya wanawake wawili tofauti wakitekwa nyara na Hamas, klipu moja ikihusisha mwanamke mwenye majeraha mabaya akiwa amelala chini ya lori na mwingine mwenye majereha akuburutwa kutoka nyuma ya gari. Picha hizi zilishirikiwa sana baada ya shambulizi hilo. Chapisho la kwanza lilishirikiwa takriban mara 4,000 na chapisho la pili lilikuwa na chini ya ushiriki 50.
Machapisho yote mawili awali yaliondolewa na Meta kwa kukiuka Viwango vya Jumuiya kuhusu Watu na Mashirika Hatari. Chini ya sera hii, kampuni hiyo imepiga marufuku picha za watu wengine zinazoonyesha matukio ya shambulizi lililobainishwa la ugaidi dhidi ya waathiriwa wanaoweza kutambuliwa chini ya hali zozote, hata kama zimeshirikiwa ili kulaani au kutoa uhamasisho kuhusu shambulizi hilo. Kando na hayo, chini ya Viwango vya Jumuiya ya Meta kuhusu Vurugu na Uchochezi, kampuni hiyo huondoa “maudhui yanayoonyesha utekaji nyara ikiwa ni wazi kwamba maudhui hayo hayashirikiwi na mwathiriwa au familia yake kama maombi ya msaada, au kushirikiwa kwa malengo ya kutoa maelezo, kulaani au kutoa uhamasisho.”
Mwanzoni mwa shambulizi la Hamas la tarehe 7 Oktoba, Meta ilianza kutekeleza kwa njia madhubuti sera yake dhidi ya Watu na Mashirika Hatari kwa video zinazoonyesha matukio kutoka kwa mashambulizi mahususi dhidi ya waathiriwa wanaoonekana. Meta ilieleza mbinu hii katika chapisho lake la Chumba cha Habari la tarehe 13 Oktoba, ikisema kwamba imefanya hivyo “ili kutoa kipaumbele kwa usalama wa wale walioshikwa mateka na Hamas.” Maudhui yote mawili katika kesi hii yaliondolewa kwa kukiuka sera ya Meta dhidi ya Watu na Mashirika Hatari.
Kufuatia uamuzi huu, mashirika mengi ya habari yalianza kutangaza picha zinazohusiana na watumiaji pia walianza kuchapisha maudhui sawa na hayo ili kutoa uhamasisho na kulaani mashambulizi hayo. Kutokana na hayo, mnamo au takriban tarehe 20 Oktoba, Meta ilisasisha sera zake ili kuruhusu watumiaji kushiriki picha tu ndani ya muktadha wa kutoa uhamasisho au kulaani madhila hayo, na ikaweza skrini ya onyo ili kufahamisha watumiaji kuwa picha zilikuwa za kutatiza. Meta ilichapisha mabadiliko haya kwenye sera yake katika sasisha la tarehe 5 Desemba kwa chapisho lake la kwanza la Chumba cha Habari la tarehe 13 Oktoba (angalia Watu Walioshikwa Mateka kutoka Israeli ili upate usuli na maelezo zaidi).
Awali Meta iliondoa maudhui yote mawili kwenye Facebook katika kesi hizi mbili. Mtumiaji alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta kwa Bodi. Baada ya Bodi kupeleka kesi ya Meta, kampuni hiyo ilibaini kuwa machapisho hayo hayakuwa yakikiuka tena sera zake, kutokana na posho iliyosasishwa na ikayarejesha yote.
Mamlaka na Upeo wa Bodi
Bodi ina mamlaka ya kukagua maamuzi ya Meta kufuatia rufaa kutoka kwa mtu ambaye maudhui yake yaliondolewa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria ndogo za Kifungu cha 3, Sehemu ya 1).
Pale ambapo Meta inathibitisha kwamba ilikosea na ibatilishe uamuzi wake katika kesi inayoratibiwa kukaguliwa na Bodi, Bodi inaweza kuchagua kesi hiyo ili kuifanyia uamuzi kwa ufupi (Sheria ndogo Kifungu cha 2, Sehemu ya 2.1.3). Bodi hukagua uamuzi wa kwanza ili kuongeza ufahamu wa michakato ya uratibu wa maudhui, kupunguza makosa na kuongeza haki kwa watumiaji wa Facebook na Instagram.
Umuhimu wa Kesi
Kesi zote mbili zinaangazia changamoto katika uwezo wa Meta wa kutekeleza maudhui katika hali za mgogoro wenye hatari ya juu ambao unakua na kubadilika kila mara. Kama ambavyo Bodi ilibaini katika uamuzi wake uliofanywa haraka, Watu Walioshikwa mateka kutoka Israeli, sera ya awali ya Meta iliyopiga marufuku maudhui yanayoonyeshwa kwa mateka ililinda hadhi ya mateka hao na ililenga kuhakikisha kuwa hawakuvutia umakini wa umma. Hata hivyo, Bodi pia ilipata kwamba, katika hali za kipekee, wakati mapendeleo ya umma au mapendeleo muhimu ya mateka yanapohitaji hivyo, vighairi vya muda na vyenye vikomo vinaweza kuhalalishwa. Kutokana na muktadha, kurudisha aina hii ya maudhui kwenye jukwaa, kwa kutumia skrini ya onyo ya “alamisha kuwa ya kutisha”, kunalingana na sera za maudhui ya Meta, maadili na majukumu ya kulinda haki za binadamu. Hatua hii pia itaambatana na sheria ya kimataifa ya binadamu na desturi ya kulinda rekodi ya ukiukaji unaodaiwa kwa ajili ya uwajibikaji siku zijazo, na vilevile kuongeza uhamasisho wa umma. Katika kesi hiyo, Bodi pia ilibaini kuwa Meta ilichukua muda mrefu mno kuzindua utekelezaji wa kighairi hiki kwa watumiaji wote na kwamba hali inayoendelea ya kampuni hiyo kubadilisha mbinu yake ya kushughulikia maudhui nyakati za mgogoro imeendeleza ukosefu wa uwazi.
Awali, Bodi ilikuwa imetoa mapendekezo yaliyo muhimu katika kesi hii. Bodi ilipendekeza kwamba Meta itangaze vighairi vya Viwango vyake vya Jumuiya, kwa kubainisha “muda wao na notisi ya muda wa matumizi, ili kuwapa watu wanaotumia majukwaa yake notisi ya mabadiliko ya sera kuruhusu kujieleza fulani,” (Kaulimbiu ya Maandamano ya Iran, pendekezo nambari 5). Meta imetekeleza sehemu ya pendekezo hili kama ilivyoonyeshwa kupitia taarifa zilizochapishwa. Hapo awali Bodi pia ilipendekeza kwamba Meta ihifadhi ushahidi wa uwezekano wa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na ukiukaji mbaya wa haki za binadamu kwa nia ya uwajibikaji siku zijazo ( Video ya Kuogofya ya Sudan, pendekezo nambari 1 na Video ya Wafungwa wa Kivita wa Armenia, pendekezo nambari 1). Meta imekubali kutekeleza pendekezo hili na kazi hiyo bado inaendelea. Bodi inasisitiza hitaji la Meta kuchukua hatua ya kushughulikia mapendekezo haya ili kuhakikisha kuwa maudhui yanayohusiana na haki za binadamu yanatekelezwa kwa usahihi kwenye majukwaa yake.
Uamuzi
Bodi imebatilisha uamuzi wa kwanza wa Meta wa kuondoa vipande viwili vya maudhui hayo. Bodi inatambua masahihisho ambayo Meta ilifanya kwenye makosa yake ya kwanza baada ya Bodi kujulisha Meta kuhusu kesi hizo.