एकाधिक मामले का निर्णय

Kasumba Mbaya kuhusu Waamerika wenye Asili ya Afrika

Bodi ilikagua machapisho matatu ya Facebook yaliyo na nyenzo za ubaguzi wa rangi, ambayo Meta iliacha. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hizi, kampuni ilibatilisha maamuzi yake kwanza na kuondoa machapisho hayo.

3 इस बंडल में केस शामिल हैं

पलट जाना

FB-LHBURU6Z

Kesi kuhusu matamshi ya chuki kwenye Facebook

प्लैटफ़ॉर्म
Facebook
विषय
Ubaguzi,Rangi na Kabila
मानक
Tabia ya chuki
जगह
Marekani
Date
पर प्रकाशित 18 अप्रैल 2024
पलट जाना

FB-1HX5SN1H

Kesi kuhusu matamshi ya chuki kwenye Facebook

प्लैटफ़ॉर्म
Facebook
विषय
Ubaguzi,Rangi na Kabila
मानक
Tabia ya chuki
जगह
Uingereza,Marekani
Date
पर प्रकाशित 18 अप्रैल 2024
पलट जाना

FB-ZD01WKKW

Kesi kuhusu matamshi ya chuki kwenye Facebook

प्लैटफ़ॉर्म
Facebook
विषय
Ubaguzi,Rangi na Kabila
मानक
Tabia ya chuki
जगह
Marekani
Date
पर प्रकाशित 18 अप्रैल 2024

Huu ni uamuzi wa muhtasari. Uamuzi wa ufupi huchunguza kesi ambapo Meta imebatilisha uamuzi wake wa kwanza kuhusu kipande cha maudhui baada ya Bodi kupeleka kesi hiyo kwa kampuni na kujumuisha taarifa kuhusu makosa ambayo Meta imekiri. Huwa unaidhinisha na jopo la Wanachama wa Bodi, badala ya Bodi kamili, hauhusishi maoni ya umma na hayana thamani ya kutumika katika marejeleo ya Bodi. Maamuzi kwa ufupi huleta mabadiliko moja kwa moja kwenye maamuzi ya Meta, yakitoa uwazi kuhusu masahihisho haya, huku pia yakitambua maeneo ambayo Meta inaweza kuboresha utekelezaji wake.

Muhtasari

Bodi ilikagua machapisho matatu ya Facebook yaliyo na nyenzo za ubaguzi wa rangi, ambayo Meta iliacha. Kila chapisho lilikuwa na picha au taswira iliyokarabatiwa ya Waamerika wenye asili ya Afrika inayoangazia kasumba mbaya, ikiwa ni pamoja na kina baba waliotoroka familia zao, kuwepo kwenye mpango wa msaada na wezi madukani. Kesi hizi zinaangazia makosa kwenye utekelezaji wa Meta wa sera zake dhidi ya Matamshi ya Chuki na Dhuluma na Unyanyasaji. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hizi, kampuni ilibatilisha maamuzi yake kwanza na kuondoa machapisho hayo.

Kuhusu Kesi hizi

Mwishoni mwa 2023, Bodi ilipokea rufaa tatu tofauti zilizohusiana na picha tatu tofauti zilizochapishwa kwenye Facebook, zote zikiwa na nyenzo hasi kuhusu Waamerika wenye Asili ya Afrika.

Kwenye chapisho la kwanza ambalo lilitazamwa takriban mara 500,000, mtumiaji alichapisha picha iliyozalishwa kwa kompyuta ya duka lililokuwa limeshika moto na watu Weusi walioonyeshwa kama wahusika vibonzo, wakiwa wamevaa sweta nzito zenye kofia, huku wakiwa wamebeba bidhaa na kutoroka kutoka dukani. Jina la duka hilo, Target, limebadilishwa kuwa “Iba” kwenye picha hiyo na kwenye manukuu yanayoambatana, mtumiaji anaeleza picha hiyo kama filamu ijayo ya Pixar.

Chapisho la pili linaangazia picha iliyozalishwa kwa kompyuta ambayo pia inaiga bango la filamu, na mwanamke Mweusi ambaye ana maumbile yaliyoundwa kupita kiasi anayeonyeshwa akiwa amebeba kikapu cha ununuzi kilichojaa Cheetoh. Jina la filamu hiyo ni “EBT,” ambalo ni jina la mfumo wa kupokea manufaa ya msaada wa kijamii nchini Marekani. Katika sehemu ya juu ya bango, badala ya majina ya waigizaji, kuna majina ya Trayvon Martin na George Floyd, wote ni Waamerika wenye Asili ya Afrika ambao ni waathiriwa wa vurugu, mmoja alipiga risasi na sungusungu waliojihami mwaka 2012 na mwingine aliuawa mikononi mwa polisi mwaka 2020. Vifo vyao vilisaidia kuchochea maandamano kuhusu tofauti za kirangi kwenye mfumo wa haki wa Marekani.

Chapisho la tatu, ambalo lilitazamwa takriban mara milioni 14, liliangazia picha ya pepe inayodai kuwa “Shirika la Adobe limeunda programu inayoweza kutambua vipengee bandia kwenye picha.” Chini ya dai hilo, kuna picha ya mwanamke mwenye alama za rangi kote usoni pake (kwa kawaida hutumika kuonyesha utambuzi wa joto) ili kuonyesha kuwa sehemu za picha hiyo zimebadilishwa. Picha hii inalinganishwa na taswria ya familia ya watu Weusi wanaoshiriki mlo ambapo baba na chakula kilicho mezani wana alama zinazofanana za rangi, hali inayooashiria kuwa vipengele hivi viwili viliongezwa kupitia uhariri. Chapisho hilo linasisitiza kuenea sana kwa hali ya kasumba mbaya kuhusu ukosefu wa baba katika familia za watu Weusi nchini Marekani, hali inayotokana na historia changamano ya ubaguzi wa kimfumo na ukosefu wa usawa kiuchumi.

Awali Meta iliacha machapisho hayo matatu kwenye Facebook, licha ya rufaa kutoka kwa watumiaji. Katika rufaa zao kwa Bodi, watumiaji hao walihoji kuwa maudhui yao yalionyesha kasumba hatari za ubaguzi wa rangi dhidi ya Waamerika wenye Asili ya Afrika.

Baada ya Bodi kufahamisha Meta kuhusu kesi hizi, kampuni hiyo ilibaini kuwa kila chapisho lilikiuka Viwango vya Jumuiya kuhusu Matamshi ya Chuki, ambavyo imepiga marufuku mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya watu kwa msingi wa sifa zilizolindwa, ikiwa ni pamoja na rangi na kabila. Sera hii pia inapiga marufuku kwa njia mahususi “ulengaji wa watu au kikundi cha watu” kwa “kauli ya kudhalilisha” kwa namna ya “ulinganishaji na wahalifu ikiwa ni pamoja na wezi,” “kudhihaki dhana, matukio au waathiriwa wa uhalifu wa chuki” na “ujumlishaji unaotaja unyonge katika ... sifa za kimaadili.”

Vilevile, Meta ilibaini chapisho la pili linalojumuisha majina ya Trayvon Martin na George Floyd pia linakiuka Viwango vya Jumuiya kuhusu Dhuluma na Unyanyasaji ambayo chini yake kampuni hiyo inaondoa “sherehe au kudhihaki kifo au hali ya kimatibabu” ya mtu yeyote. Kampuni ilieleza kwamba “picha hiyo inajumuisha jina la watu wawili waliofariki, Trayvon Martin na George Floyd ... Maudhui hayo yanadhihaki vifo vyao kwa kukisia kuwa watakuwa waigizaji nyota kwenye filamu iliyohuishwa ya kubuni.”
Kwa hivyo kampuni iliondoa machapisho yote matatu.

Mamlaka na Upeo wa Bodi

Bodi ina mamlaka ya kukagua uamuzi wa Meta kufuatia rufaa kutoka kwa mtumiaji ambaye aliripoti maudhui ambayo yaliachwa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria ndogo za Kifungu cha 3, Sehemu ya 1).

Pale ambapo Meta inathibitisha kwamba ilikosea na ibatilishe uamuzi wake katika kesi inayoratibiwa kukaguliwa na Bodi, Bodi inaweza kuchagua kesi hiyo ili kuifanyia uamuzi kwa ufupi (Sheria ndogo Kifungu cha 2, Sehemu ya 2.1.3). Bodi hukagua uamuzi wa kwanza ili kuongeza ufahamu wa michakato ya uratibu wa maudhui, kupunguza makosa na kuongeza haki kwa watumiaji wa Facebook na Instagram.

Umuhimu wa Kesi

Kesi hizi zinaangazia matukio matatu ambapo Meta ilikosa kutekeleza sera zake kwa ufanisi dhidi ya Matamshi ya Chuki na Dhuluma na Unyanyasaji, kwa kuacha machapisho ya ukiukaji licha ya malalamiko ya watumiaji. Machapisho mawili yalipata idadi ya juu ya mionekano. Makosa kama hayo ya uratibu wa utekelezaji wa chini unaweza kuathiri vibaya watu walio katika vikundi vya sifa zilizolindwa na kuchangia katika mazingira ya ubaguzi. Bodi imekuwa ikisukuma Meta iipe kipaumbele cha kimkakati Matamshi ya Chuki Dhidi ya Makundi Yaliyotengwa.

Mwaka 2022, Bodi ilipendekeza kwamba, Meta inapaswa “kufafanua Kiwango cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki na mwongozo unaotolewa kwa wakaguzi, ikieleza kuwa hata marejeleo yasiyo wazi kwa vikundi vinavyolindwa hayaruhusiwi na sera wakati marejeleo yangeeleweka vizuri,” (uamuzi wa Katuni ya Knin, pendekezo nambari 1), ambao Meta imeripoti kutekeleza sehemu yake.

Uamuzi

Bodi imebatilisha uamuzi wa kwanza wa Meta wa kuruhusu machapisho hayo matatu. Bodi inatambua masahihisho ambayo Meta ilifanya kwenye makosa ya kwanza baada ya Bodi kujulisha Kampuni kuhusu kesi hizi.

मामले के निर्णयों और नीति सलाहकार राय पर लौटें