पलट जाना

Taarifa Kuhusu Chama cha Kikomunisti cha China

Mtumiaji amekata rufaa ya uamuzi wa Meta wa kuondoa maoni ya Instagram yanayodai “kifo” cha Chama cha Kikomunisti cha China.

निर्णय का प्रकार

सारांश

नीतियां और विषय

विषय
अभिव्यक्ति की स्वतंत्रता, सरकारें, विरोध
सामुदायिक मानक
हिंसा और उकसावा

क्षेत्र/देश

जगह
Uchina

प्लैटफ़ॉर्म

प्लैटफ़ॉर्म
Instagram

Uamuzi wa ufupi huchunguza kesi ambapo Meta imebatilisha uamuzi wake wa kwanza kuhusu kipande cha maudhui baada ya Bodi kupeleka kesi hiyo kwa kampuni na kujumuisha taarifa kuhusu makosa ambayo Meta imekiri. Huwa unaidhinisha na jopo la Wanachama wa Bodi, badala ya Bodi kamili, hauhusishi maoni ya umma na hayana thamani ya kutumika katika marejeleo ya Bodi. Maamuzi kwa ufupi huleta mabadiliko moja kwa moja kwenye maamuzi ya Meta, yakitoa uwazi kuhusu masahihisho haya, huku pia yakitambua maeneo ambayo Meta inaweza kuboresha utekelezaji wake.

Muhtasari

Mtumiaji amekata rufaa ya uamuzi wa Meta wa kuondoa maoni ya Instagram yanayodai “kifo” cha Chama cha Kikomunisti cha China. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hiyo, kampuni hiyo ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na ikarejesha chapisho hilo.

Kuhusu Kesi

Mnamo Machi 2024, mtumiaji wa Instagram alichapisha maoni yanayosema, “Kifo cha Chama cha Kikomunisti cha China!” yakifuatwa na emoji za fuvu la kichwa. Hii ilikuwa jibu kwa chapisho kutoka kwa akaunti ya chombo cha habari, lililoangazia video ya Wang Wenbin, aliyekuwa msemaji mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje China, akishutumu kupitishwa kwa mswada katika Baraza la Wawakilishi la Marekani ambao unaweza kuathiri uwepo wa TikTok katika nchi hiyo.

Awali Meta iliondoa chapisho la mtumiaji huyo kwenye Facebook chini ya Viwango vyake vya Jumuiya kuhusu Vurugu na Uchochezi, vinavyopiga marufuku “vitisho vya vurugu.” Kampuni hiyo ilielezea kwamba marufuku hayo yanajumuisha “madai fulani ya kifo iwapo yana mlengwa na mbinu ya vurugu.”

Wakati ambapo Bodi iliwasilisha kesi hii kwa Meta, kampuni hiyo ilibaini kuwa kuondolewa kwa maoni hayo hakukuwa sahihi na ikarejesha maudhui hayo kwenye Instagram. Meta ilielezea kuwa, ilivyoelezwa katika miongozo yake ya ndani ya wakaguzi wa maudhui, madai ya kifo cha taasisi kama vile Chama cha Kikomunisti cha China yanachukuliwa kuwa si ya ukiukaji.

Mamlaka na Upeo wa Bodi

Bodi ina mamlaka ya kukagua uamuzi wa Meta kufuatia rufaa kutoka kwa mtumiaji ambaye maudhui yake yaliondolewa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria ndogo za Kifungu cha 3, Sehemu ya 1).

Pale ambapo Meta inathibitisha kwamba ilikosea na ibatilishe uamuzi wake katika kesi inayoratibiwa kukaguliwa na Bodi, Bodi inaweza kuchagua kesi hiyo ili kuifanyia uamuzi kwa ufupi (Sheria ndogo Kifungu cha 2, Sehemu ya 2.1.3). Bodi hukagua uamuzi wa kwanza ili kuongeza ufahamu wa michakato ya uratibu wa maudhui, kupunguza makosa na kuongeza haki kwa watumiaji wa Facebook, Instagram na Threads.

Umuhimu wa Kesi

Kesi hii inaangazia kutopatana kwa jinsi ambavyo Meta hutekeleza sera yake ya Vurugu na Uchochezi dhidi ya kauli zenye sitiari au za kitamathali katika muktadha wa kisiasa, hali ambayo inaweza kuathiri kwa kiasi kisicholingana usemi wa kisiasa ambao unakosoa mataifa na taasisi za serikali. Kesi hiyo inasisitiza umuhimu wa Meta kuzingatia mlengwa wa usemi (katika kesi hii, chama cha kisiasa) na pia jinsi watu wanavyotumia usemi wenye kutia chumvi, kejeli na tashtiti kukosoa taasisi, wakati ambapo inaunda mifumo yake ya uratibu.

Kuhusu usemi wa balagha, Bodi katika kesi ya Shairi la Urusi ilipata kuwa madondoo yenye lugha ya vurugu katika shairi la “Kill him! (Muuwe!)” yanaweza kusomwa kama “inayoelezea, sio kutia moyo, hali ya akili.” Bodi iliamua kuwa lugha hiyo ilitumika kama usemi wa balagha ili kupitisha ujumbe wa mtumiaji na kwamba, kutokana na hilo, sehemu hiyo ya maudhui iliruhusiwa na miongozo ya Meta ya ndani kuhusu sera yake ya Vurugu na Uchochezi.

Ijapokuwa inashughulikia Kiwango cha Jumuiya (Matamshi ya Chuki) tofauti na kile ambacho kinajadiliwa katika kesi hii (Vurugu na Uchochezi), uamuzi wa Boti ya Myanmar ni muhimu kwa sababu pia unahusu usemi unaolenga mataifa au taasisi za kisiasi. Hapo, Bodi ilihitimisha kuwa kwa kuwa uchafu katika chapisho hilo haukulenga watu kutegemea uasili, ukabila au taifa la asili, lakini ulilenga taifa, haukukiuka Kiwango cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki. Bodi ilisisitiza: “Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa marufuku kuhusu kuwalenga watu kutegemea sifa zilizolindwa yasiwekwe kwa njia ambayo inakinga serikali au taasisi dhidi ya ukosoaji.”

Awali Bodi imeitaka Meta kuweka utaratibu wa kutosha wa kutathmini maudhui katika muktadha wake husika ( Meme ya Vitufe Viwili, pendekezo la nambari 3). Pia imependekeza: “Kuwaarifu vyema watumiaji kuhusu aina za kauli ambazo zimepigwa marufuku, Meta inafaa kurekebisha Kiwango cha Jumuiya kuhusu Vurugu na Uchochezi ili (i) kuelezea kuwa vitisho vya balagha kama kauli za “kifo kwa X” vinaruhusiwa kwa kawaida, isipokuwa kama mlengwa wa tishio ni mtu aliye katika hatari ya juu…” ( Wito wa Maandamano ya Irani, pendekezo nambari 1); na “Meta inafaa kuegemea upande wa kutoa ruhusa zilizopimwa mahali ambapo (i) hali hii haina uwezekano wa kuleta vurugu; (ii) maudhui yaliyo na uwezo wa kukiuka yametumika katika muktadha wa mgomo; na (iii) mahali ambapo manufaa ya umma yapo juu, “ ( Wito wa Maandamano ya Irani, pendekezo nambari 2).

Meta iliripoti utekelezaji wa pendekezo la Meme ya “Vitufe Viwili” na pendekezo nambari 2 kutoka kwa uamuzi wa Wito wa Maandamano ya Irani lakini haikuchapisha taarifa ili kuonyesha hii. Kwa pendekezo nambari 1 kutoka kwa Wito wa Maandamano ya Irani, katika Sasisho lake la Q4 2023 la Baada ya Miezi Mitatu kwa Bodi, Meta ilisema: “Tumesasisha Viwango vyetu vya Jumuiya kuhusu Vurugu na Uchochezi kwa kutoa maelezo zaidi kuhusu kile ambacho kinafanyiza ‘tishio’ na kutofautisha utekelezaji wetu kutegemea mlengwa. Kama sehemu ya kazi hii, pia tulisasisha mwongozo wa ndani.”

Bodi inaamini kuwa utekelezaji kamili wa mapendekezo haya unaweza kuchangia kupungua kwa idadi ya makosa ya utekelezaji chini ya sera ya Vurugu na Uchochezi.

Uamuzi

Bodi imebatilisha uamuzi wa awali wa Meta wa kuondoa maudhui hayo. Bodi inatambua masahihisho ambayo Meta ilifanya kwenye kosa la kwanza baada ya Bodi kujulisha Meta kuhusu kesi hiyo.

मामले के निर्णयों और नीति सलाहकार राय पर लौटें