Publicados

Kushiriki Taarifa ya kibinafsi ya Makao

Katika maoni yake ya ushauri wa sera, Bodi inapendekeza kwamba Meta iondoe hali ya kipekee katika Viwango vya Jumuiya kuhusu Ukiukaji wa Faragha inayoruhusu ushirikiaji wa maelezo ya makazi ya kibinafsi wakati maelezo hayo yanazingatiwa kuwa ‘yanapatikana kwa umma’.

Tipo de decisão

Padrão

Políticas e tópicos

विषय
Jornalismo, Comunidades marginalizadas

Plataforma

Plataforma
Facebook

Leo, Bodi ya Usimamizi imechapisha maoni yake ya kwanza ya ushauri wa sera. Kupitia maoni haya ya ushauri wa sera, Bodi inakagua sera za Meta kuhusu mada husika na kutoa mapendekezo ya jinsi ya zinafaa kubadilishwa.

Ili kusoma toleo kamili ya maoni ya ushauri wa sera ya Bodi kuhusu kushiriki maelezo ya makazi ya kibinafsi, bofya hapa.

Pia unaweza kusoma muhtasari wa maoni hayo hapo chini.

Katika maoni yake ya ushauri wa sera, Bodi inapendekeza kwamba Meta iondoe hali ya kipekee katika Viwango vya Jumuiya kuhusu Ukiukaji wa Faragha inayoruhusu ushirikiaji wa maelezo ya makazi ya kibinafsi wakati maelezo hayo yanazingatiwa kuwa “yanapatikana kwa umma.” Hii ingesaidia Meta kulinda maelezo ya makazi ya kibinafsi ya watu.

Miongoni mwa mapendekezo yake, Bodi inapendekeza kwamba Meta iunde kituo cha mawasiliano kwa waathiriwa ambao maelezo ya makazi yao yamefichuliwa kwa umma, kuwapa watumiaji udhibiti zaidi wa jinsi wanavyotoa ridhaa ya kushiriki maelezo ya makazi yao ya kibinafsi na kutoa data inayoonyesha kiasi cha maudhui yaliyoondolewa kufuatia maombi ya serikali yanayohusiana na faragha.

Maelezo ya ombi la Meta

Mwaka uliopita, Meta iliomba maoni ya ushauri wa sera kutoka kwa Bodi kuhusu kushiriki anwani na picha za makazi ya kibinafsi na muktadha ambapo maelezo haya yanaweza kuchapishwa kwenye Facebook na Instagram. Meta inazingatia hili kama swali gumu kwa kuwa ingawa ufikiaji wa maelezo kama hayo unaweza kuwa muhimu kwa uanahabari na uanaharakati wa kiraia, “kuweka maelezo haya kwa umma kunaweza kusababisha hatari kwa usalama wa wakazi na kukiuka faragha ya mtu binafsi.”

Ombi la Meta lilibaini madhara kadhaa yanayoweza kuhusishwa na utoaji wa maelezo ya kibinafsi, ikijumuisha anwani na picha za makazi. Hii inajumuisha “doxing,” (ambayo inarejelea utoaji wa nyaraka, unaofupishwa kama “dox”) ambapo maelezo yanayoweza kumtambulisha mtu yamefichuliwa mtandaoni. Meta ilisema kwamba ufichuaji wa maelezo yanayoweza kumtambulisha mtu unaweza kuwa na madhara hasi katika ulimwengu halisi, kama vile unyanyasaji au unyemeleaji.

Matokeo muhimu

Chini ya Viwango vya Jumuiya ya Facebook kuhusu Ukiukaji wa Faragha, watumiaji hawafai kushiriki “maelezo yanayoweza kutambulisha mtu kuhusu wewe au watu wengine,” ikijumuisha anwani, “isipokuwa kama zimeshirikiwa au kuombwa ili kuendeleza shughuli za hisani, kutafuta watu, wanyama, au vitu vilivyopotea, au kuwasiliana na watoa huduma ya biashara.”

Hii pia inajumuisha “maelezo ya kibinafsi” kama “picha zinazoonyesha maoni ya nje ya makazi ya kibinafsi.” Picha kama hizo zinaweza tu kuondolewa, hata hivyo, ikiwa masharti yote yafuatayo yanatumika: “Makazi ni ya familia moja, au nambari ya kitengo cha makazi inatambuliwa kwenye picha/maelezo. Jiji/ujirani au msimbo wa GPS (kwa mfano, msimbo kutoka Ramani ya Google) umetambuliwa Maudhui yanatambua makazi hayo. Makao hayo yanalenga kufichuliwa kwa makao yao ya kibinafsi au kuna muktadha wa kupanga maandamano dhidi ya makao (hii haijumuishi ubalozi ambao pia ni makao).”

Sera ya Facebook ya Ukiukaji wa Faragha inasema kwamba “maelezo ya faragha yanaweza kupatikana hadharani kupitia utangazaji wa habari, uandikishaji mahakamani, matangazo ya vyombo vya habari, au vyanzo vingine. Hiyo ikifanyika, Meta inaweza kuruhusu maelezo hayo yachapishwe. Kwa mfano, ikiwa anwani ya mtu inazingatiwa kuwa “inapatikana kwa hadhara,” picha zitaruhusiwa kwenye Facebook na Instagram zinazomtambulisha mtu huyo na anwani. Mwongozo wa ndani wa Meta iliotolewa kwa wakaguzi wa maudhui unasema kwamba maelezo “yaliyochapishwa na angalau vyombo vitano vya habari” si maelezo ya faragha tena kwa madhumuni ya sera ya Ukiukaji wa Faragha ya Facebook.

Bodi inaelewa kwamba kushiriki anwani ya makazi ya kibinafsi na picha kunawakilisha ukiukaji unaoweza kuwa mbaya zaidi wa haki ya faragha kwa watu wanaotumia Facebook na Instagram na wale amba hawazitumii.

Pindi tu maelezo haya yakishirikiwa, madhara yake yanayoweza kutokea kama vile ufichuzi wa maelezo, si rahisi kusuluhisha. Madhara yanayotokana na ufichuzi wa maelezo huathiri kwa njia isiyo sawa makundi kama vile ya wanawake, watoto na watu wa kundi la LGBTQIA+, na yanaweza kuwa ya kusababisha msongo wa mawazo, watu kupoteza ajira na hata madhara ya kimwili au kifo.

Kwa kuwa uwezekano wa kutokea madhara hutegemea muktadha mahususi, kuna changamoto ya kuunda viashiria yakinifu na ya kibia vinavyoweza kuruhusu wakaguzi wa maudhui kutofautisha ushirikiaji wa maudhui yanayoweza kusababisha madhara dhidi ya ule ambao hauwezi kuwa na madhara. Hiyo ndiyo sababu Bodi inaamini kwamba sera ya Ukiukaji wa Faragha inapaswa kuwa ya kulinda faragha zaidi.

Viwango vya kimataifa vya haki za binadamu vinaruhusu vizuizi muhimu na linganifu dhidi ya semi ili kulinda haki ya watu kwa faragha. Kutokana na hayo, Bodi inapendelea kupunguza hali hizo za kipekee kwa sera ya Ukiukaji wa Faragha ili kusaidia Meta kulinda maelezo ya makazi ya kibinafsi vyema zaidi kwa watu walio kwenye au nje ya majukwaa yake.

Katika mawasiliano yake na Bodi, Meta ilisisitiza kwamba “kuhakikisha kwamba ufafanuzi wa “kupatikana hadharani” haufungii nje maudhui yanayoondolewa kwa sababu ya kuweka hatari kusababisha madhara ya nje ya mtandao” ni “wasiwasi wa kudumu.” Rekodi za umma na vyanzo vingine vya kile kinachoweza kuzingatiwa kama maelezo “maelezo yanayopatikana hadharani” bado zinahitaji rasilimali na juhudi ili kufikiwa na umma kwa jumla. Kwenye mtandao wa kijamii, hata hivyo maelezo kama hayo yanaweza kushirikiwa na kufikiwa kwa haraka zaidi, na kwa kiwango kikubwa zaidi, hali inayongeza hatari ya madhara pakubwa. Kutokana na hayo, Bodi inapendekeza kuondolewa kwa hali ya kipekee ya “kupatikana hadharani” kwa ushirikiaji wa anwani pamoja na picha za makazi ya kibinafsi zinazoafiki vigezo fulani.

Mapendekezo ya Bodi ya Usimamizi

Katika maoni ya ushauri wa sera, Bodi imetoa mapendekezo 17 ambayo yanashughulikia sera ya maudhui, utekelezaji na uwazi.

Kuhusu sera ya maudhui, Meta inafaa:

1. Iondoe hali ya kipekee inayoruhusu mtu kushiriki maelezo ya makazi ya kibinafsi yanapozingatiwa kuwa “yanapatikana hadharani.” Hii inamaanisha Meta haitaruhusu tena maudhui ambayo vinginevyo ni ya ukiukaji kwenye Facebook na Instagram ikiwa “yamechapishwa na angalau vyombo vitano vya habari” au ikiwa yana anwani au picha za makazi kutoka kwenye rekodi au taarifa za kifedha za shirika, rekodi za mahakama, leseni za kitaalamu na biashara, sajili za wakosaji wa kingono au taarifa kwa vyombo vya habari kutoka katika mashirika ya serikali au watekelezaji wa sheria.

2. Ihakikishe kwamba muktadha wa kipekee wa kustahiki kuwa habari umetekelezwa kwa njia sawa. Kama ilivyopendekezwa katika pendekezo la 3 katika kesi ya maandamano ya Kolombia (2021-010-FB-UA), Meta inafaa kuunda na kutangaza kigezo wazi kwa wakaguzi wa maudhui kuwasilisha maudhui ambayo yana uwezekano wa kukiuka Viwango vya Jumuiya lakini yanaweza kustahiki kuruhusu ustahiki wa habari kwa ajili ya ukaguzi wa ziada kwa maslahi ya umma. Kutokana na kujadiliwa kwake katika kesi nyingi, Bodi ingependa kuchunguza utekelezaji wa muktadha wa kipekee wa ustahiki wa habari katika maoni yake ya ushauri wa sera ya siku zijazo.

3. Iruhusu ushirikiaji wa “picha zinazoonyesha mwonekano wa nje wa makazi ya kibinafsi” wakati mali hiyo inayoonyesha ndiyo inaangaziwa katika hadithi ya habari, hata wakati masharti yafuatayo yaliyoorodheshwa kwenye Viwango vya Jumuiya kuhusu Ukiukaji wa Faragha yametimizwa (“Makazi hayo ni nyumbani kwa familia moja, au nambari ya nyumba ya mkazi imetambuliwa kwenye picha/manukuu. Jiji/ujirani au msimbo wa GPS (kwa mfano, msimbo kutoka Ramani ya Google) umetambuliwa Maudhui yanatambua makazi hayo. Mkazi huyo anapinga kufichuliwa kwa makazi yake ya kibinafsi.”) Hata hivyo, Meta haifai kuruhusu mtu kushiriki picha za makazi ya kibinafsi wakati kuna “muktadha wa kupanga maandamano dhidi ya makazi hayo.”

4. Iruhusu kupangwa kwa maandamano katika makazi rasmi yanamilikiwa kwa umma. Meta inafaa kuruhusu uchapishaji wa anwani na picha za makazi rasmi zilizopewa maafisa wa ngazi za juu serikalini, kama vile rais, wakuu wa serikali za jimbo au mtaa, mabalozi na wajumbe. Maafisa wa ngazi za juu serikalini kwa jumla wanatarajiwa kuvumilia hali ya kutokuwa na faragha sana, haswa katika maeneo wanapofanyia kazi na kupokea ulinzi ulioimarishwa na maafisa wa usalama. Pendekezo hili linapendekeza kuruhusiwa kwa upangaji wa maandamano katika makazi rasmi yanayomilikiwa kwa umma, si makazi ya kibinafsi ya maafisa wa serikali.

5. Iruhusu kushirikiwa kwa anwani za makazi ya kibinafsi zinapochapishwa na watumiaji husika wenyewe au ikiwa mtumiaji ameridhia kuchapishwa kwake. Kama chaguo-msingi, watumiaji wanafaa kuzingatiwa kuwa hawajatoa ridhaa kama hiyo.

6. Ihakikishe watumiaji wana mbinu ya haraka na ya ufanisi ya kuomba kuondolewa kwa maelezo ya faragha yaliyochapishwa na watu wengine.

7. Ieleze kwa uwazi zaidi kwenye sera ya Ukiukaji wa Faragha ya Facebook wakati ufichuzi wa jiji ambapo makazi fulani yapo utakuwa ni msingi wa maudhui hayo kuondolewa (m.f., kwa kurejelea upeo mahususi wa idadi ambapo kushiriki jiji pekee kama sehemu ya maudhui hayo hakutazingatiwa kama ukiukaji tena.)

8. Ieleze kwenye sera ya Ukiukaji wa Faragha ya Facebook vigezo vyake vya kutathmini iwapo mkazi huyo ametambuliwa vya kutosha kwenye maudhui hayo. Meta inafaa kueleza iwapo jina kamili au sehemu ya majina ya mtu inahitaji kufichuliwa, pamoja na maelezo ya makazi yake, au iwapo picha na/au maelezo fulani ya kijumla zaidi kwa makisio yanaweza kuna na msingi.

9. Ieleze watumiaji kwamba inatekeleza Viwango vya Jumuiya ya Facebook kwenye Instagram, ikiwa na hali kadhaa mahususi za kipekee, na ijumuishe kiungo kwenye Viwango vya Jumuiya ya Facebook kuhusu Ukiukaji wa Faragha katika ya Miongozo ya Jumuiya ya Instagram.

Kuhusu utekelezaji, Meta inafaa:

10. Iruhusu watumiaji wanaoripoti maudhui yanaweza kuwa ya ukiukaji wa sera ya Ukiukaji wa Faragha watoe muktadha wa ziadi kuhusu madai yao.

11. Iunde kituo mahususi cha mawasiliano kwa waathiriwa wa ufichuzi wa maelezo, kinachopatikana kwa watu wanaotumia majukwaa yake na wasioyatumia. Kituo hiki kinafaa kufikiwa kwa urahisi, kiruhusu waathiriwa kueleza kwa kina hali yao na hatari ambayo maudhui hayo yamewasababishia na hatua ya haraka kutoka kwa kampuni hiyo. Meta inafaa kuipa hatua kipaumbele wakati mtu aliyeathirika amesema kwamba yeye ni kutoka kundi la watu walio katika hatari zaidi kwa usalama wao katika eneo ambapo makazi ya kibinafsi yapo.

12. Izingatie ukiukaji wa sera yake ya Ukiukaji wa Faragha kama “mbaya” pale ambapo kushiriki maelezo ya makazi ya kibinafsi ya kunahusiana kwa wazi na vitendo vya njama vilivyosababisha hatari ya vurugu au unyanyasaji. Hii itasababisha akaunti kusimamishwa kwa muda.

13. Iwape watumiaji fursa ya kuondoa au kuhariri maelezo ya faragha ndani ya maudhui yao wakati yameondolewa kwa ukiukaji wa sera ya Ukiukaji wa Faragha. Mtumiaji akiondoa au kuhariri maelezo ya makazi ya faragha kwenye maudhui hayo ndani ya muda fulani wa makataa, uzuiaji wa muda wa maudhui hayo utaondolewa.

14. Iruhusu watumiaji waashirie kwenye rufaa zao kwa Meta kwamba maudhui yao yanapatikana katika muktadha wa kipekee wa sera ya Ukiukaji wa Faragha.

Kuhusu uwazi, Meta inafaa:

15. Ichapishe data kadirifu kuhusu utekelezaji wa sera ya Ukiukaji wa Faragha kwenye Ripoti ya Utekelezaji wa Viwango vya Jumuiya ya kampuni hiyo.

16. Ipange data katika ripoti yake kuhusu Vizuizi vya Maudhui Kulingana na Sheria ya Ndani ili kuonyesha kiasi cha maudhui kilichoondolewa kufuatia maombi ya serikali yanayohusiana na faragha, hata kama maudhui hayo yaliondolewa chini ya sera ya Ukiukaji wa Faragha wala si chini ya sheria za ndani za faragha.

17. Iwape watumiaji maelezo zaidi kuhusu sera mahususi kwenye Viwango vya Jumuiya kuhusu Ukiukaji wa Faragha ambayo maudhui yao ilipatikana kwamba inakiuka. Meta inafaa kutekeleza hili kwenye lugha zote zinazotumika katika majukwaa yake.

Kwa maelezo zaidi:

Kwenye kiambatisho kilicho hapo chini, unaweza kupata viungo vya nyaraka zifuatazo:

  • Ombi asili la maoni ya ushauri wa sera kutoka Meta.
  • Sasisho la sera lililopkelewa kutoka Meta.
  • Kiambatisho cha maoni ya umma yaliyopokelewa kwa maoni haya ya ushauri wa sera.
  • Toleo kamili ya maoni ya ushauri wa sera ya Bodi.

Voltar para Decisões de Casos e Pareceres Consultivos sobre Políticas