Overturned
Shairi la Kisiasa la Korea
April 4, 2024
Mtumiaji alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuondoa picha kwenye Facebook ya shairi la Kikorea kwa jina “The Scream of General Hong Beom-Do” lililoandikwa na Lee Dong Soon. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hiyo, kampuni hiyo ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na ikarejesha chapisho hilo.
Huu ni uamuzi kwa ufupi.Uamuzi wa ufupi huchunguza kesi ambapo Meta imebatilisha uamuzi wake wa kwanza kuhusu kipande cha maudhui baada ya Bodi kupeleka kesi hiyo kwa kampuni na kujumuisha taarifa kuhusu makosa ambayo Meta imekiri. Huwa unaidhinisha na jopo la Wanachama wa Bodi, badala ya Bodi kamili, hauhusishi maoni ya umma na hayana thamani ya kutumika katika marejeleo ya Bodi. Maamuzi kwa ufupi huleta mabadiliko moja kwa moja kwenye maamuzi ya Meta, yakitoa uwazi kuhusu masahihisho haya, huku pia yakitambua maeneo ambayo Meta inaweza kuboresha utekelezaji wake.
Muhtasari wa Kesi
Mtumiaji alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuondoa picha kwenye Facebook ya shairi la Kikorea kwa jina “The Scream of General Hong Beom-Do” lililoandikwa na Lee Dong Soon. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hiyo, kampuni hiyo ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na ikarejesha chapisho hilo.
Maelezo na Historia ya Kesi
Mnamo Septemba 2023, mtumiaji wa Facebook alichapisha picha ya shairi la Kikorea lenye mada “The Scream of General Hong Beom-Do” lake Lee Dong Soon, ambalo linasuta jaribio la mamlaka kutaka kuhamisha sanamu ya jenerali. Shairi hilo linaeleza kisanaa hisia za Hong Beom-Do kuhusu pendekezo la kuhamisha sanamu hiyo, na lilijumuisha neno “wae-nom” (왜놈), ambalo tafsiri yake ya moja kwa moja ni “mtu kutoka Japani.” Hata hivyo, lilikuwa linatumika kihistoria na Wakorea kama neno la jumla la kurejelea wavamizi wa Kijapani wakati wa Wajapani walitawala Korea. Miaka mingi baadaye, limetumika kwa njia ya ukiukaji, kama neno la matusi lenye maana ya “Wanaharamu wa Japani” au watu waovu. Chapisho hilo lilitazamwa chini ya mara 500.
Hong Beom-Do alikuwa mtu maarufu mapema karne ya 20 nchini Korea wakati eneo hilo lilikuwa chini ya utawala wa Japani. Alikuwa mwanaharakati na jenerali ambaye aliongoza Jeshi la Uhuru la Korea katika ushindi mwingi tajika katika vita dhidi ya majeshi ya Japani. Mtumiaji alichapisha maudhui haya katika kipindi ambapo kuliongezeka mgogoro wa kiitikadi miongoni mwa wanasiasa kuhusiana na pendekezo la kuhamisha sanamu ya jenerali kutoka katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi la Korea kwa sababu ya kujihusisha kwake awali na majeshi ya kikomunisti ya Soviet. Mtazamo wa Wizara ya Ulinzi wa kuhamisha sanamu yake ulikumbana na pingamizi kubwa la umma.
Lee Dong Soon pia alichapisha shairi hilo kwenye Facebook, lakini lililondolewa na Meta kwa kukiuka sera yake dhidi ya Matamshi ya Chuki, hatua ambayo ilisababisha mzozo. Baada ya shairi kuondolewa, watumiaji walianza vuguvugu la kushiriki shairi hilo kwingineko kwenye Facebook.
Meta awali iliondoa chapisho la mtumiaji kwenye Facebook chini ya Viwango vyake vya Jumuiya kuhusu Usemi wa Chuki, kwa maudhui yanayolenga “mtu au kikundi cha watu [kulingana na] sifa zinazolindwa [kupitia] kulaani.’’ Sera hiyo inafafanua kulaani kuwa “maneno au kauli chafu ... zenye nia ya kutusi.’’
Baada ya Bodi kufahamisha Meta kuhusu kesi hii, kampuni hiyo iliabaini kuwa neno “wae-nom” katika shairi hili halikutumika kama neno la laana, ila kama ufafanuzi wa wanajeshi wa Japani kama wavamizi. Kwa hivyo, maudhui hayo hayakukiuka Viwango vya Jumuiya kuhusu Matamshi ya Chuki na hatua ya kuyaondoa haikuwa sahihi. Kampuni hiyo kisha ilirejesha maudhui hayo kwenye Facebook.
Mamlaka na Upeo wa Bodi
Bodi ina mamlaka ya kukagua uamuzi wa Meta kufuatia rufaa kutoka kwa mtumiaji ambaye maudhui yake yaliondolewa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria ndogo za Kifungu cha 3, Sehemu ya 1).
Pale ambapo Meta inathibitisha kwamba ilikosea na ibatilishe uamuzi wake katika kesi inayoratibiwa kukaguliwa na Bodi, Bodi inaweza kuchagua kesi hiyo ili kuifanyia uamuzi kwa ufupi (Sheria ndogo Kifungu cha 2, Sehemu ya 2.1.3). Bodi hukagua uamuzi wa kwanza ili kuongeza ufahamu wa michakato ya uratibu wa maudhui, kupunguza makosa na kuongeza haki kwa watumiaji wa Facebook na Instagram.
Umuhimu wa Kesi
Kesi hii inaonyesha chapisha ambazo Meta hukumbana nazo katika kutekeleza sera yake dhidi ya Matamshi ya chuki, hususan inaposhughulikia kujieleza kisanaa na marejeleo ya kihistoria.
Kesi hii inafanana na uamuzi wa awali, kesi ya Shairi la Kirusi, ambayo Bodi ilibatilisha uamuzi wa awali wa Meta wa kuondoa chapisha chini ya sera yake dhidi ya Matamshi ya chuki ambalo lilitusi Warusi na kulinganisha jeshi la Urusi linaloviamia Ukraini na Wanazi. Katika uamuzi huu, Bodi ilibainishwa kwamba kukosa kuzingatia muktadha wa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraini wakati wa uratibu wa maudhui kwa wingi kulizuia uwezekano wa kueleza maoni kuhusu masuala ya mapendeleo ya umma. Bodi pia imetoa mtazamo katika kesi nyingi, kama vile katika maamuzi ya Kurejesha Maneno ya Kiarabu na Sifu kwa Mungu, kwamba matatizo ya kukosa kueleza dhana za kitamaduni na kiisimu yanaweza kusababisha utekelezaji usio sahihi wa sera za Meta.
Bodi imetoa mapendekezo ya kuboresha utekelezaji wa sera ya Meta dhidi ya Matamshi ya chuki katika muktadha unaofaa wa kitamaduni. Katika uamuzi wa awali, Bodi iliomba Meta “ifanye tathmini za usahihi zinazolenga posho za sera dhidi ya Matamshi ya Chuki zinazoshughulikia usemi kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu (m.f., kulaani, kutoa uhamasisho,” ( uamuzi kuhusu Mkanda wa Wampum, pendekezo nambari 3). Meta imetekeleza pendekezo hili kama ilivyoonyeshwa kupitia taarifa zilizochapishwa.
Bodi inaamini kuwa utekelezaji kamili wa mapendekezo haya unaweza kuchangia kupungua kwa idadi ya makosa ya utekelezaji chini ya sera ya Matamshi ya Chuki. Makosa haya huhusishwa mara nyingi na ukosefu wa hali ya maana zinazokaribiana, muktadha na uchambuzi wa kiisimu katika muktadha mahususi.
Uamuzi
Bodi imebatilisha uamuzi wa awali wa Meta wa kuondoa maudhui hayo. Bodi inatambua masahihisho ambayo Meta ilifanya kwenye kosa la kwanza baada ya Bodi kujulisha Meta kuhusu kesi hiyo.