पलट जाना
Makala ya Washington Post kuhusu Israeli na Upalestina
4 अप्रैल 2024
Mtumiaji alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuondoa chapisho la Facebook lenye kiungo cha makala ya Washington Post yaliyozungumzia mpangilio wa matukio ya mgogoro baina ya Israeli naUpalestina. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hiyo, kampuni hiyo ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na ikarejesha chapisho hilo.
Huu ni uamuzi kwa ufupi.Uamuzi wa ufupi huchunguza kesi ambapo Meta imebatilisha uamuzi wake wa kwanza kuhusu kipande cha maudhui baada ya Bodi kupeleka kesi hiyo kwa kampuni na kujumuisha taarifa kuhusu makosa ambayo Meta imekiri. Huwa unaidhinisha na jopo la Wanachama wa Bodi, badala ya Bodi kamili, hauhusishi maoni ya umma na hayana thamani ya kutumika katika marejeleo ya Bodi. Maamuzi kwa ufupi huleta mabadiliko moja kwa moja kwenye maamuzi ya Meta, yakitoa uwazi kuhusu masahihisho haya, huku pia yakitambua maeneo ambayo Meta inaweza kuboresha utekelezaji wake.
Muhtasari wa Kesi
Mtumiaji alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuondoa chapisho la Facebook lenye kiungo cha makala ya Washington Post yaliyozungumzia mpangilio wa matukio ya mgogoro baina ya Israeli naUpalestina. Baada ya Bodi kuifahamisha Meta kuhusu rufaa hiyo, kampuni hiyo ilibatilisha uamuzi wake wa kwanza na ikarejesha chapisho hilo.
Maelezo na Historia ya Kesi
Mnamo Oktoba 2023, mtumiaji wa Facebook alichapisha kiungo cha makala ya Washington Post yaliyozungumzia mpangilio wa matukio wa mgogoro baina ya Israeli na Upalestina. Toleo la awali la makala hayo, ambalo lilijumuishwa kiotomatiki na kiungo hicho, linataja Hamas. Mtumiaji hakuweka manukuu ili kuambatana na chapisho au kutoa muktadha wowote wa ziada.
Chapisho hili la Facebook liliondolewa chini ya sera ya Meta dhidi ya Watu na Mashirika Hatari, inayokataza uwakilishi wa kauli fulani kuhusu vikundi na watu ambao kampuni hiyo inazingatia kwa wanahusishwa na madhara makubwa halisi.
Katika rufaa yake kwa Bodi, mtumiaji alisisitiza kwamba chapisho ilo lilinuia kuripti kuhusu mgogoro unaoendelea sasa kati ya Israel-Hamas na halikunuia kuonyesha uungwaji mkono wa Hama au shirika lolote lingine hatari.
Baada ya Bodi kujulisha Meta kuhusu kesi hii, kampuni hiyo ilibaini kuwa maudhui hayo hayakukiuka sera yake dhidi ya Watu na Mashirika Hatari kwa kuwa chapisho hilo linarejelea Hamas katika muktadha wa kuripoti habari, ambao unarhusiwa chini ya sera hii. Kampuni hiyo kisha ilirejesha maudhui hayo kwenye Facebook.
Mamlaka na Upeo wa Bodi
Bodi ina mamlaka ya kukagua uamuzi wa Meta kufuatia rufaa kutoka kwa mtu ambaye maudhui yake yaliondolewa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria ndogo za Kifungu cha 3, Sehemu ya 1).
Pale ambapo Meta inathibitisha kwamba ilikosea na ibatilishe uamuzi wake katika kesi inayoratibiwa kukaguliwa na Bodi, Bodi inaweza kuchagua kesi hiyo ili kuifanyia uamuzi kwa ufupi (Sheria ndogo Kifungu cha 2, Sehemu ya 2.1.3). Bodi hukagua uamuzi wa kwanza ili kuongeza ufahamu wa michakato ya uratibu wa maudhui inayohusika, kupunguza makosa na kuongeza haki kwa watumiaji wa Facebook na Instagram.
Umuhimu wa Kesi
Kesi hii inaangazia tukio la Meta kutekeleza kupitia kiasi sera yake dhidi ya Watu na Mashirika Hatari, hususan kuripoti habari kuhusu mashirika ambayo kampuni hiyo imebainishwa kuwa hatari. Hili ni tatizo linalojirudia, ambalo limekuwa likitokea mara kwa mara wakati wa mgogoro wa sasa kati ya Israel-Hamas, ambapo mojawapo ya mashirika limebainishwa kuwa hatari. Bodi imetoa mapendekezo kadhaa yanayohusiana na posho la kuripoti habari chini ya sera yake dhidi ya Watu na Mashirika Hatari. Makosa yanayoendelea katika utekelezaji wa posho hii muhimu inaweza kuzuia pakubwa uhuru wa kujieleza, uwezo wa umma kufikia taarifa na kuhujumu majadiliano ya umma.
Katika uamuzi wa awali, Bodi ilipendekeza kwamba “Meta inapaswa kutathmini usahihi wa wakaguzi kutekeleza posho ya kuripoti chini ya sera ya Mashirika na Watu Binafsi Hatari ili kubaini masuala ya kimfumo yanayosababisha makosa ya utekelezaji ( Kutajwa kwa Taliban katika Kuripoti Habari, pendekezo la nambari 5); Meta iliripoti utekelezaji kama kazi ambayo tayari ilikuwa imefanya, bila kuchapisha maelezo ya kuonyesha hivyo. Katika kesi ya awali, Bodi ilipendekeza kwamba Meta “iweke vigezo na mifano ya kuonyesha kwenye sera yake ya Watu na Mashirika Hatari ili kuongeza uelewa wa vighairi kwa ajili ya majadiliano yasiyoegemea upande wowote, kukashifu na kuripoti habari,” ( Chapisho la Al Jazeera Lililoshirikiwa, pendekezo nambari 1). Utekelezaji wa pendekezo hili ulionyeshwa kupitia taarifa zilizochapishwa. Isitoshe, Bodi ilipendekeza kwamba Meta “ijumuishe maelezo tondoti zaidi kuhusu viwango vya makosa vya utekelezaji wa kanuni kuhusu ‘kutukuza’ na ‘kuunga mkono’ za watu binafsi na mashirika hatari,” (Kutengwa kwa Ocalan, pendekezo nambari 12). Meta ilikataa kutekeleza pendekezo hili baada ya kufanya tathmini ya uwezekano. Katika sasisho la sera zake la tarehe 29 Desemba 2023, Meta sasa inatumia neno “kutukuza” badala ya “kusifu” katika Viwango vyake vya Jumuiya.
Bodi inaamini kwamba utekelezaji kamili wa mapendekezo haya unaweza kupunguza idadi ya makosa ya utekelezaji chini ya sera ya Meta dhidi ya Watu na Mashirika Hatari.
Uamuzi
Bodi imebatilisha uamuzi wa awali wa Meta wa kuondoa maudhui hayo. Bodi inatambua masahihisho ambayo Meta ilifanya kwenye kosa la kwanza baada ya Bodi kujulisha Meta kuhusu kesi hiyo.