Anulado

Chapisho kwa Kipolandi Linalolenga Watu Waliobadilisha Jinsia

Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa kwanza wa Meta wa kuacha chapisho kwenye Facebook ambapo mtumiaji alilenga watu wanaobadilisha jinsia zao kwa usemi wa vurugu unaowataka wanachama wa kikundi hiki kujitoa uhai.

Tipo de decisión

Estándar:

Políticas y temas

Tema
LGBT, Igualdad de sexo y género

Regiones/Países

Ubicación
Polonia

Plataforma

Plataforma
Facebook

Ili kusoma uamuzi huu kwa Kipolandi, bofya hapa.

Kliknij tutaj, aby przeczytać postanowienie w języku polskim.

Muhtasari

Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa kwanza wa Meta wa kuacha chapisho kwenye Facebook ambapo mtumiaji alilenga watu wanaobadilisha jinsia zao kwa usemi wa vurugu unaowataka wanachama wa kikundi hiki kujitoa uhai. Bodi imepata chapisho hilo kuwa linakiuka Viwango vya Jumuiya vya Matamshi ya Chuki na Kujitoa Uhai na Kujijeruhi. Hata hivyo, suala kuu katika kesi hii halihusu sera hizi, bali linahusu utekelezaji wake. Meta kukosa kuchukua hatua sahihi ya utekelezaji mara kwa mara, licha ya ishara kadhaa kuhusu maudhui hatari ya chapisho hili, kumefanya Bodi kuhitimisha kuwa kampuni hii haitimizi kanuni ambazo imebainisha kuhusu usalama wa watu katika kundi la LGBTQIA+. Bodi inahimiza Meta kukabiliana na changamoto za utekelezaji, ikiwa ni pamoja na kuboresha mwongozo wa ndani kwa wakaguzi.

Kuhusu Kesi

Mnamo Aprili 2023, mtumiaji wa Facebook nchini Polandi alichapisha picha ya pazia yenye michirizi ya rangi za buluu, pinki na nyeupe ya bendera ya watu wanaobadilisha jinsia zao, maandishi yaliyo kwa Kipolandi yakisema, “Teknolojia mpya … Pazia zinazojitia kitanzi,” na zaidi ya hayo, “usafishaji wa mpukutiko <3.” Wasifu wa mtumiaji unajumuisha maelezo, “I am a transphobe.” (mimi nina chuki dhidi ya watu wanaobadilisha jinsia zao) Chapisho limepata hisia chini ya mara 50.

Kati ya Aprili na Mei 2023, watumiaji 11 tofauti waliripoti chapisho hilo jumla ya mara 12. Ni ripoti mbili tu kati ya 12 zilizopewa kipaumbele na mifumo otomatiki ya Meta ili zikaguliwe na binadamu, zingine zikifungwa. Ripoti mbili zilizotumwa ili kukaguliwa na binadamu, ili kubaini uwezekano wao wa kukiuka vya Viwango vya Jumuiya Facebook kuhusu Kujitoa Uhai na Kujijeruhi, zilipatikana kuwa si za ukiukaji. Hakuna ripoti yoyote inayotokana na Matamshi ya Chuki iliyotumwa kwa ukaguzi wa binadamu.

Watumiaji watatu kisha walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuacha chapisho hilo la Facebook, huku rufaa ya mmoja ikisababisha ukaguzi wa binadamu uliounga mkono uamuzi wa kwanza kulingana na Viwango vya Jumuiya kuhusu Kujitoa Uhai na Kujijeruhi. Vilevile, rufaa zingine, zilizokatwa chini ya Viwango vya Jumuiya kuhusu Matamshi ya Chuki, hazikutumwa kwa ukaguzi wa binadamu. Hatimaye, mmoja wa watumiaji ambaye aliripoti maudhui hapo awali alikata rufaa kwa Bodi. Kutokana na hatua ya Bodi kuchagua kesi hii, Meta ilibaini kuwa chapisho hili lilikiuka sera zake dhidi ya Matamshi ya Chuki na Kujitoa Uhai na Kujijeruhi na ikayaondoa kwenye Facebook. Isitoshe, kampuni hii ilifunga akaunti ya mtumiaji aliyechapisha maudhui haya kwa ukiukaji kadhaa wa awali.

Matokeo Makuu

Bodi ilipata kuwa maudhui haya yanakiuka sera ya Meta ya Matamshi ya Chuki kwa sababu yanajumuisha “usemi wa vurugu” kwa namna ya mwito wa kifo cha wanakikundi cha watu wenye sifa zinazolindwa kwa kujitoa uhai. Chapisho hilo, ambalo linahimiza watu wanaobadilisha jinsi zao kujitia kitanzi, liliweka mazingira ya vitisho na ubaguzi na lingechangia madhara ya kimwili. Kwa kuzingatia hali ya maandishi na picha, chapisho hilo pia lilizidisha janga la afya ya akili ambalo watu wa jamii ya wanaobadilisha jinsia zao wanapitia. Ripoti ya hivi karibuni ya Muungano wa Mashoga na Wasaganaji Dhidi ya Kushushwa Hadhi (GLAAD) ilibaini “athari kubwa ya kisaikolojia ya kuwa katika hali ya kukabiliwa na ubaguzi na tabia za chuki mara kwa mara” mtandaoni. Bodi imepata ushahidi zaidi wa hitimisho lake katika muktadha mpana wa madhara ya mtandaoni na ya nje ya mtandao ambayo jamii ya LGBTQIA+ inakabiliwa nayo nchini Polandi, ikijumuisha kushambuliwa na semi kali za kisiasa na watu mashuhuri na wenye ushawishi serikalini.

Bodi ina wasiwasi kuwa wakaguzi binadamu wa Meta walishindwa kubaini viashiria vya kimuktadha. Kwa kuwa chapisho hilo linarejelea hatari ya juu ya kujitoa uhai (“pazia zinazojining’iniza”) na kuunga mkono kifo cha kikundi (“usafishaji wa mapukutiko”), huu ulikuwa ukiukaji wa wazi wa Viwango vya Jumuiya kuhusu Matamshi ya Chuki, huku utambulisho binafsi wa mtayarishi wa maudhui hayo kama mtu anayechukua watu wanaobadilisha jinsia zao, pekee, ungekuwa ni ukiukaji mwingine. Bodi inahimiza Meta kuboresha usahihi wa utekelezaji wa sera ya matamshi ya chuki dhidi ya watu wa LGBTQIA+, hususan wakati chapisho linajumuisha picha na maandishi yanayohitaji muktadha ili kufasiri. Katika kesi hii, marejeleo ya kujitoa uhai kwa lugha fiche pamoja na taswira inayoonyesha kikundi kinacholindwa (bendera ya watu wanaobadilisha jinsia zao) yalichukua mtindo wa “ubunifu wa kudhuru.” Hii inarejelea watumiaji wenye nia mbaya kuunda njia mpya za kulenga jamii ya LGBTQIA+ kupitia machapisho na meme wanazotetea kama zenye “ucheshi au kejeli” lakini hakika ni za chuki au unyanyasaji.

Isitoshe, Bodi ina wasiwasi kuhusu taarifa ya Meta kwamba wakaguzi binadamu kukosa kuondoa maudhui hayo kunaambatana na utekelezaji madhubuti wa miongozo yake ya ndani. Hii inaweza kuashiria kuwa mwongozo wa ndani wa Meta haujanasa ipasavyo jinsi maandishi na picha zinaweza kuingiliana ili kuwakilisha kikundi kinachofafanuliwa na utambulisho wa kijinsia wa wanachama wake.

Ingawa chapisho hilo pia lilikiuka kwa wazi Viwango vya Jumuiya ya Facebook kuhusu Kujitoa Uhai na Kujijeruhi, Bodi imegundua kuwa sera hii inapaswa kupiga marufuku kwa uwazi zaidi maudhui yanayohimiza kitendo cha kujitoa uhai yanayolenga kikundi cha watu kinachoweza kutambuliwa, tofauti na ikiwa ni mtu pekee kwenye kikundi hicho.

Katika kesi hii, mifumo ya kuweka vipaumbele kwa ukaguzi ya kiotomatiki iliathiri pakubwa utekelezaji, ikijumuisha jinsi kampuni hii inavyoshughulikia ripoti kadhaa kuhusu maudhui yale yale. Meta hufuatilia na kuondoa urudiaji (huondoa) ripoti hizi ili “kuhakikisha usawa katika maamuzi ya wakaguzi na hatua za utekelezaji.” Sababu nyingine zilizotolewa za ripoti kufungwa kiotomatiki ni pamoja na kina cha chini na maudhui kutovuma sana (idadi ya mionekano ambayo maudhui imepata kwa jumla), hii ikiashiria kuwa hayakupewa kipaumbele ili kukaguliwa na binadamu. Katika kesi hii, Bodi inaamini kuwa wasifu wa mtumiaji ungezingatiwa kama mojawapo ya ishara muhimu wakati wa kubaini alama za kina.

Bodi inaamini kwamba Meta ingepaswa kuwekeza zaidi katika kuunda viainishaji vinavyotambua maudhui yenye uwezekano wa kuwa ya ukiukaji yanayoathiri jamii ya LGBTQIA+ na kuboresha mafunzo kwa wakaguzi binadamu kuhusu madhara yanayohusiana na utambulisho kwa kijinsia.

Uamuzi wa Bodi ya Usimamizi

Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa awali wa Meta wa kuacha maudhui hayo.

Bodi inapendekeza kwamba Meta:

  • Ibainishe kwenye ukurasa wake wa Kujitoa Uhai na Kujijeruhi kwamba sera hiyo inapiga marufuku maudhui yanayoendeleza au kuhimiza kitendo cha kujitoa uhai yanayolenga kikundi cha watu wanaoweza kutambuliwa.
  • Ifanyie marekebisho, mwongozo wa ndani inayowapatia wakaguzi kwa kiwango ili kuhakikisha kuwa taswira zinazoonyeshwa kwenye bendera za utambulisho wa kijinsia ambazo hazina sura ya binadamu zinaeleweka kama viwakilishi vya kikundi kinachofafanuliwa na utambulisho wa kijinsia wa wanachama wake.

* Mihtasari ya kesi hutoa maelezo mafupi ya kesi na haina thamani ya kurejelewa katika kesi za baadaye.

Uamuzi Kamili wa Kesi

1. Muhtasari wa Uamuzi

Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa kwanza wa Meta wa kuacha maudhui yaliyo kwa Kipolandi kwenye Facebook ambapo mtumiaji alilenga watu wanaobadilisha jinsia zao kwa usemi wa vurugu unaowataka wanachama wa kikundi hiki kujitoa uhai. Baada ya Bodi kutambua kesi hii ili ikaguliwe, Meta ilihitimisha kwamba uamuzi wake wa kwanza wa kuruhusu chapisho hilo kusalia kwenye jukwaa hilo ulikuwa umekosewa, ikaondoa maudhui hayo na ikaweka vikwazo. Bodi imepata kuwa chapisho hilo linakiuka Viwango vya Jumuiya vya Matamshi ya Chuki na Kujitoa Uhai na Kujijeruhi. Bodi inachukua fursa hii kuhimiza Meta kuboresha sera na mwongozo wake kwa wakaguzi ili kulinda watu wanaobadilisha jinsia zao kwa njia bora zaidi kwenye majukwaa yake. Haswa, katika kutathmini iwapo chapisho ni matamshi ya chuki, Meta inapaswa kuhakikisha kuwa taswira zinazoonyeshwa kwenye bendera za utambulisho wa kijinsia ambazo hazina sura ya binadamu zinaeleweka kama viwakilishi vya kikundi kinachofafanuliwa na utambulisho wa kijinsia wa wanachama wake. Meta inapaswa kuweka wazi kwamba kuhimiza kikundi kizima kujitoa uhai ni ukiukaji tu kama vile kumhimiza mtu binafsi kujitoa uhai. Hata hivyo, Bodi imepata kwamba, suala kuu katika kesi hii halihusu sera, ila linahusu utekelezaji wake. Hata jinsi zilivyo, sera hizi zinapiga marufuku kwa wazi chapisho, ambalo lilikuwa na viashiria kadhaa vya usemi wa chuki unaolenga kikundi cha watu kulingana na utambulisho wa kijinsia. Meta kukosa kuchukua hatua ifaayo ya utekelezaji katika kesi hii mara kwa mara, licha ya ripoti kadhaa za watumiaji, imefanya Bodi kuhitimisha kuwa Meta inakosa kutimiza kanuni zake ilizobainisha kwenye usalama wa LGBTQIA+. Bodi inahimiza Meta kushughulikia changamoto hizi za utekelezaji.

2. Maelezo na Historia ya Kesi

Mnamo Aprili 2023, mtumiaji wa Facebook nchini Poland alichapisha picha ya pazia lenye mistari ya rangi ya samawati, waridi na nyeupe ya bendera ya watu waliobadilisha jinsia. Kwenye picha, maandishi yaliyo kwa Kipolandi yanasema: “Teknolojia mpya. Mapazia yanayijining'iniza yenyewe.” Juu ya mstari huo, maandishi zaidi kwa Kipolandi yanasema: “usafishaji wa mapukutiko <3.” Maelezo kwa Kipolandi kwenye wasifu wa mtumiaji yanasema, “mimi ninachukia watu wanaobadilisha jinsia zao.” Chapisho hilo lilipata chini ya hisia 50 kutoka kwa watumiaji wengine, wengi wao wakiliunga mkono. Hisia ya emoji iliyotumika sana ilikuwa ya “Haha.”

Kati ya Aprili na Mei 2023, watumiaji 11 tofauti waliripoti maudhui mara 12. Kati ya hizi, ripoti 10 hazikupewa kipaumbele kwa ukaguzi wa binadamu na mifumo ya kiotomatiki ya Meta kwa sababu mbalimbali, ikiwemo “alama za chini na za urijali.” Kwa ujumla Meta hutanguliza maudhui ili yakaguliwe na binadamu kulingana na kina chake, urijali wake na uwezekano wa kukiuka sera za maudhui. Ni ripoti mbili tu kati ya hizo, zilizo chini ya Kiwango cha Jumuiya ya Facebook kuhusu Kujitoa uhai na Kujijeruhi, zilizosababisha maudhui kutumwa kufanyiwa ukaguzi wa binadamu. Hakuna ripoti yoyote inayotokana na sera ya Matamshi ya Chuki iliyotumwa kwa ukaguzi wa binadamu. Kulingana na Meta, wakaguzi wana mafunzo na zana za “kutathmini na kuchukua hatua” dhidi ya maudhui mbali na foleni yao ya sera zilizobainishwa (yaani., Matamshi ya Chuki au Kujitoa Uhai na Kujijeruhi). Licha ya hayo, wakaguzi wote wawili walitathmini maudhui hayo na kupata kuwa hayakiuki na hawakuyapendekeza kwa ukaguzi zaidi.

Watumiaji watatu walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Meta wa kuweka maudhui kwenye Facebook. Rufaa moja ilisababisha mkaguzi binadamu kuunga mkono uamuzi wa awali wa Meta kwamba maudhui hayajakiuka sera yake ya Kujitoa uhai na Kujijeruhi. Rufaa zingine mbili, zilizotolewa chini ya sera ya Facebook ya Matamshi ya Chuki, hazikutumwa kwa ukaguzi wa binadamu. Hii ni kwa sababu Meta “itafuata na kuondoa urudiaji” wa ripoti kadhaa kwenye maudhui yale yale ili kuhakikisha usawa katika maamuzi ya wakaguzi na hatua za utekelezaji.

Mmoja wa watumiaji ambaye aliripoti maudhui hapo awali kisha alikata rufaa kwa Bodi. Kutokana na hatua ya Bodi kuchagua kesi hii, Meta ilibaini kuwa maudhui haya yalikiuka sera zake dhidi ya Matamshi ya Chuki na Kujitoa Uhai na Kujijeruhi na ikaondoa chapisho hilo. Zaidi ya hayo, kama sehemu ya ukaguzi wa Meta wa kesi hii, kampuni hiyo ilibaini kwamba akaunti ya muundaji wa maudhui hayo tayari ilikuwa na visa kadhaa vya ukiukaji wa Viwango vya Jumuiya na ilikuwa imefikisha vigezo vya kulemazwa. Meta ililemaza akaunti hiyo mnamo Agosti 2023.

Bodi ilizingatia muktadha ufuatao katika kufikia uamuzi wake katika kesi hii:

Nchi ya Polandi mara nyingi huripotiwa kuwa na viwango vya juu vya visa vya ukatili dhidi ya watu wa jamii ya LGBTQIA+. [Kumbuka: Bodi hutumia “LGBTQIA+” (Wasaganaji, Mashoga, Wasiotambulika kwa Jinsia Yoyote, Wanaobadilisha Jinsia, Basha, Huntha na Asiye na hisia za kimapenzi kwa jinsia yoyote) inaporejelea makundi kulingana na mwelekeo wa ngono, utambulisho wa kijinsia na/au usemi wa kijinsia. Hata hivyo, Bodi itadumisha ufupisho au matumizi yanayotumiwa na wengine wanapowataja au kuwanukuu.] Baraza la Tume ya Ulaya ya Haki za Binadamu awali lilitoa angalizo kuhusu “kufanywa kwa watu wa LGBTI kunyanyapaa” kama “tatizo la muda mrefu nchini Polandi.” Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Lesbian, Gay, Bisexual, Trans and Intersex (ILGA) Ulaya ya Rangi za Upinde wa Mvua inaweka nchi katika viwango kwa misingi ya sheria na sera zinazoathiri moja kwa moja haki za binadamu za watu wa LGBTI. Ripoti hiyo inaweka nchi ya Polandi kama nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) inayofanya vibaya zaidi na nchi ya 42 kati ya 49 za Ulaya zilizotathminiwa. Serikali za kitaifa na mitaa, sawa na watu maarufu, wameendelea kulenga jamii ya LGBTQIA+ kupitia semi za kibaguzi na hatua ya kisheria.

Kuanzia 2018, ILGA-Europe ilifuatilia kile shirika hilo lilitaja kama “matamshi ya chuki ya ngazi ya juu ya kisiasa dhidi ya watu wa LGBTI kutoka kwa viongozi wa kisiasa wa Polandi,” ikiwa ni pamoja na kauli kwamba “vuguvugu zima la LGBT” ni “tishio” kwa Polandi. Mwaka huo huo, meya wa Lubin, Polandi, alijaribu kupiga marufuku Maandamano ya Usawa jijini, ingawa Mahakama ya Rufaa iliondoa marufuku hiyo kabla ya maandamano yaliyoratibiwa. Mwaka 2019, meya wa Warsaw alizindua Mkataba wa Warsaw wa LGBT+ ili “kuimarisha hali ya watu wa LGBT” jijini humo. Chama tawala nchini Polandi cha Law and Justice Party (PiS) na viongozi wa kidini walisuta mkataba huo. Rais wa Polandi na serikali kuu pia wamebainisha jamii ya watu wanaobadilisha jinsia zao kama walengwa. Kwa mfano, Mwanachama wa chama tawala PiS amerejelea watu wanaobadilisha jinsia zao kama “wasio wa kawaida.” Waziri wa Haki wa Polandi pia ameomba Mahakama ya Upeo ya Polandi kuzingatia kwamba “pamoja na wazazi wao, watu wanaobadilisha jinsia zao pia wanapaswa kuwashtaki watoto na wapenzi wao [kwa kuwapa idhini ya kubadilisha] wanapotaka kufikia LGR [Utambuzi wa Kisheria wa Jinsia].”

Polandi pia imepitisha sheria dhidi ya LGBTQIA+. Kwa maneno ya shirika la Human Rights Watch, miji zilianza kutoa wito wa “kutenga watu wa LGBT kutoka jamii ya Polandi” kwa kutekeleza, miongoni mwa hatua zingine, “maeneo wasipotakikana watu wa LGBT” mwaka wa 2019. Shirika la Human Rights Watch limeripoti kwamba maeneo haya ni sehemu “ambapo mamlaka za mtaani zimepitisha ‘mikataba ya familia’ ya kibaguzi kwa ahadi ya ‘kulinda watoto dhidi ya kuvurugwa kimaadili’ au kujitangaza kuwa huru kutokana na itikadi ya ‘LGBT.’” Zaidi ya miji 100 imebuni maeneo kama hayo. ILGA-Europe inaripoti kuwa kutokana na shinikizo la ndani, la Umoja wa Ulaya na la kimataifa, baadhi ya manispaa hizi zimeondoa “maamuzi yao dhidi ya LGBT au Mikataba ya Haki za Familia.” Mnamo tarehe 28 Juni 2022, Mahakama ya Upeo ya Kiutawala nchini Polandi iliagiza maeneo manne ya manispaa kuondoa maamuzi yao dhidi ya LGBTQI+. Hata hivyo, kulingana na ripoti ya ukadiriaji wa Polandi iliyotolewa na Rainbow Europe, hali inakaa kuwa tete kwa jamii ya LGBTQIA+ nchini humo.

Uchunguzi wa 2019 kuhusu watu wa LGBTI katika Umoja wa Ulaya, uliofanywa na Shirika la Umoja wa Ulaya la Haki za Kimsingi, ulilinganisha hali ambazo watu wa LGBTI wanapitia nchini Polandi ya kushambuliwa na kunyanyaswa na hali ilivyo katika sehemu nyingine za Umoja wa Ulaya. Kulingana na uchunguzi huo, asilimia 51 ya watu wa LGBTI nchini Polandi mara kwa mara au mara nyingi huepuka maeneo fulani kwa kuhofia kushambuliwa. Hii inalingana na asilimia 33 ya sehemu zilizosalia za Umoja wa Ulaya. Uchunguzi huu pia ulipata kwamba mtu mmoja kati ya watano wanaobadilisha jinsia walishambuliwa kimwili au kingono katika miaka mitano kabla ya uchunguzi, zaidi ya maradufu ya makundi mengine ya LGBTI.

Bodi iliwapa jukumu wataalamu wa nje kuchunguza majibu ya mitandao ya kijamii kwa kauli za madharau za maafisa wa serikali ya Polandi. Wataalamu hao walibaini “wasiwasi wa kuongezeka kwa matamshi ya chuki mtandaoni yanayolenga jamii za wachache nchini Polandi, ikijumuisha jamii za LGBTQIA+ tangu 2015.” Katika uchambuzi wake wa maudhui dhidi ya LGBTQIA+ kwa Kipolandi kwenye Facebook, wataalamu hawa walibaini kwamba ongezeko lilifanyika wakati wa “maamuzi ya mahakama yanayohusiana na sheria dhidi ya LGBTQIA+.” Haya ni pamoja na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Utawala uliojadiliwa hapo juu na maamuzi yanayohusiana na changamoto za kisheria kupitisha maamuzi kadhaa dhidi ya LGBT yaliyoletwa mbele ya mahakama za utawala na Idara ya utetezi wa wananchi ya Polandi kwa Tume ya Haki za Binadamu, hali ambayo imekuwa ikiendelea tangu 2019.

Bodi pia iliomba wataalamu wa isimu na lugha kuhusu maana ya kauli hizo mbili za Kipolandi kwenye chapisho hilo. Kuhusiana na kauli “pazia zinazojining’iniza,” wataalamu walisema kwamba katika muktadha wa “bendera ya wanaobadilisha jinsia zao iliyokuwa ikining’inia dirishani,” kauli hiyo “ilikuwa mchezo wa maneno” ambao ulilinganisha “kuning’iniza pazia” na “kujitoa uhai kwa kujining’iniza.” Wataalamu hao walihitimisha kwamba kauli hiyo ilikuwa “ubaguzi uliofichwa dhidi ya watu wanaobadilisha jinsia zao.” Kuhusu kauli ya “usafishaji wa mapukutiko”, wataalamu walisema kwamba kauli hiyo “kwa kawaida humaanisha usafi wa kina majira ya mapukutiko” lakini, katika miktadha fulani, “inamaanisha kutupa uchafu wote na kuondoa vitu vyote visivyotakikana (na/au watu).” Maoni kadhaa ya umma, ikiwa ni pamoja na wasilisho kutoka katika Wakfu wa Kampeni ya Haki za Binadamu (PC-16029) lilihoji kwamba chapisho hilo kurejelea “usafishaji wa mapukutiko” ilikuwa namna ya “”kusifu ubaguzi na kutengwa kwa watu wanaobadilisha jinsia zao kutoka katika jamii ya Polandi (kupitia vifo vyao).”

Masuala ya madhara ya mtandaoni na ya nje ya mtandao yanayohusika katika kesi hii ni zaidi ya jamii ya LGBTQIA+ nchini Polandi na kuathiri jamii zilizo kote duniani. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, kujitoa uhai ni sababu ya nne inayoongoza katika vifo vya watu wenye umri ya kati ya miaka 15–29 kote duniani. WHO inabaini kwamba “viwango vya kujitoa uhai pia vipo juu miongoni mwa makundi yaliyo hatarini ambayo hupitia ubaguzi, kama vile wakimbizi na wahamiaji, watu wenyeji; na masaganaji, mashoga, mabasha, wanaobadilisha jinsia zao, huntha (LGBTI).” Uchunguzi mwingine wa utafiti umebaini “uhusiano chanya” kati ya kuwa waathiriwa wa mtandaoni na mawazo na tabia za mtu kujijeruhi.

Hatari ya kujitoa uhai inaleta wasiwasi mkubwa kwa jamii ya watu wanaobadilisha jinsia zao na wasiojitambulisha kwa jinsia yoyote. Mradi wa Trevor wa Uchunguzi wa Kitaifa wa 2023 kuhusu Afya ya Akili ya Watu wa LGBTQ ulipata kwamba nusu ya watu wanaobadilisha jinsia zao na wasiojitambulisha kwa jinsia yoyote nchini Marekani walizingatia kujitoa uhai mwaka 2022. Uchunguzi huo pia unakadiria kwamba 14% ya vijana wa LGBTQ wamejaribu kujitoa uhai katika mwaka uliopita, ikiwa ni pamoja na takriban mtu mmoja kati ya watu watano wanaobadilisha jinsia zao na wasiojitambulisha kwa jinsia yoyote. Kulingana na Uchunguzi wa Tabia Hatari za Vijana wa CDC, 10% ya wanafunzi wa shule za upili nchini Marekani walijaribu kujitoa uhai mwaka 2021. Idadi kubwa yatafiti kutoka kote uliwenguni zimepata kwamba watu wanaobadilisha jinsia zao au wasiojitambulisha kwa jinsia yoyote wapo katika hatari kubwa zaidi ya kupata mawazo na majaribio ya kujitoa uhai ikilinganishwa na watu wanaojitambulisha kwa jinsia zao za wakati wa kuzaliwa.

Katika maoni ya umma kwa Bodi, Muungano wa Mashoga na Wasaganaji Dhidi ya Ushushaji Hadhi (GLAAD) (PC-16027) uliangazia matokeo ya uchunguzi wao wa kila mwaka, Kiwango cha Usalama kwenye Mitandao ya Kijamii, kuhusu usalama wa watumiaji wa jamii ya LGBTQ kwenye majukwaa matano makuu ya mitandao ya kijamii. Ripoti ya 2023 iliipa Facebook alama ya 61% kulingana na viashiria 12 mahususi kwa jamii ya LGBTQ. Alama hii iliwakilisha ongezeko la pointi 15 kutoka 2022, Facebook ikiwa katika nafasi ya pili baada ya Instagram na juu ya majukwaa mengine matatu makuu. Hata hivyo, GLAAD iliandika kwamba, “usalama na ubora wa ulinzi wa watumiaji wa LGBTQ bado hauridhishi.” Ripoti hiyo ilipata kwamba kuna “madhara halisi yanayofanyika kwa watu wa LGBTQ mtandaoni, ikiwa ni pamoja na athari ya kutisha dhidi ya uhuru wa kujieleza kwa watu wa LGBTQ kwa hofu ya kulengwa, na athari mbaya ya kisaikolojia kwa kukabiliwa na ubaguzi na mienendo ya chuki mara kwa mara.”

3. Bodi ya Usimamizi na Upeo

Bodi ina mamlaka ya kukagua uamuzi wa Meta kufuatia rufaa kutoka kwa mtu ambaye aliripoti hapo awali maudhui ambayo yaliruhusiwa (Kifungu cha 2 cha Mkataba, Sehemu ya 1; Sheria ndogo za Kifungu cha 3, Sehemu ya 1).

Bodi inaweza kudumisha au kubatilisha uamuzi wa Meta (Kifungu cha 3, Sehemu ya 5 ya Mkataba), na kampuni itafuata uamuzi huu (Kifungu cha 4 cha Mkataba). Meta pia lazima itathmini uwezekano wa kutekeleza uamuzi wake kuhusiana na maudhui yanayofanana yaliyo katika muktadha tofauti (Kifungu cha 4 cha Mkataba). Uamuzi wa Bodi unaweza kujumuisha mapendekezo yasiyo ya kufunga ambayo Meta lazima iyajibu (Kifungu cha 3 cha Mkataba, Sehemu ya 4); Kifungu cha 4). Wakati Meta inajitolea kushughulikia mapendekezo, Bodi hufuatilia utekelezaji wake.

Bodi inapochagua kesi kama hii, ambapo Meta, baadaye inakubali kwamba ilifanya makosa, Bodi hukagua uamuzi wa kwanza wa kuongeza ufahamu wa mchakato wa udhibiti wa maudhui na kutoa mapendekezo ili kupunguza makosa na kuongeza usawa kwa watu wanaotumia Facebook na Instagram.

4. Vyanzo vya Mamlaka na Mwongozo

Viwango vifuatavyo na kesi za awali zilikuwa msingi wa uchanganuzi wa Bodi katika kesi hii:

I. Maamuzi ya Bodi ya Usimamizi

Maamuzi muhimu zaidi ya awali ya Bodi ya Usimamizi yanajumuisha:

II. Sera za maudhui za Meta

Mtazamo wa sera dhidi ya matamshi ya chuki unafafanua matamshi ya chuki “shambulio la moja kwa moja dhidi ya watu – badala ya dhana au asasi – kwa msingi wa . . . sifa zinazolindwa,” ikiwa ni pamoja na ngono na utambulisho wa kijinsia. Meta inafafanua “mashambulizi” kama “vurugu au matamshi ya kudhalilisha, kasumba mbaya, taarifa za udhaifu, usemi wa dharau, karaha au kupuuzwa, kulaani na hatua za kutengwa au kubaguliwa.” Kwenye mtazamo wa sera, Meta inaendelea kusema kwamba: “Tunaamini kwamba watu hutumia sauti zao na kuunganika kwa urahisi zaidi wakati hawahisi kushambuliwa kwa msingi wa hao ni akina nani. Hiyo ndio maana haturuhusu matamshi ya chuki kwenye Facebook. Yanaweka mazingira ya vitisho na kutengwa, na katika visa vingine yanaweza kuchochea vurugu ya nje ya mtandao.”

Viwango vya Jumuiya kuhusu Matamshi ya Chuki vya Meta vinagawa mashambulizi katika “viwango.” Mashambulizi katika kiwango cha 1 ni pamoja na maudhui yanayolenga mtu au kikundi cha watu kwa msingi wa sifa zao zinazolindwa kupitia “usemi wa vurugu au uungaji mkono kwa maandishi au michoro.” Hatimaye Meta ilipata kwamba chapisho katika kesi hii lilikiuka mkondo huu wa sera. Mnamo tarehe 6 Desemba 2023, Meta ilisasisha Viwango vya Jumuiya ili kuakisi kwamba marufuku dhidi ya usemi wa vurugu kwa makundi yenye sifa zinazolindwa yalihamishiwa kwenye sera ya Viwango na Uchochezi.

Mashambulizi katika kiwango cha 2 ni pamoja na maudhui yanayolenga mtu au kikundi cha watu kwa msingi wa sifa zao zinazolindwa kupitia “usemi wa madharau (kwa maandishi au kupitia michoro.)” Katika Viwango vya Jumuiya kuhusu Matamshi ya Chuki, Meta inafafanua semi za madharau kujumuisha “kujijumuisha kwenye ukatili kwa msingi wa sifa zinazolindwa” na “semi kwamba sifa zinazolindwa hazipaswa kuwepo.”

Viwango vya Jumuiya kuhusu Kujitoa Uhai na Kujijeruhi vimepiga marufuku “maudhui yoyote yanayohimiza tabia ya kujitoa uhai na kujijeruhi, ikiwa ni pamoja na maudhui ya kubuni, kama vile meme na maonyesho.” Chini ya sera hii, Meta huondoa “maudhui yanayotangaza, kuhimiza, kuratibu au kutoa maagizo ya jinsi ya kujitoa uhai na kujijeruhi.”

Uchanganuzi wa Bodi ulitokana na dhamira ya Meta ya kutoa Sauti, ambayo kampuni inafafanua kuwa “muhimu,” na maadili yake ya usalama na hadhi.

III. Wajibu wa Meta wa Haki za Binadamu

Kanuni za Mwongozo wa Umoja wa Mataifa juu ya Biashara na Haki za Binadamu (UNGP), zilizoidhinishwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mnamo 2011, zina mfumo wa hiari wa majukumu ya haki za binadamu ya biashara za kibinafsi. Mnamo 2021, Meta ilitangazaSera yake ya Haki za Binadamu ya Shirika, ambapo ilisisitiza tena kujitolea kwake katika kuheshimu haki za kibinadamu kwa mujibu wa UNGP. Uchambuzi wa Bodi wa wajibu wa Meta kwa haki za binadamu katika kesi hii ulitokana na viwango vifuatavyo vya kimataifa:

  • Haki za uhuru wa kuwa na maoni na kujieleza: Kifungu cha 19, Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Kiraia na Kisiasa ( ICCPR); Maoni ya Jumla Nambari. 34, Kamati ya Haki za Binadamu 2011; Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa (UNSR) kuhusu uhuru wa maoni na kujieleza, anaripoti: A/HRC/38/35 (2018), A/74/486 (2019); na Mpango wa Hatua wa Rabat, ripoti ya Tume ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu: A/HRC/22/17/Add.4 (2013).
  • Haki ya kuishi: Kifungu cha 6, ICCPR.
  • Haki ya kufurahia kiwango cha juu kinachoweza kufikiwa cha afya ya kimwili na kiakili: Kifungu cha 12, Agano la Kimataifa kuhusu Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni ( ICESCR).
  • Haki ya usawa na kutobagua: Kipengele cha 2, aya ya. 1 na Kipengele cha 26, ICCPR;

5. Mawasilisho ya Mtumiaji

Katika rufaa yake kwa Bodi, mtumiaji aliyeripoti maudhui hayo alibainisha kuwa mtu aliyechapisha picha hiyo hapo awali alikuwa akiwanyanyasa mtandaoni watu wanaobadilisha jinsia na alikuwa ameunda akaunti mpya baada ya kusimamishwa kutoka kwa Facebook. Pia alisema kwamba kushangilia ongezeko la viwango vya kujitoa uhai kwa watu wanaobadilisha jinsia zao “haipaswi kuruhusiwa.”

6. Mawasilisho ya Meta

Hatimaye Meta iliondoa chapisho hilo chini ya Kiwango cha 1 cha Viwango vyake vya Jumuiya kuhusu Matamshi ya Chuki kwa sababu maudhui hayo yalikiuka mkondo wa sera unaopiga marufuku maudhui yanayolenga watu au kikundi cha watu kwa msingi wa sifa zao zinazolindwa kwa “usemi wa vurugu au uungaji mkono kwa maandishi au michoro.” Katika mwongozo wake wa ndani kuhusu jinsi ya kutekeleza sera hii, Meta inasema kwamba maudhui yanapaswi kuondolewa ikiwa ni “usemi wa vurugu kwa namna ya miito ya hatua au taarifa za nia ya kusababisha, taarifa za nia au hali kuhusu au taarifa zinazotetea au kuunga mkono kifo, ugonjwa au madhara (kwa maandishi au mchoro).”

Kwenye mwongozo huo wa ndani, kampuni hiyo pia inaeleza kile inachozingatia kuwa uwakilishaji wa michoro wa makundi yenye sifa zinazolindwa kwenye picha au video. Meta haikuruhusu Bodi kuchapisha maelezo zaidi yanayohusiana na mwongozo huu. Kampuni hiyo badala yake ilisema kwamba “chini ya sera ya Matamshi ya Chuki, Meta inaweza kuzingatia vipengele vya michoro kwenye maudhui inapobaini iwapo maudhui yanalenga mtu au kikundi cha watu kulingana na sifa zao zinazolindwa.”

Meta ilisema kwamba tathmini nyingi za maudhui kama yasiyo ya ukiukaji wa Viwango vya Jumuiya kuhusu Matamshi ya Chuki na wakaguzi wake inaambatana na “utekelezaji madhubuti wa mwongozo wake wa ndani.” Ilifafanua: “Ingawa pazia hizo zinafanana na bendera ya Trans Pride, tungeweza kufasiri shambulizi dhidi ya bendera, iliyopekee, kama shambulizi dhidi ya dhana au asasi, hali ambayo haikiuka sera zetu, na si mtu au vikundi vya watu.” Hata hivyo, Meta iliendelea kubaini kwamba “kurejelea kujin’ng’iniza kunaashiria kuwa chapisho hili linashambulia kikundi cha watu.” Tathmini hii ilitokana na kubainishwa kwamba kauli “pazia zinazojining’iniza” ilikuwa ikirejelea kiwango cha kujitoa uhai kwa jamii ya wanaobadilisha jinsia zao kwa sababu pazia hizo zinafanana na bendera ya Trans Pride, na pazia hizo zinaning’inia kwenye picha husika (na vilevile maandishi yaliyo juu) ni majazi yanayomaanisha kujitoa uhai kwa kujining’iniza.” Meta pia ilibaini kwamba “dhana au asasi haziwezi ‘kujitoa uhai,’ hata kama ni moja kwa moja.” Kwa sababu hii, Meta ilipata kwamba mtumiaji alikuwa akirejelea “Watu wanaobadilsha jinsia zao, si dhana hiyo.” Kwa hivyo, kulingana na Meta, “maudhui haya yanakiuka sera ya Matamshi ya Chuki kwa sababu yananuia kufasiriwa kama taarifa ya kuunga mkono kifo cha kikundi chenye Sifa Zinazolindwa kupitia kujitoa uhai.”

Kufuatia sasisho kwenye sera dhidi ya Matamshi ya Chuki, ambapo mkondo wa sera unaopiga marufuku usemi wa vurugu dhidi ya vikundi vyenye sifa zinazolindwa ulihamishiwa kwenye sera ya Vurugu na Uchochezi, Meta ilifahamisha Bodi kwamba maudhui hayo bado ni ya ukiukaji.

Meta pia iliripoti kwamba taarifa iliyo kwenye wasifu wa akaunti ya mtumiaji inayosema, “Mimi huchukia watu wanaobadilisha jinsia zao,” ilikiuka Kiwango cha 2 cha sera ya Matamshi ya Chuki kama “kujijumuisha kwenye ukatili kwa msingi wa sifa zinazolindwa.” Kulingana na Meta, taarifa hii ilipatikana kuwa ya ukiukaji kama sehemu ya ukaguzi wa Meta wa kesi hii pamoja na akaunti ya mtumiaji kufuatia hatua ya Bodi kuchagua kesi hii. Meta ilisema kwamba taarifa hii ilisaidia kuweka msingi wa uelewa wake wa nia ya mtumiaji katika maudhui ya kesi hii.

Katika majibu yake kwa Bodi ilipouliza iwapo maudhui yanakiuka sera ya Kujitoa Uhai na Kujijeruhi, Meta ilithibitisha kwamba “maudhui hayo yanakiuka sera ya Kujitoa Uhai na Kujijeruhi kwa kuhimiza kitendo cha kujitoa uhai, hali inayolinga na uamuzi wetu kwamba maudhui haya yana taarifa yanayounga mkono kifo cha kikundi chenye sifa zinazolindwa kupitia kifo.” Meta pia iliripoti kwamba sera ya Kujitoa Uhai na Kujijeruhi “haitoi tofauti iliyopo kati ya maudhui yanaendeleza au kuhimiza kujitoa uhai yanayolenga mtu binafsi ikilinganishwa na kikundi cha watu.”

Bodi iliuliza Meta maswali 13 katika maandishi. Maswali yanayohusiana na mbinu ya Meta ya kuratibu maudhui yanayohusu masuala ya watu wanaobadilisha jinsia zao na LGBTQIA+; uhusiano kati ya Viwango vya Jumuiya vya Matamshi ya Chuki na Kujitoa Uhai na Kujijeruhi; jinsi “ucheshi” na “kejeli” zinavyotathminiwa na waratibu wanapokagua maudhui ili kuona ikiwa yamekiuka matamshi ya chuki; nafasi ya alama ya “urijali” na “kina” katika kuyapa maudhui kipaumbele cha ukaguzi wa binadamu; na jinsi desturi za Meta za uratibu wa maudhui zinavyoshughulikiwa kipaumbele kwa maudhui kufanyiwa ukaguzi wa binadamu ikiwa yameripotiwa na watumiaji wengi. Meta ilijibu maswali yote 13.

7. Maoni ya Umma

Bodi ya Usimamizi imepokea maoni 35 ya umma yanayofaa katika kesi hii, ikiwa ni pamoja na maoni 25 kutoka Marekani na Kanada, saba kutoka Ulaya na matatu kutoka Asia Pasifiki na Oceania. Jumla hii inajumuisha maoni ya umma ambayo yalikuwa yakijirudia au yaliwasilishwa kwa idhini ya kuchapisha, lakini hayakutimiza masharti ya Bodi ya uchapishaji. Utengaji kama huo unaweza kutokana na hali ya matumizi mabaya ya maoni, wasiwasi kuhusu faragha ya mtumiaji na/au sababu nyingine za kisheria. Maoni ya umma yanaweza kuwasilishwa kwa Bodi kwa ridhaa au bila ridhaa ya kuchapisha, na kwa ridhaa au bila ridhaa ya kupata sifa.

Mawasilisho hayo yalishughulikia mambo yafuatayo: hali ya haki za binadamu nchini Polandi, hususan hali wanayopitia watu wanaobadilisha jinsia zao; Usalama wa LGBTQIA+ kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii; uhusiano kati ya madhara ya mtandaoni na ya nje ya mtandao nchini Polandi; uhusiano kati ya uchesi, kejeli, meme na chuki/unyanyasaji dhidi ya watu wanaobadilisha jinsia zao kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii; na changamoto za kuratibu maudhui yanayohitaji ufasiri wa muktadha.

Ili kusoma maoni ya umma yaliyowasilishwa kuhusu kesi hii, tafadhali bofya hapa.

8. Uchanganuzi wa Bodi ya Usimamizi

Bodi ilichunguza ikiwa maudhui haya yanafaa kuondolewa kwa kuchanganua sera za maudhui ya Meta, wajibu na maadili ya haki za binadamu. Bodi pia ilitathmini athari za kesi hii kwa mtazamo mpana wa Meta wa usimamizi wa maudhui.

Bodi iliteua kesi hii ili kutathmini usahihi wa utekelezaji wa Meta wa sera yake ya Matamshi ya Chuki, na pia kuelewa vyema jinsi Meta inavyoshughulikia maudhui yanayohusisha matamshi ya chuki pamoja na utangazaji wa kujitoa uhai au kujijeruhi.

8.1 Utiifu wa Sera za Maudhui za Meta

I. Kanuni za Maudhui

Matamshi ya Chuki

Bodi imegundua kuwa maudhui katika kesi hii yanakiuka Kiwango cha Jumuiya cha Matamshi ya Chuki. Bodi ilijumuisha “usemi wa vurugu au uungaji mkono” (Kiwango cha 1) kwenye namna ya mwito wa kifo cha kikundi chenye sifa zinazolindwa kupitia kujitoa uhai, hali ambayo inakiuka sera ya Matamshi ya Chuki kwa uwazi.

Bodi inakubaliana na hitimisho la Meta kwamba kurejelea kuning’inia kwenye chapisho ni shambulizi dhidi ya kikundi cha watu badala ya dhana kwa sababu “dhana au asasi haziwezi ‘kujining’iniza.’” Bodi pia imepata kwamba uungwaji mkono kwa kuhimitisha kwenye muktadha mpana kuhusu madhara ya mtandaoni na ya nje ya mtandao kwamba wanachama wa jamii ya LGBTQIA+ na hususan watu wanaobadilisha jinsia zao, kukabiliwa nao nchini Polandi. Chapisho linalotumia usemi wa vurugu kutetea na kuunga mkono kifo cha watu wanaobadilisha jinsia zao kupitia kujitoa uhai kuweka mazingira ya vitisho na kutengwa, na linaweza kuchangia madhara ya kimwili. Muktadha wa ambao lugha ya chapisho hilo ilitumika unaweka wazi kwamba lilinuia kushusha hadhi walengwa wake. Kwa kuzingatia hali ya maandishi na picha, chapisho hilo pia lilizidisha janga la afya ya akili ambalo kwa sasa watu wa jamii ya wanaobadilisha jinsia zao wanapitia. Kulingana na tafiti nyingi, watu wanaobadilisha jinsia zao au wasitojitambulisha kwa jinsia yoyote wako katika hatari kubwa ya mawazo na majaribio ya kujitoa uhai ikilinganishwa na watu wanaojitambulisha kwa jinsia zao halisi. Zaidi ya hayo, hali ya mashambulizi mtandaoni na kufanya watu kuwa waathiriwa imehusishwa kwa njia chanya na mawazo ya kujitoa uhai. Katika muktadha huu, Bodi imepata kwamba kuwepo kwa bendera ya watu wanaobadilisha jinsia zao, pamoja na kurejelea hatari ya kujitoa ushai ndani ya jamii ya wanaobadilishwa jinsia zao (“pazia zinazojining’iniza”), ni ishara wazi kwamba watu wanaobadilisha jinsia ndio walengwa wa chapisho hilo. Bodi pia imepata kwamba kauli ya “usafishaji wa mapukutiko,” na kufuatwa na “<3” (moyo) emoji ndogo, pia ni uungwaji mkono wa kifo cha kikundi. Kutokana na hayo, ni ukiukaji wa marufuku ya Viwango vya Jumuiya kuhusu Matamshi ya Chuki (Kiwango cha 2) kuhusu “semi kwamba sifa zilizolindwa hazipaswi kuwepo.”

Kuhusiana na Kiwango hiki cha Jumuiya, Bodi inaamini kwamba sera hii na mwongozo wa ndani wa utekelezaji wake ungefaa zaidi katika “ ubunifu wa ukandamizaji” katika mielekeo ya maudhui yanayolenga makundi ambayo yametengwa kihistoria. Kituo cha Wilson kilibuni kauli hii kupitia utafiti kuhusu dhuluma za kijinsia na ngono, na GLAAD pia ilibainisha umuhimu wake kwenye maoni yake ya umma (PC-16027). “Ubunifu wa ukandamizaji” unarejelea matumizi ya lugha fiche; urudiaji, picha za meme za michoro na maandishi zinazotegemea muktadha; na mbinu nyingine za kuepuka kutambuliwa kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii.” Katika kutekeleza dhana hiyo kwenye chapisho katika kesi hii, GLAAD ilisema “ubunifu wa ukandamizaji” unahusisha “watu wenye nia mbaya kuunda njia mpya za kulenga jamii ya LGBTQ” na makundi yaliyo hatarini kwa njia ya jumla zaidi kupitia machapisho na picha za meme ambazo wanatetea kama zenye “ucheshi au za kejeli,” lakini kwa “kwa hakika ni za chuki au unyanyasaji dhidi ya LGBTQ.” Hususan, “ubunifu wa ukandamizaji” ulichukua mtindo wa chapisho linalotumia lugha ambayo ni fiche kwa kiasi fulani kurejelea kujitoa uhai (“pazia zinajining’iniza” na “usafishaji wa mapukutiko”) pamoja na picha ya kikundi kinacholindwa (bendera ya watu wanaobadilisha jinsia zao) ili kuhimiza kifo kupitia kujitoa uhai. Kaitka uamuzi wa Waarmenia walio Azabaijani, Bodi ilitaja umuhimu wa muktadha katika kubaini kwamba neno linalozingatiwa katika kesi hii lililenga kikundi kulingana na sifa zinazolindwa. Ingawa muktadha wa vita ulishamiri katika kesi hiyo, matishio yanayowakabili watu wanaobadilisha jinsia zao walio nchini Polandi yanaonyesha kwamba hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa jamii, kasoro vita. Kama ilivyobainishwa hapo juu, mtu mmoja kati ya watano wanaobadilisha jinsia zao nchini Polandi waliripoti kushambuliwa kimwili au kingono katika miaka mitano kabla ya 2019, zaidi ya idadi maradufu ya watu kutoka makundi ya LGBTI yanayoripoti mashambulizi kama hayo.

Bodi ina wasiwasi kwamba wakaguzi binadamu wa Meta wa hapo awali hawakutambua vidokezo hivi vya kimuktadha ndani ya muktadha na, kutokana na hayo, wakahitimisha kuwa maudhui hayo hayakuwa ya ukiukaji. Bodi inapendekeza baadhi ya marekebisho kwenye mwongozo wa utekelezaji wa Viwango vya Jumuiya kuhusu Matamshi ya Chuki, inasema kwamba chapisho hilo lilikiuka sera hata jinsi yalivyokuwa yameandikwa wakati huo. Taarifa zote mbili zilizotolewa kwenye chapisho hilo zinaunga mkono kifo cha watu wanaobadilisha jinsia zao kupitia kujitoa uhai. Ishara ya ziada kwenye wasifu wa mtumiaji unaafikiana na hitimisho hili. Mtumiaji kujitambulisha kama mtu anayechukia watu wanaobadilisha jinsia zao – pekee ni – ukiukaji chini ya Kiwango cha 2 wa marufuku ya Viwango vya Jumuiya kuhusu Matamshi ya Chuki dhidi ya “kujijumuisha katika ukatili kwa msingi wa sifa zinazolindwa.” Ni sharti Meta iboreshe usahihi wa utekelezaji wake wa matamshi ya chuki dhidi ya jamii ya LGBTQIA+, ama kupitia mfumo otomatiki au ukaguzi wa binadamu, hususan wakati machapisho yana picha na maandishi yanayohitaji ufasiri wa kimuktadha. Kama ambavyo GLAAD ilitazama (PC-16027), Meta “hukosa kutekeleza sera zake mara kwa mara inapokagua ripoti kuhusu maudhui yanayotumia ‘ubunifu wa ukandamizaji.’”

Bodi pia ina wasiwasi kuhusu taarifa ya Meta kwamba wakaguzi kukosa kuondoa maudhui hayo” kunaambatana na utekelezaji madhubuti wa miongozo yetu ya ndani.” Taarifa ya Meta inaashiria kuwa mwongozo wa ndani kwa wakaguzi haujanasa ipasavyo jinsi maandishi na picha zinaweza kuingiliana katika chapisho la mitandao ya kijamii ili kuwakilisha kikundi kinachofafanuliwa na utambulisho wa kijinsia wa wanachama wake. Bodi imepata kwamba mwongozo huu huenda usitumike kwa wakaguzi wa maudhui katika kiwango ili kuweza kufikia matokeo sahihi ya utekelezaji wa maudhui yanayolenga makundi yenye sifa zinazolindwa ambayo yanawakilishwa kupitia michoro, lakini hayajatajwa au kuonyeshwa kupitia wahusika binadamu. Meta haikuruhusu Bodi kuchapisha maelezo ya ziada ambayo yangewezesha majadiliano mapana zaidi kuhusu jinsi utekelezaji wa aina hii ya maudhui unaweza kuboreshwa. Hata hivyo, Bodi inaamini kwamba Meta inapaswa kubadilisha mwongozo wake ili kuhakikisha kwamba maonyesho ya picha ya utambulisho wa jinsia yanaeleweka vya kutosha maudhui yanapokaguliwa kubaini mashambulizi. Bodi inatambua kuwa katika kupendekeza njia huu, hailengi kukandamiza ulinzi wa Meta kwa changamoto za dhana, asasi, mawazo, desturi au imani. Badala yake, Bodi inataka Meta iweke wazi kwamba machapisho hayapaswi kuonyesha taswira za binadamu ili ziwe za mashambulizi kwa watu.

Kujitoa Uhai na Kujijeruhi

Bodi imegundua kuwa maudhui katika kesi hii pia yanakiuka Viwango vya Jumuiya kuhusu Kujitoa Uhai na Kujijeruhi. Sera hii inapiga marufuku “maudhui yanayotangaza, kuhimiza, kuratibu au kutoa maagizo ya jinsi ya kujitoa uhai na kujijeruhi.” Kulingana na mwongozo wa ndani ambao Meta huwapa wakaguzi, “kutangaza” kunafafanuliwa kama “kuzungumza kwa njia chanya kuhusu.” Bodi inakubaliana na hitimisho la Meta kwamba maudhui hayo ni taarifa yanayounga mkono kifo cha kikundi chenye sifa zinazolindwa kupitia kujitoa uhai, na kwa hivyo yanahimiza kitendo cha kujitoa uhai.

Bodi pia ilipata kuwa Viwango vya Jumuiya kuhusu Kujitoa Uhai na Kujijeruhi, vinapaswa kupiga marufuku kwa uwazi zaidi maudhui yanayotangaza au kuhimiza kitendo cha kujitoa uhai yanayolenga kikundi cha watu kinachoweza kutambuliwa, tofauti na ikiwa ni mtu pekee kwenye kikundi hicho. Meta ilifichulia Bodi kwamba sera hiyo haitofautishi kati ya aina hizi mbili za maudhui. Kutokana na changamoto ambazo wakaguzi walikumbana nazo kutambua taarifa inayohimiza kujitoa uhai kwa kikundi katika kesi hii, hata hivyo, Bodi inahimiza Meta iweke wazi kwamba sera hiyo inapiga marufuku maudhui yanayotangaza au kuhimiza vitendo vya kujitoa uhai yanayolenga kikundi cha watu wanaoweza kutambuliwa. Meta inapaswa kuweka wazi hoja hii kwenye ukurasa wake wa sera ya Kujitoa uhai na Kujijeruhi na vilevile kwenye mwongozo wake husika wa ndani kwa wakaguzi.

II. Hatua ya Utekelezaji

Bodi imepata kwamba mifumo otomatiki ya Meta ya kutoa kipaumbele kwa ukaguzi inaathiri pakubwa vitendo vya utekelezaji katika kesi hii. Kati ya ripoti 12 za watumiaji za chapisho hilo, 10 zilifungwa kiotomatiki na mifumo otomatiki ya Meta. Kati ya rufaa hizi tatu za mtumiaji dhidi ya maamuzi ya Meta, mbili zilifungwa kiotomatiki na mifumo otomatiki ya Meta. Bodi ina wasiwasi kwamba historia ya kesi iliyoshirikiwa na Bodi ina viashiria kadhaa vya ukiukaji na hivyo inapendekeza kwamba sera za Meta hazitekelezwi kwa njia ya kutosha.

Bodi imebaini kwamba ripoti nyingi za watumiaji zilifungwa kutokana na desturi za Meta za kuratibu maudhui za kushughulikia ripoti nyingi kuhusu maudhui yale yale. Ripoti ya kwanza mtumiaji ya matamshi ya chuki haikupewa kipaumbele cha kufanyiwa ukaguzi wa binadamu kwa sababu ya “alama ya chini ya kina na urijali.” Ripoti zilizofuata za matamshi ya chuki hakikupewa kipaumbele cha kufanyiwa ukaguzi wa binadamu kwa sababu ripoti nyingi zilitolewa kuhusu maudhui hayo, Meta “itapunguza urudiaji wa ripoti hizo ili kuhakikisha uthabiti katika maamuzi ya mkaguzi na vitendo vya utekelezaji.” Bodi inakiri kwamba kupunguza urudiaji ni desturi inayofaa ya uratibu wa maudhui katika kiwango. Hata hivyo, Bodi inasema kwamba desturi hii inaweka shinikizo zaidi kwenye uamuzi wa awali uliofanywa kuhusu ripoti, kwamba utabaini hatima ya ripoti zote zinazowekwa kwenye kikundi kimoja nayo.

Bodi inaamini kwamba inaweza kuwa muhimu kwa Meta kutoa kipaumbele kwa uboreshaji wa usahihi wa mifumo otomatiki ambayo kando na kutekeleza sera za maudhui pia huweka kipaumbele kwa maudhui kufanyiwa ukaguzi, haswa wakati wa kushughulikia maudhui yenye uwezekano wa kuathiri watu wa LGBTQIA+. Maboresho kama hayo kwa uwezo wa mifumo otomatiki kutambua aina ya lugha fiche na picha zinazotegemea muktadha zilizozingatiwa kwenye kesi hii bila shaka yanaweza kuboresha utekelezaji dhidi ya maudhui yanayolenga makundi mengine yenye sifa zinazolindwa. Bodi inaamini kwamba wasifu wa mtumiaji, kwa mfano, ambao ulijumuisha kujijumuisha katika chuki dhidi ya watu wanaobadilisha jinsia zao, ungezingatiwa kama ishara moja muhimu wakati wa kubaini alama za kina kwa madhumuni ya kuamua iwapo maudhui yangepewa kipaumbele cha kufanyiwa ukaguzi na/au kuchukua hatua ya utekelezaji. Ishara hii inaweza kutumiwa pamoja na uchanganuzi uliopo wa tabia na utangamano wa kijamii ambao Meta inaweza kutumia kuonyesha maudhui yenye uwezekano wa kusababisha ukiukaji.

Isitoshe, Bodi inasisitiza kwamba inaweza kuwa muhimu kwa Meta kuhakikisha kwamba mifumo otomatiki inapimwa ipasavyo na wakaguzi binadamu wanapata mafunzo ili waweze kutathmini kwa ufanisi machapisho yanayohusiana na jamii ya LGBTQIA+ katika kiwango. Bodi ina wasiwasi kuhusu mbinu ya sasa ya Meta, ambayo chini yake wakaguzi walio na jukumu la kutathmini rufaa mara nyingi huonekana kuwa na kiwango sawa cha utaalamu na wale wanaofanya tathmini ya kwanza ya maudhui. Bodi inaamini kwamba Meta ingepaswa kuwekeza zaidi katika kuunda na kufunza viainishaji vinavyotambua maudhui yenye uwezekano wa kuwa ya ukiukaji yanayoathiri jamii ya LGBTQIA+ na kuyapa maudhui hayo kipaumbele cha kukaguliwa na binadamu. Matamshi ya chuki, hususan maudhui yenye alama ya juu zaidi ya kina yanayopatikana chini ya Kiwango cha 1 cha sera ya Meta, yanapaswa kupewa kipaumbele cha ukaguzi kila mara. Bodi pia inapendekeza kuharakishwa kwa uboreshaji wa mchakato huu kupitia; i)mafunzo ya kina kuhusu madhara yanayohusiana na utambulisho wa kijinsia kwa wakaguzi; ii) jopo kazi la kuchunguza hali ambazo watu wanaobadilisha jinsia na wasiojitambulisha kwa jinsia yoyote wanapitia kwenye majukwaa ya Meta; na iii) uundaji wa kikundi maalum cha wataalamu wa mada husika ili kukagua maudhui yanayohusiana na masuala yanayoathiri jamii ya LGBTQIA+. Ingawa kweli za kesi hii zinahusu haswa madhara ambayo watu wanaobadilisha jinsia zao wanakumbana nayo kwenye Facebook, Bodi pia inahimiza Meta kuchunguza jinsi ya kuboresha utekelezaji dhidi ya maudhui ya chuki yanayoathiri makundi mengine yenye sifa zinazolindwa.

Ingawa Bodi inatoa mapendekezo mawili pekee rasmi hapa chini, Bodi inabainisha kuwa hii ni kwa sababu changamoto zilizoangaziwa katika kesi hii hazihusu sana sera jinsi zilivyoandikwa bali zinahusu sana utekelezaji wake. Bodi inahesabu angalau viashiria vitano vya maudhui hatari kwenye kesi hii: (1) marejeleo ya “pazia ya kujining’iniza” kwenye chapisho; (2) marejeleo ya chapisho hilo la “usafishaji wa mpukutiko <3”; (3) mtumiaji kujirejelea kama “mtu ambaye anachukia wanaobadilisha jinsia zao” katika muktadha wa nchi ambapo viwango vya juu zaidi vya ukatili dhidi ya watu wa LGBTQIA+ vimeripotiwa; (4) idadi ya ripoti za watumiaji na rufaa kwenye maudhui hayo; na (5) idadi ya ripoti na rufaa ikilinganishwa na urijali wa maudhui. Bodi ina wasiwasi kwamba Meta ilikosa ishara hizi na inaamini kuwa hii inaashiria kuwa sera zake hazitekekelezwi ipasavyo. Bodi inashikilia kuwa Meta inapaswa kufikiria kwa kina na ubunifu kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto zilizopo katika ya kanuni zake za ulinzi wa watu wa LGBTQIA+ kwenye majukwaa yake na utekelezaji wa kanuni hizo.

8.2 Utiifu wa Wajibu wa Haki za Binadamu wa Meta

Uhuru wa Kujieleza (Kifungu cha 19 cha ICCPR)

Kipengele cha 19, aya ya 2 ya Mkataba wa Kimataifa kuhusu Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR) kinasema kwamba “kila mtu atakuwa na haki ya uhuru wa kujieleza; haki hii itajumuisha uhuru wa kutafuta, kupokea na kutoa maelezo na maoni ya kila aina, bila kujali vizuizi, iwe kwa maneno, maandishi au kwa chapisho, kwa njia ya sanaa, au kupitia midia nyingine yoyote.” Maoni ya Jumla Nambari 34 (2011) yanabainisha kwamba semi zinazolindwa ni pamoja na semi zinazoweza kuzingatiwa kuwa “za kuudhi mno” (aya ya 11).

Pale ambapo serikali imeweka vikwazo dhidi ya usemi, vikwazo hivyo lazima vitimize masharti ya kutii sheria, lengo halali na umuhimu na ulinganifu (Kifungu cha 19, aya ya 3, ICCPR). Masharti haya mara nyingi huitwa “jaribio la sehemu tatu.” Bodi hutumia mfumo huu kutafsiri ahadi za hiari za haki za binadamu za Meta, kuhusiana na uamuzi wa maudhui ya mtu binafsi unaokaguliwa na kile hii inamaanisha kuhusu mbinu pana ya Meta ya udhibiti wa maudhui. Kama vile Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza alivyosema, ingawa “kampuni hazina wajibu wa Serikali, aina ya athari zao huzihitaji kutathmini aina sawa ya maswali kuhusu kulinda hali za kujieleza huru za watumiaji wao” ( A/74/486, aya ya 41).

I. Uhalali (Uwazi na Upatikanaji wa Sheria)

Kanuni ya kutii sheria chini ya sheria ya kimataifa kuhusu haki za kibinadamu inahitaji sheria zinazodhibiti kujieleza kuwa wazi na zinazoweza kufikiwa (Maoni ya Jumla Nambari 34, aya ya 25). Kanuni zinazozuia kujieleza “haziwezi kutoa uamuzi usiozuiliwa kwa kizuizi cha uhuru wa kujieleza kwa wale walioshtakiwa kwa utekelezaji [wao]” na “zitoe mwongozo wa kutosha kwa waliohukumiwa na utekelezaji wao ili kuwawezesha kuwa na uhakika kuhusu aina za usemi zimewekewa kikomo vizuri na aina zisizo na kikomo” ( Ibid). Ilitumika kwa sheria zinazosimamia matamshi ya mtandaoni, Mwandishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kujieleza amesema zinapaswa kuwa wazi na mahususi ( A/HRC/38/35, aya ya 46). Watu wanaotumia majukwaa ya Meta wanapaswa kufikia na kuelewa sheria, na wakaguzi wa maudhui wanapaswa kuwa na mwongozo wazi kuhusu utekelezaji wao.

Bodi imepata kwamba hatua ya Meta ya kupiga marufuku “usemi wa vurugu au kuunga mkono” kwa maandishi au namna ya michoro unaolenga vikundi vinavyolenga vyenye sifa zinazolindwa, au semi kwamba sifa zinazolindwa hazipaswi kuwepo na semi zinazoendeleza au kuhimiza kujitoa uhai ni wazi kwa njia ya kutosha.

Bodi imebaini hata hivyo kwamba, Meta inaweza kuboresha usahihi wa utekelezaji kuhusiana na sera zinazohusika katika kesi hii kwa kutoa mwongozo wa wazi zaidi kwa wakaguzi binadamu, kama ilivyoshughulikiwa chini ya sehemu ya 8.1 hapa juu. Meta inapaswa kuweka wazi utoaji taswira za utambulisho wa jinsia, kama vile kupitia bendera, hauhitaji kuonyesha wahusika binadamu ili kuwa shambulio chini ya sera ya Matamshi ya Chuki. Meta pia inapaswa kuweka wazi kwamba mwito kwa kikundi (tofauti na mtu binafsi) kujitoa uhai unakiuka Sera ya Kujitoa Uhai na Kujijeruhi.

II. Lengo Halali

Uzuiaji wowote wa usemi unafaa kufuatilia mojawapo ya malengo halali ya ICCPR, ambayo yanajumuisha “haki za wengine.” Katika maamuzi kadhaa, Bodi imegundua kwamba sera ya Meta ya Matamshi ya Chuki, ambayo inalenga kuwalinda watu kutokana na madhara yanayosababishwa na matamshi ya chuki, ina lengo halali linalotambuliwa na viwango vya kimataifa kuhusu sheria za haki za binadamu (angalia, kwa mfano, uamuzi wa Katuni ya Knin). Kando na hayo, Bodi imepata kwamba, katika kesi hii, mkondo wa sera ya Kujitoa Uhai na Kujijeruhi kuhusu maudhui yanayohimiza watu kujitoa uhai au kujijeruhi unawezesha malengo halali ya kulinda haki za watu kufurahia kiwango cha juu zaidi kinachowezekana cha afya ya mwili na akili (ICESCR 12) na haki ya maisha (Kifungu cha 5, ICCPR). Katika kesi kama hii, ambapo kikundi chenye sifa inayolindwa inahimizwa kujitoa uhai, sera dhidi ya Kujitoa uhai na Kujijeruhi pia inalinda haki za watu za usawa na kutobaguliwa (Kifungu cha 2, aya ya 1 ya 1, ICCPR).

III. Umuhimu na Uwiano

Kanuni ya umuhimu na usawa inatoa vizuizi vyovyote vya uhuru wa kujieleza “lazima viwe vinafaa ili kufanikisha kazi yao ya ulinzi; lazima viwe ni vyombo vya ukali wa chini zaidi kati ya vile vinavyoweza kufikia lengo lao la ulinzi; [na] lazima viwe na usawa na mapendeleo ya kulindwa” ( Maoni ya Jumla Nambari 34 , aya ya 34).

Wakati wa kutathmini hatari zinazosababishwa na maudhui ya vurugu, Bodi kwa kawaida huongozwa na jaribio la vipengele sita lililofafanuliwa katika Mpango wa Utekelezaji wa Rabat, ambalo huzungumzia utetezi wa chuki ya kitaifa, mbari au kidini unaojumuisha uchochezi wa uhasama, ubaguzi au vurugu. Kulingana na tathmini ya vipengele husika, haswa maudhui na namna ya usemi, nia ya mzungumzaji na muktadha ulioelezwa zaidi hapa chini, Bodi imepata kwamba kuondoa maudhui kunatii wajibu wa Meta wa kulinda haki za binadamu kwa kuwa kunaleta au kunaweza kusababisha madhara. Kuondoa maudhui ni udhibiti muhimu na unaofaa wa usemi ili kulinda haki ya maisha, na vilevile haki ya kufurahia kiwango cha juu zaidi kinachowezekana cha afya ya kimwili na akili kwa jamii pana ya LGBTQIA+ na, haswa, watu wanaobadilisha jinsia zao wanaotoka nchini Polandi.

Ingawa Bodi awali ilibainisha umuhimu wa kuondoa maneno ya matusi dhidi ya watu wa LGBTQIA+ katika kukabiliana na upotoshaji (angalia uamuzi wa Kurejesha maneno ya Kiarabu), hali ni tofauti hapa. Chapisho hili pia haina kauli ya kisiasa wala inayostahiki kuwa habari (angalia uamuzi wa Maandamano ya Kolombia). Chapisho katika kesi hii inaangazia picha ya bendera ya watu wanaobadilisha jinsia zao inayoning’inia kama pazia, ikiwa na maeelezo kwamba pazia hujining’iniza. Kwa mujibu wa wataalamu ambao Bodi waliwasiliana nao, matumizi ya pazia – katika namna zote mbili za mchoro na matini – hayaonekani kuwa lugha fiche inayojirudia inayolenga watu wanaobadilisha jinsia zao. Hata hivyo, kama ilivyojadiliwa hapa juu, hali ya “ubunifu wa kuhujumu,” au matumizi ya lugha mpya na mikakati ya uwakilishaji ili kuonyesha chuki na unyanyasaji, ni jambo ambalo lipo katika sifa za maudhui zinazolenga watu wanaobadilisha jinsia zao. Bodi imepata kwamba maudhui katika kesi hii yanapo kabisa katika mwelekeo huo. Ingawa chapisho hili lilitumia picha ambayo baadhi ya watu walipata kuwa ya “ucheshi” (kama ilivyoonyeshwa na hisia za emoji za “Haha”), chapisho hilo bado linaweza kufasiriwa kama yenye vurugu na taarifa ya uchokozi inayolenga jamii za watu wanaobadilisha jinsia zao. Ucheshi na kejeli bila shaka zinaweza kutumiwa kusukuma mipaka ya kukosoa kwa njia halali, lakini haziwezi kutumiwa kuendeleza matamshi ya chuki. Chapisho hili linashirikisha tu mada ya viwango vya juu vya kujitoa uhai miongoni mwa jamii za wanaobadilisha jinsia zao ili kusherehekea ukweli huu.

Ilipokuwa ikizingatia nia ya muundaji wa maudhui, Bodi inabainisha kwamba wasifu wake ulitaja kwa wazi kwamba yeye ni “mtu anayechukia watu wanaobadilisha jinsia zao.” Ingawa Meta ilizingatia athari za kauli hii baada katika maudhui ya kesi yenyewe, Bodi imepata kuwa inafaa zaidi kubaini nia ya mtumiaji. Inaweza pia kuwa msingi huru wa kuondolewa kwa maudhui kama ukiukaji wa Kiwango cha 2 cha sera ya Matamshi ya Chuki. Chapisho hili pia linaeleza kitendo cha watu wanaobadilisha jinsia zao kufa kupitia kujitoa uhai kuwa “usafishaji wa mapukutiko,” ikiwa ni pamoja na emoji ndogo ya moyo inayoambatana na maelezo. Kuhusiana na kauli ya kuunga mkono kifo cha kikundi kupitia kujitoa uhai, Bodi imepata nia ya kuhimiza ubaguzi na vurugu kwa msingi wa maudhui ya chapisho, picha iliyotumiwa na maandishi na manukuu yaliyoambatana. Maudhui katika kesi hii kando na kuhimiza watu wanaobadilisha jinsia zao kuchukua hatua ya vurugu dhidi yao pia inawachochea wengine kuwabagua na kuwaonyesha ukatili watu wanaobadilisha jinsia zao. Uelewa huu unathibitishwa na ukweli kwamba emoji ya hisia ambayo imetumiwa mara kwa mara na watumiaji wengine wanaojihusisha na maudhui haya ilikuwa “Haha.”

Hatimaye, Bodi imebaini hatari kubwa za nje ya mtandao ambazo jamii ya LGBTQIA+ ya Polandi hukabiliwa nazo kupitia ongezeko la mashambulio kupitia hatua za uundaji sheria na utawala, na vilevile semi za kisiasa na maafisa muhimu serikalini na sauti zenye ushawishi katika umma. Tangu 2020, Polandi imekadiriwa mara kwa mara kama nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya inayofanya vibaya zaidi katika kulinda haki za LGBTQIA+ kulingana na ILGA-Europe. Pia ni muhimu kubaini kuwa Polandi, haina ulinzi kwa LGBTQIA+ katika sheria zake dhidi ya matamshi ya chuki na uhalifu wa chuki, suala ambalo ILGA-Europe na Amnesty International, miongoni mwa mashirika mengine, yametoa mwito kwa Polandi kutatua. Zaidi ya hayo, ongezeko la semi dhidi ya LGBTQIA+ kwa Kipolandi kwenye Facebook, limeripotiwa na wataalamu wa nje na maoni mengi ya umma, hayafanyi kivyao. Mashirika na taasisi nyingi zimeonyesha wasiwasi kuhusu ongezeko la semi dhidi ya LGBTQIA+ kwenye mitandao ya kijamii. Mtaalamu Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mwelekeo wa Ngono na Utambulisho wa Jinsia (IE SOGI) Victor Madrigal-Borloz amesema viwango vya vurugu na ubaguzi dhidi ya watu wenye namna anuwai za jinsia na wanaobadilisha jinsia zao “unaudhi razini za binadamu.” Utafiti na ripoti ya GLAAD imepata kwamba kuna “madhara halisi sana yanatokea kwa watu wa LGBTQ mtandaoni, ikiwa ni pamoja na … matatizo ya kisaikolojia inayotokana na kukabiliwa na ubaguzi na mienendo ya chuki kila mara.” Maudhui kama vile chapisho katika kesi hii, hususan yakizingatiwa katika kiwango, yanaweza kuchangia mazingira ambapo madhara ambayo tayari yapo ya kifo kupitia kujitoa uhai ndani ya jamii ya watu wanaobadilisha jinsia zao imeongezeka. Zaidi ya hayo, maudhui yanayofanya semi za vurugu dhidi ya watu wanaobadilisha jinsia zao kuwa za kawaida, kama ilivyo katika chapisho hili, zinaweka hatari ya kuchangia katika janga linaloendelea la afya ya akili inayoathiri jamii za watu wanaobadilisha jinsia zao, na vilevile ongezeko la vurugu zinazolenga jamii hiyo nje ya mtandao.

9. Uamuzi wa Bodi ya Usimamizi

Bodi ya Usimamizi imebatilisha uamuzi wa awali wa Meta wa kuacha maudhui hayo.

10. Mapendekezo

Sera ya Maudhui

1. Ukurasa wa sera ya Meta dhidi ya Kujitoa Uhai na Kujijeruhi unapaswa kuweka wazi kwamba sera hii inapiga marufuku maudhui yanayoendeleza au kuhimiza kitendo cha kujitoa uhai yanayolenga kikundi cha watu kinachoweza kutambuliwa.

Bodi itazingatia kuwa hili limetekelezwa wakati lugha ya umma ya Viwango vya Jumuiya kuhusu Kujitoa uhai na Kujijeruhi inaonyesha badiliko linalopendekezwa.

Utekelezaji

2. Mwongozo wa ndani wa Meta inayowapatia wakaguzi kwa kiwango unapaswa kubadilishwa ili kuhakikisha kuwa taswira zinazoonyeshwa kwenye bendera za utambulisho wa kijinsia ambazo hazina sura ya binadamu zinaeleweka kama viwakilishi vya kikundi kinachofafanuliwa na utambulisho wa kijinsia wa wanachama wake. Ubadilishaji huu unapaswa kuweka wazi maagizo ya utekelezwaji ya namna hii ya maudhui katika kiwango kila yanapokuwa na shambulio la ukiukaji.

Bodi itazingatia kuwa hili limetekelezwa wakati Meta itaipatia Bodi mabadiliko kwenye mwongozo wake wa ndani.

*Dokezo la Kiutaratibu:

Maamuzi ya Bodi ya Usimamizi yanatayarishwa na majopo ya Wanachama watano na kuidhinishwa na wengi wa wanachama wa Bodi. Maamuzi ya Bodi hayawakilishi maoni ya kibinafsi ya Wanachama wote.

Kwa uamuzi wa kesi hii, utafiti huru ulipangwa kwa niaba ya Bodi. Bodi ilisaidiwa na taasisi huru ya utafiti yenye makao yake makuu katika Chuo Kikuu cha Gothenburg, ambayo inashirikisha timu ya zaidi ya wanasayansi wa kijamii 50 kutoka mabara sita, pamoja na zaidi ya wataalamu 3,200 wa kila nchi kutoka kote ulimwenguni. Memetica, shirika ambalo linajihusisha na utafiti wa chanzo huria kuhusu mienendo ya mitandao ya kijamii, pia ilitoa uchanganuzi. Utaalam wa lugha ulitolewa na Lionbridge Technologies, LLC, ambayo wataalamu wake wanajua lugha zaidi ya 350 na hufanya kazi kutoka miji 5,000 ulimwenguni kote.

Volver a Decisiones de casos y opiniones consultivas sobre políticas